Siungi Mkono hoja ya Zitto

Fikra za mwanadamu zinapotawaliwa na hulka ya ushabiki zaidi ya ukweli ,maamuzi hutolewa pasipo kuzingatia ukweli.Pia maamuzi hayo huambatana na hoja nyepesi zisizo na manufaa katika utatuzi wa tatizo kuu.

Serikali ya Jk tokea imeingia madarakani awamu ya kwanza imegubikwa na vitendo vya rushwa na Ufisadi uliokithiri kupita kiasi.Hii ni kutokana na ukweli kwamba Jk kama Raisi hakuwa na uwezo wa kuongoza nchi. Kongozi yeyote asiye na uwezo wa uongozi ni dhahiri hata team/wasaidizi wake watakuwa ni wabovu.Jk amejaza washkaji zake kwenye nafasi mbalimbali kama wasaidizi wake.Hili limejirudia hata pale bunge lilipomuazibu kwa kumwondoa waziri mkuu EL ili achague team bora bado yamejirudia yale yale.

Kwa nini siungi mkono hoja ya Mh. Zitto?
Sababu nilizotoa hapo kwenye maelezo ni kuwa tatizo kwenye uongozi wa nchi yetu sio mawaziri ama waziri mkuu bali ni mfumo mzima wa uongozi wa Jk.Hapa kilichotakiwa ni kutibu ugonjwa kama sio chanjo/kinga kwa kumwadabisha JK .Kwanini Zitto amekimbilia hoja ya kumwondoa Pinda ili hali kulikuwa na nafasi ya kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na Raisi?.

Hapo ndio pale wachambuzi wanapochimba zaidi na kuangalia kwa undani juu ya tuhuma za uswahiba wa Zitto na JK.Hii hoja kwa mtazamo wangu ni kupoteza mantiki ya hoja ya msingi iliyotaka kupelekwa bungeni ya kutaka kumng'oa JK.

Mungu Ibariki Tanzania dhidi ya huu uwizi wa dhahiri dhidi ya mali za walalahoi.
Mnufaikaji wa wizi wa hela za serikali atakuwa mtu wa ajabu sana akiunga mkno hoja ya Zitto, Lakini wote ambao tumeibiwa tunamuunga mkono Zitto na kumsaidia kupata sahihi za kutosha alianzishe na tutapiga kampeni zipatikane kura za kutosha kutokuwa na imani. Hii ni hatua muhimu sana kuondoa udhalimu na wizi wa mchana
 
Zitto kathubutu kaweza na kajaribu nadhani tumpe credit kwa kuonyesha WaTz kwamba inawezekana, cha kumulika sasa ni kuona reaction ya wanafiki kutoka CCM kwamba zile kelele walizopiga jana na leo ni kweli wanauchungu na wapiga kura wao?au ndio tia tia maji liende?

check hii kutoka kwenye katiba.....

53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na
Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na
ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;


Hivi mawaziri wanawajibika kwa waziri mkuu au kwa rais?
 
Tusubiri tuone mazingaumbwe.

Yawezekana lisifanikiwe kama unavyoomba, lkn majority will never alter the fact. Kutokutosha kwa kura za kumkosea imani PM ni zao la unafiki wa watu fulani lkn hata wao ndani ya mioyo yao wanajua kuwa anastahili kutoka. Pinda ni legelege, bora mwizi Lowassa kuliko Pinda anayemwogopa Jairo. Mbona Nyoni alisimamishwa na Pinda huyo huyo kama sio ulegelege tu unamsumbua.

Kwanza kwa taarifa yako, hakuna jambo litakalomnyoosha JK kama kumtoa Pinda kwa kura
 
SinaJina1 hajagundua hilo ni rahisi kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM kuliko uraisi kutokana na ukweli baadhi ya wabunge wengi wa CCM wanajua hii ndiyo awamu yao ya mwisho kwenda bungeni kutokana na kutoendana na kasi ya mageuzi.

Hapo nimekusoma Kamanda
 
Mimi pia nilijiuliza hilo but kwa kuwa sheria ndivyo isemavyo nadhani hakuna jinsi BUT swali langu, kama Waziri Mkuu anawajibishwa na wabunge kwa kushindwa kumshawishi au kumshauri Rais juu ya maamuzi muhimu, hata akiondolewa/akijiuzulu akawekwa mwingine what if issues zinazohusika ni zile zinazomkwaza Rais au what if Rais hashauriki, watawajibishwa mawaziri wakuu wangapi??

Nakubaliana na sheria but ingerekebishwa kidogo kwa Rais kupunguziwa madaraka aliyonayo. Iwekwe kuwa pale ambapo Rais anastahili kumuwajibisha waziri flani basi BUNGE nalo liwe na mamlaka flani katika kushinikiza hilo ili Rais naye ajue kuwa yeye si mwenye madaraka ya mwisho na kama itatokea atashindwa na nguvu ya BUNGE juu ya jambo flani basi akubali kutekeleza. Mf. Kumwajibisha Pinda kwa kushindwa kumshauri Rais au kumshawishi Mkuu kumfukuza kazi Mkulo (ambaye tuseme kwa mfano ni swahiba au Mkwe wa Rais) ni kama kumwonea kwa kuwa hata Waziri Mkuu ajaye akileta same allegations za Mkulo kwa Rais (Swahiba au Mkwe wake) bado reaction zitakuwa the same.............sasa tutavote no confidence kwa Mawaziri wakuu wangapi?

Mwajibisheni Pinda kwa mujibu wa Sheria but hata madaraka ya Rais katika maamuzi pia yapunguzwe
 
Back
Top Bottom