Spika Makinda: Marufuku wabunge kuzungumzia hoja ya kupokea rushwa majimboni...

Hata enzi za mwenyekiti wa kamati ya bunge mwalimu Eliakim Simpasa pamoja na madudu yote aliyofanya lakini hakufikia kwenye upuuzi kama huu anaofanya bi.kiboroto!
Katika mikutano yetu ya M4C tutawatwanga wabunge wala rushwa wote ili katika bunge la november awaambie wananchi alitumia sheria gani au mamlaka gani kutaka kulifichia bunge aibu hii ya rushwa.
Mkuu Mwita, huyu bwana alimnyanyasa sana Mbowe 2000 - 2005. Ajabu alipopigwa chini kura za maoni CCM akataka kuja CDM. Ni ajabu Makinda kutaka kuwapangia wabunge mambo ya kuongea majmboni kwao.
 
Mkuu, umesomeka! Inafahamika kuwa uhuru lazima uwe na mipaka. uhuru usio na mipaka huwa ni wendawazimu. kuzuia wabunge wasiongelee swala hili, ni kutaka tume ifanye kazi bila kushawishiwa. Hii ni kujaribu kutaka haki itendeke. Sote tunafahamu kuwa swala hilo ni nyeti, na linagusa moja kwa moja vyama vyote, na pia hatima ya watu kisiasa. Ili haki itendeke, tukubali kutoshawishi kwa maneno mengi ya majukwaani (hasa ya m4c) ambayo kwa namna moja au nyingine, yanaweza kubadili msimamo wa tume. Hivi ubaya uko wapi?????????????? Sote tunasoma upepo, na ni kweli m4c inakubalika na jamii (hii haipingiki), hata wengine tutajiunga wakati ukifika (tunaomba msifunge milango). ila tufuate sheria, taratibu na kanuni, twende kwa upole.

Mkuu hapo kwenye red nadhani umeghafilika. Swala linagusa chama kimoja tu ambacho wabunge wamekuwa wakipewa rushwa na serikali. Sidhani kama linavigusa vyama vyetu kama tlp, sau, nra, cuf,cdm, udp, umd, dp, nk! Ni wabunge wa ccm tu!
 
Mkuu hapo kwenye red nadhani umeghafilika. Swala linagusa chama kimoja tu ambacho wabunge wamekuwa wakipewa rushwa na serikali. Sidhani kama linavigusa vyama vyetu kama tlp, sau, nra, cuf,cdm, udp, umd, dp, nk! Ni wabunge wa ccm tu!
Umesahau kama kuna mbunge ambaye hivi karibuni alisakamwa sana hapa jf kwa kumtetea bosi ambaye alichafuka. Rudisha kumbukumbu zako nyuma kidogo, utamkumbuka. hayuko chama chetu, bali yuko huko kwenu.
 
wabunge wakikatazwa kuongea basi wananchi tutatoa kauli zetu kwenye box la kura.2015 sio mbali ,hakuna marefu yasiyo na ncha.

nasikitika kwa sababu katika zuio lake hakuna kifungu cha sheria kinachokataza kimsingi kuongelea hiyo issue na hata hao wabunge wataongea tu kwa sababu wanamjua udhaifu wake na ndio maana hata ndani ya bunge huwa wanampinga waziwazi.
 
....Akihairisha kikao cha bunge leo, spika wa bunge amesema kuwa ni marufuku mbunge yoyote kuzungumzia hoja ya wabunge kupokea rushwa majimboni au nje ya bunge kwasababu hoja hiyo ipo kwenye kamati maalumu na kwa hiyo ni kuingilia kazi ya kamati hii. Ni kama ile hoja inayotumiwa sana na serikali kuwa ishu yoyote ikiwa mahakamani ni marufuku kuizungumzia nje ya mahakama.

Source: Toka Bungeni TBC1

Dead wood; kuna njia nyingi za kuelimisha umma, hii ni karne ya 21; alie tu!
 
Bora kasema mapema kuwa hatagombea ubunge mwaka 2015 manake asingepata hicho kiti tena!
 
Back
Top Bottom