Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,793
- 71,206
Soma kwa makini nichoandika.Kuna mtu hapa alituma record ya wachingiaji wa mswaada huu, Wapinzanzani wengi tu walichangia lakini hili hawakuliona??
Soma kwa makini nichoandika.Kuna mtu hapa alituma record ya wachingiaji wa mswaada huu, Wapinzanzani wengi tu walichangia lakini hili hawakuliona??
Lapigwa dana dana na mwenyekiti wa Bunge hadi saa saba mchana wakutane kikamati na watoa hoja waje na data za kueleweka juu ya kipi wananchi wanakilalamikia.
Wabunge wa CCM wamzomea Lissu kwa hoja ilipitishwa tayari na bunge
Kama hapo saa saba itabaki hivyo walivyopitisha mwanzo, basi nasisitiza kuwa na wao Wabunge mafao yao ya baada ya miaka mitano yaingizwe katika mifumo ya mifuko ya PENSHENI ya UZEENI wasilipwe mkupuo!.
Mkuu asante kwa ufafanuzi, lakini kama hapo saa saba Bunge itaagiza kama ulivyosema tayari haitakuwa kama nilivyosema hapo juu kuwa iwapo itabaki kama walivyoamua hapo awali. Lakini bunge likiona ni sawa mswada uliopitishwa awali uendelee kama sheria halali ndiyo nilichopendekeza hapo juu tukishikie bango!.kazi ya kamati ya uongozi wa bunge ni kupanga ratiba na uendeshaji wa bunge kwa hiyo hata kama kamati ikiruhusu lijadiliwe si kwamba ndio madiliko yatapitishwa leo. Bunge litaiagiza serikali kuleta mswada wa mabadiliko ya sheria hiyo ili bunge lijadili na kuidhinisha. Na huenda mabadiliko hayo wakayaleta bunge lijalo..
wabunge wasijaribu kupitisha sheria ya namna hiyo. naumia kodi kubwa then na NSSF wanaitamani! aah hilo haiwezekani. tumeona east africa wakilala barabarani wakidai haki zao za msingi, iweje tukiwa na reference mtuambie nikiwa na nguvu nisitumie mafao yangu baada ya kujitoa mwanachama ili kufanya miradi mingine....! au mnataka nguvu zikishaisha tuje tuandamane kudai haki zetu.
MP you have to swallow this and digest it properly and not to panic otherwise tutawaadhibu kwa kutoa elimu hata kwa wasiolifahamu ni jinsi gani msivyokuwa makini na uchaguzi ujao ni kupigwa chini tu.
nawakilisha
Lakini je, si wanaweza kuamua kusitisha kuanza kutumika kwa hii sheria. Na tunaomba hawa wabunge wawaambie wazi kabisa kuwa wapite kwa wafanya kazi kutaka maoni..
Mh: Jaffu aliomba muongozo wa spika kupitia kwa Jenista Mhagama na kuomba swala la mifuko ya jamii lijadiliwe bungeni kama jambo la dharura kwasababu wananchi wengi wanalalamikia mabadiliko ya sheria ya kupata mafao pale mwanachama atakapo fikia umri wa miaka 55.
Jenista Mhagama akakubaliana nae kisha akamuagiza akapange hoja yake vizuri in details aiwakilishe bungeni saa saba mchana ili ijadiliwe na wabunge.
Unadhani uwepo wao hao wachache unaweza kubadili nini? Ni wakati wa wananchi (hasa wafanyakazi) kujiuliza nini matokeo ya uamuzi wao wa kuipa kura CCM 2010. Majuto mjukuu.
Lakini je, si wanaweza kuamua kusitisha kuanza kutumika kwa hii sheria. Na tunaomba hawa wabunge wawaambie wazi kabisa kuwa wapite kwa wafanya kazi kutaka maoni..
Mh. Lugola leo amewasuta na kuwaonyesha wabunge kuwa ni wanafiki kwa kitendo chao cha kupitisha sheria ya mpya ya mifuko ya jamii na leo kuonekana kuunga mkono hoja ya Lusinge alietaka bunge lijadili kwa dharura kanuni hiyo ili ibadilishwe.
Baada ya mh. Lusinde kutoa hoja hiyo wabunge wengi waliiunga mkono kanakwamba sio wao waliipitisha sheria hiyo inayozuia mafao ya kujitoa mpaka mtu afikishe angalau miaka 55. Kweli hatuna bunge makini ila tuna bunge la ndio hata kwa mambo ambayo ni wazi si ya kupitisha kabisa.
Hivi sheria hii inatofauti gani na zile za kikoloni? Hivi kweli hawa ni wabunge kwa ajili ya kutete mwananchi au ni wabunge kwa ajili ya kutetea serikali? Hili bunge bora livunjwe kwani ni mzigo na ni janga la kitaifa.
Mh. Lugola aliomba muongozo na alipopewa nafasi aliwasuta wabunge na kusema bunge haliko makini. Mimi naungana na huyu mh. kwani ni wabunge hawahawa ndio walipitisha sheria hii mwezi Aprill mwaka huu ila baada ya kuona umma umekuja juu sasa wanajidai kutetea wananchi.
Mtu mnafiki ni hatari kuliko hata ukoma.
Hawawezi kusitisha kutumika kwa sheria. Hii sheria imeshaanza kufanya kazi tangu July 1, 2012.
Kamati inachoweza kuafnya ni kuiagiza SERIKALI ilete muswaada wa marekebisho wa sheria hiyo katika HATI YA DHARURA.