Spika aikataa kambi ya Hamad na Kafulila

CUF 2005 - 2010 walikuwa na wabunge wenye kukidhi kuunda kambi ya upinzani peke yao sasa kwa mampenzi yako kwa CDM yanakutia upofu ukasema maneno usiyo yajua
Mohamed,ishu hapa sio kwamba eti cuf 2005 - 2010 walikuwa na uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bungeni wao wenyewe bila ya kushirikisha chama kingine, hoja ya msingi ni kwamba cuf ni sehemu ya utawala kwa sasa.
 
Hamad aache usanii hii nchi sasa hivi hakuna mtu mjinga,huwezi kuwa ndani ya serikali znz eti bara uwe mpinzani,huo ni uongo na unafiki

Nakuaminia mwanangu!
Labda dogo akiri zenj sio Serkali!
 
CUF na Hamad ni sawa na CCM B, hivyo wao sio wapinzani, bali ni sehemu ya serikali iliyopo madarakani! Hivyo huwezi kumwita mtu aliye serikalini kuwa mpinzani wa serikali hiyo hiyo!!!!!!!11 Mie naona NCCR-MAGEUZI na TLP ndio waungane na CDM katika kambi ya upinzani, na siyo CUF kwani hao ni wanafiki tu wataharibu tu maana ya upinzani bungeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hamad aache usanii hii nchi sasa hivi hakuna mtu mjinga,huwezi kuwa ndani ya serikali znz eti bara uwe mpinzani,huo ni uongo na unafiki

Nakuaminia mwanangu!
Labda dogo akiri zenj sio Serkali! na kama ni serkali ni sawa na ya kijiji tu!
 
Mkuu nakubaliana na wewe lakini sioni sababu ya watu kuumiza vichwa vyao eti wanajf hawajui tafsiri ya neno "kambi isiyo rasmi" ?????? Mie siamini kama hamjui labda mmetoka kuamka.

Sasa si utoe huo ufafanuzi nini maana ya "kambi isiyo rasmi" ikiwa unamaelezo tofauti na ya Mh. Makinda?????

Kuunda kitu kingine cha aina yoyote ndani ya bunge lazima kiwe supported na kanuni za bunge.
Hakuna kitu kinaitwa "kambi isiyo rasmi" kwenye kanuni za sasa kwa hiyo viongozi waliotaka kitu hicho kiwepo tena kwa maneno makali walikuwa na lao jambo.

CDM ni waelewa; endapo waona kuungana nao ni bora sasa ama kwamba hakuna tija wasiungane nao bado ni sawa tu!
Ila kama mna taarifa za kiintelijensia kuhusu huo muungano basi wekeni hapa.
 
Marytina,nakubaliana na wewe bora kuwa na watu wachache wazalendo, ila si vibaya wakawapa nafasi,wakiharibu watolewe.

Kuhusu suala la pili, Chama chenye wabunge wengi katika upinzani ndo huunda kambi ya upinzani,baada ya uchaguzi ndo hali imebadilika,miaka iliyopita CUF ndo walikuwa wengi na chini ya Uongozi wa Hamad Rashid kama mwenyekiti wa kambi ya Upinzani,CHADEMA walishirikishwa na si UDP tu kama ulivyosema,walishirikiana vizuri navyofikiri.
1995-200 CUF waliikataa CDM na NCCR wakaunda kambi na UDP kiongozi akiwa Magdalena Sakaya. 200-2005,2005-10 walilazimika kwani CUF walipungua zaidi.CUF hawajawai kuwa na idadi 12.5% ya kuunda kambi ya upinzani wenyewe kwa hiyo hawakuwapa ofa CDM bal walibanwa na katiba
 
1995-200 CUF waliikataa CDM na NCCR wakaunda kambi na UDP kiongozi akiwa Magdalena Sakaya. 200-2005,2005-10 walilazimika kwani CUF walipungua zaidi.CUF hawajawai kuwa na idadi 12.5% ya kuunda kambi ya upinzani wenyewe kwa hiyo hawakuwapa ofa CDM bal walibanwa na katiba

Great Thinker at Work
 
Itakuwa ngumu safari hii,manake huko upinzani watu sheria na kanuni wanazijua TF wanaweza mzidi experience anayojivunia......

Mi nafikiri CHADEMA wawakubali hao NCCR,TLP,CUF,wakileta ujinga kuna vifungu vinaruhusu kuwaondoa kama ilivyokuwa kwa John Cheyo,tatizo ni kuwa hivi vyama haviaminiki,watu wana hila zao za kisiasa,i can understand CHADEMA hesitation to work with this guys but it worth trying working together.
Not worth even trying, huwezi kujaribu sumu kwa kuilamba itakumaliza. CUF wameungana na CCM Zanzibar na huku bara wanataka wawe opposition haiwezkani kisa wanataka uwaziri kivuli
 
Naona Hamad Rashid ana uchu wa madaraka au tamaa na hizo pesa za kambi ya upinzani, kwani huwezi kuwa mpinzani mpaka awe kiongozi? Nashauri Chadema wasikubali kuwaingiza kwenye uongozi kambi ya upinzani, wataharibu saaana maana wengine ni mamluki wa ccm.
 
1995-200 CUF waliikataa CDM na NCCR wakaunda kambi na UDP kiongozi akiwa Magdalena Sakaya. 200-2005,2005-10 walilazimika kwani CUF walipungua zaidi.CUF hawajawai kuwa na idadi 12.5% ya kuunda kambi ya upinzani wenyewe kwa hiyo hawakuwapa ofa CDM bal walibanwa na katiba

Nilielewa kuwa kanuni ziliwabana CUF, my point is waliweza kushirikiana na kufanya mgawanyo mzuri hata wa nafasi za mawaziri vivuli. Najua nyakati zimebadilika na CUF si ile ya hapo nyuma ila bado naamini CHADEMA wanaweza fanya kazi pamoja na vyama vingine katika kambi moja ya upinzani
 
Naunga mkono kwa 100% Hamad Rashid analilia fedha za Kambi ya Upinzani na ndo mana siku ya mdahalo na Mbowe alizungumzia hilo, pale ambapo hapakuwa na chanzo xhoxhote kilicho husisha mazungumzo ya Fedha heti akajaribu kuonyesha mchanganuo wa matumizi, wkt alipokuwa mwenyekiti hakufanya hivyo, huu ni wenda wazimu, sioni haja ya kwanini wapewe nafasi, kwani CDM watajipa wkt mgumu kwanza kuwachunga km wangali pamoja nao! pili yanayo husu maendeleo yatapungua kasi, alafu who knows kwamba wkt huu ndo suicide bomber atajilipua? mi naona ni vema kuchukua tahadhari Hakuna cha CUF, hakuna cha UDP, wala NCCR wala nani, wenyewe wanaweza, na hakuna haja ya reference heti..........oooooh! walifanya vile, huuuuu walifanya hivi, sasa kama walifanya vile au hivi, wao CUF kwa wakati ule kwanza waliku wengi lakini wachache, na walihitaji kufanya wqalivyo fanya, lkn kwasasa CDM hai itaji msaada wao ALAHHH!!!!!!!!!!!
 
Kaka maana ya walk out ni nini??

Hebu taja mbunge wa CDM aliyekuwa ukumbini na hakutoka wakati JK anaanza kutoa hotuba.

Unaweza kuniambia kwanini hawakuwepo wakati wenzao wana walk out? nadhani ifike mahali watu wakubali neno "demokrasia" kwa maana pana na si kulazimishwa wengine wanavyotaka. Nawaheshimu sana watu wenye misimamo tofauti na vyama vyao kama Dr mwakyembe, Samwel Sitta, Zitto na wengine wengi. Hiyo ndio demokrasia.
 
lakini si tayari kuna kambi isiyo rasmi? kwani kambi isiyo rasmi lazima itambuliwe na bunge?? nionavyo mimi ikishatambuliwa na bunge hiyo tayari ni kambi rasmi.
 
Please Chadema ignore them. Mnakumbuka Kafulila alisema kuwa kumtambua Rais halafu usitambue Mamlaka iliyomweka madarakani in ujanja wa kisiasa ? . unaweza kuona kafulila yuko tofauti namsimamo wa CDM. Ni vizuri hivyo vyama vingine vijipange upya vyenyewe ili visiwasumbue wapiganaji wetu. Mbele kwa mbele kitaeleweka.
 
Unaweza kuniambia kwanini hawakuwepo wakati wenzao wana walk out? nadhani ifike mahali watu wakubali neno "demokrasia" kwa maana pana na si kulazimishwa wengine wanavyotaka. Nawaheshimu sana watu wenye misimamo tofauti na vyama vyao kama Dr mwakyembe, Samwel Sitta, Zitto na wengine wengi. Hiyo ndio demokrasia.

Kaka mbona unakacha swali badala yake wanijia na swali tena. MP gani wa CDM haku-walk out??
Kina Zitto hawakuwepo wakati wenzao wana walk out ndio maana nikauliza unaelewa nini maana ya Walk Out??

Taarifa zilizopatikana ni kwamba kura ilipigwa kuunga mkono ama kutokuunga mkono. Waliounga mkono hoja wakashinda, si ndio demokrasia mzee ya wengi wape na wachache unawasikiliza???
Mbona Urais alipewa JK na sio Dovutwa?? NEC walisema JK ndo alipata kura nyingi ndio maana wakampa urais.

Ila tukirudi kwenye mjadala tukubali kwamba; ni uamuzi wa CDM kuwahurumia ama kuwatosa CUF, NCCR, TLP na UDP ila kwa walivyo-behave during and after election I find them 'wanting'.
 
Back
Top Bottom