Sina furaha, ninatamani kurudi kwa wazazi wangu

I guees mke wa bro havutiwi kuishi kwake, yani kila unachofanya it's like anachunguza, and nahic anafurahi nicpofanikiwa kwa chochote, and anatuona tunashida sana my be tunamtegemea mume wake, and huwa wana ni discuss akiwa na ndugu zake especially Dada na wadogo zake wa kike na mamake, coz wao wote wamefanikiwa na wanakaz bt kwetu only ma bro ndo amefanikiwa ndugu zangu wa2 wamemaliza degree wapo home to jobless, mm majanga siwez kuendelea na chuo cz vigezo walivyoweka vya GPA ya 3.5 mm sina, yani naona maisha magumuuu

inferiority complex
 
Pole mkuu,
Kumbuka mke wa kakako amekujua kupitia kwa kakako yeye na ndugu zake huna undugu naye. Ili ufanikiwe katika maisha yako ni lazima umtumikie huyu mama, thats the best and the easiest way, however, its not the only way.
Jamii ya Watanzania walioko makazini sasa hivi wengi wamepitia haya mazingira ya kuishi kwa ndugu mwingine asiye mzazi pamoja na mimi.

Ukiamka asubuhi badala ya kukaa kwenye kochi unaangalia tv ukisubiri housegirl akuletee chai msaidie kufanya usafi piga hata deki ikiwezekana, osha vyombo na usafi wa nje. Ukisha kunywa chai nenda Library tembea hata kwa miguu ukasome magazeti na vitabu, research kuhusu vyuo vinavyoweza kukupokea kwa matokeo yako.

Ukirudi kula halafu kafanye mazoezi hata ya kuzunguka uwanja jua likizama rudi watafute watoto wake(watoto wa kakako) ukae nao as if u care for the children hata kama ni kuwalisha, do it.
Usimwambie kakako shida yoyote mwambie yeye shemeji, hata nauli mwombe yeye.

One thing you have to remember, kakako anakufanyia msaada sio lazima ukae kwake, kwahiyo tafuta njia inayoweza kukufanya wewe uendelee kukaa kwake. Ukitaka kuwasiliana na kakako private mfuate ofisini ongea naye shida zote, huko unaweza kumwomba nauli ukarudi home. Usimwambie kuhusu hizi changamoto, ashajua au alishaambiwa mengi sana kuhusu wewe na hapo anakuchunguza, be very careful.

Jaribu haya kwanza halafu utuletee mrejesho next time.
 
Nadhani umepata ushauri mzuri kutoka jamaa hapa JF. Wewe shikilia lengo lako na jua uko hapo kwa muda ili kutimiza lengo lako, usijitie mawazo na kudhania mambo wakati mwingine sivyo unavyofikiria.
Ukituliza akili na kuweka malengo na kupata ushauri hapo DSM kuna fursa Zaidi kuliko mikoani na unaweza kufanikiwa.
 
I guees mke wa bro havutiwi kuishi kwake, yani kila unachofanya it's like anachunguza, and nahic anafurahi nicpofanikiwa kwa chochote, and anatuona tunashida sana my be tunamtegemea mume wake, and huwa wana ni discuss akiwa na ndugu zake especially Dada na wadogo zake wa kike na mamake, coz wao wote wamefanikiwa na wanakaz bt kwetu only ma bro ndo amefanikiwa ndugu zangu wa2 wamemaliza degree wapo home to jobless, mm majanga siwez kuendelea na chuo cz vigezo walivyoweka vya GPA ya 3.5 mm sina, yani naona maisha magumuuu
Mamii,sisemi uongo au utani,kama ni 3.5 million tu mimi nipo tayari kukusaidia ukasome,ingawa sikujui,ila unihakikishie utanilipa kwa awamu ukianza kazi.
 
Hapo kazi ipo, kama we ni me basi mtongoze shemeji yako awe anakupa burudani ukifanya hivyo utaona raha kuishi happ
Sasa wewe Angelaone,huo ushauri kwa nini usianze nao wewe humu jukwaani?ili uishi kwa amani humu jukwaani nipe papuchi na mimi nitakupa amani au vipi?
 
Home sweet home, hata kama nikilala na njaa poa tu mradi nna amani tele...Kwanini uwe mtumwa aisee?
Maliza kozi rudi alipojenga babaako mkuu!
Hakuna kitu nachukia kama kukaa kwa mtu, yani huwa nahisi kama muda wote napumulia kwenye tundu la sindano... nahisi hata pumzi inakata.
Huenda nawe ukawa type yangu.
 
Hata kule Libya wanafunzi waliandamana kumpinga Gadafi kwa kukosa Parking za Magari yao sasa nahisi na ww ni miongoni mwa Walibya
 
Mbona maandishi yako hayaendani na mtoto wa kiume? Halafu mtoto wa kiume unawaza kunenepa!!!!!, kahhh.... Umri wa miaka 25 bado unadeka!!!! Aaaaaaaahh broo ebu acha hizo bwana. Kwa umri wako ilitakiwa uwe umeshaanza kujitegemea, hata kwa kuziba pancha za magari coz wengi huanzia maisha huko.
 
Back
Top Bottom