Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 1,997
- 7,552
Habari wakuu, kwa mara ya kwanza nilijenga nyumba 2 in 1 mkoa wa Morogoro, kwakuwa lengo ilikuwa kuzipangisha maana sikuwa nimetulia kimaisha nilizizungushia uzio wa matofali na kuziwekea mageti ili kila mpangaji atoke na kuingia kwa geti lake.
Baada ya mwaka na nusu nilihamishwa mkoa mwingine nikakaa kwa muda badae nikarudi Morogoro, sasa nimeona huu mkoa unanipenda kwa hiyo nimejenga nyumba ya kuishi nashukuru imekamilika.
Sasa kuna vihela nimevifuma sehemu wazo la kwanza lilikuwa kuizungushia uzio, ila leo nimepata wazo la kutumia hivyo vihela kuanza ujenzi kwenye kiwanja kingine maana nikipiga hesabu za gharama nilizotumia kujenga uzio wa matofali ya block+ urembo wa vyuma + mageti kwenye nyumba za wapangaji ni kama zinafanana na gharama za kuinua boma la nyumba nzuri tu.
Sijapanga kufuga wala kuwa na biashara nyumbani, nimeona nipande miti ya matunda na kivuli, ukoka na nitengeneze vi bustani vya kuvutia ila uzio naona ni kama ushamba fulani hivi.
Naombeni uzoefu wenu, je nimefikiri kwa usahihi au kuna ulazima wa kujenga uzio?