Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Jichanganye utoe mchango wako ili uongeze idadi ya waliopingwai mkuu.

Mwamba hana ofa wala bei maalumu bali hushawishi ulipie kisha hupita na vijisent vya waathirika wa arosto kisha siku inapita ila story haina mwisho
Unao uhakika kuwa hawatumiwi au wanapigwa arosto? Nikajua utatoa support kwa mpambanaji anaetumia muda wake kutengeneza story, tupeane support!!
 
Jichanganye utoe mchango wako ili uongeze idadi ya waliopingwai mkuu.

Mwamba hana ofa wala bei maalumu bali hushawishi ulipie kisha hupita na vijisent vya waathirika wa arosto kisha siku inapita ila story haina mwisho
Kwa hili sio kweli jamaa yuko makini sana, nimenunua simulizi kama tatu hivi kwake na ya mwisho ndio alichelewa kidogo kutuma ilikaa kama dakika 20 kuipata. Hivyo usiwakatishe tamaa wenzio kama wewe hutaki kununua
 
Jichanganye utoe mchango wako ili uongeze idadi ya waliopingwai mkuu.

Mwamba hana ofa wala bei maalumu bali hushawishi ulipie kisha hupita na vijisent vya waathirika wa arosto kisha siku inapita ila story haina mwisho
Si kweli jamaa si tapeli ka unavyodhani, Mi mwenyewe baada ya kuona huku iko nyuma nlimfuata WhatsApp akanitumia zote mpaka walipofikia kwenye group na sasa tushamaliza sehemu zote 800 na sasa tunasubiri chuma kingine.
 
Jichanganye utoe mchango wako ili uongeze idadi ya waliopingwai mkuu.

Mwamba hana ofa wala bei maalumu bali hushawishi ulipie kisha hupita na vijisent vya waathirika wa arosto kisha siku inapita ila story haina mwisho
Acha Shobo na hela za.wenzio,Una uhakika haina mwisho au unaleta uswahili wa kiswazi kwenye uzi wangu
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 669.
Baada ya masaa zaidi ya ishirini na nne ndio waliweza kufika Incheon International Airport , ilikuwa ni mchana wa saa sita wakati wanafika.
Siti Zote walizokuwa wamekaa wakati wote wa safari ni za daraja la kwanza, Roma aliamua kukaa Daraja la kwanza na Clark sio kwamba ana pesa sana lakini ilikuwa ni kuepusha macho kumkodolea Clark kutokana na urembo wake.
Tokea afungue ukurasa wa mapenzi na mrembo huyo alikuwa na wivu pale anapoona wanaume wengine wakimwangalia kwa macho ya kifisi kuliko mwanzo.
Upande wa Clark yeye hakuwa hata na tatizo ni kama amezoea kuangaliwa na wanaume lakini alifurahishwa na vitendo vya wivu vya Roma na alijifanyisha hakuwa akijua kinachoendelea na safari nzima waliongea na kucheka pamoja na pale ambapo walitulia aliendelea kufanya kazi kwa kutumia tarakishi yake ya mapakato.
Ukweli ni kwamba Clark alikuwa akijisikia furaha kutokana na gunduzi hio , ijapokuwa ni gunduzi ambayo haikuwa ya kawaida na ambayo haiwezi kutangazwa kwa jamii lakini bado alijihisi kufanikiwa.
Baada ya kutoka kwenye ndege Roma alikuwa amevalia Jaketi la Leather rangi nyeusi na Clark na yeye alikuwa amevalia koti refu rangi ya Elk na jinsi lilimvyomkaa pamoja na uwepo wa Roma pembeni yake ilifanya wakorea wengi kuwaangalia.
Clark alionekana kama vile ni Star kutoka uzunguni hivyo alivuta attention ya macho ya watu wengi ndani ya uwanja huo..
“Teacher , Teacher I am here”
Sauti ya mwanamke ilisikika kutoka katika kundi la watu waliokuwa wakisubiria wageni na dakika hio hio mwanamke ambaye alikuwa amevalia suti ya rangi nyeupe na sketi ya rangi nyeusi ilioishia magotini alijitokeza.
Alikuwa ni mwanamke wa Kikorea mwenye makadirio ya umri kama miaka therathini hivi akiwa amefunga nywele zake kurudi nyuma , hakuwa amejipaka Makeup yoyote na mwonekano wake ni kama wale wanawake ambao hawajali sana kujipamba na kumfanya kutovutia kwa macho ya haraka haraka labda tu umwangalie kwa muda mrefu ndio utajua kama ni mrembo.
Mwanamke yule hakuwa na aibu na ni kama vile watu wote waliokuwa ndani ya uwanja huo wa ndege walikuwa wamepotea na alimkiimbilia Clark huku akiwa na machozi.
“Teacher Alexander ! Your Are fnally here , I have been waiting for you a longtime”Aliongea yule mwanamke kwa lugha ya kingereza akimwita Clark mwalimu Alexander na kusema alimkumbuka sana.
Ndio Clark jina lake la mwisho ni Alexander na kitendo cha mwanamke huyu kujua jina lake la mwisho basi ilimfanya kweli kuwa mwanafunzi wa Clark.
Zhang Ru ijapokuwa alikuwa kwenye furaha ya kumuona Clark lakini bado alisita sita kukumbatiana nae ni kama alikuwa akimuogopa.
“Zhang Ru Longtime no see, you haven’t changed much”Aliongea Clark kwa tabasamu huku akiwa amemkumbatia.
“Teacher….”Zhang Ru alitaka kuongea neno lakini Clark alimzuia na kumfanya kuchanganyikiwa kwani hakuelewa Clark anataka kumaanisha nini.
“Kama nitakuwa na kumbukumbu nzuri utakuwa na maika zaidi ya therathini sasa hivi , ukiendelea kuniita mwalimu watu watahisi labda nimefanya plastic Surgery ili kuongekana mdogo , hii ni Korea kusini sitaki umaarufu wa ajabu eti”
Ijapokuwa alijua Clark alikuwa akitania lakni Zhang Ru alitingisha kichwa kukubali.
“Teacher gari lipo tayari , tafadharii nifuate mpaka eneo la maegesho..”Aliongea na kisha akamgeukia Roma ambaye hakuwa hata na habari nae.
“Wewe ni..”
Ukweli ni kwamba Zhang Ru mara baada ya kumuona Clark akiwa ametangulizana na mwanaume mweusi alijikuta akishangaa na kujiuliza inakuwaje mrembo kama huyo kutangulizana na mwanaume mweusi tena ambaye hana hata muoenekano wa kitanashati , aliona kabisa ni kama hawaendani hivi.
“Mimi ni mwanaume wa mwalimu wako”Aliongea Roma kujitambulisha na palepale Clark alimsogeleaRoma na kumshika mkono.
“Zhang Ru jina lake anaitwa Roma Ramoni , kwanzia sasa unapaswa kumuheshimu kama unavyoniheshimu mmi , hupaswi kumfanya kama mdogo wako kwasababu ni mdogo kuliko wewe sawa?”Aliongea na kumfanya Roma kukunja uso wake na kujiambia ni utambulisho wa aina gani huu.
Zhang Ru macho yake yalionyesha wasiwasi lakini hata hivyo aliishia kutoa tabasamu kwa kulazimisha na kisha akawaomba waondoke.
Upande wa Roma alikuwa ashatumia Koneksheni zake kuandaliwa chumba cha hadhi ya raisi ndani ya hoteli ya Hilton sehemu ambayo ni karibu kabisa eneo ambalo Dhana hio ya mabaki ya kale ya Kibudha ingetangazwa rasmi kwa waumini wanaosalia Buddha..
Wakati wakiwa njiani kwenye gari Zhang Ru alkuwa akipiga jicho kupitia kioo cha nyuma akimwangalia Roma kwa wasiwasi , alikuwa akisikia Clark na Roma wakiongea lugha ambayo hakuwa akielewa na Clark alionekana kuwa katika furaha mno , alijua kabisa pengine wanaongea maswala ya kimapenzi na alijikuta akikunja uso wake na kujiambia mwalimu wake nani kamloga mpaka kutoka kimapenzi na mtu kama huyo mweusi.
“Teacher kwanini umevutiwa na Dhana ya Moyo wa Kibudha, unataka kufanya Research , kama nakumbuka vizuri hukuwa na matamanio kabisa na maswala ya kidini”Aliongea Zhang Ru akivuruga maongezi yao makusudi.
“Oh! ni Roma ambaye alitaka kuja kuangalia mimi nimemsindikiza tu, amevutiwa sana na kifaa hicho”Aliongea Clark na kumfanya Zhang Ru kulazimisha tabasamu.
“Mr Roma kama nitakuwa sahihi ulikuwa ukiongea na Teacher Clark kwa lugha ya kiitaliano , wewe ni raia wa nchi hio?”
“Hapana , nimeishi ndani ya mataifa mengi sana lakini nimerudi rasmi na kuanzisha maisha yangu ndani ya Tanzania sehemu niliozaliwa”Aliongea Roma.
“Oh! Unaishi maeneo gani nchini Tanzania na unafanya kazi gani?”Aliuliza.
“Naishi Dar es salaam na nafanya kazi za vibarua tu , Miss Zhang Ru kwanini unaonekana kama vile ni polisi?”
“Hamna tu ni kwamba nina shauku ya kutaka kukujua ni mwanaume wa aina gani mpaka kuweza kuushinda moyo wa mwalimu wangu , nishawahi kuishi Tanzania wakati baba yangu akiwa balozi wa China , Mr Roma unaonekana kuwa sio wa kawaida”
“Oh! Kama baba yako alifanya kazi katika ubalozi wa China basi utakuwa na wewe ni mchina , nilifikiri kwa muonekano wako ni Mkorea”Aliongea Roma akiwa na mshangao.
“Kwanini , naonekana kama Mkorea?”Aliuliza huku akikunja sura.
“Hapana ni kwamba kwangu unaonekana kama Mkorea hususani na huo mwonekano wako wa dharau”Aliongea Roma huku akionyesha kutoridhishwa na Zhang Ru tabia yake.
Zhang Ru palepale aliona aibu na hofu ya kuogopa kutomkasirisha Clark.
“Hapana Mr nilikua na shauku tu ya wapi ulipotokea , sitouliza tena”Aliongea akijitahadhari.
Upande wa Clark alikuwa kimya na alimuona Roma kama vile hakuwa akitaka kuonekana mbele ya Zhang Ru kama wa kawaida hivi.
“Mpenzi , Zhang Ru alikuwa ni msichana mzuri sana na wakati anaanza chuo pale Imperial College London miaka mitatu iliopita ilimchukua mwaka mmoja tu kuweza kuingia katika darasa la Vipaji maalumu ambalo ndio niliweza kukutana nae kwani nilikuwa nikifundisha hapo , maksi zake zilikuwa za juu mno”
“Asante sana mwalimu kwa kunisifia?”
Upande wa Roma alikuwa kwenye mshangao tu miaka mitatu iliopita msichana wa kawaida pengine angekuwa High School lakini Clark alikuwa tyari ni Profesor kwenye vyuo vikubwa ndani ya Uingereza na Marekani , ukiachana na hilo pia alikuwa akifundisha wanafunzi wa vipaji maalumu kwa mtu wa nje ambaye hakuwa akimjua Clark pengine angeishia kushangaa na kutokukubali.
“Ukiachana na hayo, Zhang Rhu nakumbuka mara ya mwisho uliniaga kwamba unarudi China kwa ajili ya kazi , nimeshangaa kukuona kwenye tangazo hapa nchini Korea kama mtafiti”
“Nimeingizwa kwenye Project maalumu ya ubadilishanaji wa walimu kati ya Korea na China , nimekubali kuja Korea kwasababu ya kutaka kupata ujuzi wa kufanya kazi katika Project za kimataifa”
Ijapokuwa walikuwa wakisikia kabisa maneno yake hayana ule udhati ndani yake lakini Clark na Roma hawakutaka kuuliza zaidi isitoshe ni maswala yake binafsi.
Roma ili kuhakikisha swala ambalo limemleta Korea ni siri hakutaka kufanya watu wengi wajue yupo nchini hapo.
Zhang Ru ndio mtafiti ambaye alikuwa akihusika na Dhana iliopewa jina la Moyo wa Kibuddha hivyo kwao ingekuwa rahisi kuhusika katika Consecration hivyo hatua ya kwanza ya uthibitishaji ilikuwa rahisi.
Baada ya kupitia hatua za mwanzo mara baada ya kuingia hotelni Zhang Ru aliweza kugundua Roma na Clark wamechukua chumba kimoja na swala hilo lilionyesha kabisa kutomridhisha na alimuomba kuongea nae pembeni.
“Unataka kuongea nini Zhang Ru”Aliuliza Clark ambaye alikuwa kidogo kwenye sintofahamu ya kile ambacho Zhang Ru alitaka kumwambia.
“Teacher kwanini unataka kulala nae kwenye chumba kimoja?”Aliuliza .
“Tatizo liko wapi , ni mpenzi wangu”
“Hapana hata kama ni boyfriend wako kwanini mwanamke kama wewe ulale nae bila taratibu maalumu , hata kama mnalala kwenye kitanda kimoja bila ya kufanya chochote hairuhusiwi , Teacher mimi nimeolewa na nina uzoefu mzuri kwenye maswala ya kimahusiano , utaharibu taswira yako kama ukilala nae kabla ya ndoa”Aliongea huku akiwa na uso uliojaa usiriasi lakini ajabu ni kwamba clark alishindwa kujizuia na kuishia kutoa kicheko.
“Zhang Ru asante sana kwa wasiwasi wako juu yangu lakini ukiachana na mwonekano wake wa kawaida ambao unakuchanganya ambao kwangi n wa thamani lakini ninachoweza kusema ni kwamba nimemjua kwa zaidi ya miaka kumi , sio kwamba nimekurupuka tu kumchagua kama mpenzi wangu , hivyo kuwa na utulivu wa nafsi , mapenzi kwangu hayanishangazi”Aliongea
“Miaka kumi! , kama ni miaka kumi si wakati huo mtakuwa wote ni watoto , unajua nini kuhusu mapenzi kwa wakati huo , Teacher hata kama umempenda kupitiliza ukweli hauwezi kubadilika na hakuna ambaye anaweza kuamini maneno yako”
Ijapokuwa Zhang Ru alishawahi kuwa mwanafunzi kwa Clark lakini ukweli ni kwamba hawakuhi kukutana mara nyingi ni kama mara moja au mbili kwa wiki na mara zote ni wakati wa kipindi chake tu , ukiachana na kwamba alikuwa akimkubali Clark kama Clark lakini hakuwa akimjua ki undani zaidi.
Alikuwa akijua Clark alikuwa ni Princess wa Wales na ndio maana hakutaka kuona analala na mwanaume yoyote ambaye hana mwelekeo kama Roma.
Alikuwa ni mtu mzima kuliko Clark na alijua wasichana wa sasa hivi mara nyingi wanapotea linapokuja swala la mapenzi na Clark Stephanie Alexander ni mmoja wao.
Zhang Ru aliishia kuwaangalia Roma na Clark wakitembea pamoja kuingia kwenye Lift kwenda kwenye chumba chao na hali ile ilizidi kumtia mawazo na kujiambia kwanini asiwe hata ni mzungu wa kawaida lakini mwafrika wa kawaida kwake ilikuwa ni kituko cha mwaka.
“Hata mimi nishawahi kupenda mwanaume mweusi lakini hakuwa wa kawaida kuliko wa Clark”Aliwaza na palepale mawazo ya namna ile yalimtengenezea kukumbuku na macho yake yalichanua na kisha alitoa simu yake na kuingia kwenye mtandao wa Watsapp na kutafuta jina la mwanaume ambaye amemsahau kwa miaka mingi tokea kuachana nae kwa muda mrefu , unaweza kusema ni X wake wa muda mrefu.
“Zhang Ru..!! ni wewe kweli , siamini ”Sauti upande wa pili ilizungumza kwa kingereza.
“Nani mwingine kama sio mimi?”
“Haha,,, ni kweli ni wewe na kisauti chako , sijawahi kuwaza kuna siku utanikumbika na kunipigia simu , unaendeleaje , vipi kazi yako?”Sauti upande wa pili ilisikika na kumfanya Zhang Ru kutoonyesha tofauti yoyote.
“Asante kwa kuwa na wasiwasi na mimi Mr X , nilisikia ulipandishwa cheo mara ya mwisho, ila sijakupigia simu kukupongeza , nitaenda moja kwa moja kwenye sababu yangu ya kukupigia , nahitaji msaada wako , upo tayari au haupo tayari?”Aliongea kibabe.
“Nilijua tu huwezi kunipigia bila sababu”
“Kwahio unaniona msumbufu si ndio , basi nakata simu”Aliongea huku akiigiza kukasirika.
“Hapana usikate , nilikuwa nikiongea tu , haya niambie ni nini unataka msaada wangu , ili mradi ni halali nitakusaidia”Aliongea yule mwanaume.
“Looh hajabadlika kabisa huyu mwanaume”Aliwaza Zhang Ru kwenye kichwa chake huku akitoa tabasamu la kejeli..
“Nataka unisaidie kumchunguza mwanaume anefahamika kwa jina la Roma Ramoni ambaye anaishi hapo Dar es salaam , ana miaka kama ishirini na tano hivi kupanda na ameishi sana nje ya nchi , amerejea nchini kwenu hivi karibuni”
“Nini !?Roma Ramoni?”
“Una tatizo gani , mbona umepaniki kusikia hilo jina , una mfahamu?”
“Ndio namjua, kama kweli umekutana nae huko Korea , kwanini unataka nimchunguze?”
“Basi ni vyema kama unamfahamu , ninachotaka ni taarifa zinazomuhusu”
“Xiao Ru sitaki kukufaicha chochote kwa makusudi lakini huyo mwanaume … siwezi kukuambia ni nani haswa na hata kama nikikuambia jua tu kwamba nakudanganya”
“Basi poa , mimi nilijua tu hujawahi kunipenda na ulikuwa ukinionja tu kubalisha radha , tokea tulivyokuwa kwenye mahusiano yetu ulikuwa msiri sana mpaka tukaachana … nilijua tu tokea mwanzo upo kwenye mfumo ., hebu niskilize kama hutaki kunisaidia basi acha nitajua mwenyewe kupitia ubalozi”Aliongea kwa kukasirka .
“Ru habu kwanza nisikilize sio kwamba sitaki kukuambia chochote lakini huyo mwanaume ni hatari, usije ukamchokoz…”Kabla hata hajamaliza kuongea Zhang Ru alikata ile smu kihasira hasira.
“Eti hatari , kila mwanaume ambaye ataweza kuwa karibu na Clark lazima awe ni hatari ndio kama sio jasiri “Aliwaza.
Aliendela kuwaza au pengine ni mhalifu kutoka huko Tanzania ambae anaogopeka , kama sio hivyo kwanini anaogopa kutoa taarifa zake.
Baada ya Zhang Ru kujifikiria kwa muda alianza kupatwa na hofu na kujiambia au yupo karibu ya Clark kutokana na ubini wake.
“Yeah nimekumbuka , Moyo wa Kibudha , Teacher Clark alisema huyu Roma yupo hapa Korea kwa ajili y a moyo wa Kibudhha …. Inamaana anajaribu kutumia ukaribu wake na Clark kutaka kuiiiba?”
Zhang Ru aliona utakuwa ni ujasiri wa aina yake kama kweli Roma atakuwa na mawazo hayo.
“Profesa Zhang unafanya nini hapa?”
Sauti kutoka nyuma yake ilimshutua na palepale aliweza kuona sura ya mwanamke Polisi alievalia gwanda za jeshi la polisi la Korea akiwa anaingia ndani ya hoteli hio.
Huyu mwanamke wa Kikorea alionekana kama alikuwa kwenye miaka arobaini hivi lakini ni aina ya wanawake ambao wanajipenda , alikuwa na lipsi nyekundu mno huku akiwa mwembamba na umbo lake tatanishi.
“Kapteni Hwang ..”Aliita Zhang Ru huku akiwa katika tabasamu .
Hwang Sooyeon ni polisi katika idara ya ulinzi ya jeshi la polisi ndani ya jiji la Seoul , alikuwa ndio mkuu wa idara ya ulinzi na alifahamiana na Zhang Ru sana tu.
“Profesa unafanya nini hapa?”Aliuliza Kapteni.
“Oh,,,Mwalimu wangu , Profesa Clark , Mkuu wa Royal Academy of Sciences kutoka Uingereza yupo hapa , amekuja kwa ajili ya kuangalia mabaki ya moyo wa Kibudha na nimemleta hotelini”Aliongea
“Mkuu wa idara ya Royal Acadamy? , basi inaonekana atakuwa mtu mzito mno kiasi cha kukufanya Profesa kama wewe kuja mpaka hapa , sishangai ndio maana umeweza kuongoza utafiti wa kuchunguza moyo wa Kibudha kwa umri huo mdogo… kama sikosei basi utakuwa ni mwanafunzi mwenye akili wakati anafundisha …”Aliongea huku akitabasamu
Upande wa Hwang Sooyeon palepale wazo lilimjia na kujiambia au akaripoti swala hilo kwa chifu , pengine Clark kama ataalikwa kama mgeni rasmi kwenye sherehe ya Consecration italetea taifa umaarufu”
NB:Consecration Ceremony mara nyingi ni sherehe za maonyesho ya kuweka Wakfu kitu flani , kwa mfano hao waumini wa Budha wanafanya sherehe ya kuweka wakfu moyo huo wa Kibudha.
 
SEHEMU YA 670.
Upande wa Zhang Ru alionyesha kama vile ana wasiwasi na kisha akamwangalia Kapteni Hwang.
“Kapteni Hwang kuna kitu kinanisumbua, naomba unisaidie”
“Niambie tu Profesa nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kukupa msaada”Aliongea na palepale Zhang Ru alianza kumwelezea Roma alivyo , alielezea kwamba mwanaume huyu mweusi alionekana ni kama jambazi ambaye anamchombeza Clark kwa ajili ya kuba moyo wa Kibudha , hivyo akamwambia kwamba litakuwa jambo la maana kama timu yao ya ulinzi kuwa makini nae.
Upande wa Kapteni Hwanga ni kama vile muonekano wake ulibadilika na alionekana kuathirika na maneno ya Zhang Ru.
“Profesa unajua kwanini nipo hapa kwanza?”Aliuliza Kapteni na kisha Zhang Ru alitingisha kichwa kwamba hajui.
“Naomba nikutambbulishe..”aliongea na kisha alimpa ishara kusogea mpaka ndani ya hoteli hio katika eneo la kusubiria mapokezini.
Katika eneo hilo lenye masofa ya gharama walionekana Monks na Nuns(Monk wa kike) waliokuwa wamevalia mavazi ya kitadamuni lakini pia kulikuwa na watu wengine ambao walikuwa wamevalia suti kama viongizi hivi na ni kama walikuwa wakijadiliana jambo.
Pembeni yao kulikuwa na kundi la mabodigadi ambao walikuwa wakitoa ulinzi lakini sio hivyo tu pia kulikuwa na mapolisi.
Kati ya kundi hilo kulikuwa na mwanamke ambaye ni Monk ambaye alikuwa kama na miaka arobaini hivi akiwa amevalia kofia aina ya hat huku mkononi akiwa ameshikilia Rozari na ndie ambaye alikuwa kinara kuongea na watu waliokuwa katika mavazi ya suti.
Nyuma ya mwanamke huyo kulikuwa na Monk mwingine wa kiume ambaye alikuwa ni bonge na mfupi na yeye alionekana kama vile yupo kati ya miaka hamsini hivi ki umri.
Monk wengine wote walionekana ni wale ambao wana vyeo vya chini na ilikuwa ni kama wanafatisha kile wakubwa zao wanachoongea.
“Jamani kila mmoja hapa naomba niwatambulishe kwenu mtafiti wa Moyo waKibudha Miss Zhang Ru”Aliongea Kapteni Hwang.
“Amitabha , Profesa hakika hatima yako ni yenye unganiko na Buddha , sisi wanyenyekevu tunapaswa kukushukuru kwa kugundua moyo wa kibudha kwa niaba ya wote”Aliongea.
“Imekuwa heshima kwangu Abbess , mimi Zhang Ru nipo hapa kwa ajili ya kutmiza wajibu wangu lakini moyo wa Kibudha umeguduliwa na watu wa maswala ya Archeology”Aliongea
“Huyu ni Abbes Wooyeon , raisi wa muungano wa Kibuddha hapa Korea , nyuma yake ni Master Tzuho mkurugenzi msaidizi na wengine wote ni ma Monk kutoka madhehebu mbalimbali , walipaswa kukaa katika hoteli yao lakini wamepanga kukaa hapa ndani ya hoteli ya Hilton”Aliongea Kapteni Hwang akimtambulisha Zhang Ru.
“Kwanini?”
Zhang Ru alikuwa akijua fika kwamba Monk mara nyingi ni matajiri mno na safari zao mara nyingi wanaandaa wenyewe na wana hata biashara kubwa ndani ya jiji la Seoul.
“Ukweli ni kwamba kuna jambo nilitaka kukuambia, waandalizi wa maonyesho ya sherehe za kuweka wakfu moyo wa Kibudha wameweza kupokea barua ya vitisho kutoka kwa umoja wa siri ufahamikio kama North Buyeo wakisema kwamba watachukua moyo huo kwa Lazima”
“North Buyeo?”Aliuliza Zhang Ru maana hakuwahi kusikia kuhusu hicho kitu.
“Ah.. Profesa nadhani utakuwa huwaju lakini kuna huo umoja ambao umejikusanya , na timu yetu ya ulinzi imekusanya wanajeshi pamoja polisi ili kuhakikisha ulinzi ndani ya hili eneo , tumeamua kuwajumuisha viongozi pamoja na hawa Mok kukaa eneo moja ili iwe rahisi kuwalinda , hoteli hii ya Hilton ina faida kubwa za ki ulinzi kutokana na eneo lake ndio maana , Profesa kwanini na wewe usikae ndani ya hii hoteli?”Aliuliza kapteni na palepale Zhang Ru alikumbuka jambo.
“Kapten Hwang unamaanisha kwamba Roma ndio mmoja wa…”
“Ndio , Asante sana kwa kunipa hizi taarifa , Profesa nitawapa kazi watu wangu kuwa macho na hicho kikundi na pia nitatafuta taarifa zinazomuhusu ili tumjue kwa undani”aliongea na Zhang Ru alitingisha kichwa huku akipatwa na ahueni , isitoshe hata hivyo alikuwa ni mwanamke ambaye hana nguvu kutokana na kuwa ndani ya taifa la kigeni..
Wakati hayo yanaendelea upande wa Roma alikuwa amejilaza kwenye kitanda kikubwa cha King Bed ndani ya chumba cha hadhi ya raisi katika hoteli hio huku akimwangalia Clark ambaye alikuwa akifunga nywele zake mbele ya kioo kwa kuzichana.
“Wewe ni mrembo tayari huna haja ya kujisumbua na hio kazi”Aliongea Roma na Clark hakuongea chochote zaidi ya kuendelea kuchana nywele zake.
“Nafanya hivi ili kupata heshima mbele ya watu ,,”Aliongea huku akisimama na kuweka skafu yake vizuri shingoni.
“All right , let us meet your darling Yezi”Aliongea akimaanisha kwamba kila kitu kipo sawa na sasa waende kukutana na kipenzi chake Yezi.
“Kuna haja gani ya kuongea hivyo ,Yezi kwangu namchukulia kama mdogo wangu”
“Kweli?”
Roma alitaka kusema ‘ndio’ akini alishindwa kuongea mara baada ya kukutanisha macho yake na Clark .
“Come on stop staring into space let us go”
Roma alijikuta akitingisha kichwa chake mara baada ya kuhisi anaumbuliwa mchana kweupe lakini muda huo huo simu ya Roma ilianza kuita. Na alijikuta akishangaa mara baada ya kuona namba ambayo ilikuwa ikimpigia.
“Kwanini unanipigia , kuna kinachoendelea tena ndani ya familia ya Mzee Sharif?”Aliuliza Roma mara baada ya kugundua alikuwa ni Afande Jamali.
“Mr Roma sio kuhusu familia ya Sharif tena”
“Kama sio hivyo kwanini umenipigia?”Aluliza Roma akiwa kwenye mshangao na kujiambia hajachokoza mtu yoyote ndani ya siku hizo chache kwanini polisi amtafute.
“Ni swala binafsi Mr Roma”Aliongea Afande Jamali huku akisita sita.
“Maswala yako binafsi yanahusiana vipi na mimi?”
“Umekutana na mwanamke anefahamika kwa jina la Zhang Ru si ndio? ana uso mdogo na pia ni mrembo”Aliuliza Afande Jamali kwa suati ndogo.
“Zhang Ru! umejuaje nimekutana nae?”Aliuliza Roma huku akikunja ndita , ijapokuwa hakuwa akitumia uwezo wake wa kijini lakini asingeshindwa kujua kama kuna mtu anamfatilia.
“Ni mama wa mtoto wangu , ni mke wangu”Aliongea na kumfanya Roma kutoa macho na palepale alijikuta akianza kutoa cheko.
“Afande Jamali utakuwa unanitania sio , unawezaje kuwa na mwanamke huku mbali hivi?”
“Mr Roma nipo siriasi, nilikutana na Zhang Ru miaka mingi iliopita wakati baba yake akiwa balozi hapa nchini na hata shule tulienda pamoja na ndipo tulipozoeana na kujikuta tukiwa wapenzi na Zhang Ru kubeba mimba yangu, mwanzoni ilikuwa ngumu kushawishi familia yake kunikubali lakini baada ya mtafaruku wa muda mrefu Zhang Ru alikubali kuishi na mimi bila ya baraka ya wazazi lakini ukweli ni kwamba kusoma shule ambayo anasoma Zhang Ru ilikuwa bahati tu kwani nilikuwa chini ya uangalizi wa serikali ni kiwa kama mdahiliwa wa kitengo , kutokana na siri nyingi nilizokuwa nazo tuliingia kwenye migogoro ya hapa na pale na ndoa yetu ilifika mwisho mara baada ya mtoto wetu kufariki…….. kwanzia hapo hatukuwahi kuonana tena na mara ya mwisho nilisiikia yupo masomoni Uingereza mpaka aliponipigia muda si mrefu kukuulizia”Aliongea kwa kirefu.
Roma alishangazwa na historia hio fupi ,lakini hata hivyo ilileta maana kwa mtazamo wake Jamali hakuwa wa kawaida kabisa na alikuwa akiheshimiwa katika kitengo cha usalama wa taifa ndio maana alikuwa akipewa majukumu makubwa.
“Kwahio unasema kwamba mmetalakiana kabisa?”
“Naweza kusema tumetengana sio kutalakiana”Aliongea kwa sauti ya chini na kumfanya Roma ajione tatizo la Jamali linafanana na la kwake.
Utofauti ni kwamba yeye alikuwa na wanawake wengine lakini kuhusu Afande Jamali yeye alikuwa single .
“Okey sawa , hebu nielezee kwanini umenitafuta kuhusiana na swala hili?”
“Mr Roma ninachotaka kukuambia ni kwamba Zhang Ru sio mwanamke mbaya lakini yupo sensitive sana na Paranoid hio ni tabia yake hata nilivyokuwa nae , pengine anajali sana usalama wa Clark hivyo anaweza kuvuka mpaka lakini ..”
“Nimekuelewa , sintomfanya chochote kwa ajili yako labda tu kama ataenda mbali zaidi na kunichokoza , nipo Korea na ni rahisi kwangu kuua yoyote ambaye ataniletea jeuri na hakuna ambaye anaweza kunigusa”Upande wa Afande Jamali alimeza mate mengi akuonekana kuna kitu alitaka kuongea lakini Roma alikata simu palepale.
“Sijawahi kudhania kama Zhang Ru alishawahi kuolewa nchini Tanzania na kuzaa kabisa , anaonekana kama mwanamke mgumu sana na mbaguzi hivi wa rangi”Aliongea Clark mara baada ya kuelezewa kwa ufupi na Roma.
“Wanasema kwenye mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake , nadhani cheo cha Jamali kilianzia mbali”Aliongea Roma huku akitingisha mabega.
Waliendelea kuongea na wakati huo walikuwa washatoka nje ya hoteli hio bila shida yoyote na kuita Taxi kuelekea Gangnam district katika makazi ya Mzee Park , babu yake Yezi.
Baada ya kuingia kwenye Taxi Roma na Clark waliangaliana kwa kupeana ishara yenye maana flani.
‘Umeona na wewe pia?”
“Ndio , inaonekana mwanafunzi wangu tayari ashaingia kazini , nadhani watakuwa wameomba polisi kutufaitilia”Aliongea. Clark.
Clark alikuwa ni mtaaluma na alikuwa na mafunzo ya msingi ya kujua nani anamfatilia au kumwangalia kwa macho ya uchunguzi.
“Aisee… nadhani jambo letu sio siri tena , inaonekana kwasasa tunapaswa kuongeza juhudi”Aliongea Roma
“Hio inamaanisha kwamba mwanafunzi wangu ananijali sana”Aliongea kwa kujigamba na kumfanya Roma kumzodoa na wote wakaishia kucheka.
Nusu saa baadae Taksi iliweza kuwafikisha nje ya jumba la familia ya Park , ilikuwa tayari ni jioni wakati wanafika .
Roma ile anataka kuingia mara baada ya geti kufunguliwa alizuiwa na mlinzi ambaye alikuwa akimshangaa.
“Tafadhari jitambulishe na upo hapa kumtafuta nani”Aliongea kwa Kikorea yuleMlinzi na ilikuwa bahati nzuri Roma alikuwa akikijua.
“Tafadhari mtaarifu Miss Yezi kwamba Mr Roma Ramoni kutoka Tanzania amefika kuonana nae”Aliongea Roma bila ya kuonyesha ujeuri na yule mlinzi alitumia simu ya upepo kuwasiliana na dakika ileile alionekana kupatiwa maagizo mengine na wote kwa pamoja waliruhusiwa kupita.
Lakini sasa mara baada ya kuingia ndani mtu ambaye amtoka kuwapokea hakuwa Yezi bali ni Eujung.
Eujung alikuwa katika mshangao mara baada ya kuwaona na alionekana kuwa na hisia mchanganyiko na alipotezea mshangao wake na kisha akaupamba uso wake na tabasamu.
“Mr Roma , Dr Clark ujio wenu sio wa kutegemea kabisa , tafadhari karibuni sana ndani”Aliongea
Ilikuwa ngumu kuwazuia Roma na Clark kuingia ndani ya jumba hilo kwani walihesabika kama watu waliomuokoa Park Juan babu yake Yezi wakati wa ugonjwa wake.
Mazingira hayakuwa yamebadiika sana tokea mara ya mwisho Roma kufika hapo akiwa na mke wake Edna na baada ya kuona nyumba ipo kimya alimgeukia Eujung.
“Yezi hayupo nyumbani nini?”
“Mr Roma , Yezi yupo kwenye masomo ya jioni na Si…”Kabla hata hajamalizia sentensi yake sauti ya kicheko cha Park Juan kilisikika kutoka juu kwenye floor ya pili.
“Haha.. Mr Roma , Dr Clark ni furaha ilioje kupatwa na ugeni huu wa heshima ndani ya nyumba yangu , naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kuwakaribisha”Aliongea kwa Kingereza huku akishuka katika ngazi.
Alikuwa amevalia sweta la rangi ya grey na kwa kuangalia uso wake tu ilionekana vile vidonge ambavyo Roma amempatia vimefanya kazi kubwa,
Dakika hio hio na Yezi aliweza kuonekana , ilikuwa imepita miezi sita tokea waonane mara ya mwisho na Yezi alikuwa amebadilika mno na kuwa sasa msichana ambaye alionekana kuwa mkubwa na urembo wake kuongezeka maradufu.
Nywele zake ndefu alikuwa amezibana na alikuwa ametawaliwa na muonekano wa kitajiri.
Roma alishindwa kutoa macho yake kwa Yezi na kujiuliza imekuwaje huyu msichana aliekuwa akionekana wa kawaida kule Tanzania amegeuka na kuwa mrembo hivi kama mwigizaji wa filamu za kikorea.
Wanasema mazingira huathiri tabia za watu na hicho ndio alichokuwa akikiona , tembea yake na muonekano wake ilimfanya Roma kuamini mpaka Yezi kufikia hatua hio basi babu yake atakuwa ametumia juhudi nyingi kumbadilisha
“Yezi, Mr Roma na Dr Clark wapo hapa kwa ajili ya kukutembelea , ni watu wakubwa hivyo unapaswa kuwasalimia kwa heshima”Aliogea Park Juan kwa tabasamu.
Yezi alimpiga jicho Roma kwa dakika kadhaa lakini alionyesha kabisa hakuwa na furaha ya kuwaona na tofauti na mategemeo alitabasamu kidogo na kisha aliinamisha kichwa kwa heshima.
“Its been a long time , Mr Roma and Dr Clark”
Roma moyo wake uliuma mara baada ya kusikia kauli ya Yezi ,ilikuwa ni kama vile haukuwa ule ukaribisho ambao alitegemea , yaani ni kama vile yeye na Yezi wana uhusiano wa mbali.
Yaani Roma alitarajia atakumbatiwa na kuitwa Mjomba au Bro lakini tofauti aliitwa Mr Roma .
“Yezi uko sawa kweli , nimezoea kukusikia ukiniita Bro au Uncle, kwanini Mr ghafla tu?”Aliuliza Roma kwa kujilazimisha
“Mr Roma you are Grandfather Saviour , you deserve my respect”
“Mr Roma wewe ni mwokozi wa babu yangu hivyo unastahili heshima yangu”Aliongea Yezi bila tabasamu.
Roma woga ulimwingia palepale na hisia zake zilimuambia pengine Yezi ambaye alikuwa akimjua amepotea , Roma hakuamini kama anaweza kukubaliana na hilo kabisa.
 
SEHEMU YA 671.
“Mr Roma kwanini hamjatutaarifu kama mnakuja , tungewaandalia tafrija kubwa kwa ajili yenu”Aliongea Park Juan kawaida.
“Hakuna haja kufanya hilo mr Park , Roma na miimi tupo hapa Korea kwa ajili ya kuangalia mabaki ya moyo wa kibudha, Sarira , hatujaonana na Yezi muda mrefu ndio tumepitia kusalimia”Aliongea Clark.
“Oh naona , Miss Edna yeye hamjaambatana nae?”Aliuliza huku akiangalia kama angemuona , hata Yezi pia alikuwa akiangalia kwa mshangao.
“Yuko bize na maswala yake ya kazi”Aliongea Roma.
Park Juan alitamani kumuona Edna na aliishia kujiambia ni huzuni kama hajaja.
“Kwasababu mmefika ,mnaonaje mkisubiria kabisa chakula cha usiku, maandalizi yanaweza yasiwe makubwa lakini kitakuwa chakula kitamu kwa ajili yenu”Aliongea na Roma hakutaka kufikiria sana na alikubali lakini kwa wakati mmoja akiwa na hali ya huzuni kutokana na namna ambavyo Yezi anamwangalia kikauzu.
Clark hata yeye alikuwa akimfahamu Yezi na aliweza kuona mabadiliko yake lakini alishindwa pia kusoma mawazo yake kwa wakati mmoja.
Baada ya kuketi Park Juan na Clark walianza kuongea kuhusu mbinu za kuendelea kuwa imara zaidi kiafya , huku upande wa Roma yeye hakuwa hata na mudi ya kufatisha mazunugmzo yao.
Yezi alikuwa ameketi pembeni ya babu yake kimya na hakumwangalia Roma hata kwa bahati mbaya.
Roma hakuzoea kabisa ukauzu wa Yezi , ijapokuwa hakutegemea sana kupokelewa kwa shangwe lakini hakuweza kujua kwanini Yezi hakuwa na furaha nae.
Kabla ya chakula cha usiku walifika wageni wengine , alikuwa ni Kim Jip na baba yake Kim Yang
“Oh sijategemea kukutana na ugeni huu wa heshima hapa ndani , Mr Roma na Dr Clark sijategemea kuwaona Korea hivi karibuni”Aliongea Kim Yang kwa bashasha akiwasalimia.
Kim Jip alikuwa vilevile lakini alisalimiana na Roma na Clark kwa kulazimisha katika hali ya heshima.
Baada ya baba na mwana kuchukua siti zao ilionekana ni kama vile walikuwa wamealikwa pia kwa ajili ya chakula cha usiku.
“Naomba mniwie radhi , nimesahau kuwapa taarifa njema kabisa …”Aliongea Park Juan huku akimwangalia Kim Jip na kisha akarudisha macho yake kwa Yezi.
“Mmekuja katika muda muafaka kabisa kesho kutwa, nikimaanisha kesho baada ya sherehe za maonyesho ya wakfu, Yez na Kim Jip watafunga ndoa yao katika temple la Jogyesa , tunatumaini Sarira atabariki tukio hili muhimu kwa familia yetu”Aliongea.
“Nini !?”
Roma ni kama vile hajasikia vizuri mpaka alivyoangalia uso wa furaha wa Park Juan na pia mtikisio wa kichwa wa Kim Yang alijua wanamaanisha , hakuamini kama ile siku ya ndoa ya Yezi hatimae imewadia.
Jogyesa ni sehemu maarufu ambayo Roma alikwua akiijua vizuri sana kutokana na kwamba enzi zake za uninja ametembelea sana maeneo hayo.
Ndio Temple kubwa katika imani ya Kibuddha ndani ya Korea yote , kwa lugha nyepesi unaweza kusema Jogyesa ndio sehemu takatifu ndani ya Korea kwa dini ya Kibudha.
Kufanya sherehe katika eneo kama hilo halikuwa jambo la kushangaza sana , lakini ilileteta mshangao kwamba familia hii imeweza kuandaa sherehe yao kufanyikia katika eneo takatifu kama hilo.
Hata hivyo sio swala la kushangaa sana kutokana na utajili wake , inaonekana mzee huyo alikuwa na koneksheni kubwa sana ndani ya serikali.
Ukiachana na ndoa za kikristo ambazo hufanyika ndani ya Korea lakini pia ndoa za kibudha ndio maarufu zaidi kuliko zote na mara nyingi familia hupenda kualika Monk kwa ajili ya kuzifungisha.
“Yezi kwanini hujawasiliana na sisi kama unaolewa hivi karibuni , tungekosa kuhudhuria harusi yako kama nisingekuja kwa bahati mbaya huku?”Aliongea Roma akiwa amekunja ndita.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa mara baada ya kugundua kama Yezi anaolewa hivi karibuni na alishangaa kwani Yezi alionekana kupinga vikali kuolewa na Kim Jip.
“Mr Roma wewe na mkeo mpo nchi ya Tanzania huko mbali sikutaka kuwasumbua maana nilijua mtakuwa bize , isitoshe ndoa ni swala la watu wawili hatukuona haja ya kusumbua watu wengi”Aliongea Yezi kwa sauti kavu.
“Usumbufu gani … unaongea kama vile hatuna uhusiano wowote na wewe”Aliongea Roma na palepale hasira ilijionyesha kwenye macho ya Yezi.
“Kwenu nyie mimi nilikuwa mgeni tu, isitoshe hatuna undugu wa damu”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia kwa macho ya mshangao.
“Yezi chunga kauli zako …”Alifoka Park Juan na kisha akamgeukia Roma na kuomba msamaha.
“Mr Roma huyu kwasasa haambiliki, inanitia wasiwasi kwani ana mambo ya kitoto wakati ndio kwanza anaolewa”
“Mr Roma ni mtu muungwana hivyo naamini hawezi kujali sana , Sir Tafadhari usimfokee hivyo Yezi , ana tabia nzuri zaidi kuliko hata mtoto wangu hapa , leo tumetoka kufanya maandalizi ya harusi ijapokuwa hajui chochote lakini alionyesha kuniletea ujeuri”Aliongea
“Mr Roma na Dr Clark mnaonaje mkihudhuria harusi hii na uzuri ni kwamba Sarira itaonyeshwa ndani ya hili Temple na kuangalia kwa ukaribu ni kwa watu maalumu tu wanaoruhusiwa , kama mnapenda nitahakikisha mnapata ruhusa ya kuangalia kwa siku mbili mfululizo”
Upande wa Roma alikuwa kwenye hali isioeleweka hakujua tabia a Yezi ilisababishwa na ndoa au nini lakini alishindwa kurudisha mudi yake kuwa nzuri kabisa.
Upande wa Clark yeye alikuwa mwepesi kufanya maamuzi hivyo alikubali kwa niaba ya Roma kama watahudhuria.
“We will attend the wedding then , here is a wedding wish in advance , we wish you a lifetime of love and happiness”Aliongea akikubali huku akitanguliza wishes kwa kuwaambia anawaombea furaha na upendo wa milele.
“Haha.. asante kwa baraka , halafu pia pengine tutahitaji msaada wako wakati wa Yezi kujjifungua hapo baadae unaonaje”
“Haitokuwa rahisi kunipata kama hamtoandaa zaidi ya milioni kumi za kimarekani”Clark alirudisha utani.
Ijapokuwa chakula cha usiku hakijaandaliwa bado hali ya hewa ilikuwa ya furaha kwa baadhi yao.
Muda huo Kim Jip ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu alinyanyua kikombe cha chai na kisha akanywa kidogo na palepale alionekana kukunja sura.
“Hii chai inaunguza”Aliongea kwa kufoka na kumwagia Eujung na kuloanisha gauni lake.
“Samahani sana, nitakubadilishia kikombe haraka”aliongea kwa hofu kidogo na palepale aliita kijakazi mwingine kwa ajili ya kusafisha.
Ijapokuwa Kim Jip mara nyingi alichukuliwa kama bodigadi wa Park Juan lakini kwa vijakazi wa familia ho walimchukulia kama mtu mzito kutokana na muda mrefu anakwenda kuozeshwa Yezi.
Ijapokuwa Eujung ni moja wapo ya vijakazi wanaopendwa na Park Juan lakini hakufua dafu mbele ya Kim Jip.
“Kwanini umefanya hivyo , ni chai tu hio lakini unakurupuka , nishakukanya na kukuambia kutawala hasira zako”Alifoka baba yake na Kim Jip alitingisha kichwa kidogo kuonyesha ishara ya kuomba radhi.
“Hupaswi kumlaumu kuna vijakazi wageni wameanza kazi na wana mengi ya kujifunza , nadhani sio mbaya kwa mwanaume kuwa na hasira na ukali , ili ufanikiwe mwanaume unatakiwa kuwa mkali sana, isitoshe namtegemea sana kumjali Yezi na kumtunza”Aliongea Park Juan akimtetea
Ijapokuwa kilikuwa kitu kidogo tu kilichofanyika lakini kilimwamsha Roma na hapo hapo alijikuta akikumbuka tukio la mara ya mwisho ambalo lilitokea hapo ndani miezi kadhaa iliopita na alianza kufikiria na kuhisi kitu kisichokuwa cha kawaida.
Wakati wa chakula cha usiku Kim Yang alikuwa bize kuongea na Park Juan kuhusu maandalizi ya harusi , na kupitia maongezi yao iliweza kuonekana Kim Jip kwa kipindi kirefu alikuwa ameacha kuwa mlinzi na sasa alikuwa akifanya kazi na baba yake
Baada ya kushiba Yezi alijifuta midomo yake na kitambaa kistaarabu na kisha akasimama.
“Babu nimechoka , naenda juu kupumzika”Aliongea
“Mbona mapema hivyo?.... haya nenda kapumzke usikeshe sana kusoma vitabu kama jana , kesho tutahudhuria maonyesho ya wakfu na sherehe yako itafanyika kesho kutwa, hivyo hupaswi kujichosha”Aliongea lakini Roma palepale aliingilia.
“Yezi subiri, hatujaonana muda mrefu , unaonaje tukiongea kidogo?”Aliongea Roma na Yezi alisimama.
“Mr Roma kwanini usiongee tu hapa hapa?
“Kuna baadhi ya vitu huwezi kuongea mbele ya kila mtu , hatujaonana kwa muda mrefu kidogo lakini hutaki hata tukiongea , au ndio umebadilika na kuwa mwanamke jeuri?”Alitania Roma. Lakini Yezi hakugeuka.
“Mr Roma sidhani kama ni sawa kuongea pembeni ilihali mchumba wangu anaangalia”Aliongea
“Yezi hebu acha jeuri zako , Roma ni mtu alieniokoa sidhani kama Kim Jip ana tatizo na hilo”Aliingilia Park Juan.
“Mimi sina tatizo”Aliongea Kim Jip kama vile ni roboti.
Yezi alikosa mbinu ya kumkwepa Roma na kujilazimisha alimwangalia Roma.
“Mr Roma basi nifuate”Aliongea Yezi na kisha alitangulia mbele kuelekea sebuleni.
Yaani sehemu waliochagua ni kama vile ni mbali na eneo la chakula , ni kama vile Yezi hakujali watakachosikia wakati wakiongea.
Roma aliwapa ishara vijakazi kuondoka na kufanya mazingira kutulia kimya.
“Unaweza kuendelea , ni kipi ambacho unataka kuongea na mimi?”Aliongea Yezi huku akibadili lugha lakini sauti yake ilionekana kama mwanamke flani ambaye amekereka.
Kauli yake ya kibabe ilimfanya Roma kujisikia vibaya na aliendelea kusimama na kumwangalia kwa namna isioelezeka.
“Yezi ni nini tatizo , Una hasira na mimi?”
“Sijaelewa unachomaanisha Mr Roma , mimi nipo sawa , asante kwa wasiwasi wako?”
“Hilo ndio jibu lako?”
“Hii ni nyumba yangu , tafadhari usiniongeleshe kwa hio sauti”Alionya Yezi na kumfanya Roma kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Yezi nataka kujua nini kimetokea ndani ya miezi syote , kwanini unaniona kama mtu mgeni , kuna kitu chochote ambacho babu yako amekuambia au una sababu nyingine , hebu niambie”
“Mr Roma hivi hujioni kama uwezo wako wa kufikiria umeshuka , sisi hatuna undugu wowote ni kweli tulishawahi kufahamina hapo mwanzo lakini hio ni kwasababu tulikuwa tukiishi kwenye nyumba moja , kwasasa hatujaonana kwa muda mrefu nadhani ni kawaida kupotezeana”Aliongea na kumfanya Roma kujitahidi kumwelewa.
“Basi hakuna shida kama ni hivyo , nina ombi moja kwako”
“Kuhusu nini”
“Ulikuwa ukiniita Bro au uncle nataka angalu nikusikie ukiniita hivyo na sio Mr Roma”Aliongea Roma na palepale Yezi alionyesha mabadiliko kwa kutetemeka na Roma alinyaka tukio lile na palepale tabasamu lilijionyesha na kujiambia huyu ndio Yezi ninaemjua mimi.
“Nadhani una matatizo , ni uhuru wangu kukuita ninavyojisikia”Aliongea Yezi na palepale aligeuka akitaka kuondoka lakini Roma alimzuia kwa kumshika mkono.
“Niachie..”Aliongea huku akionyesha hasira na aibu.
“Hatimae umerudi na kuwa Yezi ninaemjua mimi , kati ya watu wote kwanini unikaushie kama Edna anavyonifanyia , mbaya zaidi huwezi kuwa vizuri kama yeye , nimekuotea”Aliongea Roma huku akijisifu.
“Roma nimekuambia niachie mkono wangu”Aliongea huku akiuvuta
“Ukiniita Bro au Uncle nitakuachia”Aliongea Roma kijeuri na palepale machozi yalianza kumtoka Yezi sijui ni kwa hasira au kwasaabu ya nini.
“Unafanya nini sasa hivi , umenitelekeza mwenyewe na hukutaka kuongea na mimi kwa muda wote na sasa tunakutana tena eti unataka niwe kama zamani , hivi unaniona mimi kama kituko sio?”
“Yezi hebu acha kunisngizia ni lini nimekutelekeza , watu wanaweza wanipotezee na kutonifanyia vizuri lakini sitegemei wewe kunifanyia hivyo , ni lini nilipokuchukulia kama kituko, ni kweli nimekuja huku kwa ajili ya Sarira lakini siku zote nilikuwa nimekumisi na kutamani kukutana na wewe lakini vipi kuhusu wewe ndio kwanza unaolewa lakini umeshindwa hata kunitaarifu lakini nimefika kwa bahati nzuri ndani ya muda na kupata hizi taarifa bila ya kuniambia , hivi unanichukuliaje kwa mfano?”
“Eti umenimisi… unatoa wapi huo ujasiri wa kusema hivyo, kama kweli ulikuwa umennimisi kwanini hukunipigia simu hata mara moja kwa miezi yote hio , hukujisumbua hata kunitafuta”Aliongea na kumfanya Roma kuanza kukuna kichwa chake .
“Yezi sijafanya hivyo makusudi nadhani unanijua wewe mwenyewe mimi sio mpenzi wa kupigia wengine simu , nimekuwa bize sana tokea siku nilioondoka hapa.. nimeingia kwenye matatizo kibao na kidogo tu nikwame katika mazingira tatanishi milele.. hata hivyo nilikuwa na aibu kukuambia hili sasa hivi lakini dada yako Edna anataka talaka na awamu hii yupo siriasi”Aliongea Roma.
“Nini? Sister Edna anataka talaka?”Aliongea huku akiacha mdomo wazi kwa mshangao akimwangalia Roma.
Yezi alijikuta akituliza hasira zake na kutaka kumsikiliza Roma kuhusu kilichotokea na Roma alimweleza matukio yote.
“Ipo hivyo , Edna ameniambia nimchague yeye au Lanlan lakini nimekataa siwezi kumtelekeza mtoto wangu , majuto ambayo nipo nayo mpaka sasa ni kutokumlinda mama yake Lanlan hivyo siwezi kufeli kutokumlinda Lanlan”
Yezi hakuweza kujulikana muda huo kama alikuwa na furaha au alikuwa na huzuni kwani alikuwa amefunga midomo yake bila kuongea neno.
“Yezi umenidhania vibaya kumbuka kuna siku ulipiga na akapokea Bi Wema na alinipigia simu nikupigie?”
“Ndio lakini hukunitafuta”
“Hapana , nilikutafuta lakini ni Eujung ambaye alipokea na aliniambia umeshalala na utanitafuta baada ya kuamka lakini hukunipigia tena hivyo niliona pengine unaendelea vizuri”
“Ulinipigia kweli ?”
“Ndio kwanini nikuongopee … unaweza kwenda kumuuliza Eujung kama huamini”Aliongea lakini Yezi alionekana kuwa katika mshangao.
“Usiniambie hakukuambia kama nilipiga na kumwambia ukiamka akuambie”Aliogea lakini Yezi alionekana kuwa katika tafakari.
“Bro …”Aliita na kumfanya Roma kucheka.
“Naona sasa usharudi kuwa Yezi ninaemjua mimi”Aliongea Roma na kumfanya Yezi kuona aibu.
“Miezi mwili iliopita niliwapigia wewe na Sister Edna na pia nilipiga simu ya nyumbani zaidi ya mara tano ,inamaana hamkuona ..”
“Hapana sikupokea simu yako … Yezi nadhani sasa hivi ndio naelewa kwanini ulikuwa na hasira na mimi , unadhani tulikuwa tukipotezea simu zako sio?”
“Nilijua hamna mpango na mimi tena”Aliongea na palepale machozi yalianza kumtoka na alimsogelea Roma na kukumbatiana nae.
“Niliwamisi sana ,,,, nimekumisi sana… nimemmisi kila mtu”Aliongea na kumfanya Roma sasa kupatwa na ahueni.
“Yezi nishawahi kukuambia wewe ni mjinga inaonekana nipo sahihi ila tu hutaki kukubali , hata kama mimi ni mkatili , Edna hawezi kuwa mkatili kama mimi , sijui nini kimetokea lakini nadhani hata Edna hakupokea simu yako”
“Lazima atakuwa ni babu huyo … kila siku ananniambia anataka kuniweka mbali na wewe kwasababu nitamkasirisha Sister Edna”Aliongea na Roma alijua lazima itakuwa ni kweli.
Ijapoluwa Roma hakuelewa sababu ya Park Juan kufanya hivyo lakini alijua kabisa ana uwezo wa kuzuia simu ya Yezi kutotoka nje ya Korea, lakini hata hivyo Roma asingemkasirikia mzee huyo kwani alikuwa ni babu yake Yezi.
Unadhani ndoa itafannikiwa, Vipi Roma atapata Sarira kama alivyopanga na kurudisha uwezo wake,
NB:Sarira maana yake ni mabaki ya kale yanayohusiana na Buddha.

Tukutane tarehe 10

Kumalizia mpaka mwisho nitafute watsapp 0687151346.
 
Kwa style anayotumia kule wasap ni ngumu kuileta hapa lakini pia sio iingwana wala ustaarbu kuileta humu kwa kuiiba kwani Inamuumiza mtunzi lakini pia ni tabia mbaya mno! Ni vy ma tukasubiri
Yeah si tabia njema, uungwana wala ustaraabu tuwe na subra tu, ataleta tu humu mwenyewe kama siku zote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom