FuturePresident
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 321
- 54
Kwa nguvu zote wapenda haki wote vita yetu kubwa iwe kwenye katiba ya nnchi hii!! Hapa ndio ulipo umuhimu wa katiba....katiba yetu ya sasa ya kila uteuzi kufanywa na raisi wa nnchi...ni tatizo....hawa wakuu wote wa mikoa ni ccm members....wewe unategemea nini ?....haya sasa shime shime moto wote kwa wapenda haki....uhamie kwenye katiba mpya ya nchi yetu ili ituondolee umwagaji wa damu kwa taifa letu kabla hatujafika huko
wadau: Nilikuwa naumiza kichwa changu bure kwamba ilikuwaje hakimu yule wa arusha alikataa kumtoa lema mahabusu huku dhamana aliisha iweka wazi. Kumbe ni msukumo wa kisiasa kutoka kwa mkuu wa mkoa. Soma sehemu ya habari hii hapa chini na utajua kwa nini sakata lote lile ambalo alikuwa la azima lilitokea -- ni bahati tu hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Kama kawaida yao wanasiasa wa ccm hasa siku hizi huyo rc anasema uongo kabisa -- alikwenda mahakamani kufanya nini siku ile. Ni dahiri angeweza kutumia simu kumpigia simu hakimu bila ya yeye kwenda lakini simu zinaweka kumbukumbu.
Mahakimu wetu!!!! Watanzania tutakimbilia wapi? Polisi ccm, mahakimu ccm!!! Huku nchi inafilisika kwa kasi ya ajabu!!
mkuu wa mkoa wa arusha, magessa mulongo ameonya kuwa vyombo vya dola havitakubali kuwaacha baadhi ya watu kuigeuza arusha sehemu isiyotawalika akisema kuanzia sasa, yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu kwa njia au sababu yoyote atadhibitiwa kikamilifu bila kujali cheo wala itikadi yake kisiasa.
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, mulongo alisema: mtu yeyote atakayechezea amani na utulivu wa arusha atakiona cha mtema kuni. Huu ni uamuzi wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama. Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye arusha isitawalike.
mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.
alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya mahakama ya hakimu mkazi arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu judith kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa chadema.
kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa mbowe au shughuli zozote za kisiasa arusha. Nilikwenda kumsalimia jaji mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa mahakama, alisema mulongo.