Njia 10 za kuongeza thamani ya ardhi yako

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Utangulizi.

Thamani ya ardhi yako inapoongezeka huathiri bei ya ardhi husika. Mara nyingi thamani 6a ya ardhi na bei yake huenda pamoja lakini sio lazima. Thamani inaweza kupanda na bei isiongezeke. Vilevile bei inaweza kuongezeka bila hata thamani ya ardhi kuongezeka.

Thamani ya ardhi hupanda kwa sababu kuu 2. Nazo ni;

✓ Mabadiliko ya hali ya masoko yasiyotegemea juhudi, maarifa na usimamizi wa mwekezaji husika.

✓ Mabadiliko ya thamani ya ardhi yatokanayo na juhudi za kiusimamizi za mwekezaji husika.

Katika uwekezaji kwenye ardhi, ni muhimu sana kuzingatia sababu namba 1. Sababu namba 2 inakuwa matokeo makubwa sana sana pale ambapo sababu namba 1 imehusika kuongeza thamani ya ardhi.

Njia 10 Za Kuongeza Thamani Ya Ardhi.

1. Kukifanya kifikike kwa urahisi.

Ardhi inayofikika inakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na ardhi isiyofikika kwa urahisi. Ardhi inatakiwa kufikika kwa usafiri wa miguu ya watu, magari, pikipiki, baiskeli, ndege, na kadhalika.

Vilevile ardhi ambayo hufikiwa na usafiri wa kisasa kama vile usafiri wa ndege au barabara za kiwango cha lami huwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo hufikiwa na usafiri wa baiskeli tu.

Ardhi ambayo ipo katikati ya mtaa ambapo gari, bajaji haviwezi kufika kwa urahisi inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi ambayo ipo mtaa mzuri ambayo inafikika kwa urahisi na usafiri wa magari na bajaji.

Kuongeza au kuboresha geti kwenye ardhi yako huongeza thamani ya ardhi yako ukilinganisha na ardhi ambayo haina geti ya aina yoyote. Kuongeza au kuboresha daraja sehemu ambapo haipitiki vizuri pia huongeza thamani ya ardhi yako.

2. Kuweka/Kuboresha huduma za jamii kama vile maji, umeme, mfumo wa taka, n.k
Ardhi ambayo ina huduma za kijamii huwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo haijafikiwa na huduma kama vile umeme, maji, miundombinu ya usafiri (barabara na viwanja vya ndege) na mfumo wa takataka laini na taka ngumu.

Kwa mazingira yetu ya Tanzania, huduma ya umeme imeonekana KUWA na mchango mkubwa kwenye kuongeza thamani ya ardhi kwa sababu maji sio changamoto kwa maeneo mengi ya mikoa yetu.

Kwa maeneo yenye historia ya ukame au huduma mbovu za maji, umeme unakuwa ni sababu ya pili ya kuchochea ongezeko la thamani ya ardhi yako.

3. Kupima ardhi yako (land survey)
Ardhi iliyopimwa inakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na ardhi ambayo haijapimwa. Upimaji wa pamoja wa ardhi unakuwa wa gharama nafuu sana ukilinganisha na upimaji wa ardhi kwa mtu mmoja mmoja.

Kitendo cha kupima ardhi kwa gharama nafuu ni sababu nyingine muhimu sana ya kuufanya uwekezaji wa ardhi yako uwe na matunda mazuri sana.

4. Kuweka uzio (fence) kuzunguka ardhi yako
Ardhi yenye uzio inakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo haina uzio kwa sababu zifuatazo;-

✓ Faragha kubwa kwenye ardhi yenye uzio.

✓ Ulinzi na salama mkubwa kwenye ardhi yenye uzio.

✓ Utulivu wa shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo na ufugaji kwenye ardhi yenye uzio.

Ardhi yenye uzio mbovu na mbaya kwa wengi inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi yenye uzo6wa kisiasa, uzio imara na uzio wenye mvuto kwa wengi.

Hitimisho
Mwekezaji yeyote anatakiwa kununua ardhi ambayo haina thamani ili aiongezee thamani yeye mwenyewe. Vipengele muhimu vya kuzingatia ni upimaji wa ardhi na mambo ambayo huchangiwa na serikali kuongeza thamani ya ardhi.

Haya unatakiwa kuzingatia kwa umakini sana kwa sababu bado tuna changamoto kwenye maeneo haya mawili. Ninaamini umejifunza mambo mazuri ya kufanyia kazi. Zipo njia nyingine nyingi za kuongeza thamani ya ardhi kulingana na mazingira ambapo ardhi yenyewe ipo.

5. Miliki au nunua haki za umiliki wa madini, gesi na mafuta
Kwa sheria ya nchi nyingi sana ikiwemo Tanzania, umiliki wa madini, gesi na mafuta unakuwa chini ya serikali. Hii ina maana kuwa endapo mafuta, gesi na madini vitaonekana kwenye ardhi yako ambayo una hati ya hakimiliki, bado utakuwa huna umiliki wa malighafi hizi ni mpaka uwe na kibali maalumu.

Ardhi ambayo ina hati ya umiliki wa mafuta, gesi na madini inakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na ardhi ambayo ina hati ya kawaida kutoka wizara husika.

6. Panda miti au mazao yenye thamani kubwa

Katika kila eneo kuna mazao ya chakula/biashara (hasa mazao ya kudumu) ambayo yanaongeza thamani ya ardhi. Panda mazao ya aina hiyo, na ardhi yako itaongezeka thamani yake maradufu.

7. Kuwa na mpango kutoka halmashauri
Ardhi ambayo inaeleweka mipango yake kutoka halmshauri na wizara ya ardhi inakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo bado haijapangiwa matumizi yake.

Baada ya kuwa na mipango hiyo, kisha ardhi inatakiwa kupimwa. Baada ya kupimwa unatakiwa kuwa na kibali cha ujenzi. Kibali cha ujenzi kinatakiwa kuombewa kwa kutumia ramani ya nyumba inayolipa sana.

Kwa Kuzingatia haya ardhi yako itakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo haina mipango kutoka halmshauri na wizara mpaka mwekezaji mmoja mmoja.

8. Kuondoa takataka za vimiminika, gesi na taka ngumu
Ardhi ambayo imekuwa ni sehemu ya kuhifahia takataka inakuwa na thamani ndogo sana ukilinganisha na ardhi ambayo ni safi na salama kwa ajili ya makazi au biashara za watu.

9. Badili matumizi ya ardhi yako
Ardhi ya matumizi ya makazi inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi ya matumizi ya makazi na biashara. Ardhi ya makazi na biashara inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi ya biashara tu.

10. Taja unayoifahamu wewe rafiki yangu

..............

Njia Nyingine Za Kuongeza Thamani Ya Ardhi.

Njia za kuongeza thamani ya ardhi zinaweza kuwa tofauti kulingana na mahitaji na mazingira husika. Njia hizo ni kama ifuatavyo:

✓ Kupima vipimo wa udongo.

✓ Kutumia ardhi kwa shughuli za mifugo yenye tija kama vile ufugaji wa kisasa wa samaki, kuku, ng'ombe na mbuzi wa nyama.

✓ Kuwekea mifereji ya kupitishia maji kipindi cha mafuriko au mvua za masika.

✓ Kusaini mkataba wa zaidi ya miaka 5 wa ukodishaji wa ardhi yako.

✓ Kupanda, kuboresha au kutunza bustani ya ardhi yako.

✓ Kujenga nyumba, kiwanda cha matofali, na kadhalika.

Darasa hili limeandaliwa na mbobezi majengo Aliko Musa. Karibu ujiunge na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM (TRT) upate masomo ya haya BURE. Waalike jamaa zako wako wawili tu nao wapate maarifa haya. Asanteni sana.

Whatsapp; +255 752 413 711

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

flyerdesign_26012023_011949.png
 
Umetaja ardhi kwaajili ya makazi, makazi & biashara, na biashara. Hakuna ardhi kwaajili ya kilimo?
 
Umetaja ardhi kwaajili ya makazi, makazi & biashara, na biashara. Hakuna ardhi kwaajili ya kilimo?
Ipo rafiki yangu,

Vingi sitaja kama ardhi kwa ajili ya maziko, majengo ya ibada na majengo ya huduma za kijamii kama zahanati, hospitali, n.k.

Asante sana kwa mchango wako.
 
Nilidhan ukishakuwa na ardhi itajiongeza yenyewe thamani kumbe ni jukumu langu kuiongeza!
 
Nilidhan ukishakuwa na ardhi itajiongeza yenyewe thamani kumbe ni jukumu langu kuiongeza!

Zipo Njia 2 Za Ardhi Kuongezeka Thamani Yake.

Hapa ninakushirikisha aina mbili za kupanda thamani ya nyumba zako za kupangisha. Nazo ni kama ifuatavyo;-

Moja: kupanda thamani kutokana na mbinu za mwekezaji (forced property appreciation).

Hapa nyumba huongezeka thamani yake kwa sababu ya mambo ambayo yanafanywa na wawekezaji kwenye nyumba pamoja na mazingira ya nyumba husika.

Mambo yanayoweza kuongeza thamani ya ardhi na majengo bila kujali hali ya soko mahalia ya eneo nyumba ilipo ni kama ifuatavyo;-

✓ Kufanya ukarabati wa urembo (cosmetic repairs).

✓ Kufanya ukarabati wa jengo lenyewe (structural repairs).

✓ Kupima ardhi kufautana sheria za matumizi ya ardhi kutoka serikalini (zoning laws).

✓ Kubadili matumizi ya ardhi kutoka matumizi ya aina moja kwenda aina nyingine ya matumizi (transfer of the right of occupancy).

✓ Kuongeza idadi ya nyumba ya nyumba vya kulala kwenye majengo.

✓ Kuongeza idadi ya vyoo binafsi katika nyumba husika (self-contained rooms).

✓ Kuongeza idadi ya vyumba vya kuogea (Bath rooms).

✓ Kugawanya ardhi katika vipande vidogovidogo.

✓ Kubadili umiliki wa ardhi kutoka kwa mtu/kampuni moja kwenda kwa zaidi wawili (kila mtu akiwa na hati yake ya umiliki wa ardhi).

✓ Vyumba vya apatimenti kuviuza kwa wawekezaji tofauti tofauti. Na kuifanya apatimenti hiyo moja iwe chini ya wawekezaji tofauti tofauti katika vyumba vyao vya kupangisha (rental units).

Kuna njia nyingi za kuongeza thamani kwenye majengo ya kupangisha ikiwemo ardhi.

Pili: kupanda thamani kutokana na soko mahalia (local markets) la nyumba husika (market property appreciation). Hii huchangiwa na sababu tofauti ikiwemo ukomo wa ukubwa wa ardhi (limited supply). Hakuna anayezalisha viwanja, na mashamba. Hivyo ardhi huzidi kuongezeka thamani mwaka hadi mwaka.

Kwa kutumia aina hizi mbili ni rahisi kufikia uhuru wa kifedha ukilinganisha na mbinu ya kununua na kuuza ardhi/majengo ndani ya mwaka mmoja.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom