Steven Kanumba's Death and Elizabeth Michael a.k.a Lulu's Involvement; The Guide at JF

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,080
Habari wana JF...

Kifo cha Star maarufu katika Upande wa movies kwa Jina la Steven Kanumba kimetikisa taifa kuliko ilivyowahi dhaniwa; Nakubali Kanumba was good na wengine wengi wanadiriki kusema he was The Great. Kwa upande wangu nilikua namkubali kweli, sababu nilimuona alivoanza na alipofika. He was no one but was able to change that.... Na nilikua namkubali more because of the way amechangia ku evolve movie Industry nchini kuliko hata movie zake - nitakua ni Muongo nikisema I have watched more than three of his movies ila nilikua namkubali kama ninavokubali na wasanii wengine hapa nchini kwa michango yao katika entertainment Industry. I have been fortunate to meet him once, and I thot him to be so cool nikifananisha na baadhi ya Ma stars nilo wahi habatika kuwaona (Kwa mfano Hemedi; unaweza chafuka nyongo kwa kumsikiliza na kumtazama swagger zake).

Kifo chake kilikua cha kushtua mno! Wapo ambao kweli kazikwa na tumeanza kusahau, Ila believe me you bado thousands of people wana majonzi hadi dakika hii ya hii thread na post hapa. Kuna watu hawawezi angalia movie wakamaliza; Kilio kinaanza upyaaa... Discussion of his death upya... Hadi leo hii huwezi pita mahala mbali mbali ukakosa sikia randomly akiongelewa. Katika Imani zetu za Kiswahili twaweza justify kwa kusema jamaa alikua na nyota kali sana ya kukubalika na kupendwa. Siamini kama sababu tu inasemekana alikua mcheshi na mkarimu ndio sababu pekee... I don't! Nimebahatika kuongea kwa karibu na moja wa mhudumu ambae alikua zamu siku Marehemu Kanumba alipelekwa hapo hospitali akiwa katika gari yake mwenyewe kapelekwa na huyo mdogo wake na kijana mwingine Pamoja na Mama mwenye nyumba wake. Unaambiwa ilipo tambulika kua Kanumba was indeed dead ni ndani ya mda mfupi watu walikuja kwa wingi toka kona mbali mbali ya jiji kutaka kuja hakikisha kama kweli huku wengi wakiwa hawaamini.

Kama Marehemu kutajwa jina yaweza sababisha yeye kushindwa pumzika kwa AMANI - Basi Kanumba bado ana mda mrefu wa yeye kupumzika kwa AMANI hapa karibuni. Ingekua Marehem kafariki kwa njia hio hio kwa kupitia mkono wa Mwanamke mwingine; Kifo chake, jina lake na mijadala kuhusu tukio hilo la kusikitisha lingeanza kupoa sasa. Bahati mbaya saana kwa jinsi mambo yanavoenda ndio kwanza kama ni hadithi badi tupo stage ya Climax.... Na mwisho wake hautabiriki hata kwa wale ambao husoma hadithi zaidi ya 50 kwa mwaka. It is so complicated! For the simple reason kua Mhusika Mkuu katika hilo tukio ni the Late Kanumba na Elizabeth Michael alternatevly known as Lulu.

Utata wa muelekeo wa hii habari nzima ya kusikitisha wa Uhusika wa Lulu unakuja tokana na sababu nyiingi.... Hii yoote inatokana na mhusika kua mtoto/binti mdogo sana ki umri.... binti ambae yeye Marehemu kamuona na twaweza sema mlea toka utoto hadi kupevuka na kua binti. Lakini zaidi sababu ambazo zina nguvu sana ni yeye Lulu alizo zijenga mwenyewe katika macho ya Jamii. Kwamba yeye ni yeye, akiongea katika vyombo vya habari mara nyingi huwa kwa kejeli na kujidai... ni binti ambae katika macho ya tulio wengi twaona ni kama kashindikana. Na yeye alikua akiona ni sifa (I presume) kuandikwa na vyombo vya habari kila siku.... Ana maneno mengi ambayo yanam paint vibaya kama binti. Ingekua huyo huyo Lulu ni binti ambae katika jamii aonekana ni mpole, mstaarabu, adabu na heshima na kutokua na Kashfa; Kitendo cha Marehemu kufariki kusinge mkandamiza saana katika jamii. Jamii ingeuliza maswali kama Jamani Kanumba alikua akifanya nini na yule binti? Yule si mdogo wake? na maneno yafananayo na hayo.

Yule mtoto ana mtihani mkubwa.... Roho yaniuma. Nime observe asilimia zaidi ya 75 yanamlaumu kua ndio chanzo cha kifo cha Steven Kanumba kana kwamba kamuua... Hao watu wakisahau kua huyo binti hajawahi pewa chance ya kukua katika normal child environment based... toka mtoto kazungukwa na mastar, starehe, pesa, wanaume wenye tamaa na wale ambao wapo tayari kumpa lolote ili kuwez mpata.... Wakisahau kua ni mdogo akili haijakomaa. Kama mkubwa tu akipata anakua limbukeni sembuse yeye?

Sijui ataishi maisha gani? sijui kama ana mfadhili wa kumpleka nje akitoka tu... (amini nakwambia yule binti hawezi pita mtaani popote pale Tanzania); Na vile bado ni mdogo... hata akiachiwa huru anatakiwa uangalizi wa 24/7... Kwa maisha alozoea kuishi ya Kujiachia.... na hali atakua mfungwa hata akiachiwa huru; itakua mtihani mkubwa sana kwake kiasi kwamba aweza hata taka poteza maisha yake mwenyewe.... Hata hivo tuone upepo utavoenda.

Nawapa pole Wazazi, Ndugu/Jamaa, Wasanii wote, Wafanyakazi wake na Watanzania wote waloguswa na Kifo cha Marehem Steven Kanumba. May he Rest In Peace.

Nampa pole sana binti Elizabeth Michael kwa doa la maisha lililomkuta; ni kitu ambacho kingeweza mkuta yeyote yule. But in this it is her. Pole zake saana na I pray for her.... Nawapa pole wazazi wake na watu wake wa karibu wote ambao wameguswa na kuumizwa kwa kuhusika kwake katika tukio.

Lengo la hii thread ni kutengeneza kumbu kumbu ya Thread zote ambazo zimeguza hilo tukio La kusikitisha. Kwa wale ambao ni members hawapo, kwa wale ambao watakuja kua members, kwa wale ambao watataka kujikumbushia ama kusoama yote kuhusiana na shughuli nzima waweze pata kwa urahisi badala ya kutafuta randomly. Threads zipo nyingi sana hivo nimejaribu chukua baadhi ya Msingi. Kuna nyingine sijaziona Nitaomba fellow members wajaribu kuweka Links katika posts na nita update.

Tanzanian actor Steven Kanumba reported Dead - Courtesy of Jeryson

Steven Kanumba; Has a very touching story - Courtesy ya Pasco

Madaktari; Hiki ndicho Kilicho muua Kanumba - Courtesy ya Matola

Wabunge Halima Mdee na Easter Bulaya wamefurahi Kanumba Kufa?- Courtesy ya Kamura

TBC1 Wakata matangazo bungeni, wanarusha mazishi ya Kanumba Live - Cortesy ya Wakusoma

Kanumba frustrates JK's Travel Plans - Courtesy of Sijali

Ya Kanumba: Konzo ya Maji Haifumbatiki na mvumbika changa hula mbovu - Cortesy ya Babykailama

Maisha Kitendawili.... Wengi hufa bila kutegua - Courtesy ya The Boss

Kifo Cha Kanumba: Ni uzembe tu! Sio Lulu - Courtesy ya Pasco

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael - Courtesy ya Maseto

Africa Magharibi bado utata, wadhani Kanumba kagongwa na gari - Courtesy ya Misnomer

Speculations behind Kanumba's Death - Courtesy ya Jack Beur

Nyimbo ya Kanumba kabla hajafa ni kama amejitabiria - Cortesy of Hassbaby

Neno la mwisho la Kanumba kwa Mama - Courtesy of Independent Voter

Bungeni Leo; Martha Mlata: Kanumba alitakiwa awe na body guard - Courtesy of Dadio

Filamu ya Kifo cha Kanumba yanaswa kwa siri - Courtesy ya Gumzo

Mod tunaomba utengeneze Jukwaa la Kanumba kuepusha Duplicant - Cortesy of Matope (Lmao hapa)

Kifo cha Kanumba chazua Ushirikina- Courtesy ya Maseto

Kifo cha Kanumba: Wengi kupandishwa Kizimbani - Courtesy ya Allien

Kufa Kufaana; Wasanii Bongo Movies Waanza kuchangisha Pesa- Courtesy ya Ma2mbo

Michango ya Rambi Rambi ya Msiba wa Kanumba watafunwa - Courtesy ya Kimbunga

Kanumba; Holly wood nao walonga - Courtesy ya Alien

Steve Kanumba: Historia; Kazi zake na Mengineyo - Courtesy of Allien

"Nimezaa na Kanumba' - Courtesy of Ngoshwe

Ramli kali.. Nyuma ya pazia kifo cha Kanumba - Courtesy of Bujibuji

Umaarufu wa Kanumba unanitia mashaka - Courtesy of PETER JOHN MLEY


[Lulu Related Thread to the Death of Kanumba]

...........................




"Ujinai" wa Lulu katika "Mauaji" ya Kanumba (R.I.P)- Courtesy of Woman of Substance

Tetesi-UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka - Courtesy ya Rutashubanyuma

Je Lulu ana haki juu ya Kifo cha Kanumba? - Courtesy ya MPAMBANAJI.COM

Sakata la Lulu na Kifo cha Kanumba, What does the Law say?- Courtesy ya Majamba Jr.

Police wamuachie Lulu mara moja! - Courtesy of Rutashubanyuma

Ushauri alopewa Lulu na Lady Jaydee 2009 akiwa 14yrs - Courtesy of Independent Voter

Mh. Halima Mdee: Nitamsaidia Lulu kadri niwezavo - Courtesy of Mwitaz

Neno la Leo: Jamii ya walo wema Imsamehe Elizabeth Michael - Courtesy of Majid

Ushauri huu kwa Kanumba na Kifo chake - Courtesy of Kitalolo

The above ndio threads ambazo nimejitahidi ku compile. DISCLAIMER; Nimeweka threads tokana na uhusiano wake na the whole event. Kuweka kwangu hapa sio kwamba all details katika all threads ni valid and verified.


Pamoja Saana.

AshaDii...
 
Ashadi mie jana nimekiri kwa kinywa kuwa kweli kumbe Kanumba ametutoka na machozi kuanza kunitoka bila ajizi.sikuwa mpenzi wa movie zake ingawa siku za karibuni niliangalia Uncle JJ,Big Daddy and The Young B...
yaani hata sielewi ni nini hiki?
RIP Steven Kanumba- hakuna aliye msafi na kwa Neema ya Mungu uturehemu
I will always miss u
 
King Kong... Nilituma speacial Request kwa Mods... Hii issue bado itaendelea kufuatiliwa hadi pale hatma ya Lulu itapojulikana. Hivo niliomba for the benefit ya wale ambao hawana mda mwingi wa kupitia threads katika forums mbali mbali hivo taarifa nyingine kuwapita. Of coz it won't be a sticky forever.....

BTW Ndio yale yalee yepi hayo?

Hata mimi nilitaka kumuuliza ndiyo yale yale yepi tena?
 
I am humbled kwa acknoledgements Zoote....

@ Yummy mimi penda wewe pia, Nimefurahi kwa kunijulisha hilo.... THANK U.
 
Ashadi mie jana nimekiri kwa kinywa kuwa kweli kumbe Kanumba ametutoka na machozi kuanza kunitoka bila ajizi.sikuwa mpenzi wa movie zake ingawa siku za karibuni niliangalia Uncle JJ,Big Daddy and The Young B...
yaani hata sielewi ni nini hiki?
RIP Steven Kanumba- hakuna aliye msafi na kwa Neema ya Mungu uturehemu
I will always miss u


I know what you mean dear.... Mimi naomba nikiri toka habari zake za kifo, hadi mazishi hadi yoote yalotokea; Hakun a mahala niliweza ongea na mtu kuliongelea tukio... Nilikua msikilizaji tu! Hakuna hata post moja niliweza elezea kuhususiana na topics related to the event.... Niliona it was too depressing. Naona thou sio kwamba nilikua nampenda kivilee.... Imeniuma sana. Na more Imeniuma hatma ya Lulu.... I wish I had access to that kid kwa kumuona tu kuona yupo vipi na the way anategemea maisha yatakua..... Ananiuma mno. Wote yeye na Kanumba.

I concur.... Rest In Peace Kanumba.
 
Hata mimi nilitaka kumuuliza ndiyo yale yale yepi tena?


Losambo binadamu ni kazi saana. Tumetofautiana kufikiria.... Yeye kaona tu kua ni thread ya Kanumba bila kuangalia beyond... Kwamba imenichukua a lot of my time kutafuta hizo threads ili nisome yalonipita wakati sipo... Huku nikifanya hivo nikaona ni kazi kubwa mno ambayo sio lazima member mwingine apitie kuweza soma threads zote; hivo azikute pamoja in a single thread.... We have a long way to go....

Ngoja tumsubiri atueleweshe yale yale yepi.....
 
Losambo binadamu ni kazi saana. Tumetofautiana kufikiria.... Yeye kaona tu kua ni thread ya Kanumba bila kuangalia beyond... Kwamba imenichukua a lot of my time kutafuta hizo threads ili nisome yalonipita wakati sipo... Huku nikifanya hivo nikaona ni kazi kubwa mno ambayo sio lazima member mwingine apitie kuweza soma threads zote; hivo azikute pamoja in a single thread.... We have a long way to go....

Ngoja tumsubiri atueleweshe yale yale yepi.....

Sana aisee na kwa kuwa umeshalitambua hilo inabidi umpotezee tu. Binafsi nimependa jinsi ulivyoelezea hauko upande wowote umeelezea vizuri sana kwa pande zote mbili though watu tunajiuliza maswali mengi sana kuhusiana na huyo Lulu(ametuchanganya,hasa kwenye swala la umri.....naona ataendelea kutuchanganya zaidi tu huko mbele). Mimi sio mshabiki wa mastar wetu hapa kwanza huwa nasikia kizungu mkuti nikisia neno star.....lol ila kifo cha Kanumba kimenigusa yaani nimeona huruma inshort vifo vyote vya ghafla huwa vinanihuzunisha sana nakosa raha hata wiki nzima hata kama simfahamu muhusika. Huyo Lulu nilikua namsikia tu kwa wadada wa kazi ndio nimekuja kumuona picha zake kwenye hii habari ya Kanumba,ni kazuriii hakutakiwa kuingia kwenye hayo mambo bado mdogo sana. Nimechoka zaidi nilipoona picha kwa lady jay dee yani mbona mdogo sana kwa hayo mambo anayoyafanya?!
 
Losambo binadamu ni kazi saana. Tumetofautiana kufikiria.... Yeye kaona tu kua ni thread ya Kanumba bila kuangalia beyond... Kwamba imenichukua a lot of my time kutafuta hizo threads ili nisome yalonipita wakati sipo... Huku nikifanya hivo nikaona ni kazi kubwa mno ambayo sio lazima member mwingine apitie kuweza soma threads zote; hivo azikute pamoja in a single thread.... We have a long way to go....

Ngoja tumsubiri atueleweshe yale yale yepi.....
AshaDii nafikiri tuendelee na ishu zetu jammaa keshajistukia kuwa yuko peke yake ,unafikiri atarudi kuja kufafanua hiyo 'yale yale' yake? na akifanya hivyo nitatafuna buttons za keyboard zote nakuapia!
 
AD kwa kweli hadi sasa huyo bint anahitaji ushauri mkubwa sana na pia watu wanatakiwa waelewe na kukubaliana na yote yaliyotokea kama sehemu ya maisha.. ni kweli yule bint ananyooshewa sana vidole na hii imechangiwa sana na umaarufu wa kununu na hata ulimbukeni

lakin pia tumeona nini kinaendelea nyuma ya pazia kwenye tasnia ya filamu na nadhani sehemu zote
 
AshaDii napenda na kushukuru sana jinsi unavyojitolea kurahisiha mambo pale unapoona watu wanahangaika.
Nakumbuka ulifanya pia kwenye msiba wa Regia.
Kanumba aliniuma niliposikia amefariki,ilikua ghafla na mapema mno ila sasa nimeshakubali kuwa hayupo,nimeshaanza kumsahau Kanumba ila Lulu ndio kwa sasa ametawala mawazo yangu,japo kalikua kamapepe lakini hana tofauti na wadogo zetu wengi wa siku hizi ambao wana mambo makubwa wangali wadogo lakini kwa vile ni ndugu zetu kamwe hatuwaombei yawapate yaliyompata LULU.Picha za juzi akilia zimeniumiza sana,namuonea huruma ningekua na jinsi ninemchomoa ktk hali aliyoko sasa ila sina zaidi ya kumuombea kwa Mungu amvushe na kumpatia faraja tena.Japo upelelezi bado unaendelea lkn akili yangu inanilazimisha kuamini kuwa mtoto wa watu hana hatia.
 
Last edited by a moderator:
Nimeiona hii leo,
tena nimeanza kulia upya,
sikumjua huyu kijana,
lakini hata leo nina password moja natumia
jina lake, sijui niibadili au niiache sijui.

Asante AshaDii, kweli wewe ni msomi.
 
Kama kanumba tulimpenda na tutamkumbuka., mimi nikiwa mmoja wa watanzania ambaye niliguswa sana na uhangaikaji wake kimaisha na alipoifikisha bongo movies kiujumla., ila kwa sasa mimi naona turudi kwa kilichoachwa nyuma., Elizabeth Michael.. Wote tunajua lulu hajakua kwenye maisha ya kawaida kwani hajapitia utoto kama watoto wengine na kuenjoy utoto wake., cha pili kifo cha mtu kisizuie watu kuongea upande wa pili wa kanumba., kanumba nilimpenda sana sababu nilimuweka kwenye list ya watu wastaarabu sana ila Mnisamehe maana leo hii angekuwepo asingebakia kwenye hiyo list.. Jamani ufataki sio lazima uwe na mvi.,marehemu kanumba nimemjua kwenye ile tamthilia alioigiza kama kipofu" aliitwa dereck" na lulu alikuwa mtoto sana aliigiza kama mdogo wake anayemsaidia kumuongoza njia., sasa leo hii kanumba huyohuyo kuja kujihusisha na mtoto ambaye amemjua kabla hata haijui sidiria alipiga faulo., nilimpenda sana kanumba ila siwezi kuwa mnafki kwa kuongelea mazuri tu.. Hata mabaya ametenda na amemsababishia doa kubwa sana lulu., sometimes natamani angekuwa hai si kwa ajili ya fans peke yao bali kwa lulu ambaye anateseka
 
sidhani kama hizo bongo movies zitakuja ni-impress tena, i used to like them bcoz of this dude! RIP KANUMBA! he was great indeed! ashadii superb job!
 
Back
Top Bottom