Kupanda kwa nauli je, LATRA ina Mchumi mahiri kweli?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Maswali:-

1. LATRA ipo kwa ajili ya kukusanya fedha za uchaguzi mkuu au?

2. LATRA inapandisha nauli bila bei ya mafuta kupanda?

3. LATRA kama ni Mamlaka ya Udhibiti je, udhibiti maana yake ni kupandisha tu nauli na hauna uhusiano na kushusha nauli?

4. Ni lini LATRA ilishusha nauli tangu ianzishwe?

5. Kama uchumi wa nchi unakuwa kwa 6% (aliyoacha Magufuli baada ya C-19 kuishusha toka 8%) kama tunavyoaminishwa je, kwanini LATRA isiakisi ukuaji huo kwenye viwango vya nauli kwa kuvishusha?

6. Je, LATRA inajuwa kuwa watu wanakula mlo mmoja?

7. Je, LATRA inajuwa kuwa imepandisha nauli bila mishahara ya watumishi na mikopo ya elimu ya juu kupandishwa?

8. Je, LATRA inajuwa kuwa kupandisha nauli kutapaisha bei za bidhaa na huduma?

9. Je, LATRA inajuwa kama no. 8 hapo juu itazua mfumuko wa bei na kushusha thamani ya sarafu?

10. Je, LATRA inajuwa kuwa no. 8 na 9 hapo juu zitapandisha gharama za maisha na kushusha viwango vya maisha?

11. Je, LATRA inajuwa kuwa kwa kung'ang'ania kufanya kazi ya kupandisha nauli tuuu inakuza maadui 3 wa taifa huku rais akisisitiza kupambana nayo?

12. Je, LATRA inajuwa kuwa utendaji wake unakihujumu CCM au?

13. Je, tuamini kuwa LATRA inasafiri peke yake nje ya boti ya kuandama dira ya taifa ya 2025?

14. Je, ni mafanikio yepi LATRA imeiletea nchi tangu kuanzishwa kwake?

15. Je, ikipigwa kura ya maoni LATRA itapona?

16. Je, LATRA inasaidiaje kutekeleza ilani ya CCM?

17. Tanzania bila LATRA inawezekana.
 
Kwa issue ya nauli tumepigwa.

Watanzania hawana mtetezi, walioshika mpini wakikohoa serikali inaleta dawa ya kikohozi.

Hadi wanachemka kupanga nauli Dodoma to Iringa ipo juu kuliko Dodoma to Songea.
 
Back
Top Bottom