Spika wa bunge (Anne Makinda) akiri posho kuongezwa!

Nimekuwa nikitembelea Dodoma mara kwa mara kikazi.Bei ya Hotel / Lodges ukiachilia mbali guests ambazo sitaki kuwatajia kwa kuwa hawaoni kama ni za hadhi zao....hazizidi elfu 50 tena hizo ni zile classic kweli kweli coz kwa ile ya elf 25 tu mtu wa `kawaida` ambaye tungependa wabunge wetu wajirank nao its a paradise-like. !Mbunge kusema chini ya laki 1 hujalala Dodoma eti kwa kuwa mji unakuwa kwa ajili ya uwepo wa vyuo ni jibu rahisi kwa swali gumu.....!Sasa naanza kuelewa kwa nini huyu mama aliukomalia vile ule muswada. Napata shaka sana na tunakoelekea na aina hii ya Bunge.
 
Yani anasema sababu mojawapo ya kupandisha ni kupanda kwa gharama za malazi DODOMA,eti kuna wabunge wengine walishindwa hata kulipia hoteli,amesahau kuwa kuna wananchi huko kijijini kwake hawana hata hilo jamvi la kulalia,wanawaza kesho yake watapata wapi mlo mmoja huku yeye anaongelea malazi!!Mmmh ama kweli CHUKUA CHAKO MAPEMA!!
Nimesema ni wezi hao period!!!!
 
posho milion 6
mshahara milion 7.5
fuel allowance kila lita 2500
posho ya stationery
mfuko wa jimbo
posho ya ujumbe wa kamati za bunge mara 2 mbili
posho za ujumbe wa bodi
posho za safari za kamati
CHADEMA njoo na sera mpya za utawala wa nchi hii tuwapige chini wezi woote wa CCM Tanzania!!!!!! Majibu mbona tunayo!!!!

 
Spika hadhani kwakusema vile ameruhusu vitu vipande Mjini dodoma?
Je wanafunzi wa UDOm wakiandamana kudai nyongeza huku wakim-quote spika kuwa vitu vimepanda bei,spika atabisha?

Jana pia kwenye TBC nilimsikia akimtaja hata rais kuridhia,,je haoni anamchonganisha rais na wananchi wake?kulikua kunaulazima gani wa kumtaja rais waziwazi?
 
Makinda karuhusiwa na nani kuongeza Posho wakati Bunge lililopita haikupitishwa Agenda ya kuongeza UJIRA WA MWIHA?
 
safi sana enjoy guys sasa mtapata totoz dodoma kirahisi siunajua education center teh teh teh am hapi for u!
 
Ndio maana siku hizi wasomi wote na wanataaluma wote wanaacha taaluma zao na kukimbilia Ubunge kwani unalipa eti.

Tanzania kazi pekee yenye kulipa na kupata hishma kubwa kwa serikali ni Ubunge. Hongera sana wabunge wa Tz.
 
hivi haya malalamiko humu JF yanasaidia kweli?kuna waTz wengi hawajui haya na hata wakijua watawapongeza wabunge wao kwakuongzewa kupato..
 
Nimeshangazwa na kauli ya Spuka Anna Makinda jana wakti akibwabwaja na kutetea ongezeko la Posho za Wabunge toka Tshs.70,000/= mpaka Tshs.200,000/=kwa siku kuwa limezingatia hali NGUMU ZA MAISHA wanazokumbana nazo Wabunge wetu wanapokuwa Dodoma wakitekeleza majukumu yao!

Kauli hiyo ya Spika Makinda imepingana na Katibu wake wa Bunge Bwana Thomas Kashillilah.Kashillillah alitaka kuficha ukweli wa jambo hilo kwa madai kuwa hakukuwa na ongezeko hilo!Kauli hizi za Spika na Katibu wake zinatudhihirishia kwa kwa sasa HATUNA BUNGE. Bunge tulilo nalo ni la majuha,wajinga na wababaishaji wanaotumia utulivu na mshikamano wa Watanzania waendeleee kuwalaghai kila siku!

Inashangaza kusikia kauli ya Spika Makinda akitetea ongezeko la Posho za Vikao vya Wabunge kwamba ATI HALI NI NGUMU SANA.Hii inathibitisha kuwa Spika Makinda anafikiri kwa kutumia makalio yake! Iweje hali ngumu za Maisha zinaonekana kwa WABUNGE TU ilhali kwa WANANCHI WENGINE hali za MAISHA NI LAINI?Kwamba Tshs.70,000/= kwa siku eti ni fedha KIDOGO SANA KWA MBUNGE kwa hiyo shs.200,000/=ongezeko la Tshs.130,000/=si chochote!. Kwa maana hiyo basi Mbunge akiwa Dodoma anatakiwa apate jumla ya Tshs.330,000/=yaani Tshs.200,000/=za kikao+Tshs.80,000/=za per diem+Tshs.50,000/=za Mafuta ya Shangingi!Makinda anafahamu kabisa kuwa KIMA CHA CHINI cha Serikali ni shs.135,000=Mwalimu wa Sekondary School mwenye Degree anaanza na mshahara wa Tshs.240,000/= Kwa maana hiyo basi kipato cha Mbunge kwa siku akiwa Dodoma ni zaidi kwa Tshs.90,000/=ya Mshahara wa Mwalimu wa Sekondari, ni mara 2 na nusu ya KCC ya Mwananchi wa kawaida.

Hii inatudhihirishia tu Watanzania kwa sasa ni BUNGE la aina gani tulilonalo. Ni Bunge ambalo linajali zaidi MASLAHI YA WABUNGE kuliko maslahi ya Wananchi linalowawakilisha, Bunge la POROJO NA MIPASHO,Bunge lisilowajibika kwa Wananchi,Bunge ambalo ni RUBBER STAMP,Bunge la kubariki UFISADI NA UJINGA wote tunaoujua na tusioujua!

Shame on you Speaker Anne Makinda.
 
Inasikitisha sana. Kama Tanzania ingekuwa kama nchi nyingine huko Duniani pangechimbika. Jamani kuna walimu wanaidai serikali hadi shillingi elfu mbili lakini serikali inapiga chenga kulipa. Wabunge wa Tanzania ni binadamu zaidi kuliko wananchi wengine! Kashilila awajibike kwa kuudanganya umma wa watanzania ilhali wao ndio walipa kodi.
 
Swali muhimu la kujiuliza;

- Wabunge wana nini zaidi ya wengine kinachohalalisha wao wenyewe tu kuongezewa posho?
 
....Katika siku ambazo nimewai kujisikia hasira,huzuni,kukata tamaa na hii nchi ni leo,pale kiongozi anayekosa mshipa wa aibu na huruma kutamka hadharani kuwa wameongeza posho kwasababu ya kuwasaidia wabunge kupambana na maisha magumu wakiwa hapa Dodoma,ati kwasababu gharama za maisha zipo juu...Kiongozi huyu anatoa tamko hilo as if Dodoma ni mkoa uanokaliwa na wabunge tu kwahiyo maisha hayo magumu yanawasumbua wao tu wakati kuna watanzania wengi tunakufa kwa njaa hapa DODOMA..

....Kwasababu ya haya yote naomba kutoa rai kwa chama changu nikipendacho CHADEMA watoe tamko juu ya hili,na Je,wao wanachukua au walichukua hizi posho au la.LA SIVYO!! Kwa kweli dhambi hii kwa wananchi maskini itakuwa juu yao pia na tutapoteza imani kwa watanzania wengi...pia itakuwa ni unafiki mkubwa sana,ambao sipendelei uonekane kwetu...Akina Dada yangu mpenzi Regia,Kamanda Mnyika,Kamanda Zitto,Dr wa ukweli naomba tupate matamko yenu please...

Nawasilisha!!!

Naunga mkono hoja.

Wenzetu Zambia kuna siku serikali iliongeza bei ya MKATE kutoka Kwacha 1 mpaka kwacha 1 unusu. Nchi nzima Umma uliandamana kupinga ongezeko hilo na KWELI SERIKALI IKASIKILIZA KILIO CHA WANANCHI na bei ya mkate ikapunguzwa kurudi kwenye bei ya mwanzo ya Kwacha 1.

Tatizo la Watanzania TUNA NIDHAMU ZA WOGA NA UJINGA. Hili swala la ongezeko la POSHO ZA WABUNGE LILIKUWA LA KUANZISHIWA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA KUPINGA KWA NGUVU ZOTE MPAKA WARUDI KWENYE HIYO HIYO 70,000/= VINGINEVO WAKUBALI KUONGEZA MISHAHARA NA POSHO ZA WATUMISHI WOTE WA SERIKALI KWA VIWANGO SAWIA.

CHADEMA LIANZISHENI TUKO NYUMA YENU.
 
Kutoka Tbc!
Kupanda kwa posho za wabunge paka laki mbili...,ni kutokana na gharama za maisha kupanda ikiwemo malazi,chakula,usafiri na STAREHE...,wakati taifa likiwa na matatizo mengi ya msingi huku bajeti yetu ikiwa inategemea wahisani...!
Serikali kupitia spika wa bunge Anne Makinda..waliamua kupandisha posho za wabunge kutoka 70,000 hadi 200,000!

Jamani Is This FAIR!
 
Hili tatizo la kupinga pinga, linazidi kukomaa miongoni mwa magamba, Wabunge walisema zimeongezwa, katibu akapinga, leo Maddam speaker anakiri zimeongezwa! sasa yule Kashilila sijui anajiskiaje huko alipo, maana hatutarajii Dr. mzima kudanganya kitoto toto namna hiyo

Ningekuwa kashililla ningejiuzulu mara moja ila sitegemei yeye afanye hivyo kwani ndio walewale

 
si mchezo kweli tunapokwenda pabaya. eti wameongezewa posho kutokana na ugumu wa maisha, kwani mwannchi wa kawaida hafeel huo ugumu wa maisha?
 
Back
Top Bottom