Sitta mzoefu wa kuvuruga Bunge?

tutasikia mengi - wamemnunua ka mzee wa kiraracha kusadia kutafuta support ya umma. Sisi tunavyojua Sitta alikuwa sahihi - na kutubadilisha mawazo mfanye kazi ya ziada. tatizo sita hataki tu kutoka kwenye li chama lenu - halina jipya tumeshachoka.

Binafsi sioni kosa la Samweli - ukweli utawauma na mtatafuta vijitabu na vijisababu vingi tu ili aonekane ana makosa katika jamii - kazi mnayo ila muda ni mfupi sana.

kavuruga bunge au bunge lenyewe ndiyo limejivuruga?
 
Kama Sitta aliweza kuongoza watu kusimama dhidi ya Nyerere na kuandamana.. katika enzi za ujana wake.. basi ni mtu wa kupewa pongezi. Nani leo anaweza kuandamana dhidi ya JK huyu?
 
Ni bahati mbaya kwamba habari ndefu lakini haina chochote cha maana zaidi ya kuanza kampeni kabla ya wakati. Kuna haja ya kujua mmiliki wa gazeti na uhusiano wake na makundi yanayo hasimiana ndani ya CCM na Bunge.

ni Nazir Karamagi na mhariri ni Bagenda
 
Ila wataka mabadiliko wa kweli nadhani wanakubali ili mabadiliko ya kweli yatokee lazima someone ,sometime, somewhere
  • kwa kujua au kutokujua kwa ajenda binafsi au kwa uzalendo lazima aivuruge na kuigawanya CCM

Awe ni 6, RA, Lowasa , shibuda, JK ,Slaa,Zitto au yeyote yule tunahitaji watu wa kivuruga CCM kwani hivi sasa mbuzi na kondoo wanaishi zizi moja.
 
Kwa nini aliufunga mjadala wa Richmond kwa staili ile? Mbona sasa anauendeleza kwa kutumia majukwaa mengine ambayo sio rasmi kama lilivyo BUNGE?
 
Huu ni mfululizo wa habari za kijinga zinazoandikwa na gazeti la FISADI KARAMAGI kwa lengo la kumchafua Spika. Ni habari ambazo zinakuwa sponsored na akina Lowassa na kuandikwa na waandishi uchwara. Hakuna substance yoyote kwenye habari hii. Moderators bila shaka mpo.
 
Ila wataka mabadiliko wa kweli nadhani wanakubali ili mabadiliko ya kweli yatokee lazima someone ,sometime, somewhere
  • kwa kujua au kutokujua kwa ajenda binafsi au kwa uzalendo lazima aivuruge na kuigawanya CCM
Awe ni 6, RA, Lowasa , shibuda, JK ,Slaa,Zitto au yeyote yule tunahitaji watu wa kivuruga CCM kwani hivi sasa mbuzi na kondoo wanaishi zizi moja.
well said.........issue ni moja, tunahitaji CCM ivutrugwe. Haijalishi nani kaivuruga.
 
Six the Great! Cha msingi ni yeye Mzee Six kuwa na msimamo na kufanya maamuzi thabiti kwa manufaa ya Taifa asiyumbe wala kuyumbishwa. Ya mwanafunzi Samuel Sitta kijana wa Chuo Kikuu (hata kama alipotoka) yanadhihirisha jinsi alivyokuwa tayari kutetea kila alichokiamini. And that is what he has been trying to do katika Uspika wake kuendana na slogan yake ya kuwa na 'Bunge la Viwango'.
 
Kwa nini aliufunga mjadala wa Richmond kwa staili ile? Mbona sasa anauendeleza kwa kutumia majukwaa mengine ambayo sio rasmi kama lilivyo BUNGE?

Wewe ulitaka afanye nini kwa wakati ule it was point of no return vingenevyo rais angejiuzuru kumbuka ametoka nayo wapi angekuwa Msekwa ungekuwa bado hata unaikumbuka, tatizo letu tunaangalia imeishaje hatuangalii mjadala mzima na mivutano iliyokuwepo ni sawa na kumwokoa mtoto aliyezama baharini unapomfikisha nchi kavu baba yake anakuuliza mbona kofia yake siioni
 
Kwa nini aliufunga mjadala wa Richmond kwa staili ile? Mbona sasa anauendeleza kwa kutumia majukwaa mengine ambayo sio rasmi kama lilivyo BUNGE?

Mjadala ule ulifungwa kwa maridhiano yao wao ndani ya Bunge na si vinginevyo. Haikutungwa Sheria ya kuzuia watu kuendela kuzungumzia/kujadili kuhusu Richmond! Nje ya bunge mjadala unaendelea na kila mwananchi akiwemo Sitta anayo haki ya kuendelea na mjadala.
 
Kazi nzuri! Nyie mafisadi endeleeni kumsakama huyu mzee makini, Mr. 6. Atawapa six za nguvu, mkikaa vibaya....ooh!

Naamini kabisa moyono mwangu Mzee Six ni spika wa viwango as compared to the previous craps.
 
Wazee
Siku hizi serikali yetu ina magazeti mengi. Hata hili ni la serikali ya JK, lilioanzishwa na mafisadi kuhujumu agemda ya kupinga ufisadi. Hawa akina Prince Bagenda waliishiwa pumzi wakajisalimisha na ndio waendeshaji wa hili gazeti. Yako mengi kama akina Changamoto, Umma, Sauti Huru, Tazama Tanzania. Hapo usisahau media house nzima ya New Habari (Rai, Mtanzania). Haya yamejibainisha kuwa yanaunga mkono ufisadi.

Of course kuna IPPmedia na Sema Usikike, Nipashe, Taifa Letu, n.k - haya yanapinga ufisadi hata kama huwezi kukubaliana na kila kitu wasemacho.

Nikirudi kwa Sitta, niseme moja kubwa. Pamoja na jazba zake na udhaifu wa kibinadamu wa hapa na pale, yeye ni mpambanaji. Hii makala haikukusudia kumjenga, lakini imefanya hivyo kwa ajali.

-Huyu Sitta aliyethubutu mbele ya JKN akiwa mwanafunzi
-Huyu Sitta aliyethubutu wakati wa uhai wa JKN kuhoji muungano
-Huyu Sitta aliyeongoza mtandao uliomweka JK madarakani
-Huyu Sitta aliyesimama wima mbele ya NEC iliyodhamiria kumfukuza,
-Huyu Sitta aliyetamka mbele ya Rais kuwa hotuba yake haijakidhi haja kwa sababu haina ukali wa kutosha kuthibiti mafisadi
-Huyu Sitta aliyekataa kupatana na EL mbele ya Kamati ya Mwinyi,

Mimi nadhani, ni mpambanaji ukilinganisha na waliowahi kuthubuttu.
 
Well said Baija Bolobi watu wanahoji matokeo hawaangalii yamepatikanaje kutoka kiwango cha 40% cha utendaji wa bunge la Msekwa hadi 80% ya utendaji wa bunge la Sitta (hivi ni viwango vyangu tu) still hawaoni kitu wanahoji mbona hakupata 100% hata kama mtihani mtoto wako kapata hivyo lazima umpongeze ni sawa na kuhoji timu ya mpira imeshinda 1-0 kwanini haikushinda 5-0 hawajui kazi iliyokuwa uwanjani ukiwauliza wachezaji wenyewe watakuambia hata lile goli moja walilopata walikuwa nawasiwasi litasawazishwa
 
Hizi ndo siasa za Bongo! Kumbuken Sitta & Lowassa walikuwa kambi moja ya Mtandao na kazi yao kuu ilikuwa ni kumpaka matope Sumaye,mbona zile tuhuma hatuzioni.leo baada ya kupata walichotaka? kama Sitta ni mbaya kiivyo kwa nini walimsaport kumshinda Mzee Msekwa? Vivyo hivyo kama Lowassa ana historia ya Ufisadi kwanini walimsaport kuupata U premier. Kama ishu ya Richmond ilianzishwa na Dr.Slaa na Mbunge wa CUF Mr.Mnyaa,wao wameivamia ili kuvuta muda kisha wameiharibu mpambanaji wa kweli hawezi kutoka CCM, Sitta na Kina Lowassa chini ya genge lao la Mtandao walitumia fedha za EPA kumbeba MHESHIMIWA WANACHOPIGANIA NI GAWIO LA NGUVU NA PESA WALIZOWEKEZA sio wanyonge,akipatikana Rais Mwingine hamtasikia Sitta,Lowasa wala Rostam kama tulivyomsahau "FISADI' sumaye.
 
Gazeti la Taifa Tanzania limeandika:

"Wakati akijiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa sekta husika (Nishati na Madini) walijiuzulu. Baadhi ya watu wanahoji kwa nini Sitta hakujiuzulu mwaka 1994 akaondoka na Malecela?" wamehoji watu hao."

Hawa ni waongo. Mzee Malecela wakati wa sakata la G55 hakujiuzuru alibadilishwa nafasi na akateuliwa Mzee CD Msuya. Kwa hiyo Sitta asingejiuzuru tu kwa kuwa boss wake kabadilishwa. Hata hivyo, wengi waliounga mkono G55 tunawaona wanapeta bila shida yoyote, kama Mzee Marmo.

Naendelea kuona Spika Sitta katika hili ana credit za kutosha. Kila mahali penye chembechembe ya uanaharakati utamkuta. Tatizo ni umaliziaji wake. Chenga anawalamba, lakini kufunga anashindwa!

With a light touch::)
 
..mmesahau hujuma alizofanya alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ustawishaji Makao Mkuu Dodoma.

..pia msisahau madudu aliyokuwa akiyafanya alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TIC[kituo cha uwekezaji].

..kuna aliyepata kusema kwamba Sitta angekuwa msafi basi leo hii Dodoma ingekuwa imejengeka na kustahili kuwa mji mkuu wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom