Siungi Mkono hoja ya Zitto

Zitto kathubutu kaweza na kajaribu nadhani tumpe credit kwa kuonyesha WaTz kwamba inawezekana, cha kumulika sasa ni kuona reaction ya wanafiki kutoka CCM kwamba zile kelele walizopiga jana na leo ni kweli wanauchungu na wapiga kura wao?au ndio tia tia maji liende?
 
Hapo hakuna cha uswahiba huyo janki anajua analolifanya kwani katiba ya sasa inampa rais madaraka makubwa mno,wabunge wa ccm hawako tayari wanahofia madaraka yao,hv rais akivunja bunge na akajiuzulu na uchaguzi ukaitishwa upya sasa hv wabunge wangapi wa ccm watarudi mjengoni?

labda Filikunjombe peke yake tu.
 
Fikra za mwanadamu zinapotawaliwa na hulka ya ushabiki zaidi ya ukweli ,maamuzi hutolewa pasipo kuzingatia ukweli.Pia maamuzi hayo huambatana na hoja nyepesi zisizo na manufaa katika utatuzi wa tatizo kuu.

Serikali ya Jk tokea imeingia madarakani awamu ya kwanza imegubikwa na vitendo vya rushwa na Ufisadi uliokithiri kupita kiasi.Hii ni kutokana na ukweli kwamba Jk kama Raisi hakuwa na uwezo wa kuongoza nchi. Kongozi yeyote asiye na uwezo wa uongozi ni dhahiri hata team/wasaidizi wake watakuwa ni wabovu.Jk amejaza washkaji zake kwenye nafasi mbalimbali kama wasaidizi wake.Hili limejirudia hata pale bunge lilipomuazibu kwa kumwondoa waziri mkuu EL ili achague team bora bado yamejirudia yale yale.

Kwa nini siungi mkono hoja ya Mh. Zitto?
Sababu nilizotoa hapo kwenye maelezo ni kuwa tatizo kwenye uongozi wa nchi yetu sio mawaziri ama waziri mkuu bali ni mfumo mzima wa uongozi wa Jk.Hapa kilichotakiwa ni kutibu ugonjwa kama sio chanjo/kinga kwa kumwadabisha JK .Kwanini Zitto amekimbilia hoja ya kumwondoa Pinda ili hali kulikuwa na nafasi ya kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na Raisi?.

Hapo ndio pale wachambuzi wanapochimba zaidi na kuangalia kwa undani juu ya tuhuma za uswahiba wa Zitto na JK.Hii hoja kwa mtazamo wangu ni kupoteza mantiki ya hoja ya msingi iliyotaka kupelekwa bungeni ya kutaka kumng'oa JK.

Mungu Ibariki Tanzania dhidi ya huu uwizi wa dhahiri dhidi ya mali za walalahoi.
Japo umenena ukweli ila acha Zitto ajaribu kwanza, kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha.
 
zitto kathubutu kaweza na kajaribu nadhani tumpe credit kwa kuonyesha watz kwamba inawezekana, cha kumulika sasa ni kuona reaction ya wanafiki kutoka ccm kwamba zile kelele walizopiga jana na leo ni kweli wanauchungu na wapiga kura wao?au ndio tia tia maji liende?
hapo umenena kiongozi na mtihani mgumu sana kwa wabunge wa ccm labda kama kuna waliotayari kujivua gamba.nasubiri ripoti ya nishati+na ya lowasa-'ulinzi'
 
Tuko bungeni wewe unatupeleka ikulu hazimo wewe.

Hapana Paxman siyo hivyo huyu bwana anamaanisha kwaamba njia anayotaka kuitumia Zitto ni njia sahihi lakini ni ndefu kama vile kumuua nyoka kwa kumpiga mkia yeye anataka kumwangamiza nyoka kwa kupiga kichwa.
 
Hapo hakuna cha uswahiba huyo janki anajua analolifanya kwani katiba ya sasa inampa rais madaraka makubwa mno,wabunge wa ccm hawako tayari wanahofia madaraka yao,hv rais akivunja bunge na akajiuzulu na uchaguzi ukaitishwa upya sasa hv wabunge wangapi wa ccm watarudi mjengoni?

SinaJina1 hajagundua hilo ni rahisi kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM kuliko uraisi kutokana na ukweli baadhi ya wabunge wengi wa CCM wanajua hii ndiyo awamu yao ya mwisho kwenda bungeni kutokana na kutoendana na kasi ya mageuzi.
 
Kikwete ni janga la taifa hana tofauti na umaskini ujinga na maradi. Fikiria soda imefika pesa ngapi kwa sasa? Sukari je? Sementi nayo? Bei ya umeme mafuta navyo? Vyoo vya kulipia mijini haja ndogo tsh 500/= haja kubwa tsh 1000/= VAT katika inchi zote za afrika mashariki Tanzania 18% kenya 16% uganda 15% rwanda 10% burundi 12% ongeza mazao maliasili,na kodi kubwa wanazotutoza tra zinalipwa na wenye moyo na kuliwa na wenxe meno.
 
Haya mkuu kwa hiyo kama mfumo ni mbovu tusubiri mfumo mpya uletwe na nani? Anyway katiba mpya na je tuwaache waendelee kula hadi mfumo mpya? THINK BIG MKUU!

Mbona mtoa mada kaeleza wazi ..kumuuondoa kiongozi wa mfumo huo..Rais ndio dawa..kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye...si Pinda!!
Pinda ni kupoteza lengo....Kama aliondoka EL mambo yako vile vile inamaanisha tatiza ni nani zaidi ya Rais!!!!

Anyway siasa ina mambo mengi watu wengine wanaweza tumika kama fimbo bila kujijua..
 
na mimi nakuunga mkono Rais wetu hana uwezo wa kuongoza,watendaji anaoteua ni dhaifu itakuwa ni kumwonea tu Pinda kwani kila ishu nzito ikitokea rais yupo nje ya nchi kumbukeni mgomo wa madaktari halafu baada ya hapo anakusanya mafisadi kina iddi simba eti anaongea na wazee wa Dar es salaam Tatizo ni mfumo mzima kwani rais hasomi magazeti ,hapewi taarifa na watu wa usalama tusizunguke tukimwachia rais mpaka muda wake uishe tutapata hasara kubwa ni heri aambiwe waziwazi aondoe hizo takataka alizotuwekea

kura ya kutokuwa na Imani na uchaguzi wote urudiwe?,mbunge gani ana uhakika wa kurudi?,wengi hawatapiga kura

wewe umesikiliza bunge au umesimuliwa? ok sikiliza marudio umwelewe mh Zito

What is a point of having a forum...tualezee wewe vinginevyo!!! Member wanaleta wapa link,copies ,n.k
You done need to react to a guy who back up his argument with facts.
You need respond(not react)with facts in the same fashion....or let us no the claim is not true in the first place
You might be right ,who knows!!?
 
Kinachotakiwa ni mawaziri wahusika kujitoa. Wakigoma ndo watatolewa kwa njia ya kumtoa PM sababu PM akitoka, cabinet inavunjwa.

Nibora ivunjwe pm alitakiwa kuchukua hatua dhida yao kwamamlaka yako kabila halihaijawa mbaya lakn kwakua ameshindwa lazima awajibike yeye.wala simara yakwanza hapa tz hata mzee mwinyi aliwah kuwajibishwa kwa makosa ya watendaji wake.ndio maana zitto amesema wajipime wenyewe au wamtoe pm rehan kwakua yeye ndie mtendaji mkuu
 
Mleta mada ni gamba kabisa,haujamsikiliza kijana Zitto na uwezo wako wa kufikiria ni mdogo..Zitto amethubutu tena kwa kutumia akili ya hali ya juu.
 
zitto has kidnapped lissu's idea and he is now his popularity is spreading like a bushfire!since the cause is just go zitto,take that quiet secret millionare back to katavi where he belongs!prime ministry is too big for him,.what an opportunist zitto is!congrats
 
kikwete umchague wewe then zitto ndo amuondoe?
kwa nini usikosoe upumbavu wako wa kumchagua kikwete?
pia nakushauri sikiliza bunge kwa makini na kufuatilia
mtiririko wa hoja....naunga mkono hoja ya zitto.
 
naunga mkono hoja ya zita kwnia vita kubwa huanza na vita ndogo ndogo mawaziri wakiona hawawezi kujitoa waziri mkuu aondoke na akiondoka hao wengine pia hawatakuwa salama pia wataondoka mwisho wa siku watawekwa watu wengine wanaoweza kazi nao wasipoweza pia wataondoka.
 
Fikra za mwanadamu zinapotawaliwa na hulka ya ushabiki zaidi ya ukweli ,maamuzi hutolewa pasipo kuzingatia ukweli.Pia maamuzi hayo huambatana na hoja nyepesi zisizo na manufaa katika utatuzi wa tatizo kuu.

Serikali ya Jk tokea imeingia madarakani awamu ya kwanza imegubikwa na vitendo vya rushwa na Ufisadi uliokithiri kupita kiasi.Hii ni kutokana na ukweli kwamba Jk kama Raisi hakuwa na uwezo wa kuongoza nchi. Kongozi yeyote asiye na uwezo wa uongozi ni dhahiri hata team/wasaidizi wake watakuwa ni wabovu.Jk amejaza washkaji zake kwenye nafasi mbalimbali kama wasaidizi wake.Hili limejirudia hata pale bunge lilipomuazibu kwa kumwondoa waziri mkuu EL ili achague team bora bado yamejirudia yale yale.

Kwa nini siungi mkono hoja ya Mh. Zitto?
Sababu nilizotoa hapo kwenye maelezo ni kuwa tatizo kwenye uongozi wa nchi yetu sio mawaziri ama waziri mkuu bali ni mfumo mzima wa uongozi wa Jk.Hapa kilichotakiwa ni kutibu ugonjwa kama sio chanjo/kinga kwa kumwadabisha JK .Kwanini Zitto amekimbilia hoja ya kumwondoa Pinda ili hali kulikuwa na nafasi ya kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na Raisi?.

Hapo ndio pale wachambuzi wanapochimba zaidi na kuangalia kwa undani juu ya tuhuma za uswahiba wa Zitto na JK.Hii hoja kwa mtazamo wangu ni kupoteza mantiki ya hoja ya msingi iliyotaka kupelekwa bungeni ya kutaka kumng'oa JK.

Mungu Ibariki Tanzania dhidi ya huu uwizi wa dhahiri dhidi ya mali za walalahoi.

Wamekutuma. Una usingizi kalale.
 
Ameomba uungwaji mkono wa wabunge 70+ ili aweze wasilisha hoja yake ya kumchomoa Pinda
Ili kuhalalisha kumsulubu PM, Zitto alitoa hoja hii:
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho. Tatizo kubwa la Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutokutekelezwa ni ukosefu wa uwajibikaji; na kama nchi hii tunataka tuendelee, kama tunataka tupigane kwa dhati kabisa dhidi ya ubadhirifu, dhidi ya udokozi, dhidi ya uzembe, dhidi ya uvivu ni kuhakikisha tuna misingi sahihi ya uwajibikaji. Accountability, niliwahi kuwaambia vijana fulani kwamba kama kutakuwa kuna neno moja linalotakiwa liandikwe kwenye Katiba mpya, neno moja; ni ‘accountability,’ uwajibikaji na ndicho kinachokosekana. Taarifa hizi zinatolewa kila mwaka, nashukuru sana safari hii Wabunge mmekuwa wakali sana. Lakini bila kuhakikisha Executive inawajibika katika haya mwaka kesho tutarudia haya haya na tutakuwa wakali hivi hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa taarifa kwamba; mimi na Bunge hili halina mamlaka ya Mkurugenzi wa Shirika, Katibu Mkuu wa Wizara au Mkurugenzi wa Halmashauri. Mawaziri ambao wametajwa kwa njia moja au nyingine kutokuwajibika ipasavyo na kuliingizia hasara taifa wamekuwa wagumu sana kuwajibika, wanampa kazi Rais ya kuwafukuza.

Lakini sisi hatuwezi kuwaazimia hapa ila sisi tuna mamlaka na mtu mmoja tu humu ndani ya Bunge; na naomba mnisikilize kwa makini sana. Tuna mamlaka na mtu mmoja tu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bila kumwajibisha Waziri Mkuu hawa Mawaziri waliotajwa hawatatoka na wasipotoka madudu haya yatarudia. Kwa hiyo Mbunge yoyote mwenye uchungu na ubadhirifu, Mbunge yoyote ambaye anakereka na watoto kwenye Jimbo lake kukaa chini, Mbunge yoyote anayekereka na madawa kuharibiwa na MSD na MSD kushindwa kupeleka madawa kwenye vijiji vyetu, nampa taarifa kwamba kuanzia kesho tunakusanya sahihi za Wabunge 70, ili siku ya Jumatatu tutoe hoja hapa Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na kipindi hiki tunakitoa Mawaziri wote ambao wapo implicated kwenye taarifa hizi waweze kuona ama wao, au wamtoe rehani Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wabunge wote wenye uchungu kuanzia kesho tutakuwa pale mlangoni, sahihi zinazohitajika ni 70 tu, kwa ajili ya kuleta hapa Bungeni na Wabunge wanahitajika kupitisha hilo azimio ni nusu tu ya Wabunge, 50 plus one. Tukifanya hivyo tutakuwa tumewapa heshima wananchi wetu, wataona kweli tumewatendea haki badala ya kupiga kelele bila ya kuchukua action. (Makofi)
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom