Siri yafichuka: Kumbe hakimu Arusha alishawishiwa na Mkuu wa Mkoa kukataa kumtoa Lema!

Mnajiimarisha kwa lipi wakati kila kitu kimewashinda? bei juu, shilingi inaporomoka kwa kazi, sasa mnafanya nini? Nyani aoni kundule wewe nakupa siku chache tu utaimbia hata kutoa maoni hapa JF kwa aibu.
tunazidi kuimarika kutokana na nguvu ya upinzani kuzidi kushuka.
Uchumi wa nchi hii ni wetu sote na siyo wa CCM. Watu tunajisahau, tunataka serikali itufanyie kila kila kitu.
 
SERIKALI YETU, MAHAKAMA ZETU, NA BUNGE LETU LIPO MFUKONI MWA CCM, HATA MAAMUZI HUFANYWA KUZINGATIA RANGI YA MASHATI TULIYOVAA. UVCCM walifanya mikutano bila kibali Arusha, hawakukamatwa, tulisikia kuwa walileta Uchochezi kwa kumtaja kijana wa kigogo kuwa anavuruga lakini hawakukamatwa.

Hayo yatasemwa kwa CHADEMA ili waonewe, wapigwe, washitakiwe. tulisema siku moja kuwa Je, Jeshi la Polisi ni legelege vile kwanini? Tuliangalia mfano huo Mkoani Arusha kulitokea mvutano kati ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufungua matawi.

Jeshi likawanyima kibali halali cha kufanya mkutano, eti wale vijana wa CCM wakaamua kutumia walinzi wa kampuni binafsi. Jeshi la Polisi halikuona? Kama liliona mbona halikuwachukulia hatua? Waliogopa mashati ya kijani, wakaamua kuificha ile kaulimbiu yao ya utii wa sheria bila shuruti. Ni ujinga.

Baadaye wanajidai kuanza kuwatafuta eti walisema maneno ya uchochezi mkutanoni. Kwanini hawakuwakamata hapo hapo? Hakuna makachero? Je, kila chama kikija na kampuni binafsi kulinda mikutano yake nchi itatawalika?

Polisi wanafua maelekezo ya CCM kutekeleza maadili ya jeshi, wanafanya kiushemeji, kufahamiana, kihali ya kifedha na kivyama. Polisi na Mahkama Mnakokwenda mnatuharibia nchi kwa sababu ya ujinga wa kulinda chama cha Magamba hata katika uovu.

Tujiulize haya, waliotoa taarifa kuwa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wamefanya mkutano kinyume cha utaratibu ni polisi wenyewe. Tulijiuliza sana siku hiyo, iweje vijana wa Chama cha Mapinduzi watumie walinzi wa kampuni binafsi? Niliuliza tena itakuwaje kila Chama kikianza kuwa na walinzi wa kampuni binafsi? Sikujibiwa.

Tunauliza tena ilikuwaje vijana wa Chama cha mapinduzi wakafanya mkutano ndani ya mji bila kuwa na kibali? Polisi inakiri kuwa iliwanyima kibali cha kufanya mkutano lakini walifanya, wakalindwa na kampuni binafsi, wakamaliza wakaondoka. Tukaanza kusikia habari za kuhojiwa kwa James Millya, Mwenyekiti wa Arusha, na Beno Malisa, kaimu Mwenyekiti wa UVCCM taifa.

Kwa kosa hilo hilo la kukusanyika bila kuwa na kibali, Vijana wa Chama cha mapinduzi wapo nje, wanaendelea kutanua, hawana kesi mahakamani. Lakini kwa kosa hilo hilo, Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ana kesi Mahakamani, anapaswa kujibu Mnataska tusiseme kuwa hakuna haki katika utekelezaji wa sheria. Tena mbaya zaidi, Vijana wa Chama cha Mapinduzi walifanya mkutano, ukahudhuriwa na watu.

Mbunge Godbless Lema hakufanya Mkutano, aliondoka mahakamani kurudi ofisini, huku watu wakimdai awaeleze kilichojiri mahakamani baada ya Mahakama kushindwa kuweka vipaza sauti kama ilivyoahidi kabla ya siku ya kesi. Nani kati ya hawa ana kosa? Wale waliofanya mkutano bila kibali, au Yule aliyetoka mahakamani kurudi ofisini kwake na kusimama angalau awaambie ndugu zake kilichojiri mahakamani, baada ya mahakama kuwanyima ndugu zake haki ya kusikiliza kesi ya ndugu yao?

Wakati Godbless Lema anashtakiwa Mahakamani, sheria zilizopo ni zile zile kuhusu mikusanyiko ambazo ziliwaacha huru vijana wa CCM waliovunja sheria, watekelezaji ni wale wale askari wa jeshi la polisi wa Arusha, mahali ni pale pale zilipovunjwa sheria na vijana wa CCM , katika manispaa ya jiji la Arusha, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ni Yule yule Zuberi Mwombeji, Mwezi ni huo huo ambapo vijana wa CCM wamefanya kosa zaidi wakaachiwa, lakini Lema akafikishwa mahakamani na sasa yupo rumande japo ni baada ya yeye kukataa dhamana.

Wakati Lema anakamatwa kwa kosa hilo Nchi ni ile ile, Tanzania inayosema kuwa kuna demokrasia ya Vyama vingi, uhuru wa kujiunga na vyama vyovyote, au uhuru wa kuabudu. Wakati Lema anakamatwa na kufunguliwa mashtaka, Vijana wa CCM waliovunja sheria wakivinjari nje tunaambiwa katiba inayotumiwa na vyama vyote ni ile ile inayozungumzia usawa.

Ni mtanzania yupi mwenye akili timamu, mwenye uzalendo, anayepigania haki, anayepinga ukandamizaji, anayepinga dharau na manyanyaso ambaye atasema kuwa polisi wa Arusha wanatenda haki?

Hili tungesema limetokea kwa bahati mbaya, kama nisingeandika mapema kabla halijatokea. Na Sasa Mtasingizia makosa kibao. Ila Mahakamana polisi kwa utendaji huo, sio kwa
 
Sawa mkuu, miaka 50 chama chenu ndo kimetufikisha hapa.. Nyinyi mnatembelea V8 wakati MTANZANIA aliewapa kura hana hata kauwezo ka'kununulia JEMBE LA MKONO.. Mungu awarehemu sana wana'CCM.. "In allah maaswabirinah.."
Dua ya kuku haimpati mwewe. Jitahidi, fanya kazi kwa bidii, hizo V8 utaziendesha tu!
 
kwa kifupi tunataka katiba mpya maana haya mauonevu yote ni kwa sababu ya mamlaka waliopewa na katika ya sasa rais kuwachagua mahakimu, wakuu wa mikoa, wilaya ,majaji n.k so tupiganie tupate katiba mpya then tuanzie hapo, tuvumilie wana cdm kwani ukombozi ni kazi ngumu na sio rahisi tutayaona mengi zaidi ya haya tujipe moyo.haya mamlaka ya duniani yamewalevia hawa magamba.
 
Hakimu naye ana maamuzi yake...anafanya kazi yake independently, hukumu au dhamana ni maamuzi ya hakimu mwenyewe, hawezi kushurutishwa na mtu yoyote!


mkuu hakimu anaye yumia ubongo anatowamaamuz kuzingatia shelia sikwakutumia masabuli yakei
 
Nchi inaendeswa na sheria na taratibu kaka sio mambo ya kupanga mitaani tu..

Kesi uwa zinafanyika mahakamani na mahakama ndio inaamua..

Hivi wewe ukienda kumtembelea ndugu yako jela lazima atoke?
Nakumbuka maneno ya rais wa zamani wa Zanzibari..

Dr Salimin, watu waliomba amtoe Juma Duni, mahabusu, akasema muacheni akae sio papai kusema litaoza..

Na nyie subirini mpaka tarehe 14 ndio atatoka

Ulimi mwema ni sumaku ya mioyo ya watu. ni mukate wa roho ni chemichemi ya mwangaza wa hekima na ufaham

mkuu uliyo yaandika sijuwi umeyatowa wapi tanzania ipi inaendeswa kwa sheria epa kagoda lichimondi dowans mwizi wa kuku afugwe maisha mwizi epa umwambie lejesha pesa nakusamehewa mkuu nafahamu unatetea kibaruwa chako isiwe kwa huomutindo kunasiku utajutia kwauliyo yatenda
 
Kinachonisikitisha hapa JF ni watu kuendelea kujibishana na Rejeo na ritz
hawa ni watu wamekuja hapa kwa mission maalumu ya drail michango
yote ya JF na wanalipwa kwaajili hiyo. Vinginevyo watu hawataweza kutofautisha
kati ya Greater thinker na Ritz & Co.

Jamani tuwapuuzeni hawa ni wap***mb*v wachache! My two cents advise.
 
duh! Oooops!
Mkuu hivi unasoma darasa la ngapi? ndio unajifunza kuandika?[/QUOTE]

mkuu sijabahatika kusoma darasa hata 1 sababu ya hao mafisadi nakutosoma sikigezo chakukemea maovu nahao wasomi hawanafaida
yoyote kwetu waiifilisi tanzania
 
"Kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa Mbowe au shughuli zozote za kisiasa Arusha. Nilikwenda kumsalimia Jaji Mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo Lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa Mahakama," alisema Mulongo.

Yaani Mkuu wa Mkoa hana kazi mpaka anatumia muda wa kazi kwenda kumsalimia Jaji? Hivi kwa nini hakumkalibisha nyumbani kwake jioni na kupiga longolongo lao!! Inaelekea either hajui wajibu wake au hana cha kugfanya zaidi ya kuzururazurura tu na kupiga propaganda.

Kuna wakati nilishawahi kumhoji Mr. Butiku kuhusu uhuhimu wa hawa wakuu wa mikoa, alitetea uwepo wao lakini sikupenda kubishana naye sana kwa vile namuheshimu!! Kwa mtazamo wangu, wamepitwa na wakati.

May be walikuwa useful 20-30 years ago siyo sasa. Jins akina Nape wanavyotanua mjini inaonyesha ni jinsi gani Masasi haimuhitaji!!
 
Ulimi mwema ni sumaku ya mioyo ya watu. ni mukate wa roho ni chemichemi ya mwangaza wa hekima na ufaham

mkuu uliyo yaandika sijuwi umeyatowa wapi tanzania ipi inaendeswa kwa sheria epa kagoda lichimondi dowans mwizi wa kuku afugwe maisha mwizi epa umwambie lejesha pesa nakusamehewa mkuu nafahamu unatetea kibaruwa chako isiwe kwa huomutindo kunasiku utajutia kwauliyo yatenda

duh! Oooops!
Mkuu hivi unasoma darasa la ngapi? ndio unajifunza kuandika?

mkuu sijabahatika kusoma darasa hata 1 sababu ya hao mafisadi nakutosoma sikigezo chakukemea maovu nahao wasomi hawanafaida
yoyote kwetu waiifilisi tanzania
Nimesoma hizi posts zako nimeshindwa kukuelewa kabisa!
ni kwamba hujui kuandika au unaandika haraka haraka sana kwa papara?
Kiswahili siyo kigumu kiivyo..vuta sibira, jipande vizuri, tumia hata dk thelasini kuandika mstari mmoja unaoeleweka!
 
Nimesoma hizi posts zako nimeshindwa kukuelewa kabisa!
ni kwamba hujui kuandika au unaandika haraka haraka sana kwa papara?
Kiswahili siyo kigumu kiivyo..vuta sibira, jipande vizuri, tumia hata dk thelasini kuandika mstari mmoja unaoeleweka!

RC WA ARUSHA ALIKUWA DC BAGAMOYO; hatushangai kazi anazozifanya ni za kichama zaidi kuliko kusimamia shughuli za maendeleo! Ameletwa na JK ili kudididmiza maendeleo ya mkoa wa Arusha
 
tunazidi kuimarika kutokana na nguvu ya upinzani kuzidi kushuka.
Uchumi wa nchi hii ni wetu sote na siyo wa CCM. Watu tunajisahau, tunataka serikali itufanyie kila kila kitu.
Acha pumba zako, uchumi gani unaokua wakati serikali yako ya CCM imefilisika!!!! hadi mnashindwa kutoa ruzuku kwa vyma vya siasa??
 
Nimesoma hizi posts zako nimeshindwa kukuelewa kabisa!
ni kwamba hujui kuandika au unaandika haraka haraka sana kwa papara?
Kiswahili siyo kigumu kiivyo..vuta sibira, jipande vizuri, tumia hata dk thelasini kuandika mstari mmoja unaoeleweka!

kama neema itakuangukia, usifurahie, na kama udhaifu ukikujia, usisikitike kwani vyote vinapita na vitakwisha
 
Msisahau kwamba Magesa Mulongo ameletwa Arusha katika utekelezaji wa azimio la bagamoyo!!
Uyasemayo ni kweli kabisa, usisahau ziara ya Wasira hivi karibuni huko Arusha kwa kisingizio cha UVCCM. Fuatilia pia sakata la Wakuu wa Mikoa kuingilia Uhuru wa Mahakama jinsi shujaa LISSU alivyopambana na wabunge vilaza wa CCM bungeni kuhusu kubakwa kwa uhuru wa Mahakama. Sasa ametimia, Wakuu wa Mikoa sasa ndiyo Mahakimu na Majaji. Kazikweli kweli.
 
Kinachonisikitisha hapa JF ni watu kuendelea kujibishana na Rejeo na ritz
hawa ni watu wamekuja hapa kwa mission maalumu ya drail michango
yote ya JF na wanalipwa kwaajili hiyo. Vinginevyo watu hawataweza kutofautisha
kati ya Greater thinker na Ritz & Co.

Jamani tuwapuuzeni hawa ni wap***mb*v wachache! My two cents advise.

Halafu ukiangalia kwenye hili sakata la Arusha utagundua kuwa kuna kitu wanajaribu kukificha na ndio maana wako makini kuandika pumba na kuvuruga kila post inayojaribu kutoa mwanga wa yanayotokea AR.

Ila walisema wahenga ''siku ya kufa Mbwa, pua zote zinaziba''

Let us wait n see
 
Hivi aliyepaswa kwenda kumsalimia mwenzie ni Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mwenyeji au Jaji Mkuu ambaye alikuwa Mgeni hapo Mkoani! Kweli Mtu unahitajika uwe na akili kamilifu unapoamua kudanganya. Namshauri Mkuu wa Mkoa kama anaona zake hazitoshi, achanganye na za Cameroun.
 
ipo siku...but not now! wewe unawaza kesho, sisi tunawaza leo namna ya kuendelea kujiimarisha!
Mtabaki na mawazo hayo hayo...IKO SIKU!
You posses a very irritative way of expressing your views.....is this character of yours congenital or is true that you getting a pat on your back for behaving that way?
 
Back
Top Bottom