Elections 2010 SMS ya Maandamano nchi Nzima Ijumaa Imeanza

Isije kuwa tunashawishiwa kuandamana kwa sababu tu mgombea wa aliyetuma post hapa kaangakuka.
 
SIUNGI MKONO KWASABABU NIKIKATIKA MGUU HAKUNA HATA MMOJA ATAKAYE NISAIDIA KUUGUZA,, NA POLISI NI WA CCM KWAHIYO KWA UHAKIKA SANA WOOTE WATAUNGANA NA CCM KUSEMA KUWA SISI TULIO ANDAMANA TUMEHARIBU AMANI YA NCHI

AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YAKOOOOOOOOOO:doh:
 
mbona dhuluma hii haiwekwi wazi wote tukaelewa kama tuhuma za kuchakachua ni za kweli? Dr Slaa alitaka kupata kura ngapi?
 
Je watanzania ni mbumbumbu kiasi kwamba Dr Slaa akijieleza kwa mdomo hatutamuelewa hadi kuandamana? Je, Dr Slaa akitoa kauli ya kuibiwa kura inatosha kuandamana bila na sisi kufanya uchunguzi binafsi? Tuwe na subira tupate maelezo ya kutosha kutoka kwa wanasiasa wenyewe kabla ya kukimbilia barabarani. Kesho Ijumaa ni mapema sana kuandamana tunahitaji tafakari pana ambayo kila wananchi ataunga mkono badala ya kukurupuka.
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals

kesho yaweza kua miaka mia, sawa tu na kutoona maana utakua tayari haupo.
 
Kushindwa katika siasa ni jambo la kawaida na kutoa tamko umeibiwa kura ni jambo jingine lakini zaidi kuthibitisha kwamba kweli umeibiwa ni jambo pana zaidi.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Jamani tunahitaji kufikiria iwe maandamano ya salama au laa, maandamano ni maandamano hakuna jambo jema litatokea zaidi ya vurugu na kumwaga damu. Tumeishi kitulivu sana na nchi nyingi jirani zainaonea wivu nchi yetu tanzania. Tumetoka mbali na tunakokwenda mbali, napenda maisha yangu na ningependa mtoto wangu aje aishi kama nilivyoishi mimi kwa amani. Nchi ikianza vurugu haitarudia tena kua ya amani, nawaombeni ndugu zangu watanzania tuondokane na hizi siasa kali.
 
sawa kabisa mjomba, nakuunga mkono mia kwa mia ,ya nini tumwage damu eti kisa Slaa lazima aingie ikulu!!! kasoro za hapa na pale zisitufanye watanzania tuvunje rekodi yetu ya uungwana,ustaarabu,utulivu na amani.Nakumbuka huyo padre alishasema hataki kuingia ikulu damu ikimwagika sasa je ana uhakika gani maandamano hayo yataisha salama bila kumwaga damu? kama kweli anaipenda nchi hii, na ni mstaarabu kama anavyodai naomba akemee au akomeshe njama hizi za maandamano ajipange kwa kukinadi chama chake tayari kwa 2015 ,. asiyekubali kushindwa sio mshindani..
 
Kuna SMS ya maandamano nchi nzima kuanzia ijumaa amabyao inasambaa kwa kasi mno. Ujumbe wenyewe unasema "Tumeujumiwa miaka 45 imetosha. Kuanzia ijumaa ni maadandamano ya amani nchi nzima" Nawaunga mkono waandamanaji kwa maana ni haki yao ya msingi kuandamana, kwani kikwete na makamba wamezidi kuvuruga amani yetu. Tumefika mwisho wa uvumilivu na serikali yake ya kidhalimu na kiusultani

Kwa maana hiyo, ikiwa damu itamwagika, basi tume ya uchaguzi, Kikwete, Makamba na wengio wabebe mzigo. Wao ndio wanaoanza kuivuruga amani yetu na utulivu wetu kwa kuivamia haki yetu ya msingi. Kupiga kura.

Mimi sijaipata, nikiipata, nitakuwa mmoja wao. Na damu haiwezi kumwagika maana ni Maandamano ya amani. Damu yetu itamwagwa na CCM
 
sawa kabisa mjomba, nakuunga mkono mia kwa mia ,ya nini tumwage damu eti kisa Slaa lazima aingie ikulu!!! kasoro za hapa na pale zisitufanye watanzania tuvunje rekodi yetu ya uungwana,ustaarabu,utulivu na amani.Nakumbuka huyo padre alishasema hataki kuingia ikulu damu ikimwagika sasa je ana uhakika gani maandamano hayo yataisha salama bila kumwaga damu? kama kweli anaipenda nchi hii, na ni mstaarabu kama anavyodai naomba akemee au akomeshe njama hizi za maandamano ajipange kwa kukinadi chama chake tayari kwa 2015 ,. asiyekubali kushindwa sio mshindani..

Ninaamini (Slaa) anaipenda nchi yake. Asiyeipenda ni JK, Makamba, Kinana na NEC ambao wanachezea masanduku ya kura. Kinachotakiwa, kura zikiishapigwa, kura zihesabiwe na matokeo kutangazwa mara moja. Mambo ya kuchakachua, siyo mazuri na hayawezi kuleta amani na utulivu kwa kuchakachua.

Mpaka Zanzibar imefikia hatua tunayoona leo ni baada ya Seif kumtamkia Rais wa zanzibar kuwa hamtambui kwa zaidi ya miezi 36. Kwa sababu hiyo hata huku bara JK anatikisa kibiliti aone kama watz wanamsimamo na kura zao walizopiga. Bahati nzuri hata wawakirishi wa EU wameona kuwa kulikuwa udanganyifu!!
 
Vibaya kufanya fujo, sisi tunatoa hisa zetu tu kuwa mambo yameenda kombo. mbona wenzetu maandamano kila siku na hakuna shida? tatizo polisi kutaka kuzuia watu kutoa feeling zao. mbaya kuumia moyoni.
 
Kwa hiyo mnataka muandamane Slaa apewe urais hata kama hakushinda sio,acheni upuuzi,angalieni majirani zetu Kenya watu wamekufa Kibaki na Raila wanakula mikuku tu,tusijifanye sisi wazalendo zaidi!
 
Siungi mkono wazo hilo. Damu ya watanzania inaweza kumwagika. Lajufanya Wabunge wetu washinikize iundwe tume huru vyama vyote viwakilishwe 2015 ufanyike uchaguzi wa Haki vinginevyo si rahisi kuishinda dola
 
Safi saana..wamemwaga mboga sisi tunamwaga ugali,mi bado sijaipata hiyo sms
 
Siungi mkono wazo hilo. Damu ya watanzania inaweza kumwagika. Lajufanya Wabunge wetu washinikize iundwe tume huru vyama vyote viwakilishwe 2015 ufanyike uchaguzi wa Haki vinginevyo si rahisi kuishinda dola

nakuunga mkono mdau,damu imwagike unafanya mchezo nini!
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals
wacha uoga wewe hawa jamaa watazoea na 2015 wataiba tena na utasema tusubiri tena miaka mitano na baada ya hiyo mitano wataiba tena na tusubiri miaka mitano....linear proggression with a common difference 5 years kama ulisoma hesabu lakini, wakati wa ukombozi ni sasa na ni maandamano ya amani na si vita inabidi tuwaonyesha sasa kuwa hatujaridhika na huu wizi. Naunga mkono hoja 100%.
 
Am learning to hate Politics!!!

Kama hali ndio hii!! Tanzania will be ruled by CCM forever.

Wana JF na wanapapinduzi mliopo. naombeni mnisamehe Bure.

Naomba niage rasmi kwenye Jukwaa la Uchaguzi 2010.
 
Back
Top Bottom