Staa wa "Movie" Kutoka India, Sanjay Dutt atua nchini Kufanya Royal Tour kuitangaza Tanzania

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Msanii maarufu duniani kwenye eneo la filamu kutoka nchini ambaye ana zaidi ya wafuasi milioni mia mbili katika mitandao yake, Sanjay Dutt leo Septemba 18, 2023 ametua kuanza Royal Tour hapa nchini.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokewa na Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt. Thereza Mugobi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Damasi Mfugale, bwana Dutt amesema ameamua kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini kufuatia Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha hazina ya utajiri wa vivutio vya utalii nchini.

"Naipenda sana Tanzania, naiona niifanye Tanzania kuwa nyumba yangu ya pili sasa baada ya kuitazama filamu ya The Royal Tour" amesisitiza Dutt

Aidha, amesema ameamua kuwa balozi wa kujitolea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mitandao yake kutokana na mapenzi yake kwa Taifa la Tanzania.

Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt Thereza Mugobi amefafanua kuwa Tanzania imefarijika kupata ugeni wa msanii huyo maarufu duniani kutoka India eneo ambalo lina idadi kubwa ya watu takribani bilioni 1.4 ambao ni soko la kimkakati la Tanzania.

"Ujio wa Dutt ni faraja kwetu kwa vile tunatambua itasaidia kuwa vuta wageni wengi kutoka bara la Asia ambako yeye anawafuasi wengi" ameongeza Dkt. Mugobi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Damasi Mfugale amesema Serikali itaendelea kuwakaribisha watu maarufu duniani ili wasaidie kufikia azma ya kufikisha wageni milioni tano ifikapo 2025 na kuliingizia Taifa dola bilioni Sita za kimarekani.

WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.14.44 (1).jpeg
 
Kweli hii nchi ya Wasanii na Usanii.....

Hivi Hamuoni hata aibu kuleta connections ambazo hazipo ?; Mnachukua Credit ambazo sio zenu na kuacha lawama amabazo ni zenu (mfano mimi kuwepo gizani sasa hivi hayo ni matokeo ya kazi ya Serikali ya Awamu hii)

Safi sana

Mithum Chakraborty wa Disco Dancer na Kasam Paida Karne Waalek hajaja?😀🐼
Hawa wala Choroko iko ongo ongo mingi sana.
Ukiacha yule aliyepiga Maaskari na bunduki zai, akapiga watu wote eneo kama la Kariakoo lakini akaja kukutwa amefia kwenye maua, kuna mwingine alipepesuka na kuanguka baada ya kupulizwa na upepo wa kope kutoka kwenye jicho lilikonyezwa na demu.
 
Hii itakuwa mara ya tatu, alishakuja 2017, 2021 na sasa tena.

Ni mtu anaependa kuwinda, huwa anakuja vitalu vya kuwinda.
Hivi ile kesi yake ya mwaka 1993 ya kuhusika kwenye ugaidi Bombay(kwa sasa Mumbai) aliachiwa achiwaje na wakati alihusika moja kuhifadhi silaha nyumbani kwake zilizotumika kwenye tukio?! Huyu gaidi isije ikawa ni mhusika mkubwa wa usafirishani wa pembe za ndovu hapa nchini, hivyo vitalu anavyowinda isije ikawa zuga tu
 
Aisee
 
Ni movie hii au real?
 
Back
Top Bottom