Je, uwekezaji unaifanya Tanzania koloni jipya la kujitakia?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Wanangu mliopo humu hamjambo?

Leo nimesoma habari kuwa Muigizaji wa kihindi Sanjay Dutt atapewa ubalozi wa heshima ili kuitangaza Tanzania India. Kilichonishangaza ni ile hali ya Dutt mwenyewe kusema kuwa amekuwa akija Tanzania kila mwaka lakini hajawahi kuwa na hamu ya kuitangaza kama walivyo magabacholi wenzake ambao hupenda kuinyonya na kuwabagua watu wake pamoja na kwamba walikuja maskini wanatoka matajiri.

Je kwa tamaa na upofu, Tanzania imeamua kujigeuza koloni la wahindi wazungu na waarabu upya? Rais alipoteza mabilioni ya shilingi akifanya kazi za waziri wa utalii kwenye Royal isiyo royal chochote tua huku Marekani. Juzi ametuletea Deep Weed kuendesha bandari zetu. Kama haitoshi, sasa tunaletewa wahindi na kuwapa ubalozi wa heshima. Je huu ubalozi hauwezi kutumika kama chambo cha kutunyonyea kama alivyofanya Chavda alipopewa vibali haramu kuishi nchini wakati hatakiwi?

Je wewe kama mwenye nchi unasemaje kuhusu huu ubalozi wa heshima wenye kutia mashaka? Wahindi na ubaguzi wao wanaweza kufanya utalii gani Tanzania zaidi ya kuja kupiga madili? Je tumekuwa wa hovyo hivi kiasi cha kushindwa kujitangaza? Nini kazi ya wizara husika kama haiwezi kitu hadi itegemee wamanga na magabacholi?

Je tumeamua, kwa hiari, kujigeuza koloni la wageni kwa sababu ya ujinga na umaskini wetu?
Naomba kuwasilisha.
---

Dar es Salaam. Serikali imeeleza sababu ya kumwandaa kuwa balozi wa heshima msanii wa filamu kutoka nchini India, Sanjay Dutt kutokana na mapenzi yake kwa nchi na kuwa na wafuasi wengi watakaoona na kusikia kuhusu fursa za utalii nchini.

Hayo yameelezwa jana Septemba 18 na Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Thereza Mugobi baada ya kumpokea msanii huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Amesema lengo la kumchagua Dutt ni kuingia kwenye soko la India yenye idadi ya zaidi ya watu 1.4 bilioni.

“Msanii huyu ni mkubwa nchini India, ukifuatilia mitandao yake ya kijamii ana wafuasi zaidi ya 200 milioni. Kwa hiyo akituma kuhusu Tanzania, fikiria kuhusu wafuasi wote hao na siyo Wahindi peke yake bali pia ni dunia nzima, hata mimi pia ni mfuasi wake. Hivyo tunaamini kwamba kituo cha Tanzania kitasikika katika soko la India na soko kubwa la Asia, ambako pia tunalenga kufikia huko,” amesema.

Maelezo hayo yameungwa mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale akisema kwa kumchagua msanii huyo watafanikiwa kupenya kwenye soko la utalii la India.

“India ina idadi ya watu 1.4 bilioni na ni soko la watu wanaopoenda utalii. Takwimu zinaonyesha kuwa kuna watu milioni 200 wanasafiri kwenda nje kweye maeneo mbalimbali, kwa hiyo tumeliona kama ni soko la kimkakati.

“Huyu kuwa balozi wetu katika kutuwakilisha kama wananchi ni fursa kubwa kwetu. Tumeweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2025 tunatakiwa tuwe tumefikisha watalii milioni tano, kwa hiyo katika kipindi cha miaka mwili mitatu ijayo tukiongeza watalii milioni 1.5 kutoka India tutakuwa tumefikisha malengo,” amesema.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), idadi ya watalii kutoka nje ya nchi waliotembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika kipindi cha Januari hadi Mei 2022 wameendelea kuongezeka hadi 458,048 ikilinganishwa na watalii 317,270 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021, ikiwa ni sawa na asilimia 44.4.

Akizungumzia ujio wake, msaanii huyo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mazingira wezeshi ya utalii na amekubali ombi la kuwa balozi wa heshima kwa kuwa anaipenda Tanzania.

“Nimekuwa nikija Tanzania kwa miaka 30 iliyopita, nakuja kila mwaka, naipenda hii nchi. Sikuwahi kuitangaza hii kwa miaka yote lakini kwa sasa nitaitangaza Tanzania sana na nitaitambulisha kwa mashabiki wangu, watu wa nchi yangu na watu wengine wote duiani,” amesema.

Amesema mbali na maeneo maarufu kwa utalii kama hifadhi ya Serengeti na Ngorongoro, anakusudia pia kutangaza maeneo mapya kama Katavi na Ruaha.

Mmoja wa wenyeji wa msanii huyo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Africab Group Tanzania, Yusuf Hatimali amesema ujio wa msanii huyo ni matokeo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ya kutangaza utalii duniani.

“Kwa hiyo matunda yote haya ni kutokana na filamu ya Royal tour, ndio tunaona msanii huyu amekuja Tanzania. Kwa kuwa ana wafuasi wengi, ataziweka utalii wetu kwenye Instagram watu wote duniani wataona, kwa hiyo atatusaidia Watanzania,” amesema.
 
Hapana, wahindi wapo 1.5B, na Tz ndio tuna export zaidi India kuliko nchi yeyote duniani, kwa hio utaona ni suala jema sana kuwa na mahusiano nao mazuri ili kuweza kuongeza biashara baina yetu,
 
Zanzibar tayari kimewaka.
Screenshot_20230919-202532.png
 
Kama wewe huzioni fursa wenzako wanaziona na kuzitumia.

Wacha roho mbaya.
Tangu wahindi waletwe na waingereza kutunyonya hizo fursa zinaonekana leo ambapo Tanzania ina serikali uza uza?

Mama UZA UZA​

Nyumbani tuna kilio, msiba umetufika,

Twahaha kupiga mbio, jawabu tunalisaka,

Tumepatwa na kilio, kilozungukwa na shaka,

Mama yetu uza uza, mbona kaacha kilio.



Jama sie wakulima, watoto wa Mlamali,

Kwa kila tunachochuma, ghalani huenda fuli,

Hata tunavyovilima, au kuhemea mbali,

Huvitunza kwenye ghala, ili vifae baadaye.



Tuna kunde na ufuta, mbaazi hata nyonyo,

Hugawana tukipata, hugawa bila uchoyo,

Sasa roho zatukuta, kwa hali tuliyo nayo,

Mama anosimamia, ameuza kila kitu.



Walikuja wachuuzi, mama walimhadaa,

Kwa mbinu zile na hizi, walimtia tamaa,

Mama kawa mpuuzi, tokana na mnanaa,

Alifanya uamuzi, vitu vyote ameuza.



Ameuza hata nazi, tena kwa pesa kichele!

Pia na kauza na mbuzi, farasira za mchele,

Aliongea kihunzi, tulipopiga kelele,

Sasa yemeshatukuta, kaka ajiinamia.



Watoto walia njaa, ghalani hamna kitu,

Watu watunyanyapaa, atusema kila mtu,

Kaka wanamkungwaa, kapoteza hata utu,

Jamani yametukuta, wenye bongo zingatia.



Jifunzeni toka kwetu, kwa yale yanotusibu,

Si kila mtu ni mtu, wengi ni sawa na dubu,

Wameuza utu wetu, bure wametusulubu,

Sisi yameshatukuta, weledi tia akili.



Walonunua wacheka, wanatuona majuha,

Wanacho walichotaka, tumeambua fedheha,

Kaya imeshaumbuka, kweli fedha ni fedheha,

Mama yetu uza uza, yupo kajiinamia.



Alikodisha na shamba, kwa bei anayojua,

Mihogo watu wachimba, siye njaa yatuua,

Viazi wanavisomba, na miti imepungua,

Sisi tumeshanyolewa, walobaki tia maji.



Baba alifua chuma, kaka kiwanda kauza,

Hata nyuzi alifuma, pia nacho ameuza,

Lile dimbwi pale nyuma, samaki wanapokuza,

Nalo pia ameuza, tunauziwa samaki!



Lile gari la mizigo, nalo kaka ameuza,

Tulionya kawa mbogo, sasa huyo ajiliza!

Amegeuka mzigo, heshima amepoteza,

Mama yetu uza uza, na yeye amejiuza.



Baba naye marehemu, katangulia kuzimu,

Twatamani kula sumu, tumfuate kuzimu,

Tumpatie salamu, kaka ametudhulumu,

Hatunao umuhimu, na maisha ni magumu.



Kidogo alichochuma, anakula na mkewe,

Tumeambua dhuluma, hatunao mfanowe,

Kwa wakweze anatuma, amridhi mkewe,

Sisi yatuua njaa, Mama yetu ni hasara.



Uskani tumempoka, tumepa mdogowe,

Yupo anahangaika, auponye uozawe,

Lini tutanusurika, japo na sisi tupoe,

Bora tumuombe Mungu, akatuvushe salama.



Enda kwa walokodisha, afanya mazungumzo,

Mrabaha kuushusha, lau tupate punguzo,

Ni wagumu si mzaha, nalo bado ni tatizo,

Yule aliyetuuza, eti sasa ajiliza!



Hayo ndiyo masahibu, yake mama uzauza,

Yake mambo ya ajabu, mwenyewe amejiuza,

Hata vipi angetubu, ameisha tuumiza,

Huo ndiyo upuuzi, wa mametu uza uza.



Ardhi tunakodishwa, aliyoiacha baba,

Bure tunalanguliwa, kisa ni akili haba,

Kama si kubinafsishwa, tungeishi kwa haiba,

Jamani tahadharini, mlo nao Uzauza.

 
Athari hasi za ukoloni wa kale zilikuwa ni kubwa mno kiakili kuliko kimwil, na zinaendelea kutuathiri hadi hivi sasa katika kizazi chetu. Wakoloni wa kale waliathiri na kuvuruga kabisa "the basis of African civilization".
Kupitia mafundisho ya dini na tamaduni zao, walifanikiwa Waafrika wajione duni sana wakiwa mbele zao.

Walifankiwa kutufanya tuamini kila kilichokuwa bora hutoka kwao, na Afrika ni bara la giza na wakazi wake hawana hadhi yoyote ile mbele yao. Hali hii imechochea Waafrika kutokujiamini, kujikana na kujiona hawawezi kufanya chochote kilichokuwa bora wala kukisimamia ili kilete tija bila ya msaada kutoka kwa wakoloni na watawala wao.

Udumavu huu ambao pia umewaathiri viongozi wetu, ndiyo hasa chanzo cha maamuzi yao tata ambayo yatakuja kuvighalimu mno vizazi vyetu vijavyo. Viongozi wetu badala ya kuwa na maono ya karne moja ama mbili zijazo, wao wanahangaika na usalama wa vyema vyao katika chaguzi zijazo, kuhangaishwa na sifa za hadaa kutoka kwa mabeberu zikiambatana na vijizawadi na rushwa zenye kufedhehesha.
 
Tangu wahindi waletwe na waingereza kutunyonya hizo fursa zinaonekana leo ambapo Tanzania ina serikali uza uza?

Mama UZA UZA​

Nyumbani tuna kilio, msiba umetufika,

Twahaha kupiga mbio, jawabu tunalisaka,

Tumepatwa na kilio, kilozungukwa na shaka,

Mama yetu uza uza, mbona kaacha kilio.



Jama sie wakulima, watoto wa Mlamali,

Kwa kila tunachochuma, ghalani huenda fuli,

Hata tunavyovilima, au kuhemea mbali,

Huvitunza kwenye ghala, ili vifae baadaye.



Tuna kunde na ufuta, mbaazi hata nyonyo,

Hugawana tukipata, hugawa bila uchoyo,

Sasa roho zatukuta, kwa hali tuliyo nayo,

Mama anosimamia, ameuza kila kitu.



Walikuja wachuuzi, mama walimhadaa,

Kwa mbinu zile na hizi, walimtia tamaa,

Mama kawa mpuuzi, tokana na mnanaa,

Alifanya uamuzi, vitu vyote ameuza.



Ameuza hata nazi, tena kwa pesa kichele!

Pia na kauza na mbuzi, farasira za mchele,

Aliongea kihunzi, tulipopiga kelele,

Sasa yemeshatukuta, kaka ajiinamia.



Watoto walia njaa, ghalani hamna kitu,

Watu watunyanyapaa, atusema kila mtu,

Kaka wanamkungwaa, kapoteza hata utu,

Jamani yametukuta, wenye bongo zingatia.



Jifunzeni toka kwetu, kwa yale yanotusibu,

Si kila mtu ni mtu, wengi ni sawa na dubu,

Wameuza utu wetu, bure wametusulubu,

Sisi yameshatukuta, weledi tia akili.



Walonunua wacheka, wanatuona majuha,

Wanacho walichotaka, tumeambua fedheha,

Kaya imeshaumbuka, kweli fedha ni fedheha,

Mama yetu uza uza, yupo kajiinamia.



Alikodisha na shamba, kwa bei anayojua,

Mihogo watu wachimba, siye njaa yatuua,

Viazi wanavisomba, na miti imepungua,

Sisi tumeshanyolewa, walobaki tia maji.



Baba alifua chuma, kaka kiwanda kauza,

Hata nyuzi alifuma, pia nacho ameuza,

Lile dimbwi pale nyuma, samaki wanapokuza,

Nalo pia ameuza, tunauziwa samaki!



Lile gari la mizigo, nalo kaka ameuza,

Tulionya kawa mbogo, sasa huyo ajiliza!

Amegeuka mzigo, heshima amepoteza,

Mama yetu uza uza, na yeye amejiuza.



Baba naye marehemu, katangulia kuzimu,

Twatamani kula sumu, tumfuate kuzimu,

Tumpatie salamu, kaka ametudhulumu,

Hatunao umuhimu, na maisha ni magumu.



Kidogo alichochuma, anakula na mkewe,

Tumeambua dhuluma, hatunao mfanowe,

Kwa wakweze anatuma, amridhi mkewe,

Sisi yatuua njaa, Mama yetu ni hasara.



Uskani tumempoka, tumepa mdogowe,

Yupo anahangaika, auponye uozawe,

Lini tutanusurika, japo na sisi tupoe,

Bora tumuombe Mungu, akatuvushe salama.



Enda kwa walokodisha, afanya mazungumzo,

Mrabaha kuushusha, lau tupate punguzo,

Ni wagumu si mzaha, nalo bado ni tatizo,

Yule aliyetuuza, eti sasa ajiliza!



Hayo ndiyo masahibu, yake mama uzauza,

Yake mambo ya ajabu, mwenyewe amejiuza,

Hata vipi angetubu, ameisha tuumiza,

Huo ndiyo upuuzi, wa mametu uza uza.



Ardhi tunakodishwa, aliyoiacha baba,

Bure tunalanguliwa, kisa ni akili haba,

Kama si kubinafsishwa, tungeishi kwa haiba,

Jamani tahadharini, mlo nao Uzauza.

Endelea tu na hizi ngonjera zako hapa JF halafu uje ulalamike unanyonywa wakati wenzako wanachapa kazi wewe unaandika ngonjera,umasikini ndio unakufanya uone kila aliyefanikiwa ni mwizi,fanya kazi wewe.
 
Endelea tu na hizi ngonjera zako hapa JF halafu uje ulalamike unanyonywa wakati wenzako wanachapa kazi wewe unaandika ngonjera,umasikini ndio unakufanya uone kila aliyefanikiwa ni mwizi,fanya kazi wewe.
Poa, it does not cost me anything except to just educate my people against gabacholis
 
Tangu wahindi waletwe na waingereza kutunyonya hizo fursa zinaonekana leo ambapo Tanzania ina serikali uza uza?

Mama UZA UZA​

Nyumbani tuna kilio, msiba umetufika,

Twahaha kupiga mbio, jawabu tunalisaka,

Tumepatwa na kilio, kilozungukwa na shaka,

Mama yetu uza uza, mbona kaacha kilio.



Jama sie wakulima, watoto wa Mlamali,

Kwa kila tunachochuma, ghalani huenda fuli,

Hata tunavyovilima, au kuhemea mbali,

Huvitunza kwenye ghala, ili vifae baadaye.



Tuna kunde na ufuta, mbaazi hata nyonyo,

Hugawana tukipata, hugawa bila uchoyo,

Sasa roho zatukuta, kwa hali tuliyo nayo,

Mama anosimamia, ameuza kila kitu.



Walikuja wachuuzi, mama walimhadaa,

Kwa mbinu zile na hizi, walimtia tamaa,

Mama kawa mpuuzi, tokana na mnanaa,

Alifanya uamuzi, vitu vyote ameuza.



Ameuza hata nazi, tena kwa pesa kichele!

Pia na kauza na mbuzi, farasira za mchele,

Aliongea kihunzi, tulipopiga kelele,

Sasa yemeshatukuta, kaka ajiinamia.



Watoto walia njaa, ghalani hamna kitu,

Watu watunyanyapaa, atusema kila mtu,

Kaka wanamkungwaa, kapoteza hata utu,

Jamani yametukuta, wenye bongo zingatia.



Jifunzeni toka kwetu, kwa yale yanotusibu,

Si kila mtu ni mtu, wengi ni sawa na dubu,

Wameuza utu wetu, bure wametusulubu,

Sisi yameshatukuta, weledi tia akili.



Walonunua wacheka, wanatuona majuha,

Wanacho walichotaka, tumeambua fedheha,

Kaya imeshaumbuka, kweli fedha ni fedheha,

Mama yetu uza uza, yupo kajiinamia.



Alikodisha na shamba, kwa bei anayojua,

Mihogo watu wachimba, siye njaa yatuua,

Viazi wanavisomba, na miti imepungua,

Sisi tumeshanyolewa, walobaki tia maji.



Baba alifua chuma, kaka kiwanda kauza,

Hata nyuzi alifuma, pia nacho ameuza,

Lile dimbwi pale nyuma, samaki wanapokuza,

Nalo pia ameuza, tunauziwa samaki!



Lile gari la mizigo, nalo kaka ameuza,

Tulionya kawa mbogo, sasa huyo ajiliza!

Amegeuka mzigo, heshima amepoteza,

Mama yetu uza uza, na yeye amejiuza.



Baba naye marehemu, katangulia kuzimu,

Twatamani kula sumu, tumfuate kuzimu,

Tumpatie salamu, kaka ametudhulumu,

Hatunao umuhimu, na maisha ni magumu.



Kidogo alichochuma, anakula na mkewe,

Tumeambua dhuluma, hatunao mfanowe,

Kwa wakweze anatuma, amridhi mkewe,

Sisi yatuua njaa, Mama yetu ni hasara.



Uskani tumempoka, tumepa mdogowe,

Yupo anahangaika, auponye uozawe,

Lini tutanusurika, japo na sisi tupoe,

Bora tumuombe Mungu, akatuvushe salama.



Enda kwa walokodisha, afanya mazungumzo,

Mrabaha kuushusha, lau tupate punguzo,

Ni wagumu si mzaha, nalo bado ni tatizo,

Yule aliyetuuza, eti sasa ajiliza!



Hayo ndiyo masahibu, yake mama uzauza,

Yake mambo ya ajabu, mwenyewe amejiuza,

Hata vipi angetubu, ameisha tuumiza,

Huo ndiyo upuuzi, wa mametu uza uza.



Ardhi tunakodishwa, aliyoiacha baba,

Bure tunalanguliwa, kisa ni akili haba,

Kama si kubinafsishwa, tungeishi kwa haiba,

Jamani tahadharini, mlo nao Uzauza.

Historia yako mbovu kupita kiasi, Muingereza kaja hapa kamkuta Muhindi yupo.

Wewe unajinyonya nafsi yako tu.
 
Poa, it does not cost me anything except to just educate my people against gabacholis
Toka usingizini usije ukawapa watu wengine kazi ya kukulea uzeeni mwako,chuki za ukabila haziwezi kukusaidia kitu,

Amini aliwafukuza Wahindi Uganda,je baada ya wahindi kuondoka, Uganda kilibadilika kitu gani? Wale wahindi walienda UK na Canada wakaendelea na biashara na life likaenda,Muhindi ni mfanyabiashara hata umpeleke wapi,

Chuki zitakuletea vidonda vya tumbo tu,tafuta fursa kamata fursa.
 
Back
Top Bottom