Spika Makinda: Marufuku wabunge kuzungumzia hoja ya kupokea rushwa majimboni...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Akihairisha kikao cha bunge leo, spika wa bunge amesema kuwa ni marufuku mbunge yoyote kuzungumzia hoja ya wabunge kupokea rushwa majimboni au nje ya bunge kwasababu hoja hiyo ipo kwenye kamati maalumu na kwa hiyo ni kuingilia kazi ya kamati hii. Ni kama ile hoja inayotumiwa sana na serikali kuwa ishu yoyote ikiwa mahakamani ni marufuku kuizungumzia nje ya mahakama.

Source: Toka Bungeni TBC1
 
aisee baba yangu makinda huo ni udikteta utaki wabunge watufunguwe yanayotokea kuuu ni ujinga wa nyinyiemu


ngoja niagize mbege
 
kwani mbunge akiongelea suala hilo jimboni atakabiliwa na mashtaka yapi?je kuna sheria inayosupport zuio hilo la makinda?maamuzi ya makinda ni lazima yaendane na sheria za nchi na si vinginevyo.wataalamu wa katiba na sheria tusaidiane katika hili.
 
Increadible! Makinda anatumia sheria gani kuziba watu midomo? Amekuwa hodari wa kuzuia mijadala bungeni, sasa anataka watu wasiongee hata nje ya bunge? Kwa sheria ipi? I feel so angry na hii kauli ya Makinda, really angry.
 
Suala la rushwa halikwepeki, wasiposema wabunge, sisi tutaongea.
 
Increadible! Makinda anatumia sheria gani kuziba watu midomo? Amekuwa hodari wa kuzuia mijadala bungeni, sasa anataka watu wasiongee hata nje ya bunge? Kwa sheria ipi? I feel so angry na hii kauli ya Makinda, really angry.

kama sheria haibani nashauri wabunge wafunguke tu!kama kila kiongozi atafanya uongozi kwa hisia zake itakuwa ni chaos.
 
Kweli mwanamke akiwezeshwa anaweza, hiki kimama hakijijui yeye ni nani yuko wapi anatakiwa aongee vipi na nini cha kuongea. Bora liende mtajua wenyewe yeye analipwa hela yake ana shida gani
 
wabunge wakikatazwa kuongea basi wananchi tutatoa kauli zetu kwenye box la kura.2015 sio mbali ,hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
nafikiri wabunge makini wa chadema hawawezi kufungwa mdomo kirahisi namna hiyo....ukweli lazima usemwe...
 
Back
Top Bottom