Siri yafichuka: Kumbe hakimu Arusha alishawishiwa na Mkuu wa Mkoa kukataa kumtoa Lema!

Mtajiimarisha tena? Hata mkitumia mapolisi na mahakimu, siku ikifika ya kuondoka mtaondoka. Kaondoka Hosni Mubarak na gaddafi, sembuse huyo wenu mkenua meno?
Chama ni imara...kinapendwa..kina wanachama wengi na wanaojulikana, siyo wanachama wa magwandwa wa kujificha ficha!
Upinzani unahitaji kufanya kazi ya ziada kuweza kufanya mapinduzi.
kwa stahili yao hawa CDM hawafiki kokote
 

Lakini baadaye si alikubali kutoka? baada ya kushawishiwa na viongozi wa CDM na hata wakuu wa polisi waliyomtembelea. Uko wapi wewe?

Nchi inaendeshwa na sheria na taratibu kaka sio mambo ya kupanga mitaani tu..

Kesi uwa zinafanyika mahakamani na mahakama ndio inaamua..

Hivi wewe ukienda kumtembelea ndugu yako jela lazima atoke?
Nakumbuka maneno ya rais wa zamani wa Zanzibari..

Dr Salimin, watu waliomba amtoe Juma Duni, mahabusu, akasema muacheni akae sio papai kusema litaoza..

Na nyie subirini mpaka tarehe 14 ndio atatoka
 
BAK,
Hivi unaweza kuniambia Lema kwa nini alikataa dhamana wakati ni haki ya mshitakiwa

Ritz' unaweza kuniambia kwanin hakimu alikataa dhamana ya Lema wakati ni haki ya mshitakiwa?!
 
watawala wetu hawaelewi kutawala kunapaswa kuzingatie haki, usawa,taratibu na sheria wanacho jua wao ni kutawala tu kivipi hapo pagumu
 
Ritz' unaweza kuniambia kwanin hakimu alikataa dhamana ya Lema wakati ni haki ya mshitakiwa?!
Hakimu naye ana maamuzi yake...anafanya kazi yake independently, hukumu au dhamana ni maamuzi ya hakimu mwenyewe, hawezi kushurutishwa na mtu yoyote!
 
Msisahau kupigia kura Mlima Kilimanjaro
Tatizo ufisadi mkuu, sisi tutapiga mafanikio yataonekana wao watumbua pesa za umma bila aibu

ila tutapiga usijali maana tuna amini baadaye uongozi utabadilika labda hawatakuwa mafisadi

"kumbusba namna ya kuupigia basi "
 
Ushajua halafu? Acheni uchochezi wa kijinga...nchi inataka amani hii na sio migogoro kila wakati inayoletwa na wapumbavu wachache wa vyama vya siasa...
 
Ritz' unaweza kuniambia kwanin hakimu alikataa dhamana ya Lema wakati ni haki ya mshitakiwa?!

Dhamana yake ilikuwa wazi toka siku ile alipokamatwa akaandika Tamko lake, mahakama ikafanya kazi yake mpaka tarehe 14 ndio kesi ya yake itatajwa tena..

Mahakama inafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi..

Naomba unijibu na mimi kwa nini Lema, alikataa dhamana wakati ni haki ya mshitakiwa, akangangania kwenda Jela na sasa hivi anataka kutoka?

Kwa hiyo alichokuwa anakipigania mpaka kwenda Jela kakipata?
 
Magwanda kila mtu ana maamuzi yake...kila siku huwa nawafananisha na gari bovu.
Leo Zitto atasema hiki, Kesho Lissu naye atakuja na lake, Slaa naye tena ataleta lake, Regia naye hatakosekana.
Kwa kifupi chadema bado ni organization amabayo individualism imetawala!
Ni chama ambacho hakiwezi kupose threat yoyote kwa serikali.

Sawa mkuu, miaka 50 chama chenu ndo kimetufikisha hapa.. Nyinyi mnatembelea V8 wakati MTANZANIA aliewapa kura hana hata kauwezo ka'kununulia JEMBE LA MKONO.. Mungu awarehemu sana wana'CCM.. "In allah maaswabirinah.."
 
ipo siku...but not now! wewe unawaza kesho, sisi tunawaza leo namna ya kuendelea kujiimarisha!
Mtabaki na mawazo hayo hayo...IKO SIKU!

Mnajiimarisha kwa lipi wakati kila kitu kimewashinda? bei juu, shilingi inaporomoka kwa kazi, sasa mnafanya nini? Nyani aoni kundule wewe nakupa siku chache tu utaimbia hata kutoa maoni hapa JF kwa aibu.
 
Hata mimi nilishangaa vipi hakimu anakataa kutoa hati ya kumleta Lema mahakamani huku dhamana alishaweka wazi. In fact hakimu huyo alishatoa hati za namna hivyo katika kesi kadha huko nyuoma, inakuwaje ya Lema inakataliwa?
Kwanini aletwe mahakamani?
Yaani wampangie hakimu muda wao wanaotaka kuweka dhamana?

Ingekuwa sababu ni ukosefu wa fedha au wadhamini, hapo hakimu angeweza kumtendea haki na kumleta mahakamani pindi hela itakapopatikana.

Lakini kama mwenyewe alimwambia hakimu kuwa hahitaji kuwekewa dhamana, then asimpangie hakimu muda wa yeye kupewa dhamana simply because he changed his mind.

Hakimu ana haki ya kupanga ratiba zake bila kushurutishwa na mtu yoyote, but he can be conviced humbly and if he accepts, that will be a favor that needs to be appreciated.

But if he rejectcts.... well just wait for the court date.

Hakuna sheria iliyovunjwa, utemi huwa hauna mpango especially kama umeshikilia makali.
 
Serikali ya CCM sasa imefikia kikomo cha kulinda amani aliyotuachia baba wa taifa
 
Kwanini aletwe mahakamani?
Yaani wampangie hakimu muda wao wanaotaka kuweka dhamana?
Ingekuwa sababu ni ukosefu wa fedha au wadhamini, hapo hakimu angeweza kumtendea haki na kumleta mahakamani pindi hela itakapopatikana.
Lakini kama mwenyewe alimwambia hakimu kuwa hahitaji kuwekewa dhamana, then asimpangie hakimu muda wa yeye kupewa dhamana simply because he changed his mind.
Hakimu ana haki ya kupanga ratiba zake bila kushurutishwa na mtu yoyote, but he can be conviced humbly and if he accepts, that will be a favor that needs to be appreciated.
But if he rejectcts.... well just wait for the court date.
Hakuna sheria iliyovunjwa, utemi huwa hauna mpango especially kama umeshikilia makali.

Sheria sasa zimetushinda ni bora tu sasa tukubali sheria za masaburi maana hakuna tunaloliweza
 
Mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.


Alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa Lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu Judith Kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema.

“Kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa Mbowe au shughuli zozote za kisiasa Arusha. Nilikwenda kumsalimia Jaji Mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo Lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa Mahakama,” alisema Mulongo.

Yani ndio kazi za wakuu wa mikoa hizi?
Duh, kweli KAZI ipo?
 
Back
Top Bottom