Nini kinapelekea Single Movies kutokufanya vizuri Tanzania?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,862
Tangu Kanumba kufariki, soko la Movie moja moja hapa Tanzania limekuwa gumu sana, na waigizaji wengi sasa wamejikita kwenye vipande vya video fupi fupi za kupost instagram na YouTube, na waigizaji wakubwa wamejikita zaidi kwenye Tamthilia.

Soko la Movie Moja moja (Single Movie) kwa kweli limekuwa gumu sana hivi sasa. Na waigizaji wengi ni kama hawana maono au ndoto za kufanya vizuri nje ya mipaka ya Tanzania. Wengi wao hawajikiti kuuza movie zao nje ya mipaka ya Tanzania. Ni kama soko la nje limekuwa gumu ukilinganisha na kipindi cha Steven Kanumba ambapo tuliona Movie za Tanzania zikifanya vizuri kimauzo katika masoko ya nje ya Tanzania kupelekea kuanza kushirikisha Wanaijeria kwenye Movie za Kibongo. Lengo la Kanumba lilikuwa ni kuteka soko la Nigeria kwa kujaribu kushirikisha waigizaji kutoka Nchi hiyo. Jambo ambalo mpaka anafariki alikuwa amelifanya kwa kiwango kikubwa.

Ukitaka uteke soko la Nigeria, basi washirikishe wanaijeria kwenye kazi zako, kitu ambacho pia Diamond Platnumz amekishtukia na kimempa umaarufu huko Nigeria... Wazungu wanasema If you can't beat them, then Join Them... Kanumba na Diamond walichagua ku-join na wanaijeria ili kuteka soko la Afrika, maana Tanzania pekee aiwezi kukufikisha kidunia.

Swali langu kwa hiki kizazi kipya cha filamu: Mbona single movies hazifanyi vizuri kupelekea wengi kujikita kwenye Tamthilia. By the way shout out kwa Lamata Leah kwa kazi nzuri ya kuandaa Tamthilia na anajaribu kwenda kushuti hadi south Africa ili kuleta radha tofauti ya madhari.

Nini kinatufelisha kwenye Single Movies, wakati tuna Script writers wazuri, Video producers wazuri, Tanzania pia ni miongoni mwa nchi zenye locations kali duniani. Tunafeli wapi au ndio kanumba aliondoka na tambiko zake.


View: https://youtu.be/Qd-KPRhZLIs
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom