Sitta: Nina wakati mgumu

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,231
Rehema Matowo, Moshi
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta, amesema anapitia nyakati ngumu za kisiasa kutokana na uamuzi wake wa kusimamia misingi ya haki, usawa na uadilifu iliyoachiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lakini akaapa kupambana na mafisadi hadi nchi itoke mikononi mwao.

Kauli hiyo ya Sitta inakuja kipindi ambacho joto la siasa nchini limekuwa likipanda siku hadi siku huku chama chake cha CCM kikiwa katika kipindi kigumu cha mpito kutekeleza mpango mkakati ujulikanao kama kujivua gamba.

Akizungumza katika kongamano la miaka 50 ya Uhuru na maisha ya Watanzania lililofanyika katika Chuo Kikuu kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara Moshi (MUCCOBS) na kuwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya kanda ya kaskazini, Sitta alisema kamwe hawezi kubadilika na atabaki kwenye viwango.

“Nawahakikishia nitapigana vikali kuhakikisha CCM inakua safi na nitapambana na waliokiharibu chama hadi kupoteza mwelekeo,” alisema Sitta.

Waziri Sitta alirejea tambo zake akisema yeye ni mwanasiasa mwenye viwango na ndiyo maana, wengi wanamgombania, lakini akawataka watambue kuwa hawezi kuhama chama chake kwa sasa baada ya miaka 50.

Alisema kitendo cha kuhama chama kwa sasa hakipo na anachokifanya ni kupambana na maovu yote yaliyopo ndani ya CCM na kuhakikisha kinarejesha heshima aliyoiacha Mwalimu Nyerere.

Waziri Sitta alisema nyakati hizo ngumu hazitamfanya abadilike wala kurudi nyuma na kuwa atapambana kuhakikisha nchi inakua safi na kutoka mikononi mwa mafisadi.

Aliitaja misingi iliyoachwa na Mwalimu kuwa ni usawa wa binadamu, kutobaguana kwa kabila wala namna yoyote, uadilifu na umoja ambayo alisema kwa sasa Watanzania wameiacha na ndiyo maana nchi ipo kama ilivyo leo.

Akizungumzia Tanzania ijayo baada ya miaka 50 ya uhuru, Waziri Sitta alisema wananchi wanategemea nchi yenye kujitambua na isiyo maskini na kuweka bayana, hiyo itawezekana endapo rasilimali zilizopo zitasimamiwa vizuri.

Aliwataka vijana kuepuka kuwa mawakala wa wanasiasa ambao wamefilisika kiakili na wanaojali matumbo yao na kuendelea kuliingiza taifa katika giza la umaskini.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, alisema kinachoendelea nchini kwa sasa ni siasa za malumbano zisizo na tija kwa mwananchi wa kawaida hivyo vijana wasomi wanayo nafasi kubwa ya kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuwatambua.

Akizungumza katika kongamano hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Harisson Mwakyembe alisema vijana wengi wamekuwa bendera fuata upepo na kushabikia mambo ambayo hawajayafanyia utafiti kujua ukweli wake.

Dk Mwakyembe aliwataka kutoa mwongozo katika mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na kuwataka kuondoa woga katika kuijadili kwa manufaa yao na kizazi kijacho.

Alisema tatizo kubwa la Watanzania ni woga kusema na wana hulka ya kulalamika. Alisema nyakati zimebadilika na wanapaswa kuwa jasiri katika kudai haki zao.

source mwananchi
 
Tumesikia toka kwa Mpendazao juzi kuwa Sammy Sitta na Nnape Nnauye ni mojawapo ya waasisi wa Chama kilichokosa usajili na kusambaratika-CCJ. Sasa anaposema kuwa hawezi kuhama CCM baada ya 50 years si anadanganya watu huyu? CC na NEC wamhoji vizuri ili ijulikane!
 
wanatapa tapa hawana lolote atudanganyiki maanzi yetu sisi kama watanzania tunataka mabadiliko tu
 
huyu mzee napataga shida sana kumuelewa anaongeaga nini!!! very contraversial figure
 
SITTA ndio amechangia kiasi kikubwa matatizo ya CCM! Jamaa is greedy and selfish!!

Watu wanaosimamia kanuni za Mwl huwa hawajitangazi majukwaani.
 
SITTA ndio amechangia kiasi kikubwa matatizo ya CCM! Jamaa is greedy and selfish!!

Watu wanaosimamia kanuni za Mwl huwa hawajitangazi majukwaani.
gamba limeanza kuonekana, anafanya danganya toto, aseme kwanini alihaha muswada wa Famasi usipite bunge lililopita. ni fisadi huyooooowatanzania hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Ni mnafiki, sio mzalendo hana lolote huyo sita. Issue ya Richmond aliimalizaje!!. Hafai mnafiki sana huyu!. Anawakati mgumu wa kuifisadi issue ya Richmond hana lolote.
 
Kumekucha Tanzania, usiku umeendelea sana sasa karibu asubuhi tunaifikia. Tutafika tena kwa usalama kabisa kwa speed hii. Mapambano yanaendelea.
 
Na bado atakuwa na wakati mgumu sana akiendelea na tabia yake ya uzandiki!

Mguu mmoja yupo CCM mguu mwengine kaweka CCJ , mguu mmoja kaweka Chadema. I am sure hakwenda Chadema kwa sababu hawakukubali kumpa cheo cha juu alichotaka kwa sababu dream yake yeye urais tu!!

Tushamstukia huyu muzee ndio maana chama kikamtosa na huo uwaziri waliompa ashukuru sana enzi za mwalimu angerudi Tabora akaanike matovolwa.
 
Sasa sita kwanini anataka kupoteza nguvu kwenye kitu ambacho kinaonekana kimeshakufaa? Yeye angesema atahakikisha anasimamia maslahi ya wananchi na hadhi ya nchi hadi mwisho na kupambana na mafisad popote walipo sio wa CCM. Mimi nina alergy na watu wanaoipenda CCM sijui kwa nini, ila kadi ya CCM ninayo, lakini nimetokea kutokukipenda.
 
He is acting unafiki tu! Huyu ndiye alimshukia Dr Slaa during election akisema eti wanafunzi wa sekondari haiwezekani kusoma bure! Ndiye alipigwa chini kugombea uspika akasema ameonewa. Ndiye huyuhuyu alifunga mjadala wa Richmund bungeni bila maazimio yote kutekelezwa! Ni mnafiki tu!
 
na bado atakuwa na wakati mgumu sana akiendelea na tabia yake ya uzandiki!

Mguu mmoja yupo ccm mguu mwengine kaweka ccj , mguu mmoja kaweka chadema. I am sure hakwenda chadema kwa sababu hawakukubali kumpa cheo cha juu alichotaka kwa sababu dream yake yeye urais tu!!

Tushamstukia huyu muzee ndio maana chama kikamtosa na huo uwaziri waliompa ashukuru sana enzi za mwalimu angerudi tabora akaanike matovolwa.



nimeipenda hiyo ya matovolwa, pamoja na nswalu ha hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Sasa sita kwanini anataka kupoteza nguvu kwenye kitu ambacho kinaonekana kimeshakufaa? Yeye angesema atahakikisha anasimamia maslahi ya wananchi na hadhi ya nchi hadi mwisho na kupambana na mafisad popote walipo sio wa CCM. Mimi nina alergy na watu wanaoipenda CCM sijui kwa nini, ila kadi ya CCM ninayo, lakini nimetokea kutokukipenda.
hululazimishwa kuwa na hiyo kadi we vipi mbona unakuwa kama mtoto mdogo wa chekechea
 
Back
Top Bottom