Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Haya sasa ni manyanyaso aseee! Ila poa hata mimi najifunza kutunga tu!! Haiwezekani mwamba atufanyie hivi au kuna mjinga kaharibu nini🥺🥺
 
Jamaa sijui shida nin?
Muzeee fanya tumalize hii sasa kwann unaivuta hivi na ipo mwisho aroooh.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MRUNZI: SINGANOJR


Mono no aware


SEHEMU YA 694.
Ilikuwa ni kama Roma alivyokuwa ametegemea , kwani ile anafika katika makazi ya Mzee Sharif yaliopo Bagamoyo aliweza kukuta vurugu zilizokuwa zikiendelea.
“Ndio mmeanza vurugu?”Aliongea Roma mara baada ya kutua kwenye bustani ndani ya jumba hilo ambalo lilitumiwa kama makazi ya muda ya Mzee Sharif mara baada ya yale ya Kilimanjaro kuharibiwa.
Dakika hio watu waliokuwa hapo ndani waliweza kusikia sauti wanayoifahamu na mara baada ya kugeuka waliweza kumuona Jini Imrah na Maimuna na palepale wote kwa hofu walipiga magoti chini kusujudu.
Walikuwa wakijua Maimuna na jini Imrah walishakufa na wengine wote kutokana na miili yao kutoweza kupatikana , lakini ajabu sasa muda huo wamerudi wakiwa hai hivyo kila mmoja alishikwa na woga na yale mawazo ya kutaka kupata madaraka yalikufa palepale.
Lazima kuwa na hofu kwani walikuwa ni binadamu tu huku wao wakiwa ni majini wenye nguvu.
Roma aliishia kujichekea ndani kwa ndani na kujiambia kumbe kujifanyisha mtu mwingine kuna raha yake , kama sio kuwa na mipango mingine alijiambia angekaa hapo hapo kwa muda kwanza kujionea.
Dakika ileile aliwaambia kwamba yeye kama jini Imrah amemuokoa Maimuna kutoka kwenye mikono ya Roma Ramoni na kwanzia siku hio angekuwa kiongozi wa ukoo pamoja na kuongoza imani yote ya kikafara.
Maimuna ambaye ni Tannya aliweka msimamo wake juu ya mpango wa kupangua familia hio ki uongozi kutoka ngazi ya chini mpaka ya juu.
Tannya alihitajika kufanya hivyo ili kuhakikisha anaingiza watu wake ambao wangeweza kurithi nafasi za wafuasi watiifu na kuweza kupata taarifa zote juu ya familia hio kama misheni aliopewa na mfalme Pluto.
Roma mara baada ya kumalizana na swala hilo palepale aliondoka na kurudi kwenye muonekanno wake wa kawaida na moja kwa moja akafanya safari ya kwenda Los Angeles-Marekani.
Hakuwa ameonana na Christen kwa muda mrefu kidogo na kwasababu alikuwa anataka kumuuliza kuhusu kilichotokea usiku hivyo aliona amtembelee.
Wakati anaingia Los Angeles ilikuwa ni giza bado na kwa kutumia uwezo wake aliweza kugungua Christen alikuwa ndani ya jumba lake.
Kufumba na kufumbua Roma alikuja kutua kwenye balkoni katika floor ya pili ndani ya nyumba ya Christen , alikumbuka mara ya mwisho alivyofika kwenye nyumba hio aliweza kupata huduma kutoka kwa kijakazi wa Christen na alijiuliza kama bado yupo.
Upande wa Christen na yeye alikuwa ashahisia ujio wake na alifungua mlango na kutoka nje akiwa katika mavazi ya kulalia na kumfanya kuzidi kuonekana mrembo.s
“Hades nilijua utanipigia simu mchana , naona umesubiri mpaka giza lilipoingia na kuja kunifanyia surprise”Aliongea
“Nimechelewa , nilikuwa bize na mambo mengine..”Aliongea Roma na palepale alisogeza kiti karibu na kuketi.
“Kama ulitegemea ningekutafuta basi itakuwa sio mimi tu ninaepatwa na hizi hisia, hebu niambie ni nini kinaendelea , kwanini nguvu ya uungu ndani yangu ni kama imeongezeka , ninaweza kuhisia hata saivi bado inaongezeka taratibu sana”
“Such spoilsport , I’ m wearing this in front of you and yet you are talking about things like this…”Aliongea na paleplale alimsogelea Roma na kumkalia huku akimshikilia shingo kimadaha.
Roma alichoweza kuhisi ni marashi kutoka kwa mwanamke huyo , huku kidevu cha mrembo huyo kikiwa kimegusana na kifua chake.
Uzuri wa Christen pamoja na u’superstar’ ni sifa ambazo mbele ya mwanaume rijali hawezi kuepuka mtego wake lakini kwa bahati mbaya au nzuri Roma alikuwa na uwezo wa kujizuia.
“Kwa staili hii sidhani kama upo tayari kujibu maswali yangu, Christen unanifanya nione kuna kitu muhimu sana mnanificha”Aliongea Roma lakini Christen alikuwa akijisugua sugua mapajani ili kuamsha mhogo wa Roma.
Mara baada ya kuhisi ugumu ukiongezeka ndani ya suruali yake alimwinnamia na kumnong’oneza.
“Babe unaonaje tukifanya hivi , kama utakidhi haja zangu nitakuambia ukweli wote, nadhani unajua vizuri sijawahi kufanywa nikiwa na huu mwili na itabana vizuri tu”
Maneno ya Christen yalimfanya mapigo yake ya moyo kwenda kasi na kumlaani kwa kuongea maneno hayo ya kiuchokozi bila aibu na kuamsha ukichaa wake.
Kama ni mwanaume mwingine ambaye upo katika nafasi ya Roma angeishikilia fursa hio kwa mikono yote, kulikuwana wanaume wengi sana ambao wanajaribu kutoka kimapenzi na mwanamke huyo lakini wote wanaambulia kupigwa vibuti.
“Najua kuna wanaume kibao ambao wanakutaka na wanaweza kukidhi matamanio yako”
“Nilishakuwa na wanaume tofauti tofauti kila nilipobadilisha mwili lakini tokea nibadili huu mwili wewe ndio mwanaume ambaye umekidhi vigezo vangu”
“Asante kwa kunisifia lakini naomba niwe mkorofi kukukataa, unaonaje ukiniambia ukweli na kisha nikakidhi matamanio yako zaidi ya mara mbili”
Roma alishajua kama angetaka kuanzisha mahusiano na Christen jambo hilo lingetokea miaka mingi iliopita , isitoshe sio watu ambao walikuwa wakifungwa na sheria za kiimani.
Wote wana roho ya uungu ndani yao hivyo miili wanayotumia ni kama nyumba tu ya kutumia kwa muda tu.
Kilichomfanya Roma kutotaka kujihusisha kimahusiano na Chriten ni kutokana na mrembo huyo kuwa na hisitoria na Hades wa Zamani licha ya kwamba hakuwa akijua maelezo yote juu ya mahusiano yao.
Uwezo wao wa kuhamisha ‘ Consciousnes’ zao kutoka kwenye mwili mmoja kwenda mwingine ilitegemeana na nguvu ya ki uuungu ndani yao, Hades wa Zamani alikuwa ameshapoteza nusu yake mara baada ya kumrithisha Roma hivyo asilimia za kujivika mwili mwingine aliamini ingekuwa ngumu.
“Hades unachukiza mno , yaani najilengesha kwako lakini bato tu unanikataa , hivi nakosa nini ambacho mkeo na wapenzi wako wanacho mimi sina?”Aliongea huku akijifanyisha amekasirika.
“Aphrodite acha mambo yako bwana , sisi ni mrafiki na nakujua vizuri hivyo acha kuficha ukweli na niambie nini kinaendelea”Aliongea Roma huku muonekano wake ukiwa na hali ya usiriasi ndani yake.
Christen alitoa pumzi nyingi na kuzishusha na kisha alisimama na kumzodoa kwenye paji la uso kama vile hajaridhishwa na maneno yake na palepale alisimama kwenye uzio wa balkoni na kuangalia mataa ya jiji la Biverly hills.
“Ni moyo wa Gaia , Athena ameshaufufua”Aliongea bila ya kugeuka.
Roma alikuwa ashaotea muda mrefu, hivyo hakushangaa sana lakini bado hakuwa akijua moyo huo unahusu nini na athari zake ni zipi.
“Kufufuka kwa huo moyo inamaanisha kwamba mtaweza kurudiwa na nguvu zenu si ndio? , nakumbuka kule Korea Kusini Stern , Alice na Athena walivyokuwa wakiongea walitaja kuhusu huu moyo wa Gaia na kusema utaleta matokeo makubwa kwa dunia yote , nakumbuka pia ni kama walikuwa wakibishana na kusema ni kitu ambacho kitaharibu ulimwengu lakini wakati ule hawakutaka kunipa maelezo kabisa nnilipowauliza , kwanini wewe usiniambie kila kitu”
“Sidhani kama kuna maelezo yaliobakia ambayo ninaweza kukupatia , hata wewe mweneyewe umeweza kuhisia kufufuka kwa moyo wa Gaia, hivyo ni kweli nguvu zetu zitarudi taratibu taratibu na Athena mpango wake ni kufufua ndugu zetu walioptea na tayari ashafanikisha hatua ya kwanza”
“Ana mpango gani au anataka kuua binadamu kama alivyofanya miaka elfu ishirini iliopita mara baada ya kufeli kwa mpango wenu wa kutawala dunia?”
“Kusema ukweli sijui chochote , Athena hatabiriki na isitoshe hata kama tunajua anachopanga kufanya hatuna huo uwezo wa kumzuia”Aliongea na kumfanya Roma kutulia kimya.
Ukweli ni kwamba Athena uwezo wake ulikuwa wa juu kabisa na Roma alijua hata kama nguvu zake za kijini zimerudi inawezekana bado asifanikishe kushindana nae , isitoshe kufufuka kwa Moyo wa Gaia inamaanisha kwamba na nguvu zake pia zinaongezeka
Dakika ileile Roma alitaka kuuliza swali lingine simu yake iliita na alipotoa na kuangalia anaepiga ni babu yake Afande Kweka na alipokea palepale.
“Wewe mtukutu hebu rudi Tanzania haraka na tukutane Dodoma”Sauti ya kibabe ilisikika.
“Nini kimetokea Mzee?”Aliuliza Roma kwa msahngao.
“Haha… unafikiri kwa ulichokifanya utaachwa kirahisi , umemuweka baba yako katika wakati mgumu na Master namba Moja anataka kukutana na wewe kupitia yeye’Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
“Unamaanisha nini Master Namba moja anataka kukutana na mimi kupitia yeye?”
“Rudi kwanza na tukutane Dodoma ndio tutaongea vizuri”Aliongea na palepale simu ilikatwa.
“Christen natakiwa kurudi?”
“Inaonekana upo matatizoni?,GoodLuck Hades”
“I guess we’ll have to go with the flow for Gaia’s Heart , I know you didn’t tell me everything but I hope no matter what happened in the future we‘ll still be friends”Aliongea Roma akimwamia Christen kwamba anajua hajamweleza kila kitu lakini haijalishi ni nini kitatokea baadae bali wataendelea kuwa marafiki.
Christen alitaka kuongea neno lakini aliingiwa na uzito kwenye midomo yake na kuishia kutoa tabasamu la kuashiria maana na palepale Roma alipotea mbele yake.
Aliishia kuangalia upande ambao Roma amepotelea na kuishia kuvuta pumzi nyingi.
“Roma wewe ni msahaulifu sana nishakuonya mwanzo usije kumruhusu Athena kuupata moyo wa Gaia, eti marafiki wewe ni mjinga sitaku kuwa rafiki yako mimi , nataka urudiwe na ufahamu wako wote halisi ya ki’uungu na tukutane kwa mara nyingine , nikwambie maneno nilioshindwa kukuambia siku zote, Nakusubiri Hades”Aliwaza Chriten.
******
Wakati Marekani ikiwa ni usiku Tanzania ilikuwa ni alfajiri na Rufi bado alikuwa kwenye usingizi mzito sana.
Dakika hio Bi Wema alikuwa tayari amekwisha amka na kuingia katika chumba cha binti yake na kuishia kutingisha kichwa kwa kusikitika mara baada ya kuona vifaa vya tarakishi ambavyo vimezagaa ndani ya chumba chake bila mpangilio , tarakishi bado ilikuwa inawaka na namba namba ambazo hakuwa akizielewa zilionekana.
“Sijui kwanini anapenda mambo kama haya kama vile sio mwanamke , lakini nadhani ni vizuri kuwa na hobi inayomfanya kuwa bize kwani hana uwezo wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi kama wenzake”Alijiwazia Bi Wema kwenye kichwa chake na kisha alisogea na kwenda kukaa kitandani na kuanza kumtingisha Rufi.
“Rufi amka kumekucha , tunapaswa kujiandaa mapema tuanze safari”Aliongea Bi Wema.
“Mama nataka nilale kidogo, nimechoka”Aliongea Rufi kivivu na kumfanya Bi Wema kumwangalia binti yake na kutoa tabasamu ,kuna muda alijiambia ni kama miujiza kumwamsha binti yake kama hivyo.
“Rufi mwanangu tutachelewa kufika jamani”Aliongea Bi Wema.
Siku hio Bi Wema alipaswa kwenda kumtembelea mdogo wake huko Pangani mkoani Tanga.
Mwanzoni Bi Wema alijua hakuwa na ndugu kabisa lakini miezi michache aliweza kutafutwa na mwanaume aliejitambulisha kama mdogo wake , yaani mtoto wa baba yake kwa mama mwingine.
Bi Wema mara baada ya kupata taarifa hio alifurahi sana kwani ilimfanya sasa kujua alikuwa na ndugu.
Sasa mara baada ya kurudi kwa Rufi alitaka kwenda kumtembelea mdogo wake kwa mara ya kwanza na siku ambao walipanga kwenda huko ni siku hio asubuhi asubuhi ili kuwahi kufika ndio maana alikuwa akimwamsha alfajiri kwa ajili ya kujiandaa na kuanza safari.
Dakika hio wakati Bi Wema akimuamsha Rufi upande wa balkoni alikuwa amesimama mwanaume mtanashati mno alievalia joho la rangi nyeupe akiangalia ndani ya chumba cha Rufi na macho yaliojaa kejeli.
Licha ya kwamba dirisha kutokea Balkonni lilikuwa na pazia lakini alikuwa na uwezo wa kuona kila kitu kinachoendelea ndani.
Na wakati hio ndio ambao Bi Wema alikuwa akimuamsha Rufi kwa ajili ya kujiandaa kuanza safari.

















SEHEMU YA 695.
Bi Wema mwili wake ulihisi kumsisimka ajabu na ilikua ni kama amehisi hatari na kwa haraka alimuacha Rufi aliekuwa akijifikicha macho na kukimbilia upande wa dirisha na kusukuma pazia na hapo ndipo alipojikuta ni kama vile yupo ndotoni mara baada ya kukutana na sura ambayo ilikuwa ikimwangalia kwa tabasabu , manusura apige yowe lakini kwa hali ambayo hakuelewa sauti ilishindwa kumtoka kabisa.
Rufi ambaye alikuwa bado na hali ya usingizi alijikuta akigeuza macho kumwangalia mama yake na hapo ndipo alipoingiwa na ubaridi mara baada ya kuona sura anayoifahamu.
Alikuwa ni jini Lahani kaka yake na XiaoXiao ,alikuwa na muonekano ambao haukuashiria amani na ulimfanya Rufi kuingia na woga wa hatari mno
Wakati Rufi akiwa katika hali ya mshangao upande wa Lahani alisogea upande wa mlango wa Aluminium wa na kuslide mlango kwenda kulia na kufanya upepo kuingia ndani pamoja marashi makali.
Dakika ileile ni kama sasa Rufi akili ilimkaa vizuri na aliruka kutoka kitandani na kumsogelea mama yake kwa hofu.
“Mama , ondoka , ondoka haraka, kimbia kwenda nje”Aliongea Rufi akijaribu kumsukuma mama yake kutoka ndani ya chumba chake.
Bi Wema dakika hio hio alijua wapo katika hatari na aliishia kumkumbatia Rufi huku akimwangalia yule mwanaume mwenye uso wa kuvutia akingia ndani bila wasiwasi.
“Rufi unamaanisha nini , huyu mwanaume ni nani.. Rufi acha kunisukuma jamani”Aliongea Bi Wema akijaribu kushindana na Rufi
“Haha..Kwahio huyu ndio mama yako mzazi , mbona hamfanani hata kidogo”Aliongea Lahani huku akiwa amesimama akimwangalia Rufi kwa kejeli anavyohangaika kumsukumia nje mama yake.
Dakika hio hio vivuli vilitua nje ya Balkoni na Rufi mara baada ya kugeuza macho aliweza kuwajua wote , wa kwanza alikuwa ni Xiao Xiao na wa pili ni mwanaume aliekuwa akimjua vizuri alikuwa ni Mlinzi wa Lahani yaani Mzee Lao.
Wote hao walikuwa ni majini , Lahani alikuwa jini na huyo mzee alikuwa jini vilevile kasoro XiaoXiao ambaye alikuwa ni nusu jini kama ilivyokuwa yeye.
Sasa kitendo cha Rufi kumuona XiaoXiao alijua kabisa yeye ndio amemuuza na alimpiga jicho la hasira.
“Kumbe ni wewe ulieniuza , nilikuaini na hata nikamuomba mpenzi wangu kukuacha hai lakini haya ndio malipo yake>”Aliongea Rufi kwa hasira.
Ukweli XiaoXiao hakuhusika kabisa na alikuwa ameletwa hapo nje ya ridhaa yake na alionyesha kuwa na wasiwasi mno lakini kutokana na kauli ya Rufi alishindwa hata kujua namna ya kujitetea wakati huo , aliishia kutingisha kichwa chake akiwa na machozi kumuashiria Rufi kwamba hahusiki.
Upande wa jini Lahani palepale sura yake ilianza kubadilika na macho yake kubadili rangi na kusababisha upepo kuongezeka na kupeperusha vitu ambavyo vililkuwa vyepesi ndani ya chumba hicho.
“Wewe mal**ya umepata wapi ujasiri wa kunisaliti , sio tu kwamba ulitoroka ulimwengu wa majini lakini pia unamwita binadamu mpenzi mbele yangu , nadhani utakuwa umesahau jinsi ulivokuwa wa hadhi ya chini licha ya familia yako kukuuza kwetu”
Rufi aliishia kutetemeka , mpaka hapo alijua hakuna namna anaweza kuokoka , Roma hakuwa maeneo ya karibu na haelewi kinachoendelea na hata kama kulikuwa na binadamu mwenye uwezo wa kijini karibu asingeweza kushindana na huyo mzee alieambatana na Lahani.
Tena alishukuru Rose na Magdalena hawakuwepo katika maeneo hayo , pengine wangeuliwa..
Lahani ndio mrithi mtarajiwa wa ukoo baada ya baba yake na kutokana na cheo chake alikuwa akilindwa na jini mwenye nguvu sana na ndio huyo mzee ambaye alikuwa ameambatana nae.
“Siwezi kukataa kama umekuja kunichukua na kunirudisha , lakini naomba tafadhali umuache mama yangu”Aliongea Rufi na maneno yale yalimuumiza mno Bi Wema.
“Hapana .. hakuna wa kumchukua binti yangu, imenichukua miaka mingi sana kukutana nae siwezi kuruhusu mumchukue tena , labda muanze kuniua mmi”Aliongea Bi Wema huku akimkingia Rufi kwa mbele.
Bi Wema hakuwa mjinga kutokana na historia ya maisha ya Rufi alikuwa akijua waliokuwa mbele yake ni majini na ndio hao ambao walikuwa wakimsulubu binti yake kabla ya kutoroka.
“Haha.. hahaha…., kama nilivyotarajia , binadamu ni viumbe wajinga sana , wewe ni nani wa kunizuia mimi , sio mbaya hata hivyo nitaanza na wewe , nadhani itakuwa njia rahisi zaidi ya kuanza kisasi changu hapahapa”Alingea Lahan kwa hasira na Rufi alijiaribu kumshikilia kwa nguvu Bi Wema lakini chumba kilikuwa kishaanza kukumbwa na dhoruba ya upepo huku kelele kama vile ni sauti ya watu waliokufa ikisikika.
“Tafadhari kaka usmuue ni ..”XiaoXiao alitaka kumtetea Bi Wema ili kuzuia asimuue.
“Kaa kimya wewe , huna mamlaka ya kuongea mbele yangu , utapatiwa adhabu yako tukisharudi kwa kuficha ukweli kwa baba na mimi”Aliongea kwa hasira na kumfanya Xiao kuufyata.
“Master , mkuu wa ukoo ametuambia tumkamate Rufi tu na kurudi nae kimya kimya na hatupaswi kukiuka sheria kwa kuua binadamu, tafafhari fikiria mara mbilimbili unachotaka kufanya”Aliongea Mzee Lao na maneno yake yalionekana kuwa ya mantiki na palepale aliacha kile alichokuwa akipanga kufanya.
“Okey Mzee Lao nitakusikiliza na kumsamehe huyu bibi kizee”Aliongea na palepale alimsogelea Bi Wema na kumtenganisha na Rufi kwa nguvu na licha ya kutumia nguvu kidogo kwa Bi Wema alikuwa mwepesi sana kwani alikwenda kujipigiza kwenye ukuta na kupoteza fahamu palepale.
“Mamaa…!!!”
Rufi alijitahidi kufurukuta kujitoa kwenye mikono ya Lahani lakini ilikuwa ngumu na aliishia kutoa kilio , Lahani palepale alimwingizia Rufi nguvu ya kijini na kumchunguza na aliweza kugundua hakuwa bikra tena na kufanya uso wake kuzidi kujikunja kwa hasira.
“Kwahio tayari umelala nae , kwanini sumu tuliokutegeshea haijamuathiri ? hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kugusa mwanamke ambae nilimkataa , kwasababu wewe sio bikra tena hakuna haja ya kugiza ndoa yetu kama makubaliano na ukoo wenu , kwanzia leo hii utakuwa kifaa cha majaribio ndani ya ukoo wetu kwa maisha yako yote”Aliongea kwa hasira mno.
Rufi aliishia kutoa machozi tu bila ya kuongea neno na uso wake ulimwangalia mama yake mzazi ambaye muda huo alikuwa hana fahamu,alitamani hata utokee muujiza akaangalie hali yake , hakujali anapelekwa ujinini alichokuwa akijali muda huo ni hali ya mama yake.
“Master ni muda wa kuondok, nimepotea ishara kutoka kwa Mkuu wa ukoo turudi mapema kabla uwepo wetu haujajulikana”Aliongea jini Lao na Lahani alitingisha kichwa na palepale alimshikilia vizuri Rufi na kisha alipotea nae na kumfanya Mzee Lao kuvuta pumzi za ahueni na palepale alimwangalia Bi Weka kwa sekunde na kisha alimshikilia XiaoXiao vizuri na kupotea palepale.
Alibakia Bi Wema ambaye alikuwa akitokwa na damu puani na mdomoni akiwa hana fahamu.
******
Upande mwingine ndani ya mgahawa mmoja maarufu unaopatikana ndani ya jijji la Dodoma alionekana Mzee Kweka pamoja na Roma wakiwa wameketi wakipata kifungua kinywa.
Upande wa Roma alionekana kabisa akili yake haikuwa imetulia kabisa, na kila saa alikuwa akiangalia karatasi iliokuwa kwenye mikono yake.
Nusu saa iliopita alikuwa ameenda kukutana na Master Namba moja kwa mara ya kwanza tokea asikie jina lake, kilichomshangaza Roma ni kwamba licha ya kwamba alikuwa na shauku ya kutaka kumuona Master namba moja lakini alishindwa kumuona kwa sura yake halisi.
Roma mara baada ya kukutana na Afande Kweka katika hoteli ya Highland iliokuwa ndani ya jiji hilo moja kwa moja waliepelekwa mpaka kwenye chumba maalumu ambacho kwa matarajio yao ndio sehemu ambayo wangekutana na Master Namba moja , lakini katika hali ya kushangaza ni kwamba Roma na Afande Kweka hawakuweza kukutana mtu ndani ya chumba hicho zaidi ya kusogelewa na wahudumu na kuambiwa wasubiri.
Walikaa ndani ya chumba hicho kwa zaidi ya nusu saa nzima bila ya Master namba moja kijitokeza , na ilimbidi Roma kupatwa na hasira na kuona pengine mtu huyo alikuwa akiwachelewesha kwa makusudi.
Wakati Roma aliopokuwa akipoteza uvumilivu ndio muda ambao alifika Raisi Senga ndani ya chumba hicho huku mkononi akiwa ameshika bahasha.
Raisi Senga aliishia kumwangalia Roma kwa macho ambayo hayakueleweka yalikuwa ya furaha au ya huzuni , ilikuwa ni kama vile kuna kitu ambacho kimetokea.
Roma na Afande Kweka wote walishangaa kumuona Raisi Senga nndio ambaye alifika ndani ya chumba hicho tofauti na Master Namba mmoja mwenyewe.
“Mzee msishangae , nipepewa jukumu la kuwakilisha masharti kwako kwa kosa ambalo umelifanya”Aliongea Raisi Senga huku akiwa na muonekano ambao ulikuwa na wasiwasi.
“Mashart, Senga unamaanisha nini , kwanini wewe ndio upo hapa?”
“Baba haya yote ni makosa ya Roma , familia ya Mzee Sharif sio familia ya kawaida na kilichonikuta sitaki kuweka wazi na nipo hapa kama mwakilishi tu”Aliongea na kisha palepale alimpatia Roma ile bahasha na Roma alitoa nyaraka ambazo zilikuwa ndani yake na kadri alivyokuwa akiisoma uso ulikuwa ukijikunja.
“Haiwezekani?””Aliongea Roma.
“Roma hiki ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako ,mtu ambaye unashindana nae sio wa kawaida na kama unataka kuendelea kuishi kwa amani pamoja na familia yako basi unapaswa kutimiza hayo masharti”aliongea Raisi Senga kwa kwa macho yake vile ilikuwa ni kama vile hana undugu na Roma na Afande Kweka , alikuwa yupo siriasi mno.
“Naataa kutii haya masharti , kama huyo Master Namba moja amekataa kujionyesha kwangu yeye mwenyewe basi siwezi kukubali huu ujinga , haya masharti yatanigharimu zaidi ya bilioni nne hela za kimarekani mnadhani hela zinaokotwa , hili swala lilitokea kwasababu familia ya Mzee Sharif ndio ilinianza”
Roma alizidi kuongea na kumfanya Raisi Senga kuzidi kuwa na hali ya wasiwasi.
“Roma nisikilize haya ndo masharti na mimi nipo hapa kama mwakilishi tu , hivyo ni wewe kutii ama kutotii lakini kama utaamua kukaidi lazima ujiulize je na uhakika unaweza kushindana na nguvu ambayo ipo nyuma ya familia ya Sharif”
“Ndio ninao uwezo wa kushindana nayo ,ameamua kujificha kwasababu ni muoga”
“Wala hajajificha kwa taarifa yako yupo hapa hapa tokea mlivyofika ila kwasababu ya uwezo wako mdogo hujamuona”
Aliongea na dakika ileile ni kama vile maneno yake yalibadili hali ya hewa kwani alianza kuhisi msisimko wa ajabu wa hewa ukianza kuongezeka ndani ya kile chumba na dakika chache mbeleni ni kama vile mtu ambaye ameshikwa na jinamizi kwani alianza kukosa hewa.
Mabadiliko yale yalimfanya hata Afande Kweka aliekuwa yupo kimya pembeni kushangaa mabadiliko ya Roma.
Haikuishia kukabwa tu shingo Roma alijihisi maumivu makali mno , alijaribu kuita Cauldron kudhibiti ile hali lakini mtitiroko wa nguvu zake ni kama vile umefungwa.
Roma alijikuta akipagawa na kujiuliza ni nguvu gani hioo ya kijini, alijitahidi kupambana na nguvu hio na ya kwake lakini ilionekana nguvu hio kuwa kubwa zaidi ya vile ambavyo amefikiria kwani iliweza kumshinda kirahisi sana.
“Nipo tayari kutii masharti”Roma alijikuta akiripoka mara baada ya kuona anazidi kuwa mnyonge na jasho jingi kumtoka na dakika ambayo aliongea kauli hio palepale nguvu ile ilimuachia na kumfanya kuwa huru na kupumua tena.
“Nini kimekutokea?”Aliuliza Afande Kweka ambaye ni kama sasa alikuwa amtoka kwenye mshangao.
Upande wa Raisi Senga alikuwa kwenye hali ya tabasamu tu , ilikuwa ni kama vile alifurahia Roma kuwa katika hali aliokuwa nayo.
Sasa kilichomchanganya Roma zaidi ni kwamba mara baada ya kutoka nje ya chumba hicho cha hoteli alishangaa kukuta eneo la nje hakuna ulinzi wa aina yoyote , yaani walivyofika na walivyotoka hali ilikuwa ileile , hata Afande Kweka mwenyewe alishangazwa na hali hio.
Roma palepale akili ilimcheza alijua mtu ambae alikutana nae sio Raisi Senga halisi , dakika ileile alirudi nyuma kwenda kuangalia ndani ya kile chumba ambacho walikuwemo lakini walikuta kilikuwa tupu na kuangaliana.
“Wewe mtukutu hebu nipatie hio karatasi”aliongea Afande Kweka na Roma palepale alimpatia Afande Kweka ile katarasi , isitoshe hata yeye alikuwa kwenye mshangao.
“Hii sio sahihi ya baba yako”Aliongea Afande Kweka.
“Mzee unamaanisha….”Aliongea Roma huku akimwangalia babu yake usoni na palepale Roma aliweza kuelewa nini ambacho amekutana nacho,mtu aliekuwa ndani ya kile chumba sio Senga pengine ndio Master namba moja mwenyewe ambaye amekuja kwa muonekano wa sura ya Raisi Senga.
Roma alianza kujiuliza kama ni kweli ni nguvu ya aina gani ambayo anatumia kiasi cha kumfanya ashindwe kumgundua ni feki , ijapokuwa alikuwa na walakini tokea mwanzo wa mazungumzo lakini hakukuwa na dalili za wazi za kuonyesha sio yeye.
Afande Kweka alionekana kama vile alijua muda mrefu na hakuonyesha hali ya mshangao na palepale alipiga hatua na kuondoka ndani ya hilo eneo.
Roma mara baada ya kutoka ndani ya hoteli hio walikuja kuingia ndani ya mgahawa mmoja kando ya barabara inayoelekea Singida na muda wote ambao walikuwa kwenye gari walikuwa kimya tu kila mtu akiwaza lake.
“Vipi bado hujapatana na Edna?” Alivunja ukimya Afande Kweka mara baada ya wote kuingia ndani ya mgahawa na kuagiza supu.
“Mzee unaniuliza kitu ambacho unajua tayari”Aliongea Roma na kumfanya Afande Kweka kunywa supu kidogo na kumwagalia Roma.
“Nimeamua kukaa pembeni na kukuangalia usidhani sijali ,nataka unipatie tarehe leo hii ni lini unemrudisha Edna nyumbani?”
“Nilimuahidi Edna sitomlazimisha kubaki na mimi , nitakachofanya ni kumjali pekee nadhani ndio kitu ninachoweza kufanya kwa sasa , kuhusu mambo meingine sitaki sana kufikiria”
“Hibi wewe ni mwanaume kweli?”Aliongea Afande Kweka kwa kufoka huku akionyesha hasira waziwazi kwenye macho yake.
“Mzee unajua kabisa mahusiano yangu na Edna yalivyokuwa na mkanganyiko haina haja ya kunifokea”
“Man up!!! , hilo sio tatizo , tatizo ambalo lipo ni kwamba wewe sio mwaminifu na una mtoto na mwanamke mwingine, naona ni tatizo dogo tu tofauti na ulichopitia dakika kadhaa zilizopita”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake lakini alihisi ni kama yupo sahihi maana ile nguvu haikuwa mchezo.
“Nakujua upo vizuri sana kwenye kudanganya wanawake lakini kwanini swala dogo hili linakushinda , kwahio unataka kuniambia wanawake wote walikupenda baada ya kuwaambia kila kitu kuhusu wewe , kama jibu ni hapana basi kuna sababu nyingine ambayo imewafanya kukupenda ,hebu tumia ubongo wako huo, hata ni kwa kumdanganya hakikisha Edna anaendelea kuwa mkeo”Aliongea
“Mzee tatizo ni kwamba…”
“Usinipe visingizio vya kipuuzi maana havina umuhimu wowote kuliko mahusiano yako , sikutaka kuingilia maswala yenu ya ndoa kwasababu nilikuamini utayamaliza ndani ya muda mfupi lakini mpaka sasa hivi unayumba tu , mama yako anaweza kukuambia kuoa mwanamke mwingine lakini usije kumsikiliza , sitaki kuja kusikia eti tayari ushasaini makaratasi ya talaka”
“Inaonekana kama unanidhihaki vile maana ushaniona tayari nina uwezo mdogo , unafikiri nitayaingilia vipi maisha ya Edna?”
“Hebu acha kunikasirisha bwana , kama ungetumia asilimia kumi tu ya akili yako kama unavyoitumia kujifunza mafunzo ya kijini yote ya akili yako haya yote yasingetokea , kwanini unafanya maamuzi kama vile unamjua sana Edna , wewe sio Edna na anaonekana anakuigizia yule, unapaswa kuelewa wanawake wanaongea vitu ambavyo hawamaanishi na mimi najua zaidi yako, hebu fikiria tokea mtengane , vipi furaha yake imeongezeka au imepungua , vipi anaonekana kuwa na furaha kuliko mwanzo?”Aliuliza akiwa siriasi na kumfanya Roma kuona kweli maneno ya babu yake ni sahihi.
Tokea atengane na Edna hakuonekana kama mwanamke mwenye furaha kwa maelezo ya Bi Wema.
“Roma fanya chochote unachoweza kumuomba msahama , hata kama ni kumlilia, fanya chochote unachoweza akusamehe na umrudishe”
“Mzee sasa mbona unaongea mambo ya kutia aibu hivyo , yaani mimi na uanaume wangu nilie mbele yake anisamehe?”
“Mambo gani ya aibu , kwangu sijali kama uanaume wako utaathirika , ninachotaka ni kumuona umemrudisha na kuendelea kuwa mkeo , kama wewe ni mwanaume wa kweli unatakiwa kufanya chochote kile kumfurahisha mke wako , kama kweli mtafikia hatua ya kuachana hakikisha wewe ndio humpendi na sio kukuacha kwa sababu ambazo hazieleweki, unafikiri Edna nilimpatia ile bangiri bahati mbaya , nilimpatia kwasababu ilimchagua na sio vinginevyo , hivyo sitaki kusikilia sijui likipanda na likishuka nataka kuona anakuja kunisalimia nyumbani”Aliongea Mzee na kisha akasimama akionekana muda wowote anaondoka.
“Weka utaratibu wowote Lanlan aje kunisalimia nyumbani hata kama akiacha kwenda shule kwa siku kadhaa haina shida ana akili yule hata asisome, najua una mambo mengi kwasasa mimi nitaondoka , unajua mwenyewe namna ya kurudi”
“Mzee hebu subiri kwanza , unapaswa kulipia sina hata hela hapa”Aliongea Roma huku akimalizia supu iliokuwa kwenye bakuri lake na kisha kusimama.
Roma ni kweli hakuwa na hela alikuwa na kadi ya benki tu na Tanzania sio kama Ulaya kwamba unaweza kupitisha kadi na kulipia.
Afande Kweka hakuwa na hiyana alifanya malipo na ndani ya muda uleule alimpa ishara dereva wake na kusogeza gari na kuingia ndani na kumuacha Roma akiwa amesimama.
Upande wa Roma aliishia kusimama kwa muda huku akiwaza , siku hio ilikuwa ni ya ajabu kwake.
Mwanzoni Roma alijua kutokana na kurudiwa na nguvu zote na kupitia mapigo ya radi tisini na tisa basi ana uwezo mkubwa lakini siku hio ni kama amekutana na mtu ambaye alikuwa na nguvu kubwa kuliko yeye na kuona bado ana safari ndefu.
Hakutaka kuwaza masharti ambayo alikuewa amepewa kuyakamilisha ili kusamehewa kile ambacho amefanya.
Ukweli ni kwamba masharti ambayo amepewa yalikuwa yakimgharibu zaidi ya dolla bilioni nne za kitanzania lakini hakuona ni pesa nyingi , kitu pekee kilichomfurahisha ni kwamba huyo mtu anaejiita Master namba moja alionekana kutokuwa na uelewa juu ya Maimuna kuwa feki.
Hivyo Roma alijiambia atachukua utajiri aliopata kutoka kwa Masterr Wadudu na kisha ataunganisha na utajiri ambao ataupata kutoka kwa familia ya Mzee Sharif na kukamilisha masharti, alijiambia ngoja awe mjinga kwa muda huo asiongeze maadui na atakuja kupambana nae tu.
Baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa aliona hatua inayofuata ni kumrudisha Edna kwenye himaya yake kwa namna yoyote ile , hakujua kwanini Mzee Kweka ameenda mbali na kuonyesha usiriasi wa Edna kuendelea kuwa mke wake lakini aliona ni sahihi kwani hata yeye hakuwa na nia ya kumpoteza.


SEHEMU YA 697.
Ilikuwa ni mchana na jua ndani ya jiji la Dar lilikuwa likiunguza kwa wastani.
Ilikuwa tayari ni jumamosi na mitaa mingi ya kibiashara ndani ya jiji hilo ilikuwa imejaa sauti za watu na makelele ya miziki na baina ya nyimbo ambazo zilikuwa zikisikika ni za Sophia.
Kurudi kwa Sophia kwenye kiwanda cha muziki ilimfanya umaarufu wake kuongezeka zaidi na zaidi, ilionekana skendo ambayo aliipata mara ya mwisho ndio iliomfanya kuzidi kuwa maarufu.
Ndani ya makao makuu ya kampuni ya Vexto licha ya kwamba ilikuwa jumamosi lakini wafanyakazi walikuwa wako bize kufanya kazi.
Tokea kampuni hio kuwa ‘International Corporation’ wafanyakazi wengi waliajiriwa ili kupunguza wingi wa kazi na kuongeza ufanisi.
Ukiachana na ule upendeleo wa kampuni hio kuajiri zaidi wanawake awamu hio warfanyakazi wengi ambao wameajiriwa ni wanaume pia , hata hivyo wahitimu wengi wenye ujuzi mbalimbali walikuwa wakipenda sana kufanya kazi chini ya kampuni ya Vexto, sio kwasababu tu ilikuwa ikilipa vizuri lakini ilionekana kama kampuni ambayo miaka kadhaa ijayo inakwenda kuwa kampuni kubwa ndani ya bara la Afrika , pengine na dunia kwa ujumla.
Upande wa wanaume ambao wameajiriwa kufanya kazi ndani ya makao makuu ya kampni hio walikuwa na furaha kweli kwani waliweza kupata fursa ya kuweza kuongea na warembo ambao wanafanya kazi ndani ya kampun hio.
Edna hakuwa bado amehamishia makazi yake katika jengo jipya ambalo lilikuwa katika hatua za mwisho kabisa kukamilika hivyo bado ofisi yake ilikuwa ikipatikana juu kabisa ndani ya jengo hilo ambalo lilikuwa likipatikana ndani ya eneo la Posta.
Kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wengine kuwa bize upande wa Edna alikuwa amesimama mbele ye kioo akiangalia upande wa nje ambao watu wake walionekana kuwa na pilikapilika.
Siku hio alikuwa amevalia suti ya rangi nyeupe na viatu vya skuna na kumfanya kuzidi kuwa mrembo licha ya kwamba alionekana kuwa mbali kimawazo.
Nyuma yake alikuwa amesimama Recho aliekuwa amevaa suti iliochora mwili wake vizuri na ilionekana alikuwa akitoa ripoti kuhusiana na kazi aliokuwa amepewa.
“Boss , maongezi ya kibiashara kati ya kampuni ya Kijerumani ya Collins Group yamefikia awamu ya tatu, bado wanalazimisha malipo ya Euro milioni mia tatu kwa mwaka, tunapaswa kuendelea vipi..”
“Ongea na wawakilishi wao Euro milionni hamsini ndio ofa yetu ya mwisho kama bado wanakataa hakuna haja ya kuingia nao mkataba mpya na haina haja ya kuwasubiria watoe majibu , wasilimiana na kampuni ya Hofferman na wapatie ofa hio hio”
“Sawa bosi , pia mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Lorrent, Mr Thompson amekueletea kadi ya mwaliko wa kuhudhuria tafrija fupi usiku wa leo katika hoteli ya Serena ambayo itaambatana na mazungumzo ya uwekezaji kuhusiana na mradi wa ujenzi wa makazi unaondelea Bagamoyo , anasema kama hautojitokeza wewe mwenyewe basi atachukulia kama huna nia ya kufanya nae biashara na atarudi Marekani siku inayofuata”
“Muache afanye anavyotaka , ongea na Chriss na mwambie awasiliane na mwenyeketi wa bodi , na awambie Thompson ana tabia ya hovyo na kama wanataka ubia uendelee wambadilishe haraka sana”Aliongea Edna na kumfanya Recho kuitikia kwa kichwa na kisha akafunika faili lake akionekana ashamaliza kutoa ripoti.
“Bosi nishamaliza kutoa ripoti , kuna kitu kingine ambacho unataka nikusaidie siku ya leo?”
“Hali ya hewa leo ni nzuri mno Recho”Aliongea Edna mara baada ya kimya kifupi na kumfanya Recho kuwa na mshangao kidogo lakini alishindwa kongea neno.
“Recho ushapata Lunch?”
“Hapana , ndio kwanza imefika mchana boss”Alibu Recho kwa wasiwasi kwani ni Swali ambalo hakutegemea kulisikia kutoka kwa Edna.
“Unaonaje tukienda kupata chakula pamoja,… nitalipia mimi”Aliongea Edna huku akiweka sawa nywele zake ambazo zilikuwa zimemfunika sikio kutokana na kuchanguka.
Recho ilikuwa mara yake ya kwanza kuambiwa na Edna kwenda kupata wote chakula cha mchana , alijua Edna muda mwingi alipenda kufanya kazi na ni mara chache alikuwa akitoka nje ya jengo hilo kwa ajili ya chakula cha mchana.
“Nipo tayari Madam , unataka tupate chakula sehemu gani , nitaendesha mimi gari?”Aliongea Recho.
“Hakuna haja ya kuendesha gari leo , nataka kupanda yale magari ya mwendokasi”Aliongea Edna huku akinyooshea kidole gari la mwendokasi ambalo linashusha watu kituoni.
Kauli yake ilimuacha Recho kinywa wazi akiwa kama hajasikia vizuri na paepale alipotezea mshangao wake.
“Bossi kwani haujisikii vizuri au ni kutokana na kuwa na mawazo?”Aliuliza Recho.
Ukweli ni kwamba hakutaka kuamini kama Edna anaweza kupanda mwendokasi , alikuwa na uhakika tokea mwendokasi uje ndani ya jiji la Dar kama usafiri wa uma , Edna hajawahi kupanda lakini sio hivyo ni ngumu kwa mwanamke tajiri kama Edna mwenye zaidi ya Dola bilioni ishirini kupanda magari ya uma.
“Recho unafikiria nini ,tunaenda au hatuendi?””
“Ah ,,, tunaenda bosi , nisubiri kidogo naenda kuweka hivi vitu nakuchukua mkoba wangu”Aliongea Recho na palepale alitoka kwa kukimbia kwenda nje kuweka vitu vyake
Dakika chache mbele Edna akiwa anakodolewa macho na wafanyakazi aliweza kutoka nje ya jengo hilo akiwa ameambatana na Recho.
Wafanyakazi ambao walikuwa nje walijikuta wakishangazwa mara baada ya Recho na Edna kuelekea kituo cha mwendo kasi na kukata tiketi.
Edna hakujali wanaomwangalia na mara aada ya kuchukua tiketi mbili alimpatia Recho na wote kwa pamoja waliingia ndani ya eneo la kusubiria gari na bahati nzuri gari haikuchelewa na haikujaza sana na wote walipanda gari hio inayoelelekea Morocco.
Recho alikuwa akifuatisha tu maana hakujua ni wapi wanaelekea na bosi wake na mara baada ya kufikishwa Morocco Edna aliita taksi na wote wakaingia na Edna alitoa maelekezo ya kuepelekwa upepo Beach.
Na hapo ndio sasa Recho alijua ni wapi wanaelekea , lakini alifurahi na yeye pia mara baada ya kuona wanaelekea Upepo Beach , ni moja ya eneo ambalo anapenda sana kutembelea ikiwa wikiend.
Haikuwachukua dakika nyingi mpaka kufika na wote walishuka nje huku Edna akiangalia mazingira.
“Unapaonaje hapa Recho , tutakula hapa na kupunga upepo kidogo”Aliongea mara baada ya kumlipa dereva.
“Ni pazuri mno na pametulia”Aliongea Recho akitoa tabasamu , hakuwa akielewa kwanini Edna kaamua kuja mbali hivyo kwa ajili tu ya chakula cha mchana kwani kampuni ilikuwa mbali sana lakini hata hivyo alifuata nyuma nyuma kuingia ndani ya eneo hilo huku akiwa na hamu ya kupata Seafood.
Ilikuwa ni wikiend na eneo lilikuwa na watu wengi licha ya kwamba ilikuwa mchana bado.
Edna alikuwa ni kama amekariri eneo hilo kwani mara baada ya kuona sehemu ambayo alikaa na Roma mara ya mwisho alitoa pumzi ya ahueni na kunyoosha kidole akimwashiria Recho ndio wanapoenda kukaa.
Wahudumu wa eneo hilo walishangazwa na uwepo wa Edna lakini haraka haraka waliomba kuwahudumia.
Edna aliagiza aina ya chakula kilekile ambacho Roma alimwagizia mara ya mwisho na Recho na yeye alichagua hichohicho.
“Leo sio kitamu kama mara ya mwisho nilivyojaribu kula nikiwa na Roma…”Aliongea Edna huku akionyesha hali ya kukosa hamu ya kuendelea kula.
“Boss naomba niwe muwazi kwako , najua kabisa unampenda mume wako lakini kwanini unamkwepa tofauti na kukaa chini mkayamaliza, mimi na wafanyakazi wengine ndani ya kampuni tunakuchukulia kama Role model wetu , kwasababu wewe ni mwanamke mwenye maamuzi na ngangari na ndio maana umetufikisha leo tulipo lakini kwanini unakimbia changamoto za maisha yako binafsi, umenileta mbali hivi najua yote ni kutokana na kushindwa kumsahau Roma”
“Recho sio rahisi hivyo , maisha ni tofauti na biashara , kwenye biashara kama nitafeli na kampuni kufirisika naweza kuanza upya maadamu nitakuwa hai na ndio maana siogopi changamoto za biashara lakini kwenye maisha ni tofauti , kuna baadhi ya vitu kwenye maisha huwezi kubahatisha kwasababu ukipoteza ndio umepoteza na siwezi kurudisha muda nyma ndio maana nakuwa muoga”
Aliongea Edna na kumfanya Recho kushindwa kuongea neno lololote , mwanzoni alikuwa akimuonea wivu sana kwa kujaliwa uzuri , busara na mapemzi lakini kwasasa licha ya kwamba bado alikuwa akimuheshimu kutokana na uzuri wake na busara zake lakini aliona mapenzi ni kitu ambacho ni kama hakimpi furaha.
Wakati wakiendelea kuwa bize na chakula muda huo huo alionekana mtu mwingine akisogea upande wao kukaa nyuma yao.
“Wewe utakuwa ni mjinga sasa , na siku zote nakuambia hivyo, maisha ni sehemu ya mchezo wa kubahatisha , ndio unaweza kusema hutaki kubahatisha lakini usipofanya hivyo ni sawa na kujihukumu kwani hutokuwa na furaha hata kidogo”
Sauti ilisikika pembeni yao na kumfanya Edna kushikwa na mshangao kwani ni sauti ambayo alikuwa akiijua na mara baada ya kugeuza uso wake aliweza kumuona Roma akiwa na tabasamu kama kawaida yake.
“Wewe.. kwanini upo hapa??”
Hata Recho alikuwa kwenye mshangao na Roma hakujali mshagao wao na alienda kukaa kwenye meza yao.
“Niliwaona mkitoka nje ya kampuni na kupanda basi , sikujua mnaenda wapi hivyo niliwafuatia nyuma nyuma mpaka hapa , babe sijui ni jambo gani unannificha lakini siamini kama hunipendi na hujanimisi”
Edna alijikuta akiona aibu, maana alikuwa amekamatika na hakujua namna nyingine ya kuficha hisia zake.
Roma alikuwa mwepesi alichukua samaki palepale na kumtoa miba na kisha kumpa ishara Edna kuachama ili amlishe
Muda huo Edna mara baada ya kugeuka kuangalia pembeni aligundua watu wengi walikuwa wakiwaangalia kwa macho ya uchokozi hata Recho aliokuwa nao meza moja alikuwa akimwangalia kwa macho ya kichokozi.
“Unafanya nini wewe…, huoni watu wanatuangalia”Aliongea Edna kwa tahadhari.
“Wakiangalia ndio ndio , wewe ni mke wangu na naruhusiwa kukulisha , kama kuna ambaye hapendi nikimlisha mke wangu nitamfukuza hapa”Aliongea Roma kwa sauti kama vile anataka kila mtu asikie .
“Mimi , sitaki tupo kwenye mchakato wa talaka”Edna alijifanyisha kauzu lakini mashavu yake yalimaanisha kitu kingine na kumfanya kuzidi kupendeza kiasi cha kumfanya Roma kutoa kicheko.
“Wife hujui hata kuigiza hasira?”
“Mimi…”Edna hata hakujua namna ya kujitoa kwenye hio hali , hakutaka juhudi zake za kumuigizia Roma zipotee kirahisi hivyo kwa kipande cha samaki.
Upande wa Roma alipanga siku hio kuhakikisha anayamaliza na Edna kwa namna yoyote ile kama alivyoambiwa na babu yake, ilikuwa bahati kwamba Edna alitoka mwenyewe kwa ajili ya chakula cha mchana lakini mpango wake ni kufanya tukio ndani ya kampuni.
“Hey binti hebu kula basi , mumeo anajitahidi kukubembeleza vyote hivyo”Sauti ya mzee aliekuwa na mke wake pembeni walishindwa kuvumilia.
“Hehe ugomvi wa kimapenzi huo na ndio raha yake, hebu kula na wewe usimkasirikie tena , nyie ni wenza hii ndio sehemu ya kuyamaliza”Mke wa yule mzee alimuunga mkono mume wake na kumfanya Edna kuwa mwekundu kutokana na uchokozi wao.
“Ndio mpenzi wangu, sijali unasababu ya aina gani inayokufanya kunikasirikia lakini huna haya ya kuniambia na sitokulazimisha , sitaki kuigiza na kuonekana mtu mzuri mbele yako , najua mimi ni mbinafsi linapokuja swala lako , sitaki kusikia visingizio vingine na sitaki kujidanganya pia kwani najua hisia zako juu yangu na mimi najua zangu juu yako”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumpiga kibao mkono ulioshikilia samaki .
“Unajua hisia zangu kivipi wewe , nimesema sikutaki tena na usinisogelee tena”Aliongea huku akitoa machozi na palepale alisimama na kukimbilia ufukweni na kumfanya Roma kushikwa na bumbuwazi.
“Hey stop sitting there ! Go after her” Mwanaumke mmoja wa kizungu aliekuwa amekaa mita kadhaa ni kama alikuwa akijua kinachoendelea na kupendezwa na drama hizo za kimapenzi.
Roma na yeye ni kama akili yake imeshituliwa na alisimama na kumkimbilia Edna na mara baada ya kumfikia alimkumbatia kwa nyuma akipitisha mikono yake kifuani.
“Niachie mimi bwana….”
Aliongea Edna huku akitaka kumng’ata Roma mkononi lakini hakuweza kuufikia na kuishia kufurukuta huku mikono yake ikisuguana na manyonyo yake .
“Siwezi kukuachia tena kwanzia leo hii”
“Wewe … Roma niachie bwana .. nishakuambia hatuwezi kuendelea kuwa pamoja”
“Edna siwezi kukuachia , nataka kuendelea kuwa mumeo na wewe kuwa mke wangu , hakuna kitu ambacho kinaniogopesha kwenye ulimwengu huu kama kukupoteza”
“Roma nakuambia utaumia na unaweza kufa ukiendelea kuwa na mimi, huogopi?”Aliongea Edna na kauli yake ilimfanya Roma kucheka kama kichaa.
“Edna nadhani hunijui vizuri , mimi siogopi kifo , hata kama nikifa leo angalau najua sijapoteza maisha yangu bila sababu , Kwangu kitu pekee ninachoogopa kwenye huu ulimwengu ni kukupoteza wewe kipenzi changu , kwasababu najua hata kama nitakuwa naendelea kuishi bila wewe lakini moyo wangu utakuwa umekufa”
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 697
Kusikia maneno yale ni kama vile yamefungua fundo ambalo lilikuwa limejifunga funga kwenye ubongo wake.
Mpaka pale Edna alijiambia kuna kitu ambacho alikuwa amesahau , kama kuachana kunazuia matatizo kutokea basi ndio mwanzo wa matatizo mengine.
Ni kama vile amepata kisingizio cha kujishawishi yeye mwenyewe na palepale zile hasira alizokuwa nazo zote zilikoma.
Akiwa anatoa machozi alimgeukia Roma na kumwangalia usoni , wakati huo macho yake yalikuwa na ukungu na muonekanao wake aliokuwa akionyesha muda huo kwa mtu yoyote asingesema mwanamke huyu ni kauzu.
Alikuwa akithibitisha ile kauli ya mwanamke aliependa kapenda na ndio ambacho kilikuwa kikionekana.
“Kwanini usiniulize kwanza ni kwasababu gani nilikuacha?”Aliongea Edna , ukweli hakujua namna ya kuanzisha maongezi na kutoa sababu kwanini hakutaka kuendelea kuwa na Roma.
“Sijali ni sababu gani uliokuwa nayo na mimi kwa chochote kile nakuamini, najua ulikuwa na sababu zako za msingi lakini ninachojali kwa sasa ni wewe kuwa upande wangu na kuwa na furaha , kuhusu mengine naamini tutapita kila daraja ambalo lipo mbele yetu , nishakuwa kwenye hali hatarishi za kifo na uhai na siwezi kuwa na amani , watu wengi wanataka kuona kifo changu, kama nitaendelea kuwa na mawazo nitapoteza mwelekeo na kujiingiza kwenye hatari”
“Kwannini unaongea kibishi hivyo kama vile hujali chochote , kwanini usiniulize na nikakujibu , unakurupuka unajua”
“Ni sawa tu ,… Edna nisikilize maisha yangu siku zote ni ya kukurupuka, muda mwingine kuwazia sana mambo hakuleti majibu mazuri , nitakuachia wewe kufikiria ila mimi nataka maisha mepesi kama ilivyosasa”
Baada ya kauli hio alimwinamia na kisha akambusu kwenye lipsi zake na kutoa ulimi na kuutumbukiza kwenye mdomo wake kitendo kilichomfanya Edna kutoa macho huku akijaribu kurudisha kichwa nyuma lakini Roma alizidi kumsogelea.
Dakika chache tu ilimfanya Edna mwili wake kufa ganzi na kumuacha Roma afanye anachotaka.
Wakati hayo yakiendelea watu wote waliokuwa ndani ya hili eneo wakiangalia picha hio walipiga makofi na kushangilia kwa ushindi wa Roma , mambo kama hayo mara nyingi hayaonekani sana katika mazingira ya Tanzania.
Baadhi ya Wazee waliona wanachokifanya sio jambo zuri kwani kulikuwa na watoto lakini kwa vijana wako ‘exposed’ lilikuwa jambo la kufurahisha ukizingatia na urembo aliokuwa nao Edna.
Recho aliishia kusimama na kumwangalia Roma alivyokuwa amemkumbatia Edna na kumkiss , alijikuta akitoa tabasamu huku machozi ya wivu na furaha yakimtoka.
“Roma umekuwa kichaa , watu wanatuangalia ujue”Aliongea Edna mara baada ya akili yake kurudi.
Roma aliishia kucheka tu akiwa kama hajali nani anamwangalia na palepale alimshika mkono na kuondoka nae ndani ya eneo hilo.
“Tunaenda wapi?”
“Nataka kumwambia Lanlan mama yake amerudi”
Edna aliishia kushangaa kidogo na kuhisi furaha mara baada ya kujua ni muda ambao anakwenda kuwa karibu na Lanlan tena , kwa mara nyingine alikuwa ashachagua kuishi na Roma na kutazamia yajayo.
Recho ambaye alishasahaulika ndio alibeba jukumu la kulipia chakula na kisha kuitafuta njia ya kurudi mwenyewe , katika hali kama hio alijikuta akimkumbuka mpenzi wake , ijapokuwa alikuwa na hisia na Roma lakini hakutaka kuzipa kipaumbele.
Ni mara baada ya Edna kufika katika eneo ambalo watu hawakuwa wakiwaangalia na palepale walipotea na kufumba na kufumbua waliibukia mbele ya geti la shule ya Lanlan.
“Babe unajua ni darasa gani Lanlan anasomea?”
“Wewe hujui kwamba sasa hivi yupo darasani , kwanini tusije badala ya vipindi?”Aliongea na kumfanya Roma kuona Edna ana pointi
“Kama ni hivyo basi tuna muda wa kutosha kabla ya kuja tena , umekuwa mpweke mwenyewe kwa muda mrefu usiku hivyo nitafidia”
Edna kabla hajakataa tayari ashapakuliwa na kufumba na kufumbua walikuwa juu ya Balkoni katika nyumba yao na Roma alikosa hata uvumilivu wa kuingia ndani na palepale walianza kufakamiana kwa pupa nje ya Balkon na Roma alivua nguo za juu na kumvua na za kwake za juu na kisha akazirushia ndani na kuendelea kumkiss.
Edna akili ilimhama kabisa na kwenda ulimwengu mwingine wa mahaba na alichanganyikiwa zaidi mara baada ya sehemu zake kuguswa na kidole na ilimfanya miguu kuanza kukosa nguvu.
Roma palepale aliacha kumpiga denda na alianza kumbusu kuanzia shingoni kidevuni na kushuka chini kwenye chuchu na kuendeleza kupambana na kadri alivyokuwa akishuka chini ndio ambavyo alimfanya Edna kuzidi kukosa pumzi.
Roma alijkuta bize sana , wakatit huo alichokuwa akiwaza ni kumlidhisha mke wake kwa namna yoyote ile ili kuondoa sumu yote iliokuwa ndani ya moyo wake.
………
Masaa mawili mbele Roma mara baada ya kushusha mzigo alimbeba Edna na kumwingiza bafuni na kumsaidia kuoga.
“Muda umefika , nenda kamwambie Nasra tutaenda sisi kumchukua Lanlan” Aliongea Edna mara baada ya kuona dalili za Roma kutaka tena.
Roma licha ya kuambiwa maneno hayo hakutaka kumwachia na aliendelea kugusa gusa mwili wake.
“Niache kunigusa bwana la sivyo nitakasirika”Aliongea akimtoa Roma mkono wake.
Roma aliishia kutoa tabasamu tu , kwa namna flani alijisikia vizuri kufokewa.
Baada ya kuvaa nguo wote kwa pamoja walishuka chini sebulen na ndio muda ambao Roma alimkumbuka Bi Wema.
“Mpenzi , Bi Wema hayupo?”
“Aliniambia anasafiri kwenda Tanga na Rufi kumsalimia mdogo wake anaweza rudi leo jioni au kesho”Alijibu Edna na kumfanya Roma kutingisha kichwa na pia kujihisi ni mwenye hatia kwa kutokuwa makini na wanawake wengine.
Baada ya kutoka Edna alimshika mkono Roma huku wakitembea uelekeo wa nyumba ya Nasra.
“Hubby mbona hauniulizi kwanini nilitaka talaka”Aliongea Edna na kumfanya Roma kusimama na kumwangalia na Roma alionekana kufikiria na alijua kuna kitu kimetokea.
“Nini tatizo , kwanini unaniangalia hivyo?”
“Hakuna kitu , ni kwamba naona ni kama ndoto kuniita Hubby”Aliongea Roma akitoa tabasamu kwa wasiwasi.
Edna na yeye alielewa hisia zake , ilionekana kama ndoto lakini hata hivyo kuwa nae karibu kama hivyo ilikuwa ni ishara kwamba alipangiwa kuwa nae kwa shida na raha.
“Chukulia kama ndio mgogoro wetu mkubwa uliotokea baada ya ndoa , usifikirie sana”Aliongea
“Babe unaonaje ukiniita mara nyingi nyingi , nataka nisikie ukiniita ‘Hubby’, legeza sauti kama vile tuko chumbani basi”Aliongea Roma kihuni na kumfanya Edna kumfinya.
“Ukiongea tena ujinga silali na wewe”Aliongea na kumfanya Roma kuwa kimya.
Roma hakuuliza kwanini Edna alitaka talaka , ijapokuwa alikuwa akitaka kujua kwanini Edna amebadilika lakini alikuwa mzito wa kuuliza , ni kama vile ilivyokuwa kwa Edna wakati wanaanza ndoa yao wakati wa yeye kupitia mabadiliko lakini Edna hakuuliza na yeye alikuwa hivyo hivyo , alikuwa mzito kusikia sababu iliokuwa nyuma ya kila kitu.
Upande wa Edna hakutaka kuongea pia kabla ya kuulizwa , alijua pengine Roma hakutaka kuongelea mambo yaliopita.
“Sina haja ya kuwaza sana , siwezi kuepuka kinachoendelea katika maisha yangu nitapambana na nisioyajua nikiwa nae”Aliwaza Edna
Mara baada ya kufika nyumbani kwa Nasra walikaribishwa na harufu ya chakula , Nasra ambaye alikuwa amevalia apron na alionekana alikuwa bize katika maswala ya upishi.
Blandina mama yake Roma alikuwa ashasafiri kwa mara nyingine kusimamia maswala ya taasisi yake ya misaada.
Nasra mara baada ya kusikia hatua za watu aligeuza shingo yake na hapo ndipo alipomuuona Roma na Edna wakiingia wakiwa wameshikana mikono
Alijikuta akishangaa kwani hakuamini kama walikuwa wamepatana lakini hata hivyo aligeuza mshangao wake na kuwa na uso uliopambwa na tabasamu na furaha.
“Edna nyie mme…!!”
Edna muonekano wake ulibadilika mara baada ya kukutannisha macho na Nasra , mawazo mbalimbali yalipita katika kichwa chake na alijihisi ni mwenye hatia kwa kumfukuza Nasra na Dorisi katrika kampuni yake kwasababu tu ya kugombana na Roma.
Furaha ya Nasra ilikuwa ni ile ya dhati na hakuonyesha ishara ya kinyongo kabisa na ilionekana alikuwa akishukuru kwa Roma kupatana na mke wake.
Lakini hata hivyo Edna alimchukia Nasra kutokana na kuwa mchepuko wa mume wake , ijapokuwa ilitokea kipindi ambacho hakutimiza majukumu yake kama mke kwa Roma lakini bado hakuweza kujizuia kuona Nasra alimsaliti.
Lakini kutokana na historia waliokuwa nayo hakutaka kuruhusu hisia zake kumvaa kumchukia Nasra kwani ukiachana na wote wawili kumpenda mwanaume mmoja lakini mambo mengine yalikuwa sawa.
Mpaka hapo Edna alijua maji ashayavulia nguo ni kweli hapendi kuwa na mpinzani katika mapenzi yake lakini lazima akubali mume wake alkuwa na michepuko hivyo alijiambia asingeendelea kumchukia Sophia , Magdalena na Mage kwasababu ya kuwa na mapenzi na Roma.
Ukiachana na kuwachukulia kama wapinzani lakini kwa upande mwingine Edna aliwakubali, hawakuwa wanawake wa kawaida kwa macho yake.
“Nasra tumepatana , samahani kwa kilichotokea ndani ya kampuni””
“Hakuna shida , wote tulijua unasababu zako ndio maana , wewe sio mtu wa aina ile na nimefurahi umebadili maamuzi yako , Lanlan atafurahi sana wewe ndio mama yake hata hivyo”Aliongea Nasra huku akianza kutokwa na machozi na kumfanya Roma amsogelee na kumfuta na mkono wake.
“Usilie kama una furaha , kuona machozi yako inaniumiza na mimi”Aliongea Roma kwa sauti ya kiume nzito ya kubembeleza.
“Usifanye hivyo…”Nasra alitoa mkono wa Roma haraka haraka na kumwangalia Edna kwa hofu.
Upande wa Edna alijifanyisha hajaona chochote , alijiambia kama ataendelea kuwa na wivu kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo maisha yake yatakuja kuwa magumu mno.
“Nasra tutaongea vizuri baadae , ninaenda kumchukua Lanlan kwanza”Aliongea na palepale aligeuza njia na kutoka nje.
Roma mara baada ya kuona Edna katoka alimuachia na Nasra na kisha akamfuata na alipofikia mlangoni alimkonyeza Nasra na kutokomea nje.
Baada ya saa moja hatimae waliweza kurudi wakiwa na Lanlan nyumbani
Lanlan uso ulikuwa umesawajika , kwa haraka haraka ilionekana alikuwa akili njia nzima na alikuwa haamini kama mama yake alikuwa amerudi.
Roma aliekuwa akifuatisha nyuma nyuma alijikuta akiona wivu kwa namna ambavyo Lanlan anampenda Edna alijiuliza kwanini yeye hakulia kipindi kile alivyopotea kwani sio kama Edna alipotea kama yeye kwa muda mrefu.
Edna hakujali muonekano wa Roma kabisa na macho yake yote yalikuwa ni kwa Lanlan .
Mara baada ya kukaa kwenye Sofa nyumbani kwa Nasra alianza kuwa bize kumuuliza mambo ya shule na mengine mengi kwa muda wote ambao hawakuwa pamoja na Lanlan alimwelezea mama yake kwa furaha.
“Lanlan umekonda sana mwanangu, nisamehe mimi mama yako”Aliongea Edna.
“Hey!! macho yako yanaona vizuri kweli , kanenepa au kakonda”Aliongea Roma ambaye alikuwa bize kuangalia habari za kimataifa kwenye TV na kumfanya Edna kumkata jicho.
Lanlan alikuwa na furaha sana siku hio na alienda juu na kuleta kila kitu alichochora kwa muda wote na kumuonyesha mama yake.
“Mama si hautoniacha tena?”Aliuliza Lanlan kwa wasiwasi na kumfanya Edna kutokwa na machozi na kumfanya Roma kukunja sura na kujiambia ni kheri kama wakipata mtoto mwingine awe ni mwanaume, maana watoto wa kike ni ngumu sana kudili nao.
Saa moja usiku ikielekea na nusu Nasra na Qiang waliandaa chakula mezani na wote kwa pamoja walijumuika.
Muda huo wakati Roma akiwa bize na chakula palepale sura yake ilijikunja mara baada ya kuhisi ujio wa mtu.
Edna na Nasra pia waliweza kusikia sauti za hatua ya miguu zikitokea nje na ni ndani ya dakika tu waliweza kusikia mlango ukigongwa.
Dakika ileile Roma alitumia uwezo wake na kuangalia nani anagonga na palepale uso wake ulijikunja na kutoka kwenye meza na kukimbilia nje.
“Bi Wema!!, Nini kimekupata?”Aliuliza Roma kwa mshangao.




SEHEMU YA 698.
Roma alimshikilia vizuri Bi Wema ambaye alikuwa akitaka kudondoka.
Nywele zake zilikuwa zimechanguka na uso wake ulikuwa umepauka mno , huku akiwa na mchubuko mkubwa kwenye paji la uso na michirizi ya damu kwenye midomo yake.
“Binti yangu Rufi mimi jamanii… Uwii Sir naomba umuokoe Rufi tafadhari ,, jamani Rufi ”Bi Wema aliangua kilio cha kwikwi mara baada ya kumuona Roma.
“Rufi!1”Akili ya Roma palepale lilichezwa na machale na hofu kwa wakati mmoja.
“Bi Wema acha kulia na usiongee chochote , ingia kwanza ndani nikutibu majeraha”
Aliongea Roma na hio ni mara baada ya kuoa Bi Wema alikuwa amevilia damu ndani kwa ndani , ukiachana na mamivu sehemu nyingine alikuwa sawa.
Muda huo Edna na Nasra walikimbilia nje huku wote kwa pamoja wakishangazwa na hali ambayo alikuwa nayo Bi Wema na walianza kuuliza maswali mfululizo huku wakiwa na wasiwasi mkubwa kwani Bi Wema alikuwa sehemu ya familia.
Lanlan licha ya umri wake kuwa mdogo alijua kuna tatizo ambalo limemtokea Bi Wema na yeye pia aliacha kula na kukimbilia kwenye sofa na kumwangalia baba yake akitumia nguvu ya andiko kumponyesha Bi Wema.
Kwa bahati nzuri ilikuwa rahisi kuponyesha viungo ambavyo vilipata majeraha , ijapokuwa alikuwa amepona lakini hakuwa sawa kihisia na aliishia kumshikilia Roma mkono akimbembeleza.
“Roma , Rufi amechukuliwa na majini , naomba umuokoe , nadhani wamemchukua kwenda kumpa adhabu , nina wasiwasi atakuwa hatarini , tafadhari msaidie binti yangu”
Bi Wema alikuwa na bahati mno , hakuwa na uwezo wowote wa kijini na mara baada ya kutupiwa kwenye ukuta alipoteza fahamu kwa zaidi ya masaa kumi na mara baada a kushituka kutokana na kujigonga kichwani alisahau ni kitu gani kilimtokea na mara baada ya kumbukumbu zake kukaa sawa ndio alikimbia kuja kumtafuta Roma.
Roma sasa mara baada ya kusikia kwamba Rufi amekamatwa na majini uso wake ulizidi kuwa mweusi na aling’ata meno kwa hasira.
“Ni majini kutoka koo ipi ? , wamesema ni wapi wanampeleka?”Aliuliza Roma.
“Nakumbuka kuna msichana ambaye Rufi amesema anamjua , yupo kama mchina hivi na amesema sijui ulimsamehe , alikuwa nao , alienipiga anamuonekano mweuepe na nywele nyeupe, kuna mzee aliekuwa ameongozana nao , sijui nini kiliendelea baada ya kupoteza fahamu…”
Bi Wema alielezea tukio zima , Roma alikuwa akitetemeka mno kwa hasira na mara baaada ya kusikia maelezo hayo palepale akili yake ilimkumbusha sura ya msichana wa kichina aliefahamika kwa jina la XiaoXiao na hata Nasra alimkumbuka palepale.
“Atakuwa ni yule msichana tuliekutana nae Kawe”
“Ipo wazi kabisa, haikuwa bahati mbaya , nilipaswa kumuua palepale kama sio Rufi kunibembeleza…’
“Bi Wema ondoa wasiwasi , nitamtafuta Rufi popote alipo na kumrudisha nyumbani akiwa salama , vinginevyo sitoweza kukuangalia usoni”
Roma hasira zilizidi kumkaba na alikuwa akivuta picha muda huo Rufi alivyokuwa akipitia mateso.
Kabla ya kutoroka Rufi alikuwa ni kama mnyama kwenye huo ulimwengu akitumika kama kifaa cha majaribio na kuingiziwa sumu mbaya mwilini.
Roma alijiambia awamu hio wanaweza wasiishie kufanya yale yaliopita bali mara mbili yake kwani anachukuliwa kama msaliti.
Roma hakutaka kuwaza sana , kadri alivyokuwa akiwaza ndio moyo wake ulivyokuwa ukiuma , alikuwa na deni kubwa kwa Rufi , kama sio yeye asingeweza hata kutengeneza vidonge lakini licha ya hivyo hakulalamika na aliishia kumwambia awape wenzake wameze kutokana na kukosa uwezo wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
“Edna, Nasra nitaenda kumtafuta Rufi sasa hivi , naomba uwaambie wengine kuhusu hili”Aliongea Roma akiwa tayari kwa safari lakini Edna palepale alimzuia kwa kumshika mkono.
“Unatkaa kufanya nini , unafikiri kuharakisha kwenda kumtafuta ndio utampata?”Aliongea kwa sauti na kumfanya Roma kusimama.
“Kwanza kabisa huna uhakika kama Rufi amerudishwa kwenda ulimwengu wa kijini au lah na hata kama utaingia kwenye huo ulimwengu je unajua ni wapi pa kumtafutia , nakumbuka Rufi alisema ulimwengu wa kijini unafanana na dunia ki ukubwa , unataka kumtafuta bila ya kuwa na mpango? , lakini pia je unajua namna ya kuingia huko ujinini?”
“Naweza kukamata mtu yoyote na kumpa mateso , nadhani watanipa uelekeo tu”
“Hata kama ukifanya hivyo na ukafanikiwa kumpata Rufi , je una uhakika unaweza kumtoa huko akiwa salama , sawa tuseme kwamba una uwezo wa kupambana na hao watu wasioonekana, je vipi kama wakikuzidi nguvu, unaweza kwenda huko na ukawachokoza na wakamtumia Rufi kama ngao na wakamdhuru na mpaka hapo haitokuwa na maana tena”
Aliongea kwa sauti na maneno yake yalimfanya Roma kujihisi ubaridi, alikuwa sahihi , Roma alijiambia ni siku hio hio tu alikutana na mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kutisha , kuna uwezekano wa kuwa na majini wenye nguvu zaidi yake.
Roma mara baada ya kupanda levo zaidi na zaidi alijihisi ni kama vile anaimiliki dunia lakini ukweli ni kwamba pengine kuna majini wenye uwezo mkubwa kuliko yeye ambao hawakujisumbua hata kushindana nae.
Ni kama sasa akili ilikuwa imemkaa sawa na kuanza kujiuliza maswali mengi.
Edna mara baada ya kuona Roma ametulia hatimae alijikuta akiwa na ahueni.
“Mume wangu , najua una wasiwasi , hata sisi pia tuna wasiwasi juu ya Rufi lakini hupaswi kutumia nguvu kudili na hili swala , kama utaenda kwa kurupuka kwa madhumuni ya kumuokoa utasababisha matatizo zaidi na zaidi , utawakurupusha na kufanya wajikusanye na kuanza kukushambulia , sio tu kwamba utashindwa kumuokoa Rufi lakini pia wewe mwenyewe utakuwa katika hatari , ushasahu kuna watu kibao ambao wanataka mbinu yako ya mafunzo?, ulipokuwa huku kwenye ulimwengu wa kawaida kutokana na sheria hawakuwa na uwezo wa kudili na wewe lakini ukiingia kwenye ulimwengu wao itakuwa ni habari nyingine, hio ni miliki yao , ninachoshauri kufanya ni kuingia kimyakimya na kumuokoa Rufi kwanza la sivyo utamuweka katika hatari na wewe pia utakuwa katika hatati”
“Kweli nimekosa umakini , upo sahihi ninatakiwa kutafuta namna ya kuingia kimyakimya”
“Najua kwa namna yoyote utaenda hivyo siwezi kukuzuia , Rufi ni mtoto wa Bi Wema hivyo unapaswa kumuokoa lakini lazima utambue kwamba wewe ni mhimili wetu hivyo unapaswa kuwa makini , Sawa?”Aliongea Edna kwa umakini huku macho yake yakiwa mekundu.
Roma alitingisha kichwa mara baada ya kuelimishwa na mke wake na palepale mpango ambao haukukamilika uliibuka katika akili yake.
Roma alikumbuka alipopambana na jini mwenye ngozi nyeusi kule Bagamoyo alichukua medali yake ambayo mara baada ya kuwauluza wale wajumbe wa Hongmeng walisema kwamba ni Dhana ya kijini ambayo hutumika kama ufunguo wa ulimwengu wa kijini lakini pia kama ngao.
Roma alijiambia anachotakiwa kufanya ni kutumia medali hio kutafuta njia ya kuingia katika ulimwengu huo na angejifanyisha na yeye ni jini.
Muhimu zaidi ni kwamba alikuwa na Dhana ya jani la upofu ambalo linaweza kubadilisha muonekano wake na levo ya nguvu zake za kijini , ili mradi tu upande wa majini kusiwe na jini ambalo lipo katika levo ya kuipita dhiki ya mapigo tisini na tisa ya radi , angekuwa salama.
Maana udhaifu wa Dhana ya jani la upofu ni kwamba ukikutana na jini ambalo lipo juu zaidi yako ki uwezo huwezi kuficha uwezo wako na muonekano.
Ukiwa jini au mtu mwenye nguvu kubwa ya kijini unao uwezo wa kubadili sura nyingi na majini au watu wa chini yako wasijue muonekano wako halisi lakini pale unapokutana na jini au mtu ambaye ana uwezo mkubwa ziadi yako wanakuona kwa sura yako halisi(Soul Bestowed body).
Kwa maneno marahisi ni kwamba huwezi kudanganya kiumbe chenye nguvu ya kijini kubwa kuliko ya kwako hata kama una Dhana yenye nguvu kiasi gani.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba Dhana inaweza kuwa na nguvu lakini nguvu yake itatokana na nguvu ya kijini , kwa mfano Cauldron ya Roma ni Dhana yenye nguvu lakini kutokana na Roma kuwa na nguvu ya chini basi Cauldron haiwezi kuonyesha uwezo wake wote.
Roma aliamini kwa kuwa na Dhana hizo mbili yaani medali na Janni la Upofu ingemrahishia kwenye mpango wake.
Kwasababu hawakumuua mara baada ya kumuona aliamini wasingemuua kirahisi na alichopaswa kufanya kwanza ni kumuokoa kimya kimya na mara baada ya kuwa salama basi angerudi kulipa kisasi.
Baada ya kuwaza kwa muda Roma aliona kabisa familia yake isingekuwa salama kuendelea kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam na kama kitu chochote kitamtokea katika ulimwengu wa kijini basi ingekuwa hatari sana kwao.
“Edna najua inaweza kuwa ni usumbufu lakini nataka umchukue Lanlan, Bi Wema na wengine wote kurudi visiwa vya wafu , ile sehemu ni karibu na Uingereza anapoishi Stern , Alice na Raphaeli kama majini watatoka na kutaka kuwashambulia lazima wataingilia , isitoshe Clark , Rose na Magdalena wapo levo ya nafsi hivyo ni salama zaidi”
“No, Lanlan anataka kwenda shule”Aliongea Lanlan mara baada ya kutafsiri sentensi ya Roma , ijapokuwa ameongea kwa kiswahili lakini Lanlan alishaelewa.
“Kaa kimya na nisikilize , hatupo kwenye majadiliano hii ni oda”Aliongea Roma kwa kufoka na kumfanya Lanlan kuficha uso wake katka mapaja ya mama yake.
“Nimekuelewa jitahidi kuwa makini”Aliongea Edna , hakutaka kujali hisia za Lanlan kwa wakati huo na kuwa mtiifu kwa kile anachoelewa na Roma.
Upande wa Nasra alikuwa kimya muda wote huku mikono yake ikiwa inamtetemeka.
Kwasababu walipaswa kuondoka kwa haraka kwenda Visiwa vya wafu, Edna alitumia muda huo kuandaa ndege binafsi ya kuwapeleka , haikuwa na haja kwa jambo kama hilo la usafiri Roma kusaidia hivyo alitaka kuchukua nafasi yake kama mwanamke mfanyabiashara.
Kuhusu maswala ya kampuni , angekuwa na uwezo wa kufanya kwa kupitia njia ya mtandao , isitoshe alikuwa ni mwenyekiti wa bodi tu kwa muda huo na Ernest ndio aliekuwa akihusika na shughuli aote za kila siku za kampuni na pia hata kama asiende kazini hakuna wa kumuuliza kwanini haji kazini , kampuni ni ya kwake .
Wakati Edna akifanya maandalizi upande wa Roma alikuwa akifanya mawasiliano na Ron na Sauroni na kuwapa maagizo huku akiwaambia anachokwenda kufanya , baada ya kumaliza alimpigia simu Tannya na kumweleza pia na kisha akampigia Najma ambaye yupo makao makuu ya nchi Dodoma.
Kwasababu Najma alikuwa chini ya serikali katika wizara ya mambo ya nje aliamini hakuna wa kumgusa lakini hakutaka kubahatisha hivyo alipiga simu kwa Sauron kutuma Ninja wa daraja la Kwanza kutoka Zero kuja kumpa ulinzi Najma kwa siri..
Baada ya kumalizana na usalama wa wanawake zake palepale alimkumbuka babu yake Afande Kweka na kumwambia
Dakika ileile alipiga simu kwenda kwa Afande Kweka na kumuelezea msala aliokuwa nao.
“Kuna ulazima wa kwenda kumuokoa huyo msichana?”Aliuliza Afande Kweka.
“Lazima , kama nisipoweza kumlinda mwanamke wangu nadhani napaswa kuacha kuwa mwanaume pia”
“Lakini unajua hatari iliopo kama ukienda bila ya kuwa makini?””
“Sidhani kama itakuwa hatari kulingana na hali ambayo Rufi anapitia kwasasa”
“Aisee wewe ni jasiri sio lakini pia nakuona kama mjinga , utajua mwenyewe utakachofanya sitaki kuingilia kwa lolote lakini hakikisha unarudi ukiwa salama una majukumu mengi kuliko unavyofikiria”Aliongea Afande Kweka na palepale alikata simu na kumfanya Roma kung’ata mengo kwa hasira.
Baada ya maandalizi Roma palepale alimrudishia Edna ile bangiri kama ulinzi wa ziada na kisha akamwambia Lanlan asizembee kwenye kujifunza alichomwelekeza na baada ya hapo aliondoka usiku huo huo.








SEHEMU YA 699.
Katika bara la Asia neno ‘Kunlun’ ilimaanisha asili ya milima yote , ukweli ni kwamba hadithi za hapo kale zinaelezea kwamba Kunlun ni sehemu ambayo ndio makazi Mama ya malkia wa kimagharibi(Queen of the West).
Asia ndio bara lenye historia pana na ya kale zaidi duniani , ni makazi ya staarabu za zamani zaidi ambazo zilishawahi kuwepo , ikiwa ni pamoja na Wasumeri , Waakkadi , Babeli na Waashuru.
Bara hili ndio dini karibia zote kubwa za dunia hii ndio zilipoanzia ikiwemo Ukristu , Uislamu , Ubuddha , Uhindu , Jainism , Sikhism na nyingine nyingi.
Hadithi za uwepo wa majini hazikuanzia tu ndani ya dini za kiarabu za enzi hizo kabla ya Uislamu wenyewe , ukweli ni kwamba viumbe majini katika kila tamaduni ndani ya bara la Asia waliitwa kwa namna yao.
Licha ya kwamba hakuna ushahidi wa kitafiti lakini inasemekana pengine majini walikuwepo kabla hata ya binadamu kuwepo katika uso wa dunia.
Ukienda kusini mwa mlima Kunlun ndani ya miliki ya China unakutana na sehemu ambayo huitwa Kekexil, hili ni eneo ambalo lipo ndani ya eneo la mji wa Kibuddha wa Tibet upande wa Qangtang.
Katika historia za enzi hizo watu walichukulia hilo eneo la Kekexil kama sehemu hatari zaidi ambayo binadamu hapaswi kukanyaga , wanasema kwamba binadamu ni ngumu sana kuweza kutoka akiwa hai akitembelea hilo eneo.
Hizi ni hadithi za enzi hizo ambazo zilivuma kutokana na watu ambao walitembelea hayo maeneo na kutoweza kurudi kabisa.
Kuna wengine walisema eneo hilo ilikuwa ni ngumu kwa binadamu kwenda kwasababu ni sehemu ambayo miungu hufanyia ibada na mambo kama hayo.
Kekexili ndio lango la zama za kale sana la mwanzo la kuingilia katika ulimwengu wa kijini.
Ulimwengu wa kijini maana yake ni ulimwengu wa uhalisia , sehemu ambayo ni nje ya ufahamu wetu wa kawaida wa kibinadamu, ni ulimwengu ambao huhusishwa na maajabu mengi.
Ulimwengu wa kijini ni sehemu ambayo inaaminika kila kitu kinawezekana, yaani sehemu ambayo mawazo na matamanio hujidhihirisha hapo hapo , majini wenyewe wanasema ni ulimwengu ambao huwaunganisha nafsi zao na viumbe wengine katika vipimo tofauti tofauti.
Mfano katika kitabu cha Peter J. Lewis anasema Ulimwengu wa kijini ni ulimwengu safi ambao upo nje ya mipaka ya nafasi na muda(pure realm that is beyond the limitations of space and time).
Mwandishi mwingine Michael Talbot katika kitabu chake cha Holographic universe anasema kwamba ulimwengu wa kijini umebeba taarifa zote za ulimwengu na njia pekee ya binadamu kupata taarifa hizo ni kwa kupitia kujifunza tamaduni za kijini.
Wanasema mara baada ya ujio wa wa dini kubwa duniani miungu wote ambao walikuwa wakiabudiwa ndio walikimbilia katika ulimwengu huo wa kijini na hio yote ni kutokana na kushuka kwa kiwango kikubwa cha nguvu ya kiroho katika uso wa dunia.
Kwasababu ni ulimwengu ambao umejitenga na ulimwengu wa kawaida eneo lake lilikuwa kubwa mno.
Ulimwengu wa kijini ni sawa na kusema Parallel Universe , yaani ulimwengu ambao upo sambamba na ulimwengu wa kawaida ambao una msingi wa tofauti wa kanuni za kifizikia.
Kutokana na mpangilio wa ulimwengu wa kijini nguvu ya kiroho ndani ya eneo hilo ni kubwa mno kuliko ulimwengu wa kawaida na ndio maana hata binadamu ambao hupenda kujifunza mafunzo ya kijini hupenda kujichimbia katika ulimwengu huu kwani ni rahisi kupanda levo ukiwa ulimwengu wa kijini kuliko ukiwa katika ulimwengu wa kawaida.
Ulimwengu ni mkubwa mno na umejigawa kimaeneo , kwa mfano karibia upande wa eneo lote la China hukaliwa na majini ambao hujiita Hongmeng.
Koo zingine za kijini kama vile Panasi , Xiao na Kekexil zilikuwa nje ya eneo la China.
Kabla ya Roma kufika eneo la Kekexil alilerekebisha kwanza levo yake ya kijini na Dhana ya jani la Upofu na kuonekana yupo levo ya Nafsi.
Juu ya kilele alipokanyaga Roma ni Mlima Kunlun , ni mlima ambao ulikuwa umefunikwa na barafu tupu na mara baada ya kukanyaga eneo la kileleni na kuanza kuangalia mazingira ya chini hakukuonekana binadamu yoyote ndani ya eneo hilo.
Ilikuwa ni kama alivyoweza kusikia , kwani watu wengi walichukulia kama mlima huo eneo la hatari zaidi kwa binadamu kukanganya.
Roma alikuwa akijua hapo kuna lango la kuingilia katika ulimwengu wa kijini , kwa maelezo ya Rufi alimwambia kuna lango kupitia baharini lakini njia salama zaidi ni kupitia juu ya kilele hicho cha mlima.
Sasa kila kitu hakipo sawa , uliwengu wa kijini ulikuwa ni swala la kimaajabu zaidi kuliko uhalisia na ulimwengu ambao unajitegemea na hauwezi kuonekana kwa macho ya kawaida.
Roma alijaribu kutembea kuzunguka hilo eneo huku akitumia uwezo wake kujaribu kutafuta mlango na aliweza kuhisi kitu ambacho hakikuwa cha kawaida juu yake na hio ni mara baada ya kuingiza nguvu ya kijini katika ile medali.
Juu yake ni kama vile anga lilikuwa likichemka na ile Medali ilizidi kutoa mng’ao wa rangi ya njano na kufanya eneo lile la anga kuzidi kupanuka.
Ilikuwa ni kama vile Roma alipitiwa na mwanga wa macho kwa haraka sana na palepale alijikuta eneo ambalo amesimama halikuwa na muonekano kama wa mwanzo wa mlima
“Ni ulimwengu mwingine kabisa!!”
Aliongea Roma kwa mshangao huku akikagua mazingira, ijapokuwa alikuwa juu ya mlima lakini mlima aliokanyaga ulikuwa tofauti na mlima uliokuwa ukionekana duniani , ajabu zaidi mbele yake kulikuwa na safu za milima mingi ambayo kwa uelewa wake safu hizo za milima hazipo katika ramani ya ulimwengu wa kawaida.
Kwa namna alivyoingia alijua kabisa hakuna mtu ambaye alihisia ujio wake kutokana na ile medali.
Dakika hio hio alijikuta akianza kupaa juu ya safu za milima ya barafu , mandhari yake ilikuwa ni ya ajabu mno.
Roma alikuwa akihisi msisimko wa ajabu ndani ya eneo hilo , ilikuwa ni sehemu ambayo kuna msuguano mkubwa wa nguvu za kiroho mara mia zaidi ya dunia ya kawaida.
Lakini Roma alijiambia licha ya uwepo wa nguvu hii haina maana kama huwezi kuibadirisha na kuwa nguvu ya kijini, ni kama vile uwe na risasi bila bunduki.
Roma alitumia uwezo wake kuchunguza eneo hilo na aligundua kila upande ni safu za milima katika mzingo wa kilomita mia moja na uwezo wake uliishia hapo na alijikuta akikosa dalili yoyote ya kuhisi kiumbe chochote na hakujua ni upande upi anapaswa kchukua.
Roma alijikuta akikosa chaguo na palepale akili yake ilimwambia achague upande wa mashariki.
Ajabu ni kwamba katika ulimwengu huu ni tofauti na ulimwengu wa majini pepo , ulimwengu wa majini pepo ilikuwa ngumu sana kupaa kutokana na anga lake lilivyo lakini katika ulimwengu huo kupaa ilikuwa rahisi zaidi kuliko hata alivyokuwa katika anga la dunia ya kawaida.
Roma alitumia spidi katika kupaa na ndani ya dakika kumi zote za kupaa hakuweza kuona dalili yoyote ya nyumba wala kiumbe cha aina yoyote , yaani kila kitu ilikuwa ni barafu bila miti , alijihisi ni kama vile yupo ndani ya bara la Antarctica lakini alijiambia hapo sio kama Antarctica eneo hilo ambalo limetawaliwana barafu ni kubwa mno kuliko bara hilo, alijiona labda yupo sayari nyingine ya barafu.
Dakika ambayo alijiambia anapaswa kubadilisha muelekeo alianza kuhisi kuongezeka kwa nguvu ya kijini na hisia zake palepale zilimwambia kuna kiumbe kinamsogelea.
Muda huu Roma alikuwa amebadili muonekano wake kabisa , hakuwa Roma alikuwa na sura ambayo imechanganya huwezi kusema ni mwarabu , huwezi pia kusema ni Mchina au Mkorea wala mzungu yaani yupo katikati.
Roma alipanua uwezo wake wa hisia wa kijini ili kuzingira eneo lote na na hapo hapo ndipo aliweza kugundua viumbe wanaosafiri kwa kasi ambao mmoja wapo yupo katika levo ya kuiepuka dhiki yaani wakiwa na uwezo wa kudhibiti moto wa rangi ya njano huku mwingine akiwa yupo katikati mwa levo ya nafsi.
Kufumba na kufumbua tu walitokeza angani mwanaume na mwanamke wenye muonekano wa ujana na kumfanya Roma awaangalie kwa tabasamu.
Mwanaume mrefu alikuwa na mvuto wa ajabu mno na alionekana kama kijana wa umri wa miaka ishirini hivi huku akiwa ameshikilia panga ambalo lipo ndani ya ala.
Mwanamke pia alikuwa amebeba panga ambalo lipo kwenye ala akiwa amelining’iniza mgongoni na kwa muonekano wake wa ngozi ya kuchanganya alikuwa mzuri mno na alionekana mdogo kuliko yule mwanaume.
Alikuwa amevalia vazi la gauni rangi nyekundu huku akiwa amesuka nywele zake kama mkia kurudi nyuma ambao umefika mpaka kwenye kiuno,
Baada ya kumuona Roma amesimama hewani bila ya kusogea walijua pengine alikuwa akiwasubiria hivyo na wao walisimama na kumwangalia kwa macho yenye shaka ndani yake.
Muda huo Roma alionekana kuwa na levo ya nafsi hivyo hawakumuona kama tishio , ukweli walimuona Roma kama jini mwenzao tu.
“Mkubwa kwanini umesimama njiani?”Yule mwanaume aliongea kirafiki licha ya muonekano wake kuonekana kutosomeka anawaza nini.
“Ndio mara yangu ya kwanza kuingia kwenye huu ulimwengu wa kijini hivyo sina uelewa na uelekeo wa maeneo, je naweza kuuliza maswali kuhusu huu ulimwengu?”Aliuliza Roma huku akiwa makini na muonekano wao , kama wangebadili muonekano ingemaanisha kwamba kauli yake ina makosa na wangemshuku na hapo ndio wangeenda kutoa taarifa kwa walinzi na usalama wake ungekuwa hatarini.
Hivyo alijiambia kama wangemfahamu njia ya haraka ni kuwaua kabla hawajaenda kutoa taarifa.
Hata hivyo Roma hajawahi kuwa mtu mzuri , ukweli ni kwamba Roma alikuwa ni mtu mkatili sana hivyo kwa usalama wake na wa Rufi asingejali kuua.
“Oh!, kwahio wewe ni binadamu, nadhani utakuwa umeingia katika levo ya nafsi na kuletwa huku na wajumbe wa Hongmeng si ndio? .. hehe basi wewe ni mjinga , kama hujui hili eneo ulipaswa kuwaambia Hongmeng wakutembeze wenyewe , ikitokea umekosa nguvu unaweza kudondokea kwenye eneo hatarishi na unaweza usitoke ukiwa hai”Aliongea yule mwanamke ambaye alikuwa amevalia gauni jekundu.
Roma hatimae alishusha pumzi kwa ahueni na kujiambia sio mbaya wamempa ubini wao wenyewe, kwanzia muda huo yeye ni binadamu alieletwa na Hongmeng kutoka ulimwengu wa kawaida.
“Upo sahihi, mimi ni mtu wa kujitenga sana hivyo nilishindwa kuomba msaada”
“Je naweza kufahamu jina lako?”
“Naitwa Xiao Chen”Aliongea Roma , alijua kabisa kwasababu yupo hapa kwa ajili ya kumuokoa Rufi na watu waliomtekani koo ya Xiao basi anapaswa kufanana nao angalau kimajina , isitoshe muonekano wake kwa mbali ulikuwa ukifanana na mchina.
“Naitwa Zomu na huyu ni dada yangu Zato , tumefurahi kukufahamu bwana Xiao Chen”
“Zomu je naweza kujua hapa ni wapi , nimesikia katika ulimwengu huu kuna koo zingine zaidi kubwa ukiachana na Hongmeng , nimesikia ukoo wa Xiao , Kekexil na Panas, je naruhusiwa kutembelea hizi koo?”
“Wewe ni jasiri mno kwa mtu ambaye ni mgeni , hujaambiwa kwamba Hongmeng haipatani na koo zote tatu kubwa, kwa binadamu kama wewe ambaye uwezo wako ni wa chini , hakika una ujasiri usiokuwa wa kawaida”Alijibu yule mwanadada alieitwa Zato.
“Sikujua hili , nilitaka tu kujua zaidi na zaidi juu ya huu ulimwengu”
“Hapa tulipo ni juu ya Mlima Tembe ni safu za milima ya theruji inayotembea, hizi safu za milima ya zinaendelea kwenda mbali Kaskazini kwa zaidi ya mamia ya kilomita , ukoo wa Xiao upo upande wa Kaskazinimagharibi , Kisiwa cha miungu wa Hongmeng ni katikati kabisa , Kekexil ni upande wa Kaskazini mashariki na uelekeo huo maelfu ya kilomita kuelekea safu za milima ya Bareni ndio inapatikana Koo ya majini chotara ifahamikayo kwa jina la Panasi.
Roma alikariri uelekeo na alijiuliza ni wapi aanzie kumtafuta je aende Kekexil au kwenye ukoo wa Xiao , upande mwingine pia alikuwa na shauku ya kutaka kuona namna ambavyo ulimwengu huu wa kijini ulivyojipanga na tamaduni zake hisia zake zilimwambie pengine ndani ya huu ulimwengu hakuna bahari kama ilivyokuwa kwa ulimwengu wa majini pepo.
Kama Rufi amerudishwa katika huo ulimwengu ilimaanisha lazima atakuwa kwenye moja wapo ya koo aidha Kekexil au Xiao , Roma alijiuliza ni wapi aanze , hakutaka kutafuta kila mahari kwa kugogopa anaweza kukutana na mtu ambae ana nguvu kuliko yeye na kumgundua ni gaidi alievamia ulimwengu huo.
“Kama huna maswali mengine , sisi tunaondoka”Aliongea Zomu , ilionekana walikuwa na haraka.
“Je naweza kujua ni upande upi mnaelekea na kama hamtojali naweza kuongozana na nyie?”
“Tunaelekea Kekexil”Aliongea na kumfanya Roma macho kuchanua na kujiambia hapo safi , hatimae ashapata wa kumtembeza..
“Kama mnaelekea huko je tunaweza kungozana?”aliuliza Roma na kumfanya Zomu na Zato kuangaliana kwa mshangao kutokana na ombi lake , isitoshe katika ulimwengu huo Hongmeng hawakuwa wakipatana na koo zingine.
“Sisi hatuna tatizo kwenda ukoo wa kekexil kwasababu ukoo wetu una ushirika nao , lakini wewe huna sababu ya kwenda huko , kama tutaenda pamoja walinzi wa Kekexil watakukamata na itakuwa ngumu kwetu kuelezea ubini wako kama binadamu anaetokea Hongmeng , isitoshe Hongmeng ndio wanaopokea zaidi binadamu kuliko koo zingine”
“Unaonekana kama majini wazuri hivyo sina haja ya kuficha ukweli , ipo hivi, sipendi kuishi Hongmeng kabisa na niliposikia kuna koo zingine ambazo zina ustaarabu ulioendelea pamoja na mbinu za kutosha za mafunzo nilivutiwa na ndio ninapotaka kwenda kuishi”
“Unajua unachokifanya ni hatari , unachotafuta ni kukimbilia ndani ya koo zingine ambazo hazitaki kujihusisha na binadamu wa Hongmeng, una uwezo wa chini mno na Kekexil wanaweza wakakukataa , isitoshe Hongmeng watakuchukulia kama msaliti hivyo ukikataliwa utakuwa katika hatari”
“Binadamu kujifunza mbinu za kijini ni swala la kuchukua risk kubadilisha hatima zetu, bila ya kuwa na nguvu za kijini za kutosha unaweza tusikamilishe matamanio yetu naamini nitatafuta nafasi yangu katika miliki ya Kekecxil na kukubalika”
“Kama unalazimisha kwenda basi sisi hatuwezi kukuzuia”
“Kaka umekuwa kichaa , yupo kwenye levo ya nafsi na hana uelewa na ulimwengu wa kijini na tamaduni zake , kama akisaliti Hongmeng anaweza asipate hata nafasi ya kujutia akikataliwa na Kekexil”Aliongea Zato.
“Najua unachomaanisha Zato lakini kama yupo tayari hakuna haja ya kumzuia, na pia tunahitaji msaada tukifika huko hivyo hakuna tatizo”Aliongea Zomu na kumfanya Zato kuwaza jambo na macho yake kuchanua.
Roma hakujua wanachomaanisha na hakujua kama walikuwa wakimpangia jambo baya huko anakoelekea lakini kutokana na uzoefu wake wa kusoma watu Zomu hakuonekana kama mtu mbaya.
Majini hawakuwa watu wa hila na vigeugeu kama walivyokuwa binadamu, hivyo kama hakupendi hawezi kuigiza hakupendi na kama akikupenda basi amekupenda kweli.
“Tunaweza kuelekea pamoja , lakini tutaweza kuhitaji msaada wako”
“Msaada gani?”Aliuliza Roma na palepale Zomo alielezea kila kitu na kwa maneno yake ilionekana kuna koo ndogo ya kijini ambayo ilifahamika kwa jina la Miliki ya Zaola, ni koo ambayo ipo chini ya Kekexili na ukiachana na kuwa na mali nyingi ikiwemo madini ya ardhini na vito vya thamani lakini hawakuwa na vipaji ndani ya koo yao ambao wana uwezo wa kuvuna nishati ya mbingu na ardhi.
Katika ulimwengu huo nguvu haipo kwenye utajiri bali ipo katika uwezo wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi pamoja na vitendea kazi yaani umiliki wa Dhana pamoja na vidonge na vitu hivyo ndio ambavyo ukoo wa Zaola ulikosa.
Katika ukoo huo jini pekee ambaye uwezo wake ni wa juu ni babu yao afahamikae kwa jina la Zaoli ambaye amepita Dhiki sita za maji ya baridi na kufanikiwa kudhibiti maji ya kawaida.
Sasa kutokana na uzee wake ameshindwa kudhibiti maji ya kiroho kwa kila namna ambavyo amejaribu kufanya hivyo.
Na kama ataendelea kushindwa kufikia katika levo hio basi angeweza kufariki ndani ya miaka mitatu ijayo na kama atafanikiwa kutoboa kwenda kwenye levo ya kudhibiti maji ya upako basi maisha yake yangerefuka kwa zaidi ya miaka mia moja.
Hivyo ukoo huo haukuwa na chaguo lingine zaidi ya kwenda kuubembeleza ukoo wa Kekexil kwa ajjli ya kuwapatia rasilimali ambazo zingemsadia mzee wao hata kama ni vidonge daraja la kati, walichokuwa wakihitaji ni busta kidogo tu ili kumsaidia Mzee Zaoli kupanda levo.
Licha ya kwamba ukoo wa Zaola ulikuwa na ushirikiano na Kekexil lakini ukweli ni kwamba upatikanaji wa vidonge ulikuwa mgumu sana katika ulimwengu huo wa kijini , yaani ni kama dhahabu ilivyoadimu ndio vidonge vilivyokuwa adimu na thamani kubwa.
Hivyo vijana hao ambao wameagizwa kwa niaba ya ukoo walijua kabisa nafasi zao ni ndogo za kupata vidonge hivyo lakini bado waliona wana haja ya kujaribu kwenda kuomba.
Roma alijiambbia majini hao wanatia huruma , alikuwa na furushi la vidonge vya daraja la juu amejaza kwenye hifadhi yake , lakini majini hao wanakwenda kuomba.
Mpaka dakika hio aliona pengine yeye ndio tajiri kuliko majini wote ndani ya ulimwengu huo maana utajiri wao ulikuwa kwenye umiliki wa vidonge na sio mali.
Sasa unachopaswa kuelewa hawa Zaola pengine haina haja ya kuwaita ukoo bali ni vijakazi waliopo chini ya ukoo wa Kekexil hivyo hawakupewa kipaumbele hata kidogo.
Waliamini kama watakuja kuwa na majini ndani ya ukoo wao ambao wana nguvu kubwa kama koo zingine basi Kekexil wangewaheshimu na kuwafanya kipaumele.
“Mmenielezea stori yenu yote lakini hamjasema ni kwa namna gani napaswa kuwasaidia”
“Tunataka tuwe kama madalali na kukuingiza katika ukoo wa Kekexil”
“Madalali!!”
Roma alijikuta macho yake yakijifumba palepale na alionekana alikuwa ashaelewa wananchomaanisha.
Kutokana na koo zingine za kijini kutokuwa katika maelewano mazuri na Hongmeng ilikuwa ni jambo la kawaida kwao kutafuta watu wenye uwezo wa mbinu za kijini.
Yaani walitaka kuwa kama madalali na kumfanya Roma wamemuiba Hongmeng na kumleta ndani ya ukoo huo na wamtumie kuombea vidonge.
“Hakuna shida , mimi nipo tayari kwanza nina deni kwenu kwa kukubali kunipeleka huko”Aliongea Roma na kumfanya Zomu na Zato macho yao kuchanua kwa furaha.
Roma hatimae alitulia , hakutegemea angekutana na majini hao ambao walikuwa wazuri kwake mara tu baada ya kungia katika ulimwengu huo wa kijini.
Muda uleule walianza safari ya kuchanja mbuga huku Roma akitumia muda huo kujifunza mazingira ya ulimwengu huo wa kijini,vitu vingi vilimshangaza Roma na kujiuliza kama ulimwengu wa kijini upo paraller na dunia ya kawaida basi bonde ambalo lipo chini yake lingekuwa ni bahari na sio nchi kavu kama anavyoona na alijiambia au ndio maana watu husema majini huishi chini ya bahari , ukweli ni kwamba alishawahi kusikia hizo stori ila hakuwahi kuzitilia maanani.
Yaanni kwa alichokuwa akiona Roma ni kwamba pengine ulimwengu wa kijini ulikosa bahari licha ya kufanana na dunia kimuundo na sehemu ambazo zilipaswa kuwa bahari ni ardhi ambayo unaweza kukanyaga.
Walisafiri kwa spidi sana kwa zaidi ya nusu saa nzima na hatimae waliweza kutoka katika safu ya milima ya theruji na kutokea katika bonde na tambarare ambazo zimezingirwa na mito mikubwa iliokuwa iliokutana katikati na Roma hakuelewa inatiririsha maji yake upande upi.
Kwa kiasi flani eneo hilo lilifanana na ulimwengu wa majini pepo , hususani kwenye miti , kuna miti mingi ambayo kwenye ulimwengu wa kawaida huwezi kuiona na ilitangazwa kupotea lakini kwenye ulimwengu huo ilikuwepo.
Kadri walivyokuwa wakisonga mbele hatimae waliweza kuona jengo likitokeza mbele yao na kuongezeka ukubwa kadri walivyokuwa wakilisogelea huku angani wakionekana ndege wa namna mbalimbali.
Roma alishangazwa na usanifu wa jengo hilo rangi nyeupe ambalo lilikuwa mbele yake , licha ya kwamba limejengwa kwa usanifu wa kizamani lakini lilikuwa likipendeza mno na limeenda hewani mno kama ghorofa.
Pembeni yake chini ya jengo hilo kulikuwa na nyumba zimejengwa kwa staili ya kipekee ambazo zimeachana kwa umbali mrefu huku likiacha uwepo wa katikati wenye bustani na mto ambao kumejengwa Gazebo kubwa..
Kabla hawajalifikia lile jengo Roma aliweza kuona mng’ao flani kama wa rangi nyekundu hivi inayofifia umezingira lile jengo , ni kama vile vile vijitaa vinavyofungwa bar ndio ilivyokuwa na kwa haraka haraka Roma alijua lazima itakuwa ni uzio wa kijini.
“Hilo jengo kubwa na eneo lote hili ni makao makuu ya Kekexil , koo zingine ndogodogo ambazo zipo chini ya miliki zina makazi yao mbali kabisa na eneo hili lakini asilimia kubwa ya majini wote wenye nguvu hukaa hapa na hili ndio jengo Jeupe fahari ya milki na ndio mahali ambapo huhifadhiwa vitabu na vidonge , ni sehemu yenye ulinzi mkali sana na hakuna ambaye anaruhusiwa kuingia bila ruhusa ya wazee wa ukoo”
Roma mara baada ya kusikia eneo hilo lina vitabu na vidonge tamaaa pale ilimwingia na kujiambia hili ni eneo ambalo anapaswa kutembelea kwa namna yoyote ile ndio amekuja kumuokoa Rufi lakini lazima safari yake aipe vionjo onjo kwa kutalii na kujifunza mengi.
Wale kaka na dada mtu hawakujua kama Roma alikuwa na mipango yake kichwani tena miovu.
Roma hakutaka kutumia uwezo wake kumtafuta Rufi kwani alijua lazima angegundulika hivyo kwa adabbu na utii aliwafuata Zomu na Zato.
Kuna hali flani ilimfanya Roma kutamani kuishi ulimwengu huo, kulikuwa na mazingira mazuri mno na pia kutokuwepo kwa miundombinu ya usafiri kama ndege na magari pamoja na kutokuwepo kwa maviwanda ilifanya eneo hilo kuwa na hewa safi mno na ya kuvutia pua.
Roma aliweza kushuhudia majini wakiruka na kutua kwenye eneo hilo , huku eneo la mbali aliweza pia kuona majini rika la vijana wakiwa wamekaa chini mkao wa tahajudi wakiendelea na mafunzo.
Kitu pekee cha kustaajabisha ambacho Roma aliona ni ndege wa kubwa wafananao na Mwewe fulani hivi wa kupendeza wakiwa wanatambaa













SEHEMU YA 700.
Kwa maelezo ya Aoiline Roma alikumbuka kwamba ni majinni pepo tu ndio ambao walikuwa wakizaliwa na muonekano mbaya sana kutokana na asili yao ilikuwa ni kulipa pepo nguvu tofauti na kulishinda, majini hao wazuri miili yao ilikuwa ni ya kibinadamu kabisa ni sawa na kusema walikuwa ni binadamu koo ya kijini licha ya kusemekana kwamba huzaliwa kama roho yenye sura nyingi na baada ya kufika levo ya nafsi ndio hupewa miili ya kibinadamu.
Roma aliongozwa na wale majini wawili kitu na kaka yake na walienda moja kwa moja kutua katika eneo la wazi ambalo lilikuwa ni kama eneo la mafunzo kwa majini.
Na palepale walisogelewa na mzee aliekuwa na nywele nyeupe ndefu saa kwenda chini aliekuwa amepeleka mikono yake nyuma kama kafungwa pingu vile.
“Zomu na Zato mnafanya nini hapa?”
“Mkuu wa Chemba tumetumwa kwa niaba ya ukoo kuja kuomba vidonge ka ajili ya babu yetu , babu yagu yupo katika hatua za mwisho za uhai wake na kama hatoweza kuifikia levo ya maji ya upako hatoweza kuwa na maisha marefu tena , tunahitaji vidonge kwa ajili ya kubusti uwezo wake”
“Oh , kwahio mpo hapa kwa ajli ya vidonge , Zaoli bado tu hajafa , kwa uwezo wake pengine ni baraka kufikisha levo aliofikia nayo kwasasa , sidhani akipewa vidonge itamsaidia kwa lolote”Aliongea akiwa na muonekano wa majigambo na kuwafanya Zato na Zomu sura zao kubadilika.
“Mkuu wa Chemba , tumekuja na huyu binadamu , anaitwa Xiao Cheni , ni rafiki mzuri alietokea katika ulimwengu wa kawaida kuja ulimwengu wa kijini kupitia Hongmeng , ninampendekeza kujiunga na ukoo wa Kekexil”
“Kwa jina langu naitwa Xiao Cheni , nimetokea kupenda ukoo wa Kekexil kuliko koo zote na Braza Zomu hapa ndio alienishauri kujiunga na huu ukoo”Aliongea Roma ukweli kwa namna moja ama nyingine alijikuta akimchukia huyo mzee kwani alionekana kama mtu mwenye roho mbaya hivi.
Alikuwa ni mzee alievalia joho , asilimia kubwa ya majini wote walikuwa wanavalia majoho kwa wanaume na kwa wanawake walikuwa wakivaa magauni.
“Nilitaka kuuliza huyu binadamu ambaye yupo kwenye levo ya nafsi mmetoa wapi kumbe ametokea Hongmeng, sasa wewe ndio kwanza upo mwanzoni mwa levo ya nafsi , huna wasiwasi tunaweza kukukataa na ikitokea hivyo utachinjwa na Hongmeng kwa kuwa msaliti”
“Mimi bado mdogo , ijapokuwa ndio kwanza nimeingia levo ya nafsi lakini haitochukua miaka mingi nitakuwa nishaingia levo ya kuipita dhiki wakati huo nitakuwa na mchango mkubwa sana kwa miliki ya Kekexil”
“Haha.. unajitamba sio , tutaona kama utaweza kuishi hata siku moja kabla ndoto yako ya kufikia levo ya dhiki haijafutika”
Mzee huyo mkuu wa Chemba ambaye alifahamika kwa jina la Ganyo hakumkataa Roma moja kwa moja.
Kekexil sifa yake kubwa ni kupokea kila jini au binadamu ambaye anaomba hifadhi ambaye kwa namna moja ama nyingine angeweza kuwa na mchangao kwao.
Ukweli ni kwamba Hongmeng haikuwa na maelewano mazuri na Kekexil na hio yote ni kutokana na kwamba Kekexil ukiachana na utajiri waliokuwa nao lakini pia walikuwa wakiiba sana majini wa uwezo mkubwa kutoka Hongmeng kwa kuwashawishi na hata ndan ya eneo hilo kulikuwa na binadamu wengi ambao walikuwa na rangi fotafuti tofauti.
Ilikuwa ni kama ambavyo alisema Rufi , kwamba Kekexil haikubagua binadamu wanaotaka kujifunza mafunzo ya kijini.
“Mkuu wa ukoo hayupo na hatujui ni lini atarudi nyie wote watatu nitawapelekea kwa Mkubwa namba tatu ili afanye yeye maamuzi”Aliongea Ganyo.
Mkubwa namba tatu aliekuwa akimsemea ni mtoto wa mkuu wa ukoo wa kekexil ambaye aliitwa Mohi na baba yake ambaye ndio mkuu aliitwa Menui na akitoka Mohi anafuatia Mohena.
Kwa haraka haraka Roma alichojjifunza kupitia Rufi ni kwamba wakuu wote wa ukoo majina yao yalikuwa yakianza na herufi M na baba yake Rufi aliitwa Mohena .
Baada ya kutembea kutoka katika uwanja huo waliongozwa kuelekea katika jengo ambalo lilikuwa upande wa mashariki , kitu ambacho alipenda Roma ni kwamba tamaduni zao zilikuwa zikiheshimu sana mimea , yaani nyumba moja kwenda nyingine ilitenganishwa na bustani kubwa ya maua ambayo yalikuwa yakisambaza harufu nzuri.
Kwa akili ya haraka haraka Roma aliamini maua hayo yanaweza yasiwe ya kawaida lakini kwa namna moja ama nyingine alipenda harufu ya eneo hilo , eneo hilo lilikuwa na hewa safi sana ya oksijeni huku harufu ya maua kama Rose ilikuwa imezifunika pua zake.
Hata hivyo ilileta maana, majini walichobarikiwa ni kuwa na miili misafi sana kwani ndio hatua ya kwanza ya kupanda kwao levo, hupaswa kusafishwa na hapo ndio sasa huvuna nishati.
Roma aliishia kujisemea kama ingekuwa na uwezekano angefanya eneo hilo kama utalii na kuja na wanawake zake kula bata.
Baada ya kutembea mita kama mia moja hivi waliweza kuingia ndani ya jengo ambalo limejengwa kwa miti mwanzo mwisho lakini ukiangalia kwa mbali ungesema limejengwa kwa matofali.
Kwa nje ni jengo la kawaida lakini ndani yake kulikuwa kumependeza mno , kulikuwa na nashki nyingi za madini ya dhahabu kuanzia mlangoni mpaka kwenye viti na vikombe ambavyo wanatumia.
Baaada ya kufika ndani ya jengo hilo ambalo ni kama ukumbi waliweza kumuona mwanaume mzee aliekuwa amevalia joho la rangi ya bluu bahari na yeye akiwa na nywele nyeupe.
Na jambo hili lilimwambia Roma pengine walipendelea kuwa na nywele ndefu nyeupe kuliko kuwa na nywele nyeusi.
Jini huyo ndio alifahamika kwa jina la Mohi aliwaangalia mara baada ya kuingia na hakubadili muonekano mara baada ya kumuona Ganyo ndio ambaye alikuwa ametangulia.
Kwanzia madirisha mpaka milango ilikuwa imenakshiwa na maneno ya ajabu mno pamoja na picha za vuiumbe mbalimbali ambao Roma hakuwajua.
Roma mara baada ya kumchunguza huyo jimi aliefahamika kwa jina la Mohi aliweza kugundua alikuwa ashavuka levo ya Dhiki na alikuwa kwenye levo ya katikati ya kutawala nguvu ya kudhibiti maji.
“Mkubwa namba tatu , Zomu na Zato kutoka koo ya Zaola wapo hapa kwa ajili ya kuongea na wewe wakiambatana na binadamu ambaye anataka kujiunga na miliki yetu , Zaola wanataka vidonge kwa ajili ya kumsaidia babu yao kumbusti kuingia levo ya maji ya upako”
Yule mzee jini aliinua uso wake na kumwangalia Roma kwanza kwa macho ya kivivu , licha ya kuonekana mkubwa lakini alikuwa na uso ambao haukuwa na mikunjo kabisa na alikuwa ni mtanashati mno.
Kwanzia hapo Zomu na Zato wakiwa wamepiga magoti walianza kumpamba Roma na kusema kwamba atafanikiwa kuingia levo ya kuipita dhiki ndani ya muda mfupi hivyo anapaswa kumpokea na kuwalipa malipo ya vidonge kwa ajili ya babu yao.
Lakini jini Mohi alikataa na kusema Roma hana ‘potential’ ya kuweza kupanda levo kwa haraka na kuingia levo ya kuipita dhiki hivyo hawezi kutoa vidonge vyenye thamani kwa kubadilishana na mtu ambaye hana thamani kama Roma.
Waliendelea kubembeleza lakini koo hio hakika ilionekana kutowajali kabisa familia ya Zaola kwani huyo mzee hakubadili maamuzi yake , msimamo wake ulikuwa ni uleule kwamba hawezi kutoa kidonge cha thamani kwa ajili ya kumchukua Roma.
Roma mpango wae haukuwa ni kukubaliwa na familia hio ila alikuwa na misheni ya kumtafuta Rufi lakini kutokana na ukubwa wa eneo hilo pamoja na ulinzi wake aliamini isingekuwa rahisi na asingeulizia pia kwani angegundulika hivyo kwa namna yoyote ile aliona anapaswa kupata muda wa kutosha ndani ya eneo hilo ili kufanya uchunguzi wa chini chini kujua kama Rufi yupo kwenye koo hio au koo ya Xiao.
Mazungumzo hayakudumu sana na mzee Mohi alisema atawapatia Zato na Zomu kidonge cha thamani ya chini sana kwa ajili ya kumsaidia babu yake kuishi angalau miaka minne jambo ambalo liliwafanya kutoridhika kabisa na kuangusha chozi kiasi cha kumfanya Roma kuwaonea huruma na aliona ngoja awasaidie.
“Mkubwa namba tatu , mimi Xiao Chen nina jambo ambalo nataka kuongea”
“Najua una kitu cha kuongea lakini haina haja , miliki hii itakupokea na tutakupatia baadhi ya vidoge vya daraja la chini ili vikusaidie kupanda levo, ndani ya miaka michache ijayo utatumikia vizuri koo yetu ya Kekexil na kuhusu Hongmeng usiwe na wasiwasi tutakulinda”
“Nilitarajia miliki hii haiwezi kunitendea vibaya , lakini licha ya kwamba nipo kwenye levo ya nafsi nina jiamini kwamba nina kipaji kingine ambacho kinaweza kushinda vizuizi vingi , Braza Zomu anapaswa kupata angalau kitu ambacho kinaendana na thamani yangu kwani ndio alienishawishi kuja hapa”Aliongea na kuwafanya wote kumshangaa na kumwangalia kwa maswali.
“Unamaanisha nini?”Aliuliza mkuu wa Chemba bwana Ganvo.
“Tokea nilipokuwa mdogo niliaminika kuwa na mwili usiokuwa wa kawaida , ijapokuwa nipo kwenye levo ya nafsi lakini ninao uwezo wa mapigo ya jini wa levo ya nafsi bila kupata madhara , kama kipaji changu hiki mtakichukulia siriasi na kumpatia Zomu na dada yake vidonge vya daraja la kati basi mimi Xiao Cheni nitahakikisha naitumikia vizuri miliki ya Kekexili”
“Haha,… hahaha.... ni adimu sana kuona mtoto kama wewe tena binadamu ambaye huogopi kifo , nakataa maneno yako maana sidhani unao hata uwezo wa kuhimili nguvu ya msisimko kutoka kwa jini mwenye uwezo wa levo ya nafsi au umemeza roho ya kobe wa kimilenia ndani yako”.
Mwanamke mrembo sana mwembamba mwenye shingo kama ya twifa ambaye ana manyonyo ya wastani aliingia ndani ya eneo hilo kwa kicheko , alikuwa amevalia gauni kama vile ni binadamu wa kawaida , yaani mavazi ya kileo lakini ya heshima.
Muonekano wake iwe ni kama anatabasamu , anacheka au amenuna alikuwa akivutia mno.
Hakuwa peke yake , nyuma yake kulikuwa na mwanamke na mwanaume
Mwanamke alikuwa amevalia kitamaduni zaidi kama vile ni mjapani lakini hakuficha urembo wake , alikuwa na nyusi nyingi ambazo zimejichora kama vile ni jani la mti.
Upande wa mwanaume ndio alimshngaza zaidi Roma kwani alikuwa amevalia mavazi ya kileo kabisa , alikuwa amevaa suti na buti kubwa za rangi nyeusi
Mara baada ya mwanamke yule kusogea kuingia ndani ya eneo hilo alimwangalia Zomu na Zato ambao walikuwa wamepiga magoti mbele ya Mohi.
Roma alishangaa huyo mwanamke na mwanaume wote ni kama ndio wanarudi kutoka ulimwengu wa kawaida kwani walikuwa wapo kifasheni zaidi kuliko majini wote aliowaona.
“Lilsi Shemeji yangu na Manyani naona mmerudi mapema hahaha….habari za huko mlikotoka , vipi kaka yangu Shagoni amekuja na yeye?”Aliongea yule mkubwa namba tatu na palepale majina yao yalimfanya Roma kuyatambua.
Rufi alimwelezea kila kitu kuhusu familia ya baba yake ilivyokuwa, huyo mwanamke aliekuwa ameingia kwa kicheko alifahamika kwa jina la jina lilsi ni mke wa baba yake Rufi na msichana alieitwa Manyani alievalia kama mjapani alikuwa ni mdogo wake Rufi yaani dada yake wa kambo
Ijapokuwa Roma hakuelezewa vizuri na Rufi lakini alichojua ni kwamba mama yake wa kambo ndio alikuwa kinara kwenye kumtesa na ndio ambaye alipendekeza Rufi kuuzwa kwa kivuli cha ndoa kwenda ukoo wa Xiao.
Roma alifuatisha maongezi yao kwa makini na habari nyingi zilikuwa zikizungumzia kuhusu jini alieitwa Shagoni ambaye ana uwezo wa ajabu wa kimapambano na alimuuliza Zato huyo Shagoni ndio nani na hapo ndio yule mwanamke aliefahamika kwa jina la Lilsi alimsonya Roma kwa nguvu.
“Wewe ni mjinga kutokea wapi mpaka usimjue Shagoni”Aliulizwa na palepale ili kumuokoa Roma Zato alimwelezea Roma huyo Shagoni ni nani na hapo ndio alielewa.
Shagoni alikuwa ni kaka yake Lilsi ambaye anatokea ukoo mwingine kabisa uliofahamika kwa jina la Sholi na kwa maelezo ya Zato ni kwamba ni ukoo wa kijini ambao una mahusiano ya siri sana na binadamu kwa namna ya kiimani na ndio ambao huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta malighafi kutoka ulimwengu wa kawaida kupitia hao binadamu.
Kwa lugha nyepesi Roma alielewa kwamba Sholi ni ukoo ambao una mahusiano na binadamu kwa namna ambayo sio ya moja kwa moja.
Roma alishawahi kusikia kuhusu binadamu ambao wanamiliki majini katika dunia ya kawaida na kwa maelezo ya Zato palepale alielewa alichomaanisha lakini kuna kitu kimoja ambacho hakikuwa cha kawaida ambacho aliweza kukiona kwa mwanamke huyo aliefahamika kwa jina la Lilsi.
“Hey! wewe mvulana nimesikia ukisema unao uwezo wa kuhimili mapigo ya jini ambaye upo mwishoni mwa levo ya nafsi . una uhakika au unajitutumua tu?”Aliuliza Lilsi.
“Kama huamini njia rahisi ni kunitafutia jini ambaye yupo kwenye levo ya nafsi nipigane nae , ninaweza nisishinde lakini pia siwezi kupoteza pambano”
“Ukifeli unapaswa kuelewa miliki yetu haiwezi kukupokea tena”Aliongea yule mwanamke alikuwa na mapozi flani ambayo yalimkumbusha Roma kuhusu Aoiline kutoka ulimwengu wa majini pepo.
“Kama ndio hivyo basi natoa wito wa kuitwa kwa Fileo hapa apambane na Xiao Cheni.
Baada ya kuongea vile palepale yule bwana alievalia kileo aliagizwa kwenda kutafutwa kwa mtu alietajwa jina la Fileo kuja kupambana na Roma.
“Shemeji itakuwa ni ukatili , unapaswa kuelewa Fileo yupo mwishoni mwa levo ya nafsi lakini pia ana mbinu za hatari sana kimapambno , huyu binadamu atakufa hapo hapo kwa pigo moja tu kutoka kwa Fileo”Aliongea Lilsi kwa dharau.
“Xiao Cheni kama utafanikiwa kuhimili mapigo kumi kutoka kwa Fileo nitatoa vidonge vitatu vya daraja la kati kwenda kwa familia ya Zaola, kama utahimili mapigo therathini nitakupatia kidonge cha daraha la juu , je upo tayari kupokea ofa yangu na kushindana?”
Yule Mkubwa namba tatu alikuwa na mipango yake kichwani , Roma alijigamba kwamba ana mwili mgumu sana wa kuvumilia mapigo hivyo aliamini kama Roma kweli atahimili mapigo therathini basi maneno yake yatakuwa sahihi.
“Mimi Xiao Cheni licha ya uwezo wangu kuwa mdogo , nipo tayari kupambana kwa ajili ya marafiki zangu kutoka koo ya Zaola na kupokea mapigo”Aliongea Roma.
Unafikiri kuna Amanni huko , Je Roma atampata Rufi ??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom