Sitta: Sikukejeli vielelezo vya Dk Slaa kuhusu BoT

Kwa kweli ni aibu tupu kwa Mtu kama Six tena mwanasheria Mzuri tu, lakini anasaliti umma na watu wake wa Urambo kwa kisheti, wenzie wamekula mabilioni , yeye kambulia kisheti, na watu wake wa Urambo wanateseka.
Anakuwa kama Samuel Kiviutu yule wa ECK ya Kenya, tena nafikiri walikuwa UDSM pamoja, sasa sijui walifundishwa kula Visheti badala ya kusimamia Sheria na Kusimama kama wanaume.
Maana ukiangalia na kule kwa Ndugu zetu wa Kenya, Kibaki na team yake Mafisadi, kiviutu anaishia kupata Makombo.
 
we have a long way to democracy.
spika wa bunge anafanya kama bunge mali yake! wala haoni haya kabisa
 
kama watanzania wenyewe wanakubali kudanganywa sasa yeye afanye nini ?

kweli kabisaa Katibu Tarafa,

Hata mimi najuliza swali hili kabisa kuwa mbona watanzania wanakubali kudanganywa? Lakini ukichunguza kwa makini utagundua kuwa sio kweli kwamba watanzania wanakubali kudanganywa ila ni vile watu wengi hawako informed.

Watu wengi wanafichwa habari. Redio Tanzania haisemi ukweli kwa hiyo wengi huko vijijini hawapati hizi habari. Vyama vya upinzani havina pesa za kutosha (narudia pesa za kutosha) za kucounter nguvu ya ccm inayotumia pesa za kodi kudanganya watz.

Kazi ipo, taratibu tu tutafika na ninafurahi kuona mzimu wa BOT kama ule wa Buzwagi ukiwaandama Sitta na wenzake.

Thanks!
 
Kama sikosei katika hii forum kuna ushahidi unaoweza kuthibitisha kwamba fisadi Sitta alitamka bungeni kwamba amevifikisha vielelezo vya ushahidi polisi ili vichunguzwe na hatimaye kumfungulia mashtaka Slaa. Sasa anayakimbia maneno yake mwenyewe! Mwe! kazi ipo mwaka huu.
 
Six alikuwa anania ya kumtisha Silaa, alia-siendele na hiyo issue kwa kumuomba alitee vielelezo na kusema ni vya kugushi.Naona sasa ime-backfire, na pia tunapata somo jingine hapa kuhusu uteuzi wa watu uwe unathibitishwa na Bunge, kuwafanya wawe answerable kwa Bunge instead of a Excutive ambao wakiwa mafisadi since wana control nearly everything wanaweza kuficha ukweli, kama vile takukuru ilivyo isafisha Richmond, yale ya Dito yalivyokwenda au yanavyokwenda.
 
Kwa kweli ni aibu tupu kwa Mtu kama Six tena mwanasheria Mzuri tu, lakini anasaliti umma na watu wake wa Urambo kwa kisheti, wenzie wamekula mabilioni , yeye kambulia kisheti, na watu wake wa Urambo wanateseka.

Huyu Six ni wa kumeka hadharani, kwa vile amesema siyo lazima ukweli uwe 100% ili jambo lichunguzwe, hebu atueleze haya yako vipi

1. Kuiba na hatimaye kufukuzwa CDA na kuangushwa ubunge.
2. Kwa nini alifukuzwa kama mbwa kwenye nyumba ya serikali aliyokuwa akiishi.
3. Ufujaji wa pesa TIC na kula hongo toka kwa investor wa shughuli za uchimbaji wa mafuta
4. Kupewa TShs 200 million through TRA Customs Commissioner,za kugembea ubunge na kuhonga awe spika.

5. Na hiyo nyumba ya masaki uliyojenga na mali za wizi toka toka CDA, uka kwama nayo five years hadi ulipopata kazi TIC ukaanza kupora na kuimaliza.

6. When did you last practice as a lawyer au ndiyo ma-lawyers wa bongo, once a lawyer always a lawyer even without practicing.

Kama kuna mtu aliye uchi ni Sita na asithubutu kufungua mdomo wake kujidai kukejeli watu wasiokuwa wezi kama yeye.

You have been warned Mr. Speaker.
 
kweli kabisaa Katibu Tarafa,

Hata mimi najuliza swali hili kabisa kuwa mbona watanzania wanakubali kudanganywa? Lakini ukichunguza kwa makini utagundua kuwa sio kweli kwamba watanzania wanakubali kudanganywa ila ni vile watu wengi hawako informed.

Watu wengi wanafichwa habari. Redio Tanzania haisemi ukweli kwa hiyo wengi huko vijijini hawapati hizi habari. Vyama vya upinzani havina pesa za kutosha (narudia pesa za kutosha) za kucounter nguvu ya ccm inayotumia pesa za kodi kudanganya watz.

Kazi ipo, taratibu tu tutafika na ninafurahi kuona mzimu wa BOT kama ule wa Buzwagi ukiwaandama Sitta na wenzake.

Thanks!

MwK:
Nafurahi umeisahihisha sentensi yako: "Lakini ukichunguza kwa makini utagundua kuwa sio kweli kwamba watanzania wanakubali kudanganywa ila ni vile watu wengi hawako informed."
Huu ndio ukweli wenyewe, na hawa wapinzani inabidi wakubali kufanya kazi ya ziada kuwafahamisha ukweli wananchi.

Akina Kitila Mkumbo wasikate tamaa, na wala wasikalie kutusimanga wengi tuliomo humu JF, kwa sababu tu za kutojiunga na vyama vyao vya siasa ndipo waridhike kuwa na sisi tumo kwenye harakati za mapambano. Inabidi watambue kuwa mapambano yamo nyumba hadi nyumba sasa. Kama Kalamu atakuwa ameshawishi na kuhamasisha kaka zake, bibi yake, babu yake, n.k., atakuwa amekwisha fanya mchango mkubwa zaidi wa kuleta mabadiliko, hata bila kuwa amejiunga na chama cha upinzani. Sote tunauchukizwa na mwelekeo wa siasa za CCM ni wajibu wetu tuanzie mapinduzi haya kwa wananchi walio karibu na sisi kwanza. Haba na haba hujaza.....
 
Kalamu I buy your arguement .Imetulia na sasa ni kiti na kiti hata kwenda daladala .
 
Si kuna mtu alidai Sitta ni Jiniasi kwenye zile mada za BOT na watoto wa vigogo? Sasa Ujiniasi wake uko wapi?

Ushahidi wa maandishi na matamshi upo kuwa alipuuzia hoja ya Slaa. Cha aibu sana kwa yeye kama Kiranja Mkuu wa Bunge, ni kudai hakuwa na muda kupitia vielelezo na kurasa alfu ulela ulela!

Hivi leo waambowa hazina ya taifa inaibiwa unadai hukuwa na muda wa kutosha kupita vielelezo au kuunda kamati haraka kuchunguza jambo hili?

Same thing happened on Buzwagi, alilizembea mpaka mkataba ukafanywa wa hadhara sasa kamati ya Raisi na si Bunge lenye mamlaka linatalii nchi kukusanya mawazo.

Again he alsmost did it on Richmond, mpaka mabango yalipomzidi ndipo akakubali kuunda kamati.

Ni mpaka lini Viongozi wetu wataendelea kucheza gombe sugu na kuwa wazito kufanya maamuzi ya haki na ya maana?

Mimi nafikir Sitta inabidi ajiuzulu Uspika maana hiyo mifano mitatu katika Mwaka mmoja ni tosha kuwaonyesha Wananchi kuwa Bunge letu ni Hovyo na Spika ndiye hamnazo kabisa.

Just like Mgonja, Mramba and Ballali, Sitta must go!!
 
Nina ngoja Slaa aje na hoja binafsi Bungeni na Zitto ili tuone nini kitatokea . By the way Mudhihiri yuko wapi ? Mzee wa Pekecha je naye kimya ?

Unafikiri Mudhihir ana hamu tena na kutetea ufisadi tangu akatike mkono? Thubutu! Atabaki kugonga meza bungeni tu! Aibu imemshuka sana, kwani alimkandamiza Zitto na bado akaja kugundua kwamba Zitto alikuwa sahihi. Kama ilivyokuwa kwa Malecela vile!
Sasa Sitta ndio anatapatapa, naye yamemkuta. Tunakomaa naye tu hadi kieleweke. Sasa tunasaka ushahidi wa kile alichoiba alipokuwa kule kwenye uwekezaji, TIC, kwani nako kuna takataka kibao sana ambazo zinanuka uozo. Naye ataanikwa siku siyo nyingi sana hapa JF.
 
hivi hawa viongozi hawajui kuomba radhi? yaani kila mmoja anatatufa udhuru wa kuhalalilisha alichofanya...

Kikwete analaumu Benki Kuu
Meghji anamlaumu Balali
Balali anawalaumu "vigogo" kwa kumtumia
Sitta analaumu waandishi wa habari kwa kupotosha
n.k n.k Kuna mtu anaweza kuwajibika kwa vitendo au maneno yake au wote ni wale "viongozi wasiokosea" kwenye "Taifa la wasiokasirika"?
 
tafadhari mwenye data za huyu fisadi Sita AKA spika wa mafisadi atuletee hapa tuanze kumchambua utumbo wake na kufoward dunia nzima ili ajue internet ina akili kuliko yeye....nia ni kumwaibisha tuu,na vipi kuna mtu ana clip ya wakati anamtuhumu Slaa ni muongo
 
Zalendo Halisi Wacha Hilo:::

Kuna Nyumba Na Nafikiri Alikuwa Ametoka Kupokea Mgao Mwezi Huo Pale Kimara Korogwe Ukifikakorogwe Ukiuliza Nyumba Ya Sita Utaonyesha Alimnyeshea Mama Wa Watu Million 50
Na Kama Zilikuwa Ni Za Laana Yule Mama Akanunua Vi Hiace 4 Havikufika Hata Miezi Sita Maara Viegongwa Watoto Wameinba Spare...pesa Zenu Za Laana Msiaribie Watu Wengine Maisha Yao Jamani Muwe Makini Wekeni Bank Si Kugawia Watu Na Huku Wakiteseka Na Pesa Zenu ,,,
 
Hii Inaonyesha Ile Report Ya Richmond Inaelekea Wapi!!!!!
Kama Ameshindwa Kusoma Makaratasi 1000 Je Ataweza Kusom Vile Vitabu Page Zaidi Ya 3000,,jibu Litakuwa Hakuwa Na Muda Kusoma Pg Zote

"""kila Mwenye Sikio Na Asikie""
 
...........Watu wengi wanafichwa habari. Redio Tanzania haisemi ukweli kwa hiyo wengi huko vijijini hawapati hizi habari. Vyama vya upinzani havina pesa za kutosha (narudia pesa za kutosha) za kucounter nguvu ya ccm inayotumia pesa za kodi kudanganya watz................!

MWK

Ni kweli kabisa huko vijijini hawajui chochote kinachoendelea kuhusu ufisadi Tanzania unaoendelea.........hili nimelithibitisha mwenyewe kwa kuongea na baadhi ya watu huko vijijini na katika mikoa tofauti tofauti.....wengi hawaelewi kabisa.......nafikiri ukiondoa upinzani hata NGOs zinazojihusisha na demokrasia nchini and other pressure groups hawafanyi kazi yao........

nakumbuka hapa JF tulishaliongelea sana suala la kufikisha hizi jumbe kwa wananchi vijijini hata kwa kutumia simu......tuendelee kuelimisha wananchi pale tunapopata nafasi
 
Kuna records za Bungeni mtu unaweza pata full transcript (hansard) tena in electronic format and can be shared kwa wote

Wenye nyenzo wazitume hii pressure isiishe hata kama utawala uncheza mazingaombwe nasi

Taasisi
 
Mwanakijiji:

Safi sana.

Hapa ni Establishment inastruggle. Hii pressure ikilegeza tuu utaona kimyaa.

Ikizidi, dog will eat dog!

Hiyo idea ya hizi hoja kufika mitaani ni kali sana na zinafahamika.

Nimepitia now unclassified data za CIA juu ya Zanzibar, na kuona jinsi Babu alivyoogopwa na U-Communits wake na Jinsi Karume (all data allegedly) alivyoogopa Babu na Nyerere alivyoogopa U-Comunist na Arab Influence zikafanya Union iwe the best bet. Somo hapa ni kuwa ukianza kutoa hamasa na elimu kwa wingi wa watu in what you believe and stand for, the establishement will start to panic. Nisieleweke kama mwelekeo wangu ni wa akina Babu kisiasa, ila ni approach I am talking about here.

Pia kujenga agencies au NGOs ambazo ni politically alligned or affiliated with certain approach ni strategy nzuri.

Wenye kupenda haya mabadiliko ya lazima, la kujifunza ni kuweka kibano hadi somo lieleweke - gonga hapa ([media]http://www.foia.cia.gov/CPE/ESAU/esau-28.pdf[/media]). Knowledge is power. Empowering people with knowledge is the game feared by all establishments since the days of Adam!

Gazeti la kupeleka haya maoni kwenye distribution kwenye vijiji na mikoa na wilaya, itakuwa nusu ya kazi imeanza.
 
Nadhani kuwa Sitta ana uwezo wa kuendesha Bunge ila ana kasoro ya kutokujiamini. Hii inatokana na ukweli kuwa post ile aliipata kwa kupewa na watu fulani; kwa hiyo kila anachofanya, hujitahidi kuona kuwa hatawaudhi waliompa post hiyo. Hiyo ndiyo gharama ya kuongozwa na kibaraka hata kama ana uwezo wa kuongoza. Ukibaraka huu ndio uliomfanya atumie mamilioni ya pesa zetu kuchunguza kesi ya Malima na Mengi halafu mwishoni eti "akatumia busara zake" kumaliza kesi ile. Hoja zote zilizoletwa na upinzani pale Bungeni, hakutaka kuzipa uzito ili kulinda umaarufu wa waliompa post ile. Matokeo yake leo hii bunge limekuwa kama kilabu cha pombe za kienyeji kilicho na walevi wengi ambao kila mmoja wao anajiongelea lake bila kujua anaongea nini; kesho yake atakana yote aliyoongea kilabuni pale.

-Leo hii Spika Sitta anakana kukataa hoja ya Slaa.

-Miezi michache iliyopita, Naibu Spika alikana kuwa Zitto hakuadhibiwa kwa madai ya uwongo bali ni kutokana na "lugha aliyotumia"

Spika na naibu wake ni walevi tu hawa.
 
Kuna records za Bungeni mtu unaweza pata full transcript (hansard) tena in electronic format and can be shared kwa wote

Wenye nyenzo wazitume hii pressure isiishe hata kama utawala uncheza mazingaombwe nasi

Taasisi

Nilijaribu kusearch pale kwenye tovuti ya Bunge lakini server yao iko slow sana. Unahitaji kuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom