Spika aikataa kambi ya Hamad na Kafulila

Hapo kwenye bold sio CUF peke yao mkuu hata CDM kuna wabunge hawaku walk out au ndio ukipenda sana hata kama ana kasoro huzioni? Mwenzenu mie napenda sana lakini ukweli nauona nauvumilia nachukua kama ni changamoto kwani vyama vina ongozwa na watu wengi kila mmoja mwenye uono wake. Unachukia lakini unasonga mbele. Kikubwa hapa nadhani tuangalie jinsi gani ya kutatua matatizo yanayotukabili Umeme, Maji, Gas, Matibabu na Elimu sidhani kama haya mambo ya kambi ya upinzani yana tija kubwa sana kwetu na isitoshe kambi yenyewe kumbe sio "rasmi" yaani kwa kiswahili fasaha haitambuliki yanini tuumize vichwa vyetu yaani sisi hatujui maana ya isiyo RASMI??????????????????????????? Kweli?????????? Siamini haki ya Mungu!!!!
Nafikiri unachanganya madesa, kuna kambi mbili zinazoongelewa moja isiyo rasmi ya kina Hamad na nyingine rasmi ya Chadema.
 
Nafikiri unachanganya madesa, kuna kambi mbili zinazoongelewa moja isiyo rasmi ya kina Hamad na nyingine rasmi ya Chadema.

Nini maana ya neno "siyo rasmi" na nini maana ya neno "rasmi" ? naomba nisaidie mkuu labda nina matatizo ya kutofahamu lugha.
 
Nini maana ya neno "siyo rasmi" na nini maana ya neno "rasmi" ? naomba nisaidie mkuu labda nina matatizo ya kutofahamu lugha.
Usitake kujifanya hujui maana ya neno rasmi, soma maelezo ya Makinda uone kambi gani inatambulika bungeni 'rasmi' na isiyotambulika 'siyo rasmi'
SPIKA wa Bunge Anna Makinda amesema ni jambo lisilowezekana kuwepo na kambi zaidi ya moja ya upinzani bungeni.

Akitoa ufafanuzi huo Dar es Salaam jana wakati wa semina ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Spika huyo alisema kambi ya upinzani inayotambuliwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge ni moja ya (Chadema) hivyo kuwa na kambi nyingine ni jambo lisilowezekana.

Alisema utaratibu wa kuwa na kambi ya upinzani ni uwepo wa asilimia 12.5 ya wabunge wa upinzani bungeni ambao kwa mujibu wa kanuni za Bunge ndio wenye uwezo wa kuunda kambi hiyo.

"Ni vizuri hivyo vyama wabunge wao wakakaa pamoja ili kuwa na kambi yenye nguvu kwa wapinzani wote… ili kuwa na kambi ya upinzani ni lazima upate asilimia 12.5 sasa CHADEMA wamefanikiwa katika hilo, kinachotakiwa ni kuridhia kwa jambo hilo," alisema Spika huyo.
Kama hutayaelewa maelezo haya utakuwa unatafuta kitu tofauti.
 
Usitake kujifanya hujui maana ya neno rasmi, soma maelezo ya Makinda uone kambi gani inatambulika bungeni 'rasmi' na isiyotambulika 'siyo rasmi'

Kama hutayaelewa maelezo haya utakuwa unatafuta kitu tofauti.

Soma hapa ili uelewe ukishindwa niambie lugha yako nikueleweshe kilugha.

Kiswahili ni kuwa mfano ukiambiwa wewe si mume rasmi wa xyz maana yake wewe ni mzamiaji jamaa anapokuwa kazini.
Ukiitwa mume rasmi basi wewe ndio unaejulikana na kutambulika kuwa mume wa xyz.

Soma maneno uliyo copy na ku paste kama kichwa cha habari unless hukujapitia u just copied and paste.

"Juzi aliyekuwa kiongozi wa Kambi ya Upinzani wakati wa Bunge la tisa Hamad Rashid (CUF) na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi), waliungana kuweka azimio la kutaka kuwepo na kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni kwa madai kuwa CHADEMA imejitenga nao"
 
Siafiki kwa sasa Chadema kuwakaribisha CUF kwenye kambi ya upinzani kwa vile CUF wamejidhihilisha ndani ya serikali kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ngumu sana kwa CUF kuwa na sauti moja na CDM linapokuja swala la kuibana serikali.

Tunatambua wazi kuwa hata ndani ya Chadema kuna watu wenye misimamo tofauti ambao wanaweza kudhibitiwa na chama refer walk out scenario sasa ukiongeza wanachama wengine ambao huwezi kuwadhibiti toka CUF ni kuongeza kansa, wanaweza kuiyumbisha Chadema katika masuala mengi ya bunge hata kupelekea kuudhoofisha uongozi wa Chadema.

Nionavyo mimi ni bora CDM iwaweke nje ya kambi waonekane wazi wanapinga hoja za Chadema kuliko kuwa ndani ya kambi wakiipinga CDM kichinichini.
 
Not worth even trying, huwezi kujaribu sumu kwa kuilamba itakumaliza. CUF wameungana na CCM Zanzibar na huku bara wanataka wawe opposition haiwezkani kisa wanataka uwaziri kivuli

Mbaya zaidi 99% ya wabunge wao wanatoka visiwani ambapo CUF+CCM = Revolutionary Government
 
Msemo wa "Umoja ni Nguvu" si wa kila mahali. Na si lazima kifkra.

CDM wana sera yao, malengo yao, mbinu zao katika dhima nzima ya siasa & dola...... kadhalika CUF wana za kwao, TLP, NCCR nk kila moja ana za kwao. Umoja unakuja tu katika dhana ya taifa na maslahi yake. Kisiasa na Kijamii hivi vyama ni muhimu vikibaki vilivyo sasa (visiungane). Labda watafute hifadhi ya muda CCM.

Kwa nini? Viongozi wengi wa vyama vya upinzani Tz ni dhaifu, wana njaa, wabinafsi na wenye upeo mdogo wa kuelewa mambo na kuona mbali. Tz was there for taking after the storms of 1995 elections (by implications a proof of the fakeness of whitepaper for multi-partiism democracy's referendum in Tz), where with no unapparent reasons the oppositions has been skirmishing and destroying from within and killing one another leaving CCM to continue looting the country.

I don't borrow weight on CCM killing these parties....they do, firstly and foremostly, contributing significantly on their own downfall. Mapindikizi ya CCM wamo lakini sio sababu ya msingi.

Wake bench, wajifunze kuwa siasa si tu madaraka na vyeo basli lengo lilpaswa kuwa ni kuwatumikia wananchi wa Tz, kulikomboa Taifa na umsakini, ujinga, maradhi na ufisadi. CCM haichukiwa kwa sababu ya jina au rangi yake bali ni kwa sababu ya sera na matendo yake maovu kwa jamii ya wananchi wa Tz.
 
Ndugu wanaJF hapa tunaelekea kuona ni kiasi gani CDM inaweza kufanya uamuzi mgumu. Nasema ivi kwa sababu Hamad Rashid alishaenda mbali na kuomba mdahalo na Mbowe,akatukana sana cdm,wakaenda bungeni wakampa kura makinda na Marando akapata kura za cdm pekee,tukio la Arusha,hamad alichekelea tu! ,leo hii Makinda kasema hawawataki wakae Ccm ndo Hamad anaomba kurudi cdm? Yeye alishaamua kuupinga upinzani lakini amekuta sheria aziruhusu ndo anaitaka cdm?? Cdm amueni kwa ueledi. Binafsi nlipenda kambi kubwa ya upinzani,lakini kwa kuwa hapa cuf wamekuja baada ya kubanwa wala si kwa kuimarisha upinzani,wataingia na hawatawapa support! Kaeni wachache muisulubu ccm kama bunge la9,bora Mbowe nawe uwafungie milango!
 
Siafiki kwa sasa Chadema kuwakaribisha CUF kwenye kambi ya upinzani kwa vile CUF wamejidhihilisha ndani ya serikali kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ngumu sana kwa CUF kuwa na sauti moja na CDM linapokuja swala la kuibana serikali.

Tunatambua wazi kuwa hata ndani ya Chadema kuna watu wenye misimamo tofauti ambao wanaweza kudhibitiwa na chama refer walk out scenario sasa ukiongeza wanachama wengine ambao huwezi kuwadhibiti toka CUF ni kuongeza kansa, wanaweza kuiyumbisha Chadema katika masuala mengi ya bunge hata kupelekea kuudhoofisha uongozi wa Chadema.

Nionavyo mimi ni bora CDM iwaweke nje ya kambi waonekane wazi wanapinga hoja za Chadema kuliko kuwa ndani ya kambi wakiipinga CDM kichinichini.

dah!yani bila kuongeza neno wala kupunguza,mchango wako unaleta dira pana sana. Waachwe cdm waendelee na maamuzi magumu,wakiongezeka cuf na yule kafulila ambaye kila siku ktk vyombo vya habari anasema anamchukia mbowe,hapa mwisho wa chadema unaandaliwa kijanja. Cuf wako 33,tlp1 nccr4 jumlisho wale10 wapinzani ndani ya cdm ,jumla 48 dhidi ya wale wa cdm minus10,hapa kambi ya upinzani haitokaa ijenge hoja ya pamoja. Nawasilisha.
 
Tujikumbushe yaliyopita ingawa si ndwele.

The Civic United Front (CUF) and the Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yesterday differed in their approaches of demanding the new Union Constitution during a debate broadcast live by ITV and Radio One.

While Mr Hamad Rashid Mohammed of CUF said the party would not boycott the 2015 General Election if the Constitution was not overhauled, Mr Freeman Mbowe of Chadema feared that taking part in the next General Election before reviewing the electoral system and the Constitution would erode the people's trust of opposition parties.
Mengine ya kuangalia ni haya....
Matokeo ya Meya wa Mwanza yatangazwa.

Wajumbe wa CDM: Madiwani 15 + wabunge 2 = 17
Wajumbe wa CCM: Madiwani 13
Wajumbe wa CUF: Madiwani 2

Matokeo:
Mgombea wa CDM amepata kura 17
Mgombea wa CCM amepata kura 15 i.e 13 za CCM + 2 za CUF why?????????????????????
 
Quinine kula TANO za ukweli.

Huo mfano wa uchaguzi meya wa Mwanza ndo umemaliza kila kitu, wanakumbusha ile habari ya: CHAKO ni CHANGU, wakati CHANGU ni....???

Asiyejua maana haambiwi maana.
 
Back
Top Bottom