Star tv na bunge

Shagiguku

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
407
133
wadau naomba mnifahamishe hili suala, maana mimi nashindwa kuelewa, sasa sifahamu labda ni kwa sababu nashinda kazini muda wote kuanzia asubuhi hadi jioni..!! hata hivyo jioni nirudipo nyumbani huwa sioni STAR TV wakirusha matangazo yao LIVE kutoka bungeni Dodoma kama ilivyozoeleka siku zote.

SASA NAPENDA KUFAHAMISHWA HALI HII HUWA INATOKEA HATA ASUBUHI AMA NI JIONI TU...??
JE, NI SABABU GANI ZILIZOPELEKEA STAR TV KUTORUSHA LIVE MATANGAZO YAO KUTOKA MJENGONI DODOMA...!
JE, KUNA MKONO WA SERIKALI AU WA NGEREJA NA JAIRO? (YAANI star TV hawana umeme katika kituo chao...?)

Naomba kuwasilisha..................!!!!!!!!!!!
 
WAMEACHA KWA SABABU HAKUNA UMEME !!!! Diallo kaniambia business hailipi... ndo hilo tu.
 
Lakn jana wameonesha mkuu huku maeneo yetu ya Dom na walionyesha session zote mbili mkuu cjui nyie pande zenu huko wap
 
Makubwa!!!!!!!!!

Star TV ndio mambo gni hayo tena??? Ndio tuseme mmeanza KUDEKA kama TBC na kutuchagulia kitu gani tukitazame, kipi hatukistahili na lini msiwepo kabisa hewani kuhusu mambo ya Bungeni Dodoma sio???

Wewe Hamisi Dammbaya, kapeleke Mlimani TV Bungeni Dodoma mara moja Watanzania tuhitaji kurekodi kwa kila nukta mchango wa kila mbunge azungumzapo hapo mjengoni na jinsi gani atakavyokua akitetea maslahi yetu kitaifa au vinginevyo.

Rekodi hizi ni muhimu sana kwetu sisi wapiga kura kwani tutazihitaji si kipindi kirefu KUWACHUJA wale wabunge wa kurudi mjengoni kando na wale wa kurejea kushika jembe vijijini!!!!!!!!!

Dambaya na uongozi wa UDSM Mlimani TV, kazi kwenu.


WAMEACHA KWA SABABU HAKUNA UMEME !!!! Diallo kaniambia business hailipi... ndo hilo tu.
 
Back
Top Bottom