Elections 2010 SMS ya Maandamano nchi Nzima Ijumaa Imeanza

sawa kabisa maandamano yaje, ccm imemwaga mboga wananchi kuanzia ijumaa tunamwaga ugali, mbwai mbwai bwana, tumechoka ala! nasisitiza: Ni bora nife nimesimama kuliko kuendelea kuishi huku nimepiga magoti.

Du! na avatar yako inaonyesha kweli umedhamiria na unaweza... sina shaka u-miongoni mwa wasambazaji wa SMS hiyo.
 
Ibnabdillahi...elimu yako itakuwa ya Madrasati ndiyo maana most of u ur still poor, stupid and nothing. There will be no developemnt if we have such stupid people like u. Yo never reason, U never think, ispokuwa ni kubeba chochote anchosema shekhe wako au maalimu wako, that is nonsense. How dare can u vomit stupid things like these.....tunapozungumzia afya mbovu, elimu mbovu, how do we relate this with imani ya mtu? Be composed, be thinker please. Hii ni degree ya juu kabisa ya umbumbumu...............@ Acid is Banned: For ur information we all have families, lakini inapokuja kwenye suala la haki, nadhani we don't need to think about that. By the way majority of women hapa nchini wanhitaji purnishment kubwa sana, coz are the ones wanaoshabikia ujinga while at the same time wao ndio wanakabriwa na matatizo mengi sana ya nchi hii........itimke wapate akili stupid

Utoto unakusumbua.. ukikua utaelewa
 
One of the many options has to take-off. so far kuna mambo kama 3:
A,kusimamisha utangazaji matokeo.
B.Kufungua kesi mahakamani.
C. kuandamana.
which is which?...what i suggest is tht in any step tht we can choose lazima tufanye second look! kila decision ina implications zake. For me maandamano kwa muda huu tete yana possibilities za kuwa fatal, regardless of whatever the name that we may brand to it, like -maandamano ya amani, or whatever the creature!
 
dawa ni moja vijana wote nchini tuanzeni kampeni zetu mapema ili mwaka 2015 uwe wa kihistoria. kwani tukijihamasisha sote kujiandikisha kwa wingi, mijini na vijijini kwa lengo la mapinduzi ya mtanzania mabadiliko yanawezekana. na hii italeta changamoto kwa vyama na hata kizazi kijacho hakita kuwa na fikira finyu kwamba bila ccm nchi haiendi au amani itatoweka. tusipo angalia na kutokubali mabadiliko tunako kwenda ni kubaya kila kizazi kinakuja na nguvu zake kimaono. kumbuka kizazi kilicho pita kilikuwa ni kizazi cha kufuata bendera..kidumu chama chamapinduzi,hakuna mtu anaweza kukosoa wal uhuru wa kutoa kashfa, kizazi kilichopo ni kizazi kinacho elewa ila kina hofu juu ya amani na mambo ya kufukirika, kizazi kinacho kuja ni kizazi kinacho elewa na kisicho ogopa, mfano maudhi yanayo fanywa na tume ya uchaguzi mambo haya yakiendele yaani itakuwa ama zangu ama zako. kama hatuta jiandaa kwa hilo tuelewe ni wazi kunamachafuko mbeleni
 
Decision sahihi
Ni kuchanganua mambo na jinsi ilivyo na mrudi kwa wapiga kura mkiwashukuru lakini mmedhulumiwa. Mnachotakiwa kuelewa Mwal NYERERE hayupo tena pale kamebaki kakikundi kaodog sana ambako hakatafika salama 2015. Naamini hata ambition za Lowasa zimekufa rasimi jumapili.

Mnachoshindwa kutambua ni kuwa tupo ktk bara la GIZA. mkianza kuandamana wale jamaa ndo wanafurahia kuuwa siyo kwamba mtamshitua kwa watu kufa.

Kama huamini tuko bara la kiza na soln mnayotaka kufanya sio WORKABLE, angalia kenya wamechomana sana moto uchaguzi uliopita, lakini nakuhakikishia uchaguzi unaokuja watachakachua tena na KUVIUTU ama KIMAKAME.
 
Hii ni sisiemu tu inataka kuonesha kuwa wapinzani wanafujo ni yaleyale tu waloyafanya wakati wa kampeni!
 
thanks acid and ruta for great posts! Jamani nchi hii ni yetu. Let us try our best to get our right while avoiding all means of bloodshed. Hapa tukianza kupigana, wezi wa mali zetu watatuuzia silaha na kujimilikisha rasilmali zetu kama Kongo. So please, calm down and let us look for coup de peace than coup de tat
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals

- Ujumbe mzito sana huu ndugu na ubarikiwe sana!

William.
 
Mch is speechless! Mungu Usiache hili taifa kwenye fisi washioshiba CCM
 
count me in, hakuna mabadiliko yasiyo na garama, twendeni barabarani na hao wanaoogopa ni wanafiki maana unafuu wa maisha unapokuja hawajitoi wakasema sisi hatukuandamana. Moto mbele kwa mbele hakuna kuuzima, tumekataa kuchaguliwa watu na wakina RA washibe watoto wa wakina JK wetu sisi tunaishia vyandarua vyenye dawa wakati chakula cha kuwapa hatuna.
 
Acid usitupoteze,Njowepo uko sawa.msg inasema maandamano ya amani hakieleweki nini.Hizi dhuluma zote zinatokea kisa ubinafsi,hata huyo aliyechakachua ndio mawazo ya umimi oooh nina watoto,nyoko zako nani siye mtu nani hana watoto nani hahitajiki duniani ila siku ya mafaniko nyie ndo mtakuwa wa kwanza mara oh nlifanya hivi.Slaa angekuwa hivyo hata leo hii mada isingekuwepo labda tungeongelea kupaka hina apa.Nafikiri kabla ya kufikiria kuielimisha jamii inabidi humu humu JF kuna watu wanahitaji elimu sana.
 
Mimi naunga mkono hoja. Niliwahi kuandika humu kuwa ccm kamwe haiwezi kutoka kwa sanduku la kura, sasa leo tumeyaona. Katika mapinduzi yoyote duniani ni lazima pawe na watu brave wa ku-sacrifice hata ikibidi maisha yao. Tuandamane kwa amani, kuiambia dunia kuwa tumeibiwa kura, sasa wakileta mabomu yao watakuwa wamejitakia wenyewe.

Lakini kabla ya yote tungependa kusikia kauli thabiti ya Chadema kuwa wameyakataa matokeo kwa uthibitisho wa uchakachuaji, kisha makamanda tuingie barabarani. Dr Slaa ndiye raisi wetu, tumechoka kuonewa, tumechoka kunyanyaswa sasa tunasema basi.

Yah hii ni point tuone kwanza ushahidi wa hayo matokeo yaliyo chakachuliwa. kama ni kweli tuyaorodheshe majina ya wahusika tuandamane kuelekea majumbani kwao tuhamie huko mpaka kieleweke sio kuharibu mali za raia wasio na hatia mitaani wakati wachakachuaji wanapeta. Hapo ndipo mtatenda haki vinginevyo tutakaoumia ni walalahoi katika jina la kutafuta haki.
 
mkuu nielewe kidogo tu

1995 - hatukua hata na avenue za kujua kieneleacho, nakumbuka ya mrema na dar, tulirudia uchaguzi wote mkoa huu wa dar
2000 - tulianza kugundua hayo lakini sauti haikua kubwa
2005 - walicheza mapema na kila kitu kikawa offside
2010 - tunayajua haya kwani hata walio ndani ya CCM hawapendezwi
2015 - kila sehemu itakua imefikiwa, lazima ukubali coverage ya chadema haikuzidi 50% na hata huko ukerewe waliposhinda ni nguvu ya upepo wa mwanza na hulka ya watani zangu

upepo huu ni mkubwa sana na hauzimiki tena, CCM wanajua na utasiki 2012 watavyosambaratika... na ili kutumia opportunity hiyo basi cha maana ni kutulia

kumbuka ukiandamana wewe, wataokufa ni wanawake na watoto, na wana haki ya kuishi

siungi mkono jitihada zote za kuvunja amani kwani naamini with or without siasa tanzania ipo

salute mkuu
 
Acheni Uzembe na Uoga mwadhani Uhuru wa nchi hii ulikuja hivi hivi tu watu walijitoa mhanga na wengine walipotea Sasa usiwape watu uoga wakiwa wanatafuta Haki yao Kila mwaka whapa tunapumzika one day kukumbuka mashujaa wetu Tushachoka kwani hata mimi nataka niwe shujaa huu utawala wa kijeshi tushauchoka ndani mwa raia kuna makanali, luteni . makaptain na vyeo vingi tu kuanzia presidar sijui ni luteni kanali kivyake Tunataka hakiiiiiiiiiiiiiiii
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals

Japo sielewi hiyo message imetoka wapi lakini ni haki yao wananchi kuelezea hisia zao. Kama inavyosema ni maandamano ya amani na wala si ya vurugu. Ili kulinda amani, polisi wanatakiwa kuwalinda wanaoandamana na kuahakikisha amani inadumu. Kuzuia wasiandamane ni jambo lingine baada ya hili la Makame na CCM la kuvuruga demokrasia.
Na kiuhalisia ni kwamba ukiwaruhusu waandamane munkari wao utaisha polepole, lakini ukiwakataza wasiandamane unazidi kuwajengea saikolojia kwamba wananyasisika katika nchi yao. Na hilo ndilo litaleta fujo na vurugu.
 
NON-VIOLENCE PROTESTS FRIDAY!!!!!

Ndugu zangu watanzania, tangu uhuru, ni karibia miaka 50 sasa imepita. Hali ya mtanzania wa leo na yule wa mwaka 60 ni mbaya zaidi. Masikini anazidi kudidimia kwenye umasikini, na matajiri, masultani na wenye madaraka wanaishi kama wafalme.

Tutazidi kuishi kama watumwa kwenye nchi yetu hadi lini?
Tutazidi kuwatumikia watu, hadi lini?
Tutazidi kuishi kwenye ufukara hadi lini?
Tutazidi kuvumilia unyanyasaji hadi?
Tutazidi kunyimwa haki zetu za msingi hadi lini?
Tutazidi kuwaonga wenye nguvu ili kupata haki kwenye mahakama zetu hadi lini?
Tutazidi kuonewa na watu wenye uchu wa madaraka na ulafi usio na kikomo hadi hadi lini?

Ukombozi wa nchi ni lazima iletwe watu wenyewe,na gharama hiyo muda mwingine inakuwa na maisha yetu. Utulivu na amani tunayoidumisha imekuwa ni kama sababu ya wenye madaraka kutunyanyasa ni lazima tujitoe mhanga leo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Nipo tayari kufa leo ili mtoto wangu apate maisha mazuri hapo baadae.Hatuwezi kuwaachia wachache watuamulie tunavyoishi tunavoishi.

Tumechoka na Kikwete, Tumechoka na Makamba, na viongozi wengine walio madarakani. Huu ndio muda wa mabadiliko. Fedha nyingi zimechotwa kwenye hazina ambazo zingewawezesha watoto wetu kusoma bure, lakini wezi hadi leo wapo huru. Baadhi ya vijana walioiba kuku wapo jela kesi zao wala hazijaguswa, mafisadi wapo huru na wanazidi kutumia hela zetu za kodi.

Tumechoka!

Wanamagari ya kurusha maji ya kuwasha,
Wana maaskari wenye bunduki wanaolipwa na kodi zetu,
Wana walinzi wao wanaowalinda tusiwafikie, haina shida.
Lakini sisi tuna mikono mitupu na matawi yanayoashiria amani.
Watuue, dunia yote itashuudia. Lazima tuandamane kudai haki yetu ya kuwachagua tunaowapenda. Uhuru tulishaupata lakini wachache wanatunyang'anya

Ikiwa kudai haki yetu itaitwa uchochezi, basi iwe ni uchochezi, lakini hatuwezi kulazimishwa kuwakubali watu ambao hatukuwachague watuongoze. Kikwete, na mwanae Ridhiwani wanatuona kama wapumbavu. Makamba na familia yake wanaitumia nchi yetu kama shamba lao. Kwa nini tusilalamike?

Huu ndio mda wa ukombozi, lazima vita vya amani vianze. Maandamano ni haki yetu ya msingi, hatutumii silaa ya aina yoyote zaidi ya kuandamana. Watanzania wenzangu, tunaanza maandamano ijumaa kwa wiki moja, ni lazima matokeo yabatilishwe au kura zihesabiwe upya ili wale tuliowachagua watuongoze.

Ikiwa mtu atapoteza maisha yake, genge zima la majambazi, NEC (Jaji makame na kundi lake) Familia ya Kikwete, Makongoro Mahanga na wengine wengi wawajibishwe na kama itawezekana wafikishwe katika makama ya kimataifa. Wao ndio chanzo cha matatizo yote, wamtuchokoza. Bila kuiba kura zetu tusingefikiria kuandamana.Hii itakuwa fundisho, kwa kizazi hiki na vijavyo kwamba anayekubali, kuonewa atazidi kuishi kwenye umasikini na ukiwa

Tupo tayari kupigania kile tunachoamini ni chetu; Haki yetu!!!
Mungu awabarikini wote
 
- Ujumbe mzito sana huu ndugu na ubarikiwe sana!

William.

William, yaani mimi sina hata kukujibu, kwa maana una matatizo makubwa sana. Mzee wako kafulia kisiasa, na kwa vile unalo jina lake, kaburi la kisiasa ni moaja. habari ndo hiyo, siye wana mageuzi ndio tunaanza
 
Back
Top Bottom