Story ya mapenzi ya kweli: Nakupenda JK

Status
Not open for further replies.
Hpa lazima kesho asubuhi nikinukishee..yaaanii lazima ije story pendwa..NAKUPENDA JK Mapemaaa..nikiamka tu..Stay tuned for Episode 17 guyz..
 
STORY: Nakupenda JK
MTUNZI & MWANDISHI: Jumaa Khatib Mdharuba(Jk).

+255718274130
+255654727266

EPISODE 017
★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA...
Rukia bado alikua amesimama nyuma ya mlango ule, akaangalia chumba vizuri kisha huku akiwa amenipa mgongo, akainama na kuanza kufungua viatu vyake, sketi yake fupi yenye mpasuo ikanipa nafasi ya kuona asilimia 90 ya paja lake...Nikajikuta nang'ata kidole...
Nikanyanyuka pale nilipokuwa, nikamsogelea na kumshika kiuno.

TWENDE PAMOJA SASAA..
Rukia alishtuka, akashindwa kuendelea na zoezi lake la kufungua kiatu chake cha mguu wa kulia, kile cha kushoto alishakifungua tayari..
“Jamaaaniii Jk, mimi nipo kwa ajili yako hapa leo, mbona kama una haraka?” Rukia alinambia maneno haya huku akiniangalia kwa uchokozi na macho yake makubwa yaliyoonekana kulegea kama mtu aliyekula 'kungu'. Nikaamua kumuacha amalizie kufungua kiatu chake bila kuongea kitu chochote..
Nikarudi pale kwenye sofa, nikakaa..kisha nikatoa simu yangu, nikaiangalia sana na kujiuliza maswali mawili matatu, nikaamua kuizima. Rukia akaja pale nilipokua nimekaa akakaa kwenye mapaja yangu, nikawa nimempakata. Nikaizungusha mikono yangu miwili katika kiuno chake ambacho kilikuwa laini sana kama wale wachezaji wa 'baikoko'. Rukia yeye wakati huu alikua akinitazama, mikono yake ameizungusha kwenye shingo yangu..
“Sijui nianzie wapi, lakini naweza kusema kiufupi tu, NAKUPENDA JK, nakupenda sana, na sijui ni kwanini nimejikuta nakupenda hivi..sielewi” Rukia aliongea maneno haya huku akitabasamu, wakati huu mkono mmoja alishautoa kwenye shingo na kuuleta kidevuni kwangu. Akawa anapapasa kidevu kile ambacho kilikua na dalili za ndevu kwa mbaali..
“Asante sana Rukia, hata mimi nakupenda sana, afu kuna kitu kimoja.. ” Niliamua 'kuunga mkono' hoja ya kupendwa na Rukia, ingawa ukweli ni kuwa nilimtamani tu kwa ajili ya hii kazi tu na si vinginevyo.
“Kitu gani hicho Jk?” Aliniuliza kwa shauku.
“u r so so cute, yaanii..nakufananisha na Kajol yule wa Bollywood” Hapa nilijaribu kutumia rule #1 ya "Msifie ajione yuko juu azidi kukupenda", ndivyo wanawake wanavyotaka, sheria hii ni muhimu sana, sasa naachaje kumsifia? Alikua mzuri ndio, lakini sio wa kufikia kufananishwa na Kajol, huko mbali sana..Lakini kwa kuwa akili ya mwanamke ilipenda zaidi kusikia akisifiwa, niliamua kufanya hivyo.
“Aaasaaante Jk, ila mi mbona wa kawaida tu” Rukia aliamua kujishusha kule nilikompandisha.
“Vya kawaida navijua mimi banaa.. Kuna kawaida iko wapi hapa Rukia..” Nilimwambia maneno haya kumrudisha kulekule nilipompeleka halafu nikamtekenya kidogo, akaruka juu huku akicheka.. Nikambeba, nikamtoa pale kwenye sofa na kumhamishia kitandani.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Darling, waambie nyumbani watoe siku ya kuleta barua, sisi tupo tayari huku, kwahiyo tunawasikiliza nyinyi tu” Feisal alikuwa akimwambia Nuro kuhusu mpango wa kuleta barua ili utaratibu wa kuoa ukamilike..
“Sawa MyLove, nitafanya hivyo haraka..” Nuro ambaye alikuwa na hamu zaidi ya kuishi na mume ampendaye, wala hakupoteza muda, moja kwa moja kwa bibi yake na kumueleza habari ile. Akamuomba bibi yake aongee na wazazi wake ili waweze kutoa ruhusa jambo hilo litendeke na waseme ni siku gani ambayo watakua na nafasi..
Hatimaye siku ikapangwa na Feisal akaambiwa siku rasmi ya kuleta barua.. Hapa Nuro furaha yake iliongezeka maradufu.
“I can't blv..my Fey jamaanii...hatimaye tunaishi pamoja..Alhamdulillah” Nuro alikuwa mwenye furaha sana, akiyasema haya baada ya kumpa majibu yaliyotoka nyumbani kwao bwana Feisal.. Wakaongea mengi sana ya kimapenzi na kufarijiana..mpaka walipoagana. Nuro akashindwa kujizuia kukaa na furaha ile peke yake.. Akaamua awatafute wanawe angalau awaeleze habari ile njema juu ya mama yao kuolewa na mtu ampendaye. Akaamua kuanza na Sophy, akapiga simu yake lakini haikupokelewa..akaamua kupiga tena mara ya pili na ya tatu lakini bado hakukuwa na majibu. Akaachana nae na kuamua kumpigia simu Jessca, simu yake iliita lakini nayo haikupokelewa..akawaza kwa muda amewakosea nini wanawe wale wa kuwazaa mwenyewe..tayari ilishakua ni saa 12:30 jioni, akapiga tena simu ya Jessca, ikaita kwa muda mrefu sana, baadae ikapokelewa..
“Haloo, mgonjwa amepumzika kwahiyo nadhani akiamka atakutafuta” Ndio majibu aliyoyapokea Nuro kutoka upande wa pili wa simu.
“Mgonjwa? Mgonjwa gani tena?” Aliuliza Nuro akiwa amehamaki.
“Mwenye simu hii ni mgonjwa amelazwa hapa hospital ya mkoa, ndiye ninayekwambia” Alijibu mtu yule na kuzidi kumueka Nuro katika wakati mgumu.
“Yaani..unataka kunambia Jessca amelazwa hospitali ya mkoa? Kafanyaje? Na kalazwa tangu lini?”
“Kaletwa leo asubuhi na kijana mmoja hivi.. Na hapa alipo ametundikiwa dripu ya damu”
“Wewe ni nesi?” Nuro alimuuliza mtu yule hapa presha ilishakua juu.. Kwa jinsi anavyompenda Jessca ilikua haielezeki kwa maneno ya kawaida. Jessca kwake alikua ni zaidi hata ya Feisal, mume wake mtarajiwa..
“Ndio, mimi ni nesi na ndo niko zamu leo hapa wodini.. Jina langu ni Gyna”
“Ok sawa Gyna, nakuja sasa hivi hapo hospital”
“Hapana, saa hizi muda wa kuona wagonjwa ulishapita, kwahiyo labda uje asubuhi”
“Hapana, kwani mgonjwa yupo na nani?”
“Yuko peke yake tu, hata huyo aliyemleta simu yake haipatikani”
“Sasa nisikilkze mwanangu, mimi huyo Jessca ni mwanangu kabisa wa kumzaa, sina taarifa kuwa yupo hapo hospital, sasa naomba ushirikiano wako ili nije kumuona na nijue yuko kwenye hali gani..pliiizzzz”
“Kama ni hivyo sawa, wewe njoo mpaka hapa hospital halafu nitakuombea kwa walinzi”
“Ok asante sana” Nuro alitoa shukrani wakati huu alikua akifunga mlango wa nje wa nyumbani kwao, kila alichotaka kukifanya alihisi anachelewa, alichokiwahi ni kukumbuka pochi yake tu ambayo ilikua na kiasi cha pesa, akashikilia simu yake mkononi. Alipotoka nje akatembea kidogo mpaka barabara ya 4 palipokua na vijana wa bodaboda..akapanda pikipiki ya kijana mmojawao na kumuamuru ampeleke hospitali ya Mkoa.
Alipofika hospital akapiga ile namba.
“Haloo, Gyna..nimeshafika hapa hospitali, nipo getini”
“Ok, sawa nakuja, ila pita hapo getini ingia ndani tu, hawawezi kukuzuia, wanazuia kuingia wodini tu”
Gyna alipokuja wakaongozana mpaka katika mlango wa kuingia wodini. Gyna akamuombea Nuro kwa mlinzi aliyekua amekaa pale ili amruhusu dakika tano tu akamuone mgonjwa maana ni mwanawe na yeye hakuwa na taarifa. Bahati nzuri mlinzi huyu alielewa japo ilkua ni nje ya utaratibu. Dharura hutokea, ingawa wapo watu ambao wakikaa sehemu kama hizi huwa hawaamini kuwa kuna dharura.
“Oooh, my God!! Jamaanii Jessca wangu..mumy..Aaaghh..” Nuro alishindwa kuzuia kilio baada ya kumuona mwanawe yule kipenzi akiwa ametundikiwa dripu pale wodini..Jessca mpaka sasa alikua hajitambui. Gyna alipata kazi ya ziada ya kumbembeleza mpaka hapo alipofuta machozi.
“Unaweza kunambia sababu ya kupoteza damu nyingi kiasi hiki ni nini?” Nuro alimuulza Gyna baada ya kufuta machozi.
“Mimi sijui, labda nikupe namba ya simu ya Dokta umuulize” Gyna alikwepa lile swali asije akajibu halafu akawa ameharibu, maana kwa sheria ya nchi kutoa mimba ni 'illegal'.
“Nitashukuru pia” Nuro alijibu kuashiria anahitaji namba ya Dokta. Akapewa na kupiga, haikuchukua muda mrefu tangu simu ianze kuita ikapokelewa.
“Haloo Dokta habari,?”
“Nzuri tu, nani mwenzangu?”
“Mimi naitwa Nuro, mama Mzazi wa huyu mgonjwa hapa hospitali Jessca, ndio nimefika hapa hospitali kutaka kujua nini kimempata mwanangu mpaka kupoteza damu nyingi, ndo huyu Gyna hapa amenipa namba yako”
“Ooh..mama Jessca, duuh kumbe Jessca ana wazazi wanaomjali? Mimi nilipoletewa na yule kijana asubuhi ambaye alitaka watoe mimba sikua najua kuwa Jessca ana wazazi wanaomjali, nilidhani ni hawa watoto waliokimbia kwao..”
“Dokta, unasemaje? Jessca ametoa mimba? Muungu wanguu” Nuro aliishiwa nguvu na simu yake ikaanguka sakafuni.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nilipomuangusha pale kitandani, nikaanza na shingo yake iliyokua inaonekana safi na ya kupendeza.. Ilinishawishi kupeleka mdomo wangu bila kusita. Cheni ndogo ya dhahabu iliyomeremeta ilizidi kuipamba shingo ile maridhawa.. Nikaanza kuipitishia ulimi taratibu huku vidole vyangu vikitalii katika masikio yake. Baada ya kupita dakika tano tu ya zoezi hili, Kinyume na matarajio yangu, Rukia alitoa sauti ya juu sana akilalamika kimahaba.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Let's col it A day..

Tusubiri hatma ya Rukia Episode ya 18..
Nice weekend!!

Usisahau kufollow instagram @jk.stories upate story tamu zaidi.

Kama kuna lolote pia tuwasiliane: +255718274130/+255654727266
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom