Sintosahau nilivyosota miaka miwili bila kukutana kimapenzi na mama mtoto wangu

NINAENDELEA

N.B Nitajitahidi kuandika kadri niwezavyo maana naona kuna baadhi ninawekera na hizo nitaendelea...(tuko na majukumu mengine nje ya jamvi)

HATIMAE NIKAPATA CHOMBO KIPYA

Katika pita pita zangu kwenye mitandao ya jamii nilipata kumuona mdada mmoja hivi ni mrembo haswaaa na hakua mgeni machoni mwangu kwani ni mtu ambaye tunaishi sehemu moja. Ni muda sasa tulikua hatuonana hivo alikua amebadirika sana (kawa mkali tofauti na mwanzoni naanza kumuona).
Basi nikatupa ndoano yangu na nikabahatika kuipata namba yake ya simu. Siwezi sahau tarehe wala siku hadi muda napewa namba. Nilikua mazingira ya chuo (kwenye vimbweta) nasubiri muda niingie maktaba kula pindi. Kwenye saa 9 hivi alasiri ndo alinitumia namba yake kiukweli nilifurahi sana na nikamuahidi nikitoka kula pindi nitamtafuta.
Kwenye saa 11 jioni nilitoka na nilipofika magetoni nikakoga haraka baada ya kutuliza wenge nikaona huu ni muda wa kutupa karata yangu ya kwanza kwa huyu mrembo.
Nilimpigia simu na akaipokea haraka sana,nkamjulia hali na kujua pia anaendeleaje toka muda ule wa mchana. Hakua na nyodo wala mbwembwe za kina dada wa siku hizi, yeye alinijibu alinipa ushiriano wa kutosha kabsa.

Me: Mambo P
Mrembo: Poa tu nambie...
Me: Sina neno ila nimefurahi sna ulivyopokea simu yangu na kunikirimu vizuri.
Mrembo: Usijari mbona kawaida tu!
Me: Me Prince sijui unanikumbuka?
Mrembo: Sio kukukumbuka tu sema ninakujua vizuri sana.
Me: Ahaaa basi ni vyema.
Mrembo: Poa
Me: P Samahani sana kama nitakua nimekuboa kwa hili ninalotaka kukuambia.
Mrembo: Kwani kuna nini tena??
Me: Wala hakuna kitu.
Mrembo: Sawa nimekuelewa we nambie ila ni kama unajua kitanikera ni bora tu usinambie kabisa.
Me: Hapana siwezi kufanya hivo(kumkera)
Mrembo: Basi sawa
Me: Bila kupepesa wala kufumba macho P nimetokea kukupenda sana na ningefarijika zaidi endapo ningalipita wasaa kwa kua na wewe katika hiki kipindi kifupi cha maisha yangu.
Mrembo: Na X je??(alikua anamjua yule bibie aliyeenda Dar kua nilikuaga natoka nae)
Me: Mmmh!! Yule bhana mambo hayakwenda sawa hivyo tumeshaachana!
Mrembo: Kisa nini tena hadi mkaachana na mlivyokua mnapendana vile?
Me: Naona haikua riziki yangu tu ndo mambo yalienda mlama.
Mrembo: Ahaa basi sawa
Me: Umeniacha njia panda sasa P.
Mrembo: Haya nimekubali!
Me: Kweli??
Mrembo: Ndio ni kwel kabsa.
Me: Asante sana P ninashukuru sana kwa hii nafasi uliyonipa me nakuahidi tu furaha tele katika maisha yangu
Mrembo: Nitashukuru sana endapo utasimamia maneno yako
Me: Ni kweli tena sintokuangusha kabisa!
Mrembo: Haya nitaona
Me: Karibu sana kwenye moyo wangu upate tulizo la roho yako!
Mrembo:(akacheka sana) ila nyie wanaume bhana
Me: Wanaume wamefanyeje?
Mrembo: Mkiwa mnamtaka mtu hata kwa kutimiza haja zako tu si hua mnatuambiaga kua oooh nakupenda sana mara sijawahi kumuona mwanamke mrembo kama wewe ila mkipata mnachokitaka mnakimbia...
Me: Hao ni hao hao mimi ni mimi mama angu kwani sijaja kwako kwa ajiri ya kuwawakilisha wanaume wote duniani kwani kila mtu yukogo na namna ya interest zake akiwa anamtaka mwanamke.
Mrembo: Mmmh!! Nyie ni waongo sana mjue??
Me: Waongo ni hao mimi nimenyooka kama mchele wa Kyela sinaga hizo mambo mimi!
Mrembo: Yangu macho
Me : Asante sana P asante mnooo na Mungu atufungulie njia sahihi yenye mapito yaliyo mema!
Mrembo: Ameeen!

Kuanzia hapo ndo nikaanza mahusiano na mwanamke mwinginie ingawa yeye alikua nasoma chuo kilichopo mbali kidogo na mkoa ninaosomea.
Yule bibie mwingine nilikua nachati nae vizuri tu. Kuna siku nilikaa na kutafakari matendo aliyonifanyia huyu mwanamke (kwani yule jamaa nilapata namba za simu na nilimpigia na yeye akasema vile vile kua yule bado ni manzi yake na hawajahi kuachana, na hata hiyo siku anakuja mjini alilala kwangu mbona??).
Asubuhi moja nilimpigia simu akasema anaenda kanisani hivo akitoka tutaongea. Alivyotoka tu akanipigia. Sikua na muda wa kupotezea mimi nilimuambia kua kuanzia leo mimi na yeye basi yaani asithubutu kuyasogela maisha yangu kwani habari zake zote ninazo mkononi hivyo hana la kujitetea tena)
Kama kawaida yake alifoka sana. Mi nilimsililiza tu na nikaa kmya ila ipomaliza kuongea nikamwabia aingie whatsup. Alipoingia tu nilimtumia zile picha pamoja na screenshots za mazunguzo na yule jamaa akimwambia kua ataenda kulala kwake baada ya sherehe.
Alinipigia simu huku akiwa na wenge la hatari akaniomba msahama na kunambia huyo jamaa ni kweli ilitokea hivyo ila sasa ameamua kabisa kua na mimi na hawezi rudiana na huyo jamaa tena kwani anachofikiria ni maisha yake tu basi.
Msimamo wangu ulikua ni ule ule kwamba mimi na yeye ni basi. Akanambia ananipa wiki mbili nijifikirie juuu ya maamuzi yangu ili nisije jutia baadae.
Jibu langu lilikua ni."hata kama nitaishi miaka 1000 kwenye hii dunia, jibu lang halitobadika hadi naondoka duniani.
Alilia sana ila me nlikua kama naangalia Isidingo "The Need" maana sikua nampa attention tena.
Nilikata simu nikaendelea mamb yangu Hiyo siku alipiga simu sana wala sikuitafuta tena no yake..

Me na baby mama wangu mpya mambo yalikua niya moto sana.
Zilipita kama siku 5 hivi yule manzi wangu wa Dar alinipigia simu huku alikilia kwa uchungu sana kwani aliona nimemuweka dp baby wangu mpya(walikua wakifahamiana vizuri sana).
Aliniomba namba zake ampigie waongee kama wanawake ili walimalize hilo jambo la kichukuliwa mwanaume na mwanamke anayefahamiana naye.
Nilikaa chini nikatafari juu ya kumpa no ila jibu lilikuja ni NO kwani nilihofia angeweza kuongea uongo ambao ungepelekea mimi kupigwa chini.
Nilichomwambia tu kua nitampigia na wewe nitakupigia baadae halafa nitawaweka kwenye CONFERENCE
Ili kila mtakalo ongea na mimi nisikie na endapo utaongea maneo ya kichinganishi nitakata simu na hautoongea nae tena.
Alikubali na niapiga simu na nikawa nawasikiliza:
X: P mambo vipi?
P: Safi tu za kwako?
X: Ni njema kabisa
P: haya nambie maana nimeambiwa ulikua unaniulizia sana
X: Ni kweli niko na shida sana na wewe na shida yenyewe ni kuhus Prince.
P: Shida gani hiyo?
X: Ni kuhusu Prince
P: Sawa nakusikiliza...
X: Hivi P kwani ulikua hujui kama Prince ni mpenzi wangu?? Mimi na yeye tuligombana tu na nipo tayari kuzitoa tufauti zetu ili tuendelee na mapenzi yetu hivo ninakuomba uniachie Prince wangu kwani ninampenda sana.
P: Sawa mi sina neno kazi ipo kwa Prince
X: Hivi Prince kati ya mimi na P unampenda nan hasa?
Me: Ninampenda P, ninampenda sana!
X: Tafadhari P usinifanyie hivo yaliyopita si ndwele tugange yajayo baba angu!!
Me: Kama imeshindikana kurudisha masaa nyuma basi ujue mimi siwezi kurudi kwako abadani!! Naomba uniache na usinisumbue tena!!!
X: Akaanza kulia na alilia hadi kamasi zikawa zinatoka kwani nilimiskia akipyenga mara kadhaa wakati akilia.
Sikupindish maneno hata kidogo mi nilimueleza hali halisi na nilipoona anazidi kulia nikamwambia nitaikata simu muda si mrefu akiendelea kulia.
Alipunguza kulia ila akanambia," kama mimi X mimi nilikutoa huko kusikojulikana hadi P akakuona kua unafaa kua nae basi Mungu atanilipia, ila tu P nikuahidi kua hamtadumu hata miezi 6 na Prince kwani tabia ya kutorizika na mwanamke pia kama mtadumu zaid ya hiyo miezi 6 labda mimi sio X. Akakata simu huku bado analia

BAADA YA MIAKA MIWILI PENZI LANGU JIPYA LIKAINGIA DOSARI

NITAENDELEA
 
We **** nini tumechoka kusubiri kila siku stori zako za kutunga watu tuna mambo mengi ya kufanya sio tunakaa tusubiri hadi uchapishe tena kama vipi wewe andika maelezo ya kutosha umalize funga uzi full stop usiwe na tabia za kike kidogo itaendelea ebhana eeh unatuchosha bhana uzi wenyewe una karibia wiki 2 na hamna cha maana wala cha manufaa yoyote kwetu zaidi tu ya mapenzi yako binafsi na kujisifia uongo tu badidirika bhana tumechoka kusubiri kila siku stori za kipumbavu ambazo hazierimishi kima wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Qoumah nini tumechoka kusubiri kila siku stori zako za kutunga watu tuna mambo mengi ya kufanya sio tunakaa tusubiri hadi uchapishe tena kama vipi wewe andika maelezo ya kutosha umalize funga uzi full stop usiwe na tabia za kike kidogo itaendelea ebhana eeh unatuchosha bhana uzi wenyewe una karibia wiki 2 na hamna cha maana wala cha manufaa yoyote kwetu zaidi tu ya mapenzi yako binafsi na kujisifia uongo tu badidirika bhana tumechoka kusubiri kila siku stori za kipumbavu ambazo hazierimishi kima wewe

Sent using Jamii Forums mobile app



Sent using Jamii Forums mobile app
 
We **** nini tumechoka kusubiri kila siku stori zako za kutunga watu tuna mambo mengi ya kufanya sio tunakaa tusubiri hadi uchapishe tena kama vipi wewe andika maelezo ya kutosha umalize funga uzi full stop usiwe na tabia za kike kidogo itaendelea ebhana eeh unatuchosha bhana uzi wenyewe una karibia wiki 2 na hamna cha maana wala cha manufaa yoyote kwetu zaidi tu ya mapenzi yako binafsi na kujisifia uongo tu badidirika bhana tumechoka kusubiri kila siku stori za kipumbavu ambazo hazierimishi kima wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio usubiri sasa
 
We **** nini tumechoka kusubiri kila siku stori zako za kutunga watu tuna mambo mengi ya kufanya sio tunakaa tusubiri hadi uchapishe tena kama vipi wewe andika maelezo ya kutosha umalize funga uzi full stop usiwe na tabia za kike kidogo itaendelea ebhana eeh unatuchosha bhana uzi wenyewe una karibia wiki 2 na hamna cha maana wala cha manufaa yoyote kwetu zaidi tu ya mapenzi yako binafsi na kujisifia uongo tu badidirika bhana tumechoka kusubiri kila siku stori za kipumbavu ambazo hazierimishi kima wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimecheka hadi kidogo nidondoshe cm yangu😂😂😂😂😂hakika umejua kunifurahia mkurugenzi
 
Nilimuachia Mke wangu nyumba... Kuna Uzi niliweka humu.... Watoto nikawa nasomesha na nyumba nimemuachia ... Nikaanza upya.... Acheni tu...makosa yake sikupeleka kwetu Wala kwao.... Ila tu nikahama nyumbani.... Ndio alijua Nini maana ya "Mume" na "Bwana"... Tumezaaa watoto wa4 ..Mkubwa wa kiume wengine wa kike.... Nasomesha wote shule za kulipia .... Ni mwezi wa nane Sasa .... Anaomba tukapime ......nshamwambia naishi Kwa ajili ya watoto.... Sio wewe... Najitafuta Bado maana hata kama sio wa kwangu.... Maana alichonifanyia .. nyieeeee.... Bado najitafuta.... Uzuri watoto wote nimewalea tangu wanazaliwa.... Ila wanawake Mungu anawaona.... Hawa watoto naamini ni wangu hata Kwa nililo mkuta anafanya.... Ameshajaribu kujiua mara mbili tunamuwahi...
Duh!....akijiua halafu hujasamehe hutapata amani.
 
Back
Top Bottom