george aloyce
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 1,177
- 1,827
Naitwa John niko kwenye ndoa mwaka wa 9 na tumejaaliwa na mke wangu watoto wawili. Nilikuwa muajiriwa lakini niliacha kazi na kuanza biashara zangu binafsi miaka miwili iliyopita. Kiukweli mke wangu ni muajiriwa wa Serikali na kipato chake ni kikubwa kuliko mimi.
Msema kweli mpenzi wa Mungu tangu nilivyoacha kazi mke wangu kwa asilimia kubwa ndiye amekuwa akiibeba familia kwa mambo mengi yanayohusu pesa kuanzia nyumbani mpaka kwenye ada za watoto shule.
Nilichogundua kwa miaka hiyo miwili amekuwa haniheshimu hata kidogo yaani amekuwa akionesha dharau kubwa saa nyingine mpaka mbele za watoto wangu lakini nimekuwa nikimvumilia.
Kilichoniudhi kuliko vyote ni Jumamosi hii alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na nilipomuhoji akaniambia nikae kimya kwani wanaume wenzangu wenye hela zao ndio waliomnunulia pombe na ndio wanaompa hela za kutunza familia nikiwemo mimi.
Jambo hilo liliniuma sana na naomba nikiri kusema nililia kwa masaa mawili peke yangu. Cha ajabu asubuhi nilipomkumbusha akaniambia nimsamehe kwani zilikuwa pombe tu na hatarudia tena.
Naomba ushauri nifanyeje? Natamani kuondoka nikapange nyumba nyingine lakini watoto wangu sijui watanichukuliaje.