Story ya mapenzi ya kweli: Nakupenda JK

Status
Not open for further replies.
STORY: Nakupenda Jk
MTUNZI & MWANDISHI: Jumaa Khatib Mdharuba(Jk)

+255718274130

EPISODE 16
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Baby, mimi nahisi nina mimba yako” Sophy ambaye alikua ameegesha kichwa chake katika kifua cha Zassor, aliamua kueleza kile anachohisi. Ni takriibani wiki tatu sasa tangu ahamie pale kwa Zassor. Zassor ambaye hakupenda kusikia habari za mimba, alishtuka kidogo, akatoa kichwa cha Sophy pale kifuani na akaamua kukaa pale kitandani. Sophy nae alipoona hivyo akaamua akae wakawa wanatazamana.
“Unasemajee??”
“Nina mimba yako, kwani hujanisikia?”
“Wewe una masikhara sana, nani kakwambia nalea mimba mimi? Aliyekutuma unitafutie lawama ni nani? Acha ujinga wewe”
“Sasa maneno yote hayo yanatoka wapi Zassor?, wewe si ndiye uliyekua unakataa condom hapa? Au sio wewe unaenambia kila siku kuwa condom hazikupi ladha unayostahili? Sasa ulitegemea matokeo gani?” Sophy aliamua 'kumkazia' Zassor lakini kwa upole..
“Daah, kweli..lakini mmmh..unanipa wakati mgumu sana Sophy..biashara yenyewe vocha hapa na wewe unaniletea kuzaa tena..”
“Na ukae ukijua kuwa mimba hii HAITOKI, hilo ulijue mapema, ” Sophy alitoa tahadhari kwa sababu alimfahamu vizuri Zassor..
Wakaongea sana kuhusu mimba na maisha yao, Zassor alishaona mzigo mzito upo mbele yake, ila atafanyaje sasa..?! Aliwafikiria wasichana zake ambao alikua akitembea nao wote, akaona sasa ni muda wa kubadilika na kuanza kuishi na Sophy, kuachana kabisa na habari za kijinga.
Sophy licha ya kumkazia Zassor, wasiwasi wake mkubwa ulikua huenda ile mimba ilikua ni ya Ahmed.. Kwa jinsi alivyokua siku ile, na asubuhi baada ya kuamka na kuondoka pale nyumbani, Sophy alihisi ameondoka na mimba ya babaake-Ahmed, lakini aliamua kukimbilia kwa Zassor maksudi kwani ndiye mnyonge wake, mtu asiyeweza kustahmili mbele ya mwanamke. Na ndio maana siku ileile alipofika tu, Zassor aliamua 'kumstarahamu' Sophy bila hata kinga. “Ujinga wake huu ndio utakaofanya asingiziwe vitu hata kama si vya kwake, hata kama nampenda sana, lakini sina jinsi, atalea tu” Kila siku Sophy alijisemea maneno haya akikumbuka jinsi Zassor alivyompupia baada ya kutoka kwa mamaake ile siku.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya Dokta Mwinyi kusema vile, tukaongozana nae mpaka kwenye kile chumba ambacho Jessca alikuepo.
“Zoezi nimelimaliza ila mgonjwa amepoteza damu nyingi sana, na mpaka sasa bado anaendelea kupoteza damu, nimemwekea drip ya damu kama unavyoona, ingawa inabidi uongeze pesa kidogo kwa ajili ya hii damu hapa, maana nimefanya kuiba tu kutoka hazina, sina ruhusa ya kufanya hivyo kwa wagonjwa wangu binafsi kama hawa” Dokta Mwinyi aliongea akinipa wakati mgumu sasa..alikua hajui kuwa kuniambia kuhusu pesa ni kunichanganya..
Nikamtolea elf 15 nikampa, jumla nikawa nimemlipa elf 45 kwani mwanzoni nilimpa elf 30, bado nilikua na pesa iliyobaki nikitegemea Jessca apate nauli, na matumizi yake ya siku mbili hizi, na pia nilitamani pia pesa hiyohiyo nikalipie sehemu ambayo ningepata usingizi wa leo na Rukia...
Kichwa kiliuma kwani ilikua imebaki hela kidogo sana kutoka katika ile laki moja ambayo niliiba kutoka katika akaunti ya mama.
“Kwahiyo unataka kunambia kuwa leo Jessie atalala hapa?” Niliamua kumuuliza Dokta Mwinyi nikitamani anipe jibu la Ndio ili malengo yangu ya kulala na Rukia yatimie.
“Utalipia kitanda? Kama utalipa gharama za kitanda nitampeleka wodini kule akalale, hapa hawezi kulala mgonjwa, hiki ni chumba cha mapumziko tu baada ya matibabu”
“Gharama za kitanda kwani ni shilingi ngapi?” Niliuliza kwa kujiamini..
“Kwa siku ni elfu 15 tu ”
“Elfu 15?? Mmmh hii hospitali si ni ya serikali?”
“Ndio, wewe bei unazozijua za hospitali ya serikali ni zipi?”
“Mmmh mimi sijui sababu sijawahi kulazwa..”
“Sasa kama hujui kwanini unanibishia mimi ninayejua?”
“Basi Dokta, yaishe..”
Nikazama mfukoni nikatoa elf 15 na kumkabidhi Dokta, nikabakiwa na elf 17 tu..
Niliamua kumlipia Jessca ili alale pale hospitali kwani ndio nafasi ya pekee itakayonifanya nikaenjoy na Rukia leo hii.. Nilijua kuwa elf 17 haitoshi kwa matumizi ya huduma za kulala na kula tena kwa watu wawili, bali niliamini Rukia ambaye alikua akinipigia simu mara kwa mara, alikua na pesa tu, na alikua amejiandaa..isitoshe Rukia alifahamu kuwa mimi ni mwanafunzi na nimemaliza shule juzi tu, kwahiyo ni lazima alijipanga kugharamia..
Dokta Mwinyi alituambia tumuache Jessie apumzike kwanza pale, halafu baadae kidogo atafanya utaratibu wa kumuhamishia wodini. Baada ya maelezo haya Nira aliniaga, akaondoka.. Nikabaki na Dr..
“Naweza kwenda nikarudi baadae kujua hali ya mgonjwa na amewekwa wodi gani?” Nilivunja ukimya, nilishamtumia sms Rukia kuwa niko njiani nakuja maeneo aliyopo. Nikaona sina muda wa kupoteza tena hapa, Dr Mwinyi alinishangaa kwa jinsi nilivyoonekana kuwa na haraka kama ninayewahi jambo flani muhimu.. Hali ya haraka nilishindwa kuizuia..sms za Rukia anazotuma mfululizo zikanifanya nianze kupata hisia katika mwili wangu.
“Ngoja nikukabidhi kwa Nurse kabisa, usije ukakimbia hapa, maana naona una haraka sijui unataka kwenda wapi?”
Kisha tukatoka hadi wodini ambapo Dr alinikabidhi kwa dada mmoja mrembo aliyevalia 'uniform' nyeupe. Alikua na kimo cha wastani, alikua na umbo flani la muonekano wa kawaida, lakini hips zake zilinidatisha.. Sura yake ya duara, na macho yake ya wastani yaliyokaa vizuri pale usoni yalinivutia, lips zake ambazo alizipaka 'shine' ya kung'aa zilikuwa nazo zipo vizuri mno, chini alipigilia raba nyepesi.. Nilipata nafasi pia ya kugundua jinsi anavyotembea, kwakweli alikua 'nurse' haswa..
“Huyu ana mgonjwa wake yupo kule kwangu, baada ya kuzinduka itabidi umuhamishie wodini, ila huyu bwana kama kuna sehemu anataka kuwahi, sasa naomba umuelekeze utaratibu ulivyo ili asipate shida baadae, kila kitu ameshalipia, na faili la mgonjwa utakuja kuchukua pale ofisini kwangu” Dr Mwinyi alitoa maelezo kwa ufupi na 'Nurse' yule akaonekana kuyaelewa.. Kisha akatuacha sisi wawili. Hapa wazo langu lilikua moja tu, kupata namba ya simu ya huyu nesi, fullstop!!.
“Ok, sasa dadaangu mi naomba unisaidie tu kukamilisha hizo taratibu, mimi nawahi sehemu, nitarudi soon”
“ok, sawa hakuna shaka kakaangu”
“Sasa wewe cha kufanya hapa, nipe namba yako ya simu, ili tuwasiliane, si unajua tena tusije tukawa tunaenda 'manually' wakati tupo kidigitali zaidi siku hizi..” Nilitamka maneno haya huku nikimkabidhi nesi yule simu yangu ili aandike namba yake. Aliandika kisha akanikabidhi simu yangu..
“Nisave nani Jina?” Niliuliza.
“Andika Gyna” Wala sikuuliza mara mbili baada ya jibu hili. Nikaagana nae nikaondoka kuelekea mjini ambapo Rukia alitaka tukaonane.
Nikaelekea moja kwa moja mpaka maeneo flani hivi ya Malindi Hotel ambapo ndipo kina Rukia walikuwa wamefikia, hotel hii ilikua karibu na Mkwakwani.
Baada ya kuonana tukatoka pale Rukia akinitaka nitafute sehemu ambayo atakua huru na mimi. Nikachekecha kichwa changu, kisha nikamwambia anifuate tu..Moja kwa moja mpaka maeneo ya Raskazone, nikampeleka kwenye hotel za mitaa ile.. Moja ikisomeka kwa jina la Nyinda Classic., tukazama ndani. Nilijua kuwa Rukia anazo pesa za kutosha tu, kwahiyo sikuwa na shida..maana elf17 yangu hapa isingeweza kulipia hata chumba tu.
“Kwenu kuzuri saana, yaani kama huku pametuliaaa.” Rukia aliamua kupasifia Tanga, haswa maeneo haya ya 'vigogo' mitaa ya Raskazone, kama ilivyo mitaa ya Oysterbay jijini Dar.
“Yaah Tanga raha..” Nilijibu.
Tukaingia mapokezi, nikamtanguliza Rukia mbele, akalipia, tukapewa chumba, nakumbuka ilikua namba 123 ila kilikua chini, sio juu ghorofani ingawa hotel ilikuwa ya ghorofa.
Tulipofika ndani, Rukia akavua kikoti chake alichokua ametupia juu ya ile blauzi yake.. Akatundika katika msumari uliokuwa nyuma ya mlango.. Hapa nikapata nafasi ya kuyona vizuri maziwa yake yaliyobanwa vizuri ndani ya sidiria.. Yalikua nusu wazi kabisa, meupe, yaliyokosa hata doa.. Baada ya hapo akawasha feni, mim nilikua nimekaa katika sofa lililokua chumbani mle, Rukia bado alikua amesimama nyuma ya mlango ule, akaangalia chumba vizuri kisha huku akiwa amenipa mgongo, akainama na kuanza kufungua viatu vyake, sketi yake fupi yenye mpasuo ikanipa nafasi ya kuona asilimia 90 ya paja lake.. Nikajikuta nang'ata kidole..
Nikanyanyuka pale nilipokuwa, nikamsogelea na kumshika kiuno.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Watch Out Episode 17👉soon

+255718274130

Follow insta: jk.stories
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom