Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

Ahsanteni sana na karibuni nyote

habari king'amuzi changu kimekata channel zote jana leo nimejaribu kusearch upya zikaja channel za ajabuajabu na zimepungua sana yaani napata channel 13 wakati zilikua zaid ya 35 ndo mambo gani haya sasa nimechukia sana leo,mi nipo tanga.
 
Mm tatizo langu ni moja tu nataka kujua mchanganuo wa malipo ya vifurushi vyote ikiwemo SIBUKA Kwa mwezi ni sh ngapi baada ya hapo ndo nitaandika ninachotaka kueleza.
 
je ukiwa nacho cha antena unaweza badili utumie dish naona kama hiki cha antena ya ndani KINANISUMBUA SANA NO SIGNAL NYINGI sana na bei yake kweli ni hiyo inayotangazwa 48000 mbona mawakala wanauza ya zamani 139000?
 
Hongera huduma zenu nzuri kingamuzi changu kinanisumbua mwezi sasa ofisi zenu kwa dar ziko wapi nataka nikilete mkiangalie
 
Habari,
Mimi nipo kimara kilungule natumia kingamuzibcha antena ya nje tena nimeweka pole ndefu lakini honeshi chanel yeyote kwa muda mrefu pamoja na kujaribu kulipia lakini karibu inaexpire lakini nimeshindwa kuona chochote.

Nimejaribu kugeuzia antena sijui kisarawe, mara makongo lakini bado ni ziro. Na hivyo nimeamua kukitelekeza kwani ni zaidi ya kero hiki kingamuzi chenu.
 
Na je kingamuzi cha dish kwa local chanel nazo ni bure au lazima ulipie ndio uzione
 
mwanza mitambo ya startimes njooni mng'oe tu hatuna tunachofaidi ni kero tupu,habari ikifika ni inaaaaaagaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaandaaaaaaaaaaa yan had unjilaumu kununua kifurushi pmj n king'amuzi chenyewe
 
Nadhani Hii Account Ni Ya Mfanyakazi Wa Kawaida Tu, Tena Mchina!! Ndio Maana Hajibu Hoja, Maswali, Kero, Malalamiko Na Shida Za WATEJA Wao!!! Sasa Bora Waitoe Tu, Haina Tija Kwetu, Ila MTAZAME Tu Kitaa Jinsi Dish Za King'amuzi Kile ZIKIENDELEA KUSHIKA Kasi!!!!
 
IMEI zenu tukisajiri tcra hakuna kitu je simu zenu ndio mnadhihirisha kuwa ni famba sasa kiama kinakuja tcra wanakuja mtajua hii ndio tzeee ya magufuli
 
sijawahi pata simu mbovu kama hizi za p40 ukijumlisha na customer care yenu mbovu ni shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiidaaaaaaaaaaaaaaaaaah
 
Startimes king'amuzi ni bei gani jibu tafadhali nahitaji kununua.


habari yako, bei ya vingamuzi

kinachotumia dish kama unadishi sh 48,000 tu, kama hauna dish ni shilingi 88,000

kinachotumia antena, 34,000 pia kuna cha 79,000 bei inatokana na kifurushi utachounganishwa nacho awali
 
sijawahi pata simu mbovu kama hizi za p40 ukijumlisha na customer care yenu mbovu ni shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiidaaaaaaaaaaaaaaaaaah


habari yako Concious, simu zetu ni simu imara kabisa, kama inatatizo inatakiwa upeleke kituo chetu cha huduma kwa wateja utapata msaada bure, na kumbuka simu zetu zina guarantee na hata zikikusumbua inatakiwa urudishe utasaidiwa. nafikiri ni kampuni pekee tunayouza simu ukiwa na uhakika wapi unaweza pata msaada

pia kuhusu huduma kwa wateja tafadhari napenda kukujulisha startimes tumeboresha sana na vitengo vyetu vya huduma kwa wateja, kwa mfano simu yetu ya huduma kwa wateja ukipiga inapokelewa ndani ya sekunde 10. na pia watoa huduma wetu wamepatiwa mfunzo mengi ili kutoa huduma bora. ahsante
 
Back
Top Bottom