Siri kubwa ya mafanikio ya CCM NI kubeba agenda muhimu za kitaifa na kubadilika kulingana na wakati

Fukua

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
546
479
Salaam wanajukwaa.

Sio Siri miongoni mwa Mambo muhimu kabisa niliyokuwa nawaombea viongozi wetu wa Chama na serikali kuyatafakari na kuchukua hatua NI Kama yafuatayo.

Moja, maridhiano ya kitaifa.

Mbili, kuufufua mchakato wa katiba mpya.

Tatu,tume huru ya uchaguzi japo itapatikana ndani ya katiba mpya.

Watanzania wote NI mashahidi Mambo mengi mabaya Kama mateso, mauaji,vipigo na vifungo vya kisiasa kwa wapinzani wa CCM kama lissu,azori,been saa8, n.k. hata wale waliokuwa ndani ya ccm lakini wakawa wapinzani wa JPM Kama wakina Nape, Membe, makamba's, kinana n.k shida, fedheha na tanuru la Moto walilopitishwa na mwendazake hayo yote yalitosha kuwa na maridhiano ya kitaifa kwani NI kweli watu wengi Sana waliumizwa.

Tusingeweza kusonga mbele Kama taifa wakati wananchi wengi wanalia kwa maumivu makali.

Maridhiano yataliponya taifa, yatarejesha matumaini ya wananchi kwa serikali na Chama,yataleta umoja wa kitaifa na hatimaye maendeleo ya haraka kwani waleta maendeleo NI wananchi ambao ni lazima wawe na upendo,kuthaminiana umoja,kuaminiana,kushirikiana, kuheshimiana na kupendana.

Katiba mpya NI mwarobaini wa matatizo mengi Sana ya wananchi, utatuepusha na kujirudia kwa hatari kubwa ya ubabe Kama wa mwendazake.

Itasaidia kuwa na utaratibu unaoendana na Aina ya siasa tuliyonayo tanzania na dunia kwa kipindi na wakati huu wa utandawazi.

Itasaidia kuwa na umoja wa kweli na itasaidia kuleta uwajibikaji wa viongozi.

Tume huru NI muhimu Sana hasa kwa kipindi hichi ambapo tunaelekea kwenye uchaguzi 2025.kama katiba mpya itakuwa bado kwani ninaamini chakato utachukua mda kidogo.

Ninashukuru Mungu na viongozi wa Chama cha mapinduzi na serikali kwa kuyatafakari na kuyasimamia Mambo haya ambayo NI muhimu Sana kwa taifa letu kwa wakati huu.

Pia ninavishukuru vyama vya upinzani hasa chadema chini ya kiongozi wao Mh. MBOWE kwa kuishauri serikali na CCM pia kusisitiza umuhimu wa agenda hizi kwa jasho na damu Tena kwa kutumia njia za kistaarabu kabisa.

Tunajenga taifa moja tusiparuane, na tusiumizane vyama vyetu vinaweza kupita au kufa lakini TANZANIA haitopita milele.

Nimeandika mafaKama mtanzania huru niliye acha ukada wangu pembeni kabisa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania, Mungu mbariki raisi wetu Mama Samia, Mungu ibariki CCM na Mungu vibariki vyama vya upinzani.

Ameeeen!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Ccm inabebwa na tume ya uchaguzi na vyombo vya dola.

..siku mmoja wapo wa vyombo hivyo viwili akiitupa mkono Ccm chama kitaporomoka.
 
Sio kweli hata kidogo Chama Cha CCM kina wanachama wengi na kina Sera/agenda nzuri zinazoeleweka kwa wananchi na kinabadilika kutokana na mahitaji ya wakati na hiyo ndio Siri kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaji wa CCM ni mazuzu na masikini, acha kuzunguka sana.
Ukisema mazuzu na maskini bado utakuwa unajidanganya na hamtaweza kuitoa CCM madarakani milele, CCM inabeba watu wa makundi yote yaani matajiri wakubwa, wafanyakazi, maskini, wenye akili kubwa na wazalendo kwa ujumla
 
Ukisema mazuzu na maskini bado utakuwa unajidanganya na hamtaweza kuitoa CCM madarakani milele, CCM inabeba watu wa makundi yote yaani matajiri wakubwa, wafanyakazi, maskini, wenye akili kubwa na wazalendo kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni nani anataka 'kuitoa' madarakani?

Haitafaa lolote ikiwa mazuzu bado wengi namna hii au zaidi.
 
Sio kweli hata kidogo Chama Cha CCM kina wanachama wengi na kina Sera/agenda nzuri zinazoeleweka kwa wananchi na kinabadilika kutokana na mahitaji ya wakati na hiyo ndio Siri kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app

..sasa hivi hakina mvuto tena.

..kinategemea zaidi mabavu na kujiegemeza ktk vyombo vya dola.

..hata bungeni kumejaa Ccm watupu tunashuhudia wasivyokuwa na hoja.
 
Ni nani anataka 'kuitoa' madarakani?

Haitafaa lolote ikiwa mazuzu bado wengi namna hii au zaidi.
Na NI kweli hakuna wa kuitoa madarakani pia watanzania wengi NI wasomi na Wana uelewa labda zuzu lililobaki ni wewe tu
 
..sasa hivi hakina mvuto tena.

..kinategemea zaidi mabavu na kujiegemeza ktk vyombo vya dola.

..hata bungeni kumejaa Ccm watupu tunashuhudia wasivyokuwa na hoja.
CCM haijawahi na haitowahi kukosa mvuto ndugu na haitumii mabavu labda Kama utafafanua zaidi lkn Sera zake nzuri ndizo zinakibeba hiki chama na hata wabunge so wa CCM tu wapo chadema, act n.k
 
Salaam wanajukwaa.

Sio Siri miongoni mwa Mambo muhimu kabisa niliyokuwa nawaombea viongozi wetu wa Chama na serikali kuyatafakari na kuchukua hatua NI Kama yafuatayo.

Moja, maridhiano ya kitaifa.

Mbili, kuufufua mchakato wa katiba mpya.

Tatu,tume huru ya uchaguzi japo itapatikana ndani ya katiba mpya.

Watanzania wote NI mashahidi Mambo mengi mabaya Kama mateso, mauaji,vipigo na vifungo vya kisiasa kwa wapinzani wa CCM kama lissu,azori,been saa8, n.k. hata wale waliokuwa ndani ya ccm lakini wakawa wapinzani wa JPM Kama wakina Nape, Membe, makamba's, kinana n.k shida, fedheha na tanuru la Moto walilopitishwa na mwendazake hayo yote yalitosha kuwa na maridhiano ya kitaifa kwani NI kweli watu wengi Sana waliumizwa.

Tusingeweza kusonga mbele Kama taifa wakati wananchi wengi wanalia kwa maumivu makali.

Maridhiano yataliponya taifa, yatarejesha matumaini ya wananchi kwa serikali na Chama,yataleta umoja wa kitaifa na hatimaye maendeleo ya haraka kwani waleta maendeleo NI wananchi ambao ni lazima wawe na upendo,kuthaminiana umoja,kuaminiana,kushirikiana, kuheshimiana na kupendana.

Katiba mpya NI mwarobaini wa matatizo mengi Sana ya wananchi, utatuepusha na kujirudia kwa hatari kubwa ya ubabe Kama wa mwendazake.

Itasaidia kuwa na utaratibu unaoendana na Aina ya siasa tuliyonayo tanzania na dunia kwa kipindi na wakati huu wa utandawazi.

Itasaidia kuwa na umoja wa kweli na itasaidia kuleta uwajibikaji wa viongozi.

Tume huru NI muhimu Sana hasa kwa kipindi hichi ambapo tunaelekea kwenye uchaguzi 2025.kama katiba mpya itakuwa bado kwani ninaamini chakato utachukua mda kidogo.

Ninashukuru Mungu na viongozi wa Chama cha mapinduzi na serikali kwa kuyatafakari na kuyasimamia Mambo haya ambayo NI muhimu Sana kwa taifa letu kwa wakati huu.

Pia ninavishukuru vyama vya upinzani hasa chadema chini ya kiongozi wao Mh. MBOWE kwa kuishauri serikali na CCM pia kusisitiza umuhimu wa agenda hizi kwa jasho na damu Tena kwa kutumia njia za kistaarabu kabisa.

Tunajenga taifa moja tusiparuane, na tusiumizane vyama vyetu vinaweza kupita au kufa lakini TANZANIA haitopita milele.

Nimeandika mafaKama mtanzania huru niliye acha ukada wangu pembeni kabisa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania, Mungu mbariki raisi wetu Mama Samia, Mungu ibariki CCM na Mungu vibariki vyama vya upinzani.

Ameeeen!!

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM ni wahuni tu na wabeba agenda za wapinzani kuzifanya za utekelezaji wa Ilani! Nami asiyejua kwamba mmeshindewa?? Angalizia mwendakwao alivyokuwa anawapa wa upinzani nafasi kwani huko ndani mwa CCM kulishaoza na ndicho kinawarejesha mamluki wote.
 
Hata wapinzani NI watanzania Wana haki ya kupewa nafasi ya uongozi Kama watavutiwa na Sera nzuri za CCM pia agenda ikiwa na maslahi na taifa bila kujali inatolewa na Nani kuipima, kuijadili na kutekeleza sio dhambi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na NI kweli hakuna wa kuitoa madarakani
Haya ndiyo mawazo ya mazuzu kama wewe mliohifadhiwa ndani ya hicho chama...hamuoni, hamfikiri wala hamsikii.

Ikitokea vyombo vya dola vikaacha kuipakata, CCM haiwezi kudumu madarakani hata kwa siku moja yenye saa 24.
 
Sioni sababu ya kukasirika kwa kiwango hiki, pia nyie mnaojiita upinzani hamna agenda yoyote yenye mashiko kwa wananchi na kisingizio chenu miaka yote NI CCM inakumbatiwa na dola na mkiambiwa mthibitishe mnabaki kulialia tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siri ni kuwafanya watz wengi wawe wajinga na masikini. Masikini hana analofikiria maisha nje ya shibe
 
Mashule yanajengwa Kila kukicha ili kuondoa/ kupambana na ujinga na wajinga hawawezi kuwa mtaji wa ccm
 
Back
Top Bottom