Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANI A KAHABA KUMBE BIKRA . MTUNZI: DR SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 637.
Roma alijisikia maumivu makali kwenye moyo wake , hakuwahi kuwaza Edna anaweza kupotezea ndoa yao kirahisi namna hio huku yeye akiwa hayupo tayari ,lilikuwa swala la kushangaza kwake.
Ilimshangaza kutokana na kwamba ilionekana kabisa Edna alikuwa akimpenda Lanlan licha ya kwamba alikuwa akijua sasa kuhusu wazazi wake, lakini Roma alijiuliza inakuwaje anataka kuacha kila kitu.
Roma alijiambia hapana ni kweli amemumiiza lakini haikuwa ikimaanisha washaachana , pale pale alimgeukia mama yake.
“Mama mchukue Lanlan”Aliongea Roma.
Upande wa Blandina awamu hio alikuwa na shauku ya kumbeba Lanlan kweli,ilikuwa ni kama mara ya kwanza kwake kumbeba, lakini yote hayo yalitokana na hisia zake kubadilika juu ya Lanlan mara baada ya kumjua sasa ni mjukuu wake kamili , hakujali nani amemzaa Lanlan na alichojali muda huo ni kwamba Lanlan ni mtoto wa Roma, kwake aliona ni kama baraka kubeba damu ya Roma mkononi mwake.
Afande Kweka aliishia kumwangalia Lanlan aliekuwa kwenye mikono ya Blandina na misuli yake ya macho ikacheza , pengine kama angekuwa na Zenzhei basi angetoa cheko kubwa kwani ndio watu wawili pekee waliokuwa wakiujua ukweli kuhusu Lanlan.
Afande Kweka hakujali sana kuhusu Edna , kwake Lanlan alikuwa muhimu zaidi kuliko Edna ambaye alikuwa ni mwanamke mgumu sana.
“Edna kwa sasa ana hasira sidhani kuongea nae katika hali yake kunaweza kuleta majibu , kwanini usimuache kwanza kwa muda , ni mtu mzima na hakuna baya litakalo mkuta, akitulia utaongea nae”Alishauri Blandina.
“Mama tulia ,siamini kama Edna ni mkatili kiasi cha kutaka kumalizana na mimi bila ya kunisikiliza”Aliongea Roma na hakutaka kupoteza muda na alitoka nje .
Roma mara baada ya kutoka alifanikiwa kumuwahi Edna nje ya geti na Roma baada ya kumfikia alimshika mkono kumzuia.
“Niachie mimi , sitaki kukuona tena”Aliongea
“Mimi siamini , kwanini unataka kuvunja uhusiano wetu uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili kirahisi hivyo?”
“Roma nadhani kuna kitu umesahau?”
“Nini ?”
“Unakumbuka makubaliano yetu siku ambayo tuliingia dili la mimi kumlea Lanlan??”
“Unazungumzi… unamaanisha yale makubaliano ya miaka miwili ya mdomo?”Aijiuliza Roma huku akiwaza na kuona ni kama ujinga na kujiuliza hata kama ni kweli walikubaliana kwanini huyu mwanamke kila kitu kwake anajali makubaliano tu.
Ni kweli Roma alikubaliana na Edna lakini siku ile hakuzingatia maneno yale kwani waliyaongea katikati ya kutaniana.
“Nilikuambia kabisa ukinichokoza kwa kuruhusu matatizo ya wanawake wako kuniathiri ndio mwisho wetu , je umesahau?”Roma alijikuta akiwa kama haelewi , ukweli ni kwamba makubaliano hayo hayakuendana kabisa na kinachoendelea hapo.
Asichokuwa akijua Roma kwa wakati huo anachomaanisha Edna ni swala la Salihi kumpigia simu Edna na kuanza kumtishia.,
“Wewe ndio Roma unaejuliakana kama mtoto pekee wa kiume wa kuendeleza familia ya ukoo wenu , Mfalme Pluto , Hades , naamini huwezi kuvunja ahadi yako?”Aliongea.
Roma licha ya kwamba hisia zake zilimwambia tukio la leo halikuwa likiendana na makubaliano yale lakini alijua pengine kuna maongezi mengine ambayo amesahau na wakati huo kila ambacho Edna alikuwa akiongea alijiona alikuwa na makosa.
“Roma nishachoka muda mrefu , kama isingekuwa kuvumilia kwa ajili ya mpendwa wangu Lanlan nisingefikiria hata kufika hapa , lakini sio mbaya sasa hivi Lanlan ashajulikana ni mtoto wako wa kumzaa hivyo simuhitaji tena , ninataka kurudi katika maisha yangu ya mwanzo kuliko kuendelea kuzungukwa na mtu ambaye moyo wako unaugawa kila mahali”
“Unaongea upuuzi , wewe sio mwanamke wa kawaida na huwezi kurudi kwenye maisha yako ya mwanzo”
“Najua pengine unaona nitakuachaje licha ya kwamba tumelala pamoja na kufanya mapenzi mara nyingi , si ndio?, usiwe mjinga mimi pia ni mwanamke wa kawaida ambaye nahitaji mwanaume wa kunituliza , siwezi kukataa ukweli kwamba wewe upo vizuri kitandani lakini hilo pekee sio la kunibakisha kwako , It’s just the toxic hormones doing its job”Hakusita kuongea hayo maneno tena akimalizia na neno la Kingereza.
Roma aliguswa mno na maneno hayo na alitamani hata kuziba masikio ake , ilikuwa ni kama vile kumbukumbu zote walizotengeneza na mwanamke huyo zimegeuka kuwa kitu kisichokuwa cha maana.
“Hakuna zaidi ya vitu viwili ambavyo mwanamke anavitaka kutoka kwa mwanaume , cha kwanza ni mapenzi ya kweli na cha pili ni matunzo , mimi Edna Adebayo hela za kujitunza ninazo , lakini mapenzi yako ya kimanyanyaso hayakidhi mahitajio yangu ya kihisia , hivyo ni rahisi kwa wewe sasa kuelewa kwamba ninakuacha na pengine ulipaswa kujiandaa kwa hii siku”.
Baada ya kumaliza Edna aligeuka na kutaka kuingia kwenye gari lakini Roma palepale alilipiga teke na hasira zake pamoja na mdudu wake aliekuwa ndani yake ni kama alishituliwa na nguvu iliotumika ililifanya gari lile kupinduka.
“Roma unafanya nini?” Edna aligeuka kwa hasira akimwangalia Roma.
“Hmmp..”Aliguna na palepale alibadilika na kutoa tabasamu la kifedhuli na kumwangalia Edna kwa ujeuri.
“Edna , ukiburi wako , kujitegemea kwako na kujiamini kwako vinatokana na hali yako ulionayo sasa hivi kitu ambacho ni tofauti na nyuma , Sasa hivi huna haja ya kudili na washindani wako wa kibiashara na huwezi kumuona tena baba yako wa kambo ambaye alikuwa akifanya hali yako kuwa ngumu, huna haja ya kuogopa wale majambazi wanaotaka mwili wako kwasababu una hela, nguvu na Koneksheni na sasa pia umekuwa mtu mwenye uwezo hata wa kupigana … sasa nakuambia hivi kama bado unataka kuchezeana akili na wanafiki ambao hata mwanzoni huku wajua na wakakuingizia kwenye hatari basi nakuruhusu fanya kama mwanzo uone, fanya michezo yako ileile ya kibiashara na hila zingine tuone kama unaweza kunikataa mimi mume wako kwa kiburi namna hio, Kwahio unasema kwamba hali yetu ya kindoa inabadilika kulingana na hali yako uliokuwa nayo pamoja na hadhi yako?,
Hicho ndio unachojaribu kuniambia sasa hivi?”Aliongea Roma na palepale alijipiga kifuani mara mbili ishara ya majivuno.
“Ndio , Mimi Roma Ramoni nina uwezo wa kupata kila ninachohitaji katikadunia hii, Mimi ni tajiri na pia nina nguvu na ninao uwezo wa kufilisi matajiri wakubwa zaidi ya mia tano kirahisi sana tena ndani ya siku moja na sio hivyo tu ninao uwezo wa kuvamia nchi na kuiweka chini yangu ndani ya siku moja , ninao uwezo wa kufanya mambo ambayo ni nje ya fikra za binadamu ili mradi nataka kufanya hivyo , Kiwango cha utajiri wangu , nguvu zangu na uwezo wangu unaweza kuvutia idadi ya watu wasiohesabika , nina ujuzi ambao unawafanya watu kuwa na wivu lakini kwa wakati mmoja wakashindwa kuiga wala kujifunza , lakini hayo yote nimeyapata hatua kwa hatua bila kupotezea fursa , ni vitu ambavyo nimevipata kupitia jasho langu , kupitia maisha yangu.
Hebu jiulize kama ningekuwa Roma mwanaume masikini ambaye naishi kwa kipato cha siku , au ningekuwa mwanaume wa nyumbani tu nisie na uwezo wowote ungeendelea kuwa na mimi , naamini usingeweza hata kuniangalia usoni mara baada ya mkataba ule wa miezi sira kuisha , usingefikiria mara mbili mbili hata kunisogelea na kulala na mimi kitanda kimoja , umeweza kufika hapa leo na mimi na kunivumilia miaka yote hiyo kwasababu ya kitu nilichokuwa nacho , ulijua kuendelea kuwa na mimi ingekusaidia katika vitu vingi , there is no love for no reaseon and no hate for no reason.
Ninakuambia hivyo kwamba mimi sio aina ya mwanaume ambae ninaweza kukusindikiza kwenda kazini kwanzia asubuhi mpaka jioni , wala kukuita CEO Edna ili kukupa heshima yako , mimi ni mwanaume ambaye siwezi kukusubiria kurudi nyumbani nianze kukunyenyekea na kuanza kukufanyia masaji na udambidamwi mwingineili tu kukufurahisha kama vile wewe ndio mwanamke mmoja tu ndani ya dunia hii , mimi ndio mimi na najulikana tokea nikiwa mdogo kwa msimamo wangu , Mtu dhaifu atakuwa mawindo ya mwenye nguvu , mwenye nguvu siku zote ni mtawala , hivyo unapaswa kujua mimi nina nguvu kuliko wanaume wengine na hiki ndio nilichokuwa nacho , ndio sifa yangu kubwa , nina wanawake wengi wa kuwajali na sina mpango wa kumuacha hata mmoja , hivyo ndio ilivyo na siwezi kugeuka nyuma , kama kweli unanipenda basi nikubali na uendelee kuishi na mimi.”
“Hivi unajua mtazamo wako wa uwazi na ujasiri wako utamfanya mtu asieogopa chochote mbele yako aonekane ni mnyonge?”Aliongea Roma kwa sauti huku akimwangalia machoni bila kupepesa.
“Sawa na mtazamo wako wa kifalme, lakini kwangu mimi sitaki kuendelea kuishi katika hali ya unyenyekevu na unyonge”Aliongea Edna.
“Kwani vipi , unapaswa kujua hakuna usawa kwenye ulimwengu huu , mimi nina nguvu ndio maana nina kundi la wanawake wanaonizunguka kwa hiari zao wenyewe , ulikuwa ni wewe mwenyewe ambaye ulisema hutojali na sasa unasema mimi nachukiza , ndio, najua kwamba nina deni kubwa kwako lakini je huna hata punje ya hatia ya uwajibikaji?, Unataka nifanye mangapi kwako ili nionekane ni wa thamani?”
“Haina maana kuongea hivyo kwa sasa , kama hao wanawake wako wanataka kuendelea kukaa na wewe basi ni juu yao , ndoa yetu ambayo ilianzia kama mkataba inaishia hapa , nilijituma pia na kujitoa kwako kama unaona haitoshi basi nakuruhusu nilazimishe kwasababu una nguvu nibakie kwako , lakini nimemaliza na siwezi tena kwa hiari yangu kuwa mkwe wa familia ya ukoo wa kweka kwani siwezi kuendelea kuwa mkeo , kama kweli wewe ni mwanaume mwenye nguvu na jasiri basi hutoshindwa kuniacha mwanamke mnyonge kama mimi nikichukua njia zangu , hatukuweza kuendana vizuri ndani ya ndoa yetu hivyo tunapaswa kuachana kwa amani..”
Aliongea Edna akiwa hana chembe ya hasira na kumfanya Roma kumwangalia kwa muda na kisha akavuta pumzi yake na kuishusha na akaingiza mkono kwenye mfuko wake na kuibuka na ufunguo wa gari wa BMW na kumuwekea mkononi.
“Unaweza kwenda , lakini sipendi kuona mwanamke ambaye nishawahi kuwa nae akimilikiwa na kufurahiwa na mwanaume mwingine … unaweza kusema mimi ni mnyama au shetani na sitojali lakini nakushauri tu usije kuthubutu kuwa na mwanaume mwingine kwani nakuhakikishia nitamuua na akijitokeza mwingine itaendelea hivyo hivyo..”
Baada ya kusema hivyo Roma aligeuka na kuingia ndani ya geti pasipo kugeuka nyuma na kivuli chake kilipotelea ndani akiwa katika hali ya upweke.
Edna alijikuta akiwa amesimama bila kusogea , maneno yake ya mwisho ambayo yalikuwa kama onyo yalimshangaza , alijikuta akivuta pumzi na kushikilia ufunguo wa gari uliokuwa kwenye mikono yake kwa muda na kisha aligeukia gari ambayo imeegeshwa kando ya geti.
Haikuwa ikieleweka anaenda wapi , lakini moja kwa moja ilieleweka hakuwa tena na sababu ya kukaa tena Iringa.
Baada ya kuingia barabara kuu aliendesha kuelekea mjini , ilikuwa ni usiku sana na giza limetawala na alikanyaga pedeli kwa nguvu na kusonga mbele na kuifanya gari hio kutoa mngurumo kama wa mnyama alieona kitoweo.
Spidi ya mwendo wa gari hio ni kama ilikuwa njia pekee ya kutuliza wasiwasi wake na maumivu na kilichoonekana ni michirizi ya machozi ambayo ilishakauka kuanza tena kupitisha maji.
Ghafla tu palepale alijikuta akihisi maumivu makali kwenye moyo wake na maumivu yale yalishitua kichwa chake na alijikuta akihisi maumivu makali ya kichwa yalioambatana na kengele kwenye masikio huku macho yakianza kuingiwa na ukungu wa kutokuona mbele.
“Pipiiii … Papaaaa…..!!!”
Ilikuwa ni gari iliobeba mbao iliokuwa mbele yake ikipiga honi kwa nguvu ikimwashiria Edna kupunguza mwendo na kutoka katikati ya barabara.

SEHEMU YA 638.
Ilikuwa ni bahati kwake kwani akili yake iliweza kurudi haraka na alifanikiwa kuzungusha usukani kwa nguvu na kukwepa gari ile.
Baada ya kujiimarisha katika usukani alijikuta akishindwa kujizuia tena na palepale jasho lilianza kumtoka kwenye paji la uso wake na alijikuta akianza kulia kwa kwikwi kiasi cha machozi ya chumvi kuingia kwenye midmo yake.
“Honey .. I’ m sorry … this is last thing ,, that I can do for you..”Alionekana kuongea akimaanisha kwamba ni kitu pekee ambacho anamfanyia Honey wake.
Lakini licha ya sauti yake hio , kutokana na upepo pamoja na ngurumo ya gari sauti yake haikuweza kusikika, isitoshe hakuna ambaye alikuwa akimsikiliza kwa wakati huo.
*****
Roma mara baada ya kuingia eneo la sebuleni alionekana kama mtua mbaye hakuna chochote ambacho kilikuwa kimemtokea , aliweza kutoa tabasamu lake hafifu na kisha akaenda kukaa mezani kwa ajili ya chakula.
Alipoulizwa kilichotokea alisema tu bila ya kuonyesha wasiwasi kwamba Edna amemua kutalakiana nae.
Tabasamu lake na utulivu ilifanya kila mtu aliekuwa akimwangalia kumuonea huruma mno , walijua ni kwa kiasi gani Roma anampenda Edna hivyo kuonyesha tabasamu ni shara ya kuficha maumivu.
Ukweli ni kwamba maumivu ambayo alikuwa akiyasikia hayakuwa yakivumilika , lakini licha ya hivo Roma hakuwa mtu dhaifu , hakuwa mtu ambaye ni wa kutaka kufarijiwa katika matatizo yake kwa kuonewa huruma.
Wanafamilia hao na wenyewe walionekana kujua mpango wake kwani hawakuongea chochote zaidi ya kuongea topiki tofauti.
Hakuna ambaye alitaka kuhoji kosa ni la nani au kumuuliza kama angejaribu kuokoa ndoa yake , hakuna ambaye alikuwa mjinga mpaka kufikia hatua hio.
Baada ya Show ya Sophia kuanza kila mmoja alikaa kwenye masofa na kuangalia kama vile ni familia ya kawaida ambayo maisha yao ni ya furaha.
Upande wa Lanlan wakati Roma anaingia aliangaza macho yake kila saa mlangoni kuona kama mama yake ataingia lakini hakuweza kuona kitu na aliishia kuwa na huzuni na hali ya kujikatia tamaa.
Lanlan hakuwa akielewa kwa undani hali halisi lakini aliweza kuhisi baba yake alikuwa na huzuni mno hivyo hakunyanyua mdomo wake na kuuliza mama yake yupo wapi.
Baada ya kumuona Shangazi yake Sophia kwenye runinga akiimba macho yake yalichanua na kusahau huzuni yake kwa muda.
Ilikuwa ni kama Sophia alivyosema ,ilikuwa ni kama hakuna ambacho kimetokea , aliweza kuonekana katika steji akivutia mno na vazi lake la kimtindo , huku kuimba kwake na namna ambavyo anacheza , ukijulimsha urembo wake ulipagawisha watu na kilichosikikika ni sauti za watu kushangilia.
Kwa jinsi watu walivyoweza kujaa pamoja na ‘engagement’ ya tukio hilo ilidhihirisha kitengo cha ‘Public relation’ kilivyokuwa imara .
Kuanzia namna ambavyo ujio mpya wa Sophia kwenye tasnia ilivyokuwa ukisambaa kwenye mitandao ilikuwa ni jambo la ya kushangaaza mno, ilikuwa ni kama vile wale ‘influencers’ wakubwa kwenye mitandao walikuwa wamelipwa kufanya hivyo, kuongea topiki inayohusiana na Sophia pekee.
Lanlan aliekaa alijikuta na yeye akionyesha furaha yake na kusimama na kupiga makofi huku akianza kumwigizia Sophia anavyoimba mpaka mwisho.
Baada ya Show kuisha wanafamilia hao walianza kumuuliza Roma kuhusu maisha ya Seventeen , mama mzazi wa Lanlan na Blandina alijikuta akisikitishwa mno na jambo hilo na kumuonea na Lanlan maisha yake yalivyokuwa mpaka kuja kumpata baba yake na Blandina alijiambia atachukua nafasi hio kumjali mjukuu wake ili tu kumsaidia mtoto wake kupunguza hatia aliokuwa nayo moyoni.
Upande wa Afande Kweka licha ya kwamba kila kitu kilianzia kwake , lakini kusikia stori fupi ya
Seventeen hatia na yenyewe haikumuacha salama, lakini kwa kujua kwamba Edna na Seventeen ni ndugu hakutaka kutia neno lolote.
Ijapokuwa Edna alisema anaachana nae kwa maneno lakini upande wa Roma hakutaka kuendelea kubakia mkoani Iringa na aliaga kabisa siku inayofuata angeondoka na Lanlan, lakini kabla ya hapo alipaswa kwanza kwenda Kigombola Medical Research institute kumtafuta Clark ili kujua matokeo ya uchunguzi wake wa kiafya.
Asubuhi yake wakati Roma na Lanlan wanataka kuondoka , waliweza kupokea ugeni wa Neema Luwazo aliekuwa ameambatana na binti yake Donyi.
Wazazi wa Neema Luwazo walikuwa na ukaribu na Afande Kweka hapo mwanzo na alifika hapo kwa nia ya kumsalimia kwani ni miaka mingi hajawahi kukutana nae, lakini ukiachana na hilo alionekana kama mwanamke ambaye ni kama alikuwa akijaribu kutafuta nafasi yake kama mojawapo ya wanawake wa Roma katika familia hio.
Afande Kweka alifurahi pia kuwaona na alipendezwa na namna Donyi alivyokuwa mkubwa , ijapokuwa ni mtoto wa marehemu Kigombola ambaye alikuwa ni hasamu wake kwenye baadhi ya mambo lakini hakuwa akimchukia Kigombola , wazungu wanasema hakuchukulia utofauti wa mitazamo yao kuwa ‘personal’ .
Roma alimuuliza Neema Iringa anafanya nini na Roma alishangaa mara baada ya kujua Neema alikuwa ni mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe.
Roma hakuwa na uwelewa na maswala ya kisiasa sana hivyo siku zote alikuwa akijua Neema Luwazo alikuwa ni naibu waziri na mbunge kwa wakati mmoja.
“Neema nimesikia kuna kaka yako ambaye anasimamia biashara zako Urusi ni kweli?”Aliuliza Afande Kweka.
“Ndio , anaitwa Msechu amerudi juzi nchini kwasasa yupo Dar es salaam kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka na atarajea kazini Janauri”
“Oh..nadhani ni vyema vijana wakaenda kuishi nje ya nji uli kujua ulimwengu vizuri … nimesikia habari za jeshi letu kuwa katika mazungumzo ya kusafirisha silaha kutoka Urusi kuja Tanzania mwaka ujao katika muda wa nusu mwaka , biashara yako inafanya vyema nchini Urusi kuliko kampuni yoyote hapa nchini , nadhani hili ni swala zuri kwa taifa..”Aliongea na kumfanya Neema macho yake kuchanua , alikuwa ashaelewa ni taarifa gani Mzee Kweka anajaribu kumfikishia.
Ukweli ni kwamba mataifa mengi ya Afrika yalikuwa yakitumia fursa ya Vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine kununua siraha kwa wingi kuingia nchini, ilikuwa ni fursa kwani vita ilikuwa ni kama mpango wa Urusi kupumbaza mahasimu wake wa kibiashara ili kuweza kuuza zaidi na zaidi siraha katika mataifa yaliohitaji bila ya kushitukiwa na Marekani kwa kivuli cha kusaidia mataifa hayo Nafaka.
Ilikuwa ni ngumu Kwa Neema kujua mchakato wa serikali katika kuagiza siraha kutoka nje ya nchi na watu ambao walikuwa na koneksheni za aina hio ni kama Afande Kweka ambaye mzizi yake ndani ya jeshi ilikuwa mirefu sana hivyo alikuwa akijua kila mipango iliokuwa ikiendelea.
Ukiwa na njaa ya pesa ni rahisi pua zako kunusa harufu ya chakula , hivyo Afande Kweka alichokifanya ni kuachia harufu ya chakula kwa Neema mwenye njaa.
Baada ya Neema kuelezea muundo wa biashara yake ndani ya taifa la Urusi alionekana kuridhika na kisha alitoa simu yake na kupiga sehemu na kisha akatoa maagizo flani ambayo yalimfanya Neema moyo kudunda, alijua hata kama alikuwa akienda kuisaidia serikali kuingiza siraha nchini lakinni faida yake ingekuwa mara mbili na biashara yake ya mahoteli.
Baada ya kuongea na Neema kwa muda Afande
Kweka aliitwa na kuambiwa kuna wageni wamefika kwa ajili ya kikao na aliwaacha Roma kuendelea kuongea.
“Lanlan naona unachukulia faida ya uwepo wa mimi shangazi yako hapa , haya niambie mama yako yupo wapi?”Aliuliza Neema.
Alishangazwa na kutokumuona Edna lakini tofauti na kumuuliza Roma aliona atumie akili kumuuliza Lanlan.
“Mommy was angry and she left..”Alijibu Lanlan akimaanisha mama yake alikuwa na hasira na akaondoka.
Neema alishangazwa na maneno ya Lanlan na alijikuta akimwangalia Roma kwa namna ya kutaka maelezo.
Upande wa Roma aliishia kutoa tabasamu la uchungu na alijikuta akielezea kwa ufupi kile kilichotokea usiku wa jana yake
“Kama ni hivyo basi naamini atakuwa amerudi moja kwa moja Dar es salaam kwa sasa?”
“Kwanini unaongea kwa uhakika hivyo?”
“Kwanini nisiongee hivyo, kwanza kabisa hapa Iringa kwasasa ni eneo ambalo hana mtu wa kuongea nae na lenye huzuni na pili kampuni ya Vexto ipo katika mabadiliko makubwa ambayo yanapangwa kufanyika kwanzia mwezi wa kwanza mpaka wa sita na Edna anapaswa kuyasimamia mwenyewe.. “Aliongea Neema na kumuona Roma kuwa kwenye mshangao na alijua fika pengine hakuwa akijua kuhusu hilo.
“Usiniambie hujui kitu ambacho Edna alikuwa akifanya kwenye siku hizi za hivi karibuni?”
“Huwa hatuongei sana kuhusu maswala yake ya kikazi , lakini si alikuwa akimsaidia Sophia kurudi katika tasnia ya sanaa?”
“Ah..! ni kwasababu ndio kwanza umerudi hivyo huwezi kujua kilichokuwa kikiendelea kwa mwezi mzima , kurudi kwa Sophia ni ili kuipa nguvu kampuni ya Vexto kama sehemu tu ya mipango yake , Kujiuzulu kwa Edna ilikuwa ni mwanzo wa kitu kingine kabisa , wakati alipojiuzulu alipunguza hisa zake zote kutoka asilimia tisini mpaka asilimia hamsini na moja,kwa ajili ya kuongeza ‘Shareholder’s’ wengi kwenye kampuni yake ili aweze kukidhi vigezo vya kimataifa kuibadilisha kampuni kutoka katika uhalisia wa jina la Vexto International kwenda Vexto Group”
“Vexto Grup , lakini si ilikuwa ni Vexto Group hapo kabla?”Aliuliza Roma na kumfanya Neema kutoa kicheko.
“Inaonekana kufanya kwako kazi ndani ya Vexto kulikuwa ni bure kabisa, ni kweli ilikuwa hivyo lakini haikuwa imekidhi vigezo vyote , unapaswa kuelewa kwamba ili kampuni kuweza kuitwa Group of Companies na kushiriki katika masoko ya hisa kimataifa inapaswa kuwa na Bodi ya wakurugezi ambayo ina nguvu ya kumuondoa na kumuweka Mkurugenzi mkuu kwa kumchagua ili kulinda maslahi yao ndani ya kampuni, hio ni sifa ambayo Vexto haikuwa nayo,yaani Edna alikuwa ndio mwamuzi wa mwisho kutokana na kuimiliki kampuni yote , lakini mara baada ya kuuza hisa za umiliki wa kampuni kwa nusu nzima inamaanisha kwamba kampuni sio ya kwake peke yake bali yeye
ni mmiliki mkubwa hivyo maamuzi makubwa ya kikampuni lazima yapite kwenye bodi kabla hayajafanyiwa kazi, Mpango wa Edna ni kuifanya Vexto kuwa kundi la makampuni huku yeye akiwa ni mtendaji mkuu na atakuwa amejiongezea nguvu mara mbili na ile ya mwanzo , kwanza kampuni itapanuka sana , lakini pia atakuwa na uwezo wa kujiingiza katika biashara ambazo hana hata uwelewa nazo , kwa mfano anaweza kuunda kampuni ya maswala ya kiteknolojia na ikafanya vizuri kwa kuajili watu wenye uwezo huo au anaweza kufunga zilizopo na kununua nyingine”
Neema alimpa shule Roma na kumfanya kukosa neno la kusema , alijiambia ndio maana Edna alikuwa mwepesi kumpisha Ernest kushika wadhifa wake kumbe kulikuwa na mpango mwingine anawaza kichwani.
Haikuwa hivyo tu Roma alikuwa akijua Edna alijiuzulu kwa ajili ya kujiweka bize na familia kama alivyoongea kumbe yote ni uongo alikuwa akitafuta kujipa thamani zaidi na zaidi.
Ilionekana Ernest siku zote ataendelea kuwa chini ya Edna na kupokea maagizo kutoka kwake.
Kwa maelezo ya Neema ni kwamba kampuni ya Vexto ambayo anaongoza kwa sasa Ernest Komwe ingekatwa kati na kubakia kuwa Kampuni inayohusiana na mavazi na fasheni pamoja na usimamizi wa usambazaji wa malighafi mpya , huku ikiundwa kampuni nyingine Tanzu ambayo ingehusika na maswala ya mafuta ya petroli na mambo mengine.
“Umeliona lile jengo refu zuri ambalo linajengwa pale Mwenge?”Aliuliza Neema.
“Unamaanisha lile lenye urefu kwenda hewani ambalo ndio lipo hatua ya mwisho?”
“Ndio hilo?, lile ndio jengo ambalo litakuwa makao makuu mapya rasmi ya kampuni ya Vexto Group”
“Nilijua lile jengo linajengwa na Vexto Constructor na mmiliki wake ni kampuni ya Nebula inc, maelezo hayo niliyapata kwa Daudi nilipokuwa mkurugenzi?” “Upo sahihi linajengwa kwa ajili ya kuwa makao makuu ya Nebula Inc lakini mmiliki wa kampuni ya Nebula Inc kwasasa ni Edna , sijui kilichotokea lakini ninachojua ni kwamba safari yake ya mwisho ya kikazi kwenda Hongkong iliwezesha hilo”Aliongea Neema na Roma kuhisi kuchanganyikiwa na kujiuliza Edna sio mwanamke wa kawaida.
Roma alikumbuka siku ambayo Edna ameenda
HongKong kikazi alimuunganisha na Edward wa Rothchild kumrahisia shida yake, pengine aliamini kuna mengi zaidi ambayo yaliendelea na Edward hata hakumwambia.
“Kwanini unayajua hayo yote?”
“Kama mpango wa Edna utafanikiwa basi sio kwamba tu atakuwa mshindani wangu wa kibiashara bali makampuni mengi ndani ya Tanzania yanaweza kumezwa, hivyo lazima na mimi nijiandae namna ya kuifanya kampuni yangu iendelee kuishi, ndio maana napanga kujiuzuru nafasi yangu ya uwaziri nibakie katika uendeshaji wa biashara”Aliongea na Roma hakutia neno.
Roma aliishia kujikuna kichwa chake , alijiambia mbona anazidi kuwa butu wa kifikra au ni kwasababu hakuwa na uwezo wa kutumia uwezo wake , maana IQ yake ilikuwa imeshuka mno”
“Halafu ukichana na hayo , nahishi kilichotokea jana yake sio kawaida”Aliongea Neema akimwangalia Roma anaejikuna kichwa.
“Unamaanisha nini?”
“Sidhani kama Edna ni mtu wa kushindwa kujizuia na kutaka kumuua Sophia kwasababu tu ya wivu , kama ni hivyo si anapaswa kuniua na mimi?”Aliongea.
“Unaongea utani mpaka sasa hivi tu?”Aliongea Roma akitoa tabasamu la kulazimisha.
“Najaribu kukufurahisha , wewe mwanaharamu usie na shukrani”
“Unapaswa kutania vitu vingine , sitaki kuona yeyote kati yenu akiumia la sivyo itanifanya kuonekana nimefeli”Aliongea na kumfanya Neema kujisikia vizuri.
“Nilichokuwa nikitaka kumaanisha ni kwamba , Edna anaonekana na tatizo ambalo linamsumbua hata kabla hujarudi nilishawahi kumuuliza lakini hakuongea chochote”
“Kwahio unamaanisha hujui chochote kwasababu hajakuambia chochote?”Aliongea Roma akijikatia tamaa.
“Mimi naongea tu , nitajuaje anachoficha kwenye moyo wake ,isitoshe si vizuri tu kwani nimepunguza mshindani mwingine , unajuaje siku moja nikabakia peke yangu”Aliongea na kumfanya Roma kumchapa kibao cha mapajani.
“Ukiendelea hviyo nitaondoka sasa hivi na Lanlan nimtafute nimuulize mwenyewe”
“Haha.. ukweli ni kwamba najua swala la Lanlan lilikuwa kubwa kwake lakini kwa ninavyoona kwa kutoshindana kwake na wewe katika maswala ya nani amlee Lanlan ,naamini wewe anakuchulia ni wa muhimu zaidi kwake”
Roma aliona maneno ya Neema yapo sahihi , ijapokuwa Edna mara baada ya kujua kuhusu Lanlan hakuonyesha kutatizwa na hilo na alichokuwa akiongea ni tofauti kabisa kama sababu ya kumuacha.
Roma mara baada ya kuachana na Neema moja kwa moja alichukuana na Lanlan na kuelekea nae chuoni maaabara kwa ajili ya kumtafuta Clark ili ampatie majibu yake.
Baada ya kufika na kuongea kidogo na Clark kwa kumtambulisha Lanlan kama mtoto wake wa damu aliemzaa na Seventeen waliingia kwenye maswala ya matibabu lakini licha ya hivyo Clark alionekana kushangaa kwani hakutegemea kama Seventeen aliacha mtoto.
Lakini licha ya hivyo alifurahi na kumbeba Lanlan na alijiambia ndio maana alikuwa anafanana sana na Edna kumbe alikuwa ni mtoto wa Seventeen ambaye alikuwa akifanana na Edna.
“Huu ndio uchambuzi wa taarifa za uchunguzi niliokufanyia , unaweza kujionea mwenyewe”Aliongea Clark akimpatia Roma makaratasi.
“Mimi sijui chochote hapa , nadhani ni vyema kama utanielezea mwenyewe”
“Kwa haraka haraka naweza kusema kwamba kuna taarifa nzuri na mbaya , ipi ndio unataka ianze”
“Tuanze na hio taarifa nzuri kwanza”
“Taarifa nzuri ni kwamba mwili wako umekuwa na nguvu zaidi ya mara tatu kuliko mwanzo tokea mara ya mwisho nilipokufanyia vipimo , hii ni tofauti kwasababu nilitegemea uvimbe wako kuongezeka kwake ndio kupungua kwa uwezo wako , lakini vipimo vinaonyesha ni tofauti , kwasasa naweza kusema mchakato wako wa ukuaji wa kimwili ni kama ‘Metarmophosis’.. lakini umeruka hatua mbili mbele za kiukuaji”Aliongea na Roma alielewa kwa haraka.
“Vipi kuhusu taarifa mbaya”
“Taarifa mbaya ni kwamba ni nusu ya taarifa nzuri , sikujua mwanzo lakini mara baada ya kuvuna nishati za mbingu mwenyewe nimeweza kujua baadhi ya vitu ambavyo havina maelezo ya kisayansi … utendaji wako wa kazi katika ubongo umekuwa wa tofauti sana na nilikosa taarifa za kisayansi kugundua sababu ya mabadiliko hayo , lakini kwa haraka haraka naweza kusema kuna nguvu iliopo ndani yako inayoshindana na mfumo wako wa mawasiliano wa kawaida wa mwili , ni nguvu ambayo naweza kusema haipaswi kutokea kwa wakati mmoja(Mutual exclusive)… na kwasasa nguvu hizo zipo katika hali ya uwiano sawia… kwa maneno marahisi ni kwamba licha ya nguvu zote kuwa kubwa kwa kulingana itakuwa ngumu kwako kuishinda na kuvunja huo uwiano ,,, kwahio ni kama umefungwa”

SEHEMU YA 639.
Roma alishika kichwa chake akionyesha hali ya kushikwa na mawazo na palepale alivuta hewa nyingi na kuitoa nje akionyesha hali ya huzuni kidogo.
“Ulivyoelezea ni kama ambavyo nimefikiria na umethibitisha tatizo langu, lakini tatizo lingine ni kwamba ni kipi napaswa kufanya”
“Kwa ninavyoona kutumia njia za kawaida za kisayansi haziwezi kuwa na ufanisi , lakini … umesahau kwamba wewe sio mtu pekee ambaye unamiliki nguvu za kijini?”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha ni swala la kinadharia … ninajiuliza je haitowezekana kutumia nguvu kubwa ya nje kukuongezea uwezo wa kuweza kutawala nguvu inayoshindana na ya kwako , kitu pekee ambacho kwasasa unaweza kufanya ni kuendelea kushikilia uwiano lakini vipi kama kuna nguvu nyingine ya nje ambayo inaweza kukusaidia kwa kukuongezea nguvu , Rose na Magdalena wote washaingia katika levo ya Nafsi , licha ya kwamba wanaweza kuwa na nguvu ambazo ni za chini na ya kwako watakuwa na nguvu ya kijini ya kuweza kukusaidia na kuvunja uwiano na wewe kushinda”
Roma macho yalichanua mara baada ya kusikiliza pendekezo hilo zuri lakini alitingisha kichwa kukataa .
“Hapana , itakuwa ni hatari sana kwao, roho ya mnyama ni ya hatari sana na ina nguvu ya giza , kama mambo yakienda vibaya Rose na Magdalena wanaweza kupatwa na tatizo”
“Basi usiwe na wasiwasi naamini kutakuwa na mbinu nyingine zaidi , isitoshe nitaelekea Dar na nitakutana na Rufi na atanipa baadhi ya taarifa ambazo zinaweza kunisaidia kutengeneza njia mbadala ya kukusaidia”
Roma aliishia kukubali, ijapokuwa swala lake hakutaka lifahamike kwa wanawake wake lakini kwa upande wa Rufi aliona tu ngoja ajue ,lakini alijihakikishia kwamba asingetumia pendekezo la Clark la kuwatumia Magdalena na Rose kumsaidia mpaka awe na uhakika wa usalama wao.
******
Upande wa Dar hali ya hewa ilikuwa ya mawingu na vipindi vya jua ikiashiria muda wowote mvua inaweza kunyesha , ilikuwa ni kama ilivyotabiriwa katika kipindi cha hali ya hewa jana yake kuonya mvua kubwa ingeweza kunyesha.
Najma alikuwa na ugeni ndani ya sehemu anayoishi , alikuwa ni Shangazi yake na wifi yake ambao walilala hapo na asubuhi hio walikuwa wakijiandaa kwenda kutembea.
Shangazi yake Najma hakupata utulivu , tokea mara ya kwanza kuonja utamu wa kupanda gari ya pesa nyingi kila saa alitaka kulipanda na siku hio ambayo Najma alikuwa Off alilazimisha kwa kumtaka Najma kwenda kutalii talii kupoteza muda ndio warudi nyumbani kwao.
Najma hakuwa na tatizo kwani alikuwa off lakini ukweli ni kwamba alitamani siku hio kuitumia katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi na jioni kwenda kumtembelea rafiki yake Nasra lakini ujio wa shangazi yake na wifi yake ni kama ulivuruga ratiba zake.
“Katika maisha yangu sijawahi kuwaza kama kuna mwanafamilia katika ukoo wetu ambaye anaweza kumiliki gari kama hii”Aliongea Shangazi yake Najma huku akitoa kicheko .
“Shangazi unasemaje hivyo , lilikuwa swala la muda tu kwa Najma , uzuri wake sio wa kawaida hata hivyo”
“Haha.. umeongea kweli mwanangu, Najma amezaliwa kwa ajili ya vitu kama hivi.. Najma kama asingekuwa ubishi wake kipindi kile angekuwa sasa hivi ashazalishwa na yule Ahmed kina kifupi na gari angekuwa anaiota ndotoni tu”Aliongea huku wakicheka na kugongesheana mikono na mke wake Juma.
Najma alishindwa kuchangia neno na maneno ya shangazi yake yalimkumbusha mwaka uliopita namna ambavyo Shangazi yake na kaka yake walivyokuwa kidedea kumtaka aolewe na Ahmedi ,lakini kwa namna ambavyo shangazi yake anaongea ni kama amesahau kabisa na hakuonekana kuwa na hatia tena saivu anamwita Ahmedi kina kifupi.
Ni mara baada ya Najma kuingiza gari barabarani ghafla tu ilitokea gari aina ya Ford SUV ya rangi nyeusi na kuwazibia njia mbele yao.
Najma aliekuwa ni dereva alijikuta akikunja sura na alijaribu kupiga honi na kuwasha taa kuashilia kwamba apishwe njia lakini dereza wa gari hio alionekana hawakuwa na nia yoyote ya kumpisha.
Baada ya dakika kama tatu kupita gari ile ilifunguliwa milango yote na waliweza kutokezea wanaume wanne wenye miili mikubwa ya mazoezi wote wakiwa weusi waliovalia mavazi ya suti nyeusi kama mabodigadi pamoja na miwani za jua huku wote kwa pamoja wakiwa wameshikilia mitalimbo ya chuma mkononi.
Najma palepale alijikuta akinusa hatari na alimwangalia Shangazi na Wifi yake ambaye alikuwa amepakata mtoto mdogo na kuwaambia watoke kwenye gari haraka.
Lakini licha ya Najma kuongea wale wanaume kwa haraka walisogelea gari na kwenda kusimama kwenye mlango wa gari huku kiongozi wao aliekuwa akivuta sigara alitoa cheko la kebehi akiwa mbele ya gari.
“Bang!!”
Yule kiongozi wao mara baada ya kusogea mbele aliinua chumba chake kigumu na kupiga kwa nguvu mbele ya boneti ya gari ya Najma na kulifanya libonyee kwa mbele palepale na taa zote kuvunjika.
Waliokuwa ndani ya gari waliishia kutoa kilio cha mshituko huku sura zao zikijawa na wasiwasi na kuanza kutetemeka kwani sio tukio la kawaida.
Ilikuwa ni kama wameagizwa vile kwani wale watatu waliokuwa wamesimama kwenye milango ya kutokea walianza na wao kulipiga na vyuma lile gari kuanzia nyuma mpaka juu ya paa.
Hawakujali mtoto aliekuwa akitoa kilio ndani ya gari na wao waliendeleza kazi , Mke wa Juma alijikuta akimziba mtoto wake masikio huyu yeye akitetemeka kwa hofu.
Ilikuwa ni bahati kwamba waliweza kufanikiwa kutoka bila kupata madhara lakini gari iliharibika sana na kubadilika muonekano na haikuwa gari tena ile mpya ambayo ilikuwa ya bei ghali.
Tena mara baada ya Najma na ndugu zake walivyotoka ndio walivyozidi kuliharibu lile gari kwa spidi kubwa na walipasua vioo vyote na kuchokonoa na eneo la injjini na moshi ulianza kufuka.
“Nyie ni wakina nani , kwanini mnatufanyia hivi?”Aliuliza Najma aliekuwa akitetemeka kwa hasira , hakuamini gari ambayo amepewa kama zawadi na mpenzi wake imepatwa na majeraha ya aina hio tena ndani ya siku mbili tu.
Yule kiongozi mara baada ya kumuona Najma amenyanyua mdomo na kuongea alimwangalia kwa dharau.
“Mrembo , ni kosa lako mwenyewe kutoka kimapenzi na mwanaume ambaye sio saizi yako na kumkasirisha yule mwanamke, hili ni onyo tu ambalo tumejaribu kukufikishia kutoka kwa mwanamke uliemchokoza , usije kuthubutu kuwa karibu na Boss wa kiume tena , siku nyingine haitoishia kwenye kuharibu gari tu bali ni …”Aliongea huku akionyesha ishara ya kuua.
Baada ya kuongea maneno hayo Najma palepale alijua nani ambaye amewatuma hao majambazi , kumbe ni mwanamke ambaye anamjua kama mama yake Naibu waziri Salihi ndio ambaye amekuja kumshambulia kwa kuagiza watu wake bila sababu za msingi kisa kumuona akiongea na Salihi.
Najma alijikuta akitokwa na machozi na kumwangalia shangazi yake ambaye amekatwa na kioo kwenye bega na alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kuona mtoto hajapatwa na majeraha.
“Kama ni hivyo kwanini mnaingiza watu wengine ambao hawahusiki, hawa ndugu zangu wamefanya nini , kwanini msingesuburi nikiwa peke yangu ndio mnishambulie”
“Haha… wewe msichana tena nyamaza, nishaharibu magari mengi tu kama hivi lakini sijawahi kuona msichana jasiri kama wewe ambaye unaongea mara baada ya kukushambulia kama hivi , ni bahati mbaya kwamba licha ya kutufokea kwako ni bure , kazi nilioagizwa leo hii ni kuharibu gari yako basi nikirudi jua ni zamu yako”
Najma alijikuta akikosa neno la kuongea na kuishia kuwaangalia kwa hasira lakini wanaume wale hawakuonekana kuwa na hofu kabisa licha ya kufanya tukio hilo mchana kweupe na baadhi ya watu wanaangalia.
Najma palepale wazo la kupiga simu polisi lilimjia na alitoa simu yake na kutaka kupiga , lakini wale watu walikuwa wakimwangalia tu anachotaka kufanya.
“Hehe ndio unajaribu kupiga simu polisi.. haha utakuwa unachekesha , kama tungekuwa tunaogopa polisi tusingeharibu gari yako wale watu wakiwa wanaangalia tena mchana kweupee”Aliongea na kuwafanya wale wanaume wengine kucheka na kisha walipeana ishara na kuingia kwenye gari yao .
Najma licha ya kuona gari yao imeondoka hakughairisha kwenye kupiga simu polisi na mara baada ya kuelekzea kila kitu palepale alimkimbilia wifi yake.
“Wifi mtoto yupo salama?”Aliuliza na mke wake Juma alishia kutingisha kichwa huku machozi yakimtoka.
“Najma umemchokoza nani , hawa majambazi ni wakina nani?”Aliuliza Shangazi yake Najma huku akishika jeraha lake ambalo lilikuwa likivuja damu.
“Sijui chochote Aunt , ngoja tusubiri polisi wafike na tuone watapata nini kupitia uchunguzi wao”Aliongea kwa kutetemeka.
“Najma inaoneana aliefanya hivi anakisasi ,ijapokuwa sijasikia vizuri lakini inaonekana ni mwanamke aliegiza ufanyiwe hivi , Najma hebu niambie ni mke wa Roma ndio kakufanyia hivi?”Aliuliza Shangazi yake Najma kwa wasiwasi.
Ijapokuwa alikuwa akijua Edna alikuwa mtu mzuri mpaka kumsaidia Juma kupona kwa kulipia matibabu lakini swala la Najma kujihusihsa kimapenzi na Roma lilikuwa ni tofauti hivyo aliona kwa upole wa Najma ambaye ni ngumu kutengeneza maadui basi mtu pekee anaeweza kutuma kumshambulia ni Edna.
“Shangazi hapana, Sister Edna hawezi kunifanyia hivi, ni swala ambalo halihusiani na Roma kabisa , msiwe na wasiwasi hili nitalimaliza mwenyewe”Aliuongea
“Utalimaliza vipi Najma? , licha ya kwamba unafanya kazi wizarani nafasi yako ni ya kawaida na huna koneksheni yoyote , nadhani umewasikia wenyewe hawaogopoi polisi , unadhani bila ya kuwa na nguvu unaweza kuwashitaki , mpigie Roma umwelezee sasa hivi , ndio mtu pekee anaeweza kukusaidia mpigie umwambie kila kitu…nimechukia sana”Aliongea huku akionyesha kukosa uvumilivu na kuongea kwa sauti ya kufoka.
“Lakini Roma hayupo hapa Dar”
“Mpigie kama kweli anakupenda hawezi kudharau matatizo yako, fanya hivyo Najma kwa usalama wako , awamu nyingine watakuja kukua wewe mwenyewe ohoo”
“Najma kweli fanya kama Shangazi anavyosema, inaonekana mtu aliefanya hivi ana kinyongo na sio mwepesi kudili nae kupitia polisi”
Najma alijikuta aking’ata lips zake kwa aibu , alikuwa pia akitamani kumpigia Roma simu na kumwambia yaliotokea lakini aliogopa Roma angemwelewa vibaya kuhusu kuhusika kwa mama yake Waziri Salihi , isitoshe gari la mamilioni ya pesa ambalo amemnunulia juzi tu ndio hilo lishaharibiwa na hakujua namna ya kumwelezea Roma , ki ufupi aliogopa.
Najma aligeuza macho yake na kumwangalia Shangazi yake aliekuwa akimkodolea macho akiwa na hasira kwa udhalilishaji waliofanyiwa na Najma aliishia kujawa na hofu na kisha palepale aliitafuta namba ya Roma na kupiga.
Lakini alikuja kugundua namba ile haikuwa hewani kwani aliambiwa simu ilikuwa imezimwa.
“Amezima simu yake na hapatikani pengine kuna kinachoendelea”
“Basi nadhani hatuna jinsi , subiri baadae umpigie kwasasa tunapaswa kusubiri hao polisi tuone wataongea nini mara baada ya kufika,Looh zote hizi ni laana ya umasikini inayotunyanyasa…pukeee!!”Aliongea Shangazi huyo akitema mate chini huku hata yeye licha ya kushambuliwa lakini alihurumia gari mbaya ambayo haikuwa na ule muonekano wa mwanzo.
“Najma ikitokea anataka kununulia gari nyingine mwambie akunulie hata ka Spacio , nadhani mizimu ya ukoo haitaki tupande magari ya kifahari”Aliendelea kuongea.
*****
Upande wa Roma muda huo ndio alikuwa akiingia ndani ya ndege na alitii sheria na kuzima simu yake.
Roma alikuwa amekaa na binti yake katika daraja la kwanza katika ndege hio ya shirika la taifa na ilichukua dakika chache tu mara baada ya kutulia Lanlan alipitiwa na usingizi.
Mdada mrembo mhudumu mara baada ya kufika kuwahudumia abiria wa daraja la kwanza alijikuta akivutiwa na mwonekano wa Lanlan na mara baada ya kujua baba yake na yeye amefumba macho alitoa simu yae akitaka kupiga picha lakini Roma aliyafumbua na kumwangalia.
Roma hakuonyesha kufurahishwa na kitendo cha muhudumu huyo anachotaka kufanya na alinyoosha mkono kama vile anataka kitu kutoka kwa mhudumu huyo lakini yule mrembo aliishia kutabasamu huku akiona aibbu amekamatwa.
“Samahani kwa kukusumbua Sir , je naweza kukuuliza ni kipi unahitaji?”
“Pesa bila shaka , kipi kingine naweza kutaka , huwezi kumpiga picha binti yangu mrembo bila malipo , hata ukienda mbuga za wanyama kuna kiingilio cha pesa unacholipia sembuse binti yangu mzuri hapa,”Aliongea Roma akiwa siriasi.
Yule mrembo aliishia kuona aibu lakini kwa siri akivuta mdomo na kujiuliza imewezekanaje mwanaume asie na aibu kama huyo kukaa daraja la kwanza , alijiambia ashukuru Mungu kwa kumtunuku binti mrembo kama huyo maana hakuwa akiendana na mwonekano wake.
Ijapokuwa alikuwa akimdhihaki Roma ndani kwa ndani lakini kutokana na taaluma yake iliendelea kumwonyeshea tabasamu la ukarimu.
Palepale alitoa baadhi ya matunda na Sambusa wa nyama kwenye kijitoroli chake na kumpatia Roma kama rushwa ya kumtuliza.
Roma mara baada ya kushika sambusa aliisogeza karibu na pua za Lanlan na palepale alishituka kutoka usingizini na kupokea ile sambusa na kuila yote ndani ya dakika na kisha Roma akachukua na nyingine na kumpatia na aliipiga yote ikaisha na kisha aligeuza macho yake na kumwangalia mhudumu wa ndege.
Mhudumu yule aliishia kushangaa tu na ilikuwa afadhali kwani ndani ya daraja la kwanza chakula cha abiria kilikuwa cha kutosha hivyo alimpatia Lanlan nyingine na kisha akawaacha.
“Daddy , are we going to find mommy?”Aliuliza Lanlan na kumfanya Roma kukakamaa mwili na kumwangalia Lanlan akitafuta jibu la kumpa.
“Mama sasa hivi hana furaha baada ya kugombana na Daddy, .. Daddy atamshawishi mama baada ya muda ili arudi , kwasasa uwe mtiifu kumsubiri mpaka arudi”
“Kwahio Daddy unamaannisha siwezi kulala na mama tena?”
“Ndio , mama yako hatoturuhusu turudi nyumbani kwasasa”Aliongea Roma akionyesha mwonekano wa kimawazo.
“Can Lanlan Sleep with Aunt Nasra?”Aliuliza kwamba je anaweza kulala na shangazi yake Nasra.
“Wewe mtoto msaliti , unataka kumuacha mama yako kirahisi hivyo , unampenda Aunt Nasra sana?”
“Bibi amesema watoto hatupaswi kuingilia maswala ya wakubwa na kama nitaendelea kuwa mtiifu basi nitaendelea kula chakula kitamu , Aunt Nasra anapika chakula kitamu”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa sasa kumbe ukaribu wa Lanlan na Nasra ni kwenye mapishi.
Roma kwa alivyokuwa akijua wanaojua kupika sana ni Nasra na Najma , Dorisi alikuwa fundi kwenye upishi lakini alikuwa mvivu ila Nasra alikuwa akipenda kupika sana na chakula chake ni kitamu ,hakujua Lanlan amekionja lini lakini hakutaka kuuliza sana.,
Ukweli ni kwamba Blandina alimwambia Lanlan akakae kwa Nasra mpaka mama yake atakapomtafuta.
Roma licha ya kwamba alijua Lanlan kwenda kukaa kwa Nasra kunaweza kumfanya Edna azidi kukasirika lakini hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kumpeleka huko alikotaka.
Baada ya lisaa limoja na nusu Roma aliweza kufika Dar es salaam huku Lanlan akimwambia baba yake kama wangepaa wangekuwa washafika , lakini Roma aliishia kumjibu Lanlan atapaa nae siku nyingine ila ajitahidi aweze kupaa mwenyewe.
Roma mara baada ya kuwasha simu yake alishangaa baada ya kuona Missed call ambazo zilikwua zimeingia kwenye simu yake zikitoka kwa Najma.
Roma alisimama akiwa amemshikilia mkono Lanlan na kuanza kufanya mawasiliano kwani alihisi kuna kitu hakipo sawa na mara baada ya kupiga kwa dakika kadhaa simu haikupokewa kwani haikuwa ikipatikana hewani na jambo hilo lilimpa mashaka
na palepale aliitafuta namba ya simu ya Juma na kupiga na iliita mara moja tu na kupokelwa.
“Roma Bro mbona hukuwa ukipatikana hewani , tafuta namna ya kumsaidia Najma , amekamatwa na polisi”Aliongea Juma akiwa na wasiwasi na kumfanya Roma kushangaa.

SEHEMU YA 640.
Roma alijikuta akipatwa na wasiwasi na kujiuliza imekuwaje Najma akaishia kwenye mikono ya polisi.
“Juma hebu ongea taratibu taratibu uniambie nini kimetokea”Aliongea Roma na pale Juma alimpatia simu shangazi yake na kuanza kuelezea tukio.
Ilionekana mara baada ya polisi kufika ndani ya nusu saa walijairbu kumhoji Najma juu ya kilichotokea na mara baada ya kuelezea polisi walimchukua na kuondoka nae huku wakisema anaenda kusaidia maswala ya uchunguzi zaidi.
Lakini ajabu ni kwamba baada ya lisaa Najma simu yake haikuwa ikipatikana tena na wamejaribu kwenda kwenye kituo cha Oysterbay ambacho inasemekana alipelekwa lakini walikosa ushirikiano kutoka polisi.
“Basi naomba mpunguze wasiwasi nitadili na hili swala mwenyewe”Aliongea Roma na muda huo walikuwa tayari washaingia kwenye taksi.
Roma aliambiwa Najma alipelekwa kituo cha Oysterbay na alitamani kwenda moja kwa moja lakini alijiambia anaweza kafanya kitu kibaya hivyo aliona hatua ya kwanza ni kumpeleka kwanza Lanlan nyumbani huku yeye akitumia koneksheni zake kujua nini kinaendelea.
Baada ya kufikiria nani ambaye anaweza kumsaidia swala lake palepale jina la Omari Tozo liliibuka kwenye kichwa chake na hakutaka kupoteza muda na alimpigia.
“Hey! Bro ni mzimu gani umekupitiia mpaka ukakumbuka kunipigia simu leo , sio kawaida yako?. Nimefika Iringa jana na mpango wangu ni kukutafuta leo kwa ajili ya kwenda kupata moja moto moja baridi baada ya kupewa ruhusa na mke wangu..”
“Hebu acha ngonjera zako kwanza ,,, nina shida ya haraka nataka unisaidie, nipo Dar sasa hivi nishatoka Iringa”
“Kwanini umerudi haraka hivyo , nilijua bado upo Iringa ndio maana nimekuja huku tuonane, anyway ni jambo gani ambalo unataka nikusaidie”
“Mwanamke wangu mmoja anaefahamika kwa jina la Najma amekamatwa na watu wa polisi na kupelekwa kituo cha OysterBay na ndugu zake wameenda huko lakini hakuna ushirikiano , hebu nisaidie kutuma mtu wa kueleweka akarahisishe hilo swala na atoke polisi, najua hukosi koneksheni ndani ya jeshi la polisi maana upo kitengoni” Ukiachana na baba yake Omari kuwa mkuu wa majeshi lakini pia mjomba wake Omari yaani kaka yake mama yake ni mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa na pengine ndio maana ilikuwa rahisi kwa Oamri kujiunga na usalama wa taifa tofauti na kitengo cha jeshi.
“Hahaha.. kuna watu wanajiamini aisee , nani kapata ujasiri wa kukuchokoza kwa kumkamata mrembo wako”
“Hebu acha utani na fanya jambo la haraka upigie mtu afanye kurahisisha hili”
“Sawa bro usiwe na wasiwasi najua ni kipi nifanye”Aliongea Oamri na kisha akakata simu palepale.
Roma asingeweza kumpigia simu Mage kumsaidia katika hilo kwani Mage alishaachana na maswala ya upolisi na alikuwa akijiandaa kuelekea Visiwa vya wafu, lakini pia hakutaka kufanya hivyo kwani aliona sio vizuri kumpigia mwanamke wake kumsaidia mwanamke wake mwingine .
Upande mwingine ndani ya kitua cha polisi Masaki alionekana mwanaume mzee kidogo ambaye kwa kumwangalia tu ni makadirio ya miaka hamsini hivi akiwa ameketi ndani ya ofisi ndani ya kituo hicho akiwa na sigara ameishikilia mkono wa kushoto huku kulia akiwa ameshikilia gazeti la mwananchi.
Alikuwa ni Mkuu wa kituo mpya ambaye amepandishwa cheo hivi karibuni mara baada ya Mage kujiuzulu , alikuwa akifahamika kwa jina maarufu la Afande Mkanye.
Afande Mkanye alikuwa na miaka hamsini na saba na alikuwa mkali mno kiasi cha watu kuanza kumfananisha na jina lake na ilikuwa hata polisi wenzake walikuwa wakimuogopa.
Licha ya ukali wake huo kutokana na elimu yake kuwa ndogo hakuweza kupata cheo kikubwa kwa muda mrefu lakini mara baada ya Mage kuachia ngazi ndio sasa akaweza kupata nafasi ambayo ilikuwa ni ya ndoto yake kabla ya kustaafu.
Unaambiwa tokea apewe cheo hicho alikuwa akilala kituoni ndani ya ofisi yake kwenye masofa na alipoulizwa alisema anafidia siku ambazo serikali imemcheleweshea kumpandisha cheo.
Wakati akiendelea kuwa bize kusoma gazeti lake linalohusiana habari za kitaifa palepale mlango wa ofisi yake uligongwa na kuruhusu mgongaji kuingia.
Mlango mara baada ya kufunguliwa alionekana mwanaume kijana aliekuwa katika sare za polisi mwenye makaridio ya miaka therathini , alienyoa upara na ndevu zote , huku akiwa na Komwe pana na kumfanya kuonekana kama mtu mwenye kichwa kikubwa.
Bwana huyo ndio alikuwa mkuu msaidizi(Junior Superintendent) wa kituo hicho ambaye alihamishiwa mwaka huo kituoni hapo , kabla ya kuja jijini Dar es salaam alikuwa ni polisi wa kawaida wilayani kisarawe.
Baada ya kusalimiana na Afande Mkanye palepale alienda kwenye mada ya kitu kilichomfanya kuingia ofisini hapo kwa mkuu wake.
“Chief nipo hapa kuulizia kama kuna mwanamke anaefahamika kwa jina la Najma Waziri kushikiliwa hapa kituoni ,ni mfanyakazi wa Wizara ya elimu”Aliongea na kumfanya Afande Mkanye kukunja ndita na kuweka gazeti lake chini huku akizima sigari yake kwenye sahani ya udongo.
“Afande Jamali kwanini unaniuliza swala hilo mimi , ulipaswa kujua wewe kabla ya mimi kuju”Aliongea.
“Afande ni kwamba nimepokea simu ambayo inasema mwanamke huyo anazuiliwa hapa kituoni kwetu lakini mara baada ya kuulizia taarifa zake inaonekana hakuna jina lake kati ya wanawake waliokamatwa , nimekuja kuuliza kama swala hili ni la kimya kimya,Chief nadhani unajua mabadiliko ambayo yamefanyika ndani ya jeshi la polisi na msisitizo ni kufanya mambo kwa uwazi na kutoa ushirikiano kwa watu wote wanaongiziwa ili kuepusha lawama”
Uso wa Afande Mkanye ulijikunja , swala la Najma yeye ndio alikuwa nyuma yake lakini mtu ambaye amempa kazi ya kumkamata Najma alikuwa akibweka sana, ijapokuwa alijua Najma alikuwa ni mfanyakazi wa wizara lakini nafasi yake haikuwa tishio sana kumletea shida , isitoshe watu ambao wamempatia kazi hio walikuwa wakubwa zaidi ya wizara yenyewe.
“Jamali hio taarifa umetoa wapi au ndio umepokea simu kutoka kwa watu wasiofahamika na upo hapa kuniuliza maswali ya kijinga , nadhani unajua kwamba miaka yangu ya kuhudumu katika jeshi la polisi inaheshabika napanga hii nafasi yangu wewe kuichukua , hivyo hupaswi kuuliza maswali mengi , kama kuna mtu amekuliza wewe mpotezee”Aliongea akimwashiria kuondoka ofisini kwake lakini Afande Jamali alionekana kusita.
Afande Mkanye mara baada ya kuona Afande Jamali yupo kimya na anaonekana kukosa ujasiri wa kuongea aliona kabisa huyo mwamba atakuwa anamuogopa na alitoa tabasamu la ushindi.
Lakini alikuwa amedhania vibaya kwani upande wa Afande Jamal alikuwa akijishauri kama aweke wazi utambulisho wake mwingine tofauti na kuwa polisi au akae kimya.
Baada ya kufikiria kwa muda mfupi aliingizia mkono kwenye kombati yake na kutoa kitambulisho na kumpatia Afande Mkanye.
“Chief , lazima nipate majibu kwa maswali yangu muda huu , hivyo niambie ukweli wote”Aliongea huku akiwa anatabasamu na Afande Mkanye alitoka katika kuegamia Sofa kibosi na kisha aliinama na kuchukua kitambulisho ambacho kilikuwa kama
Passport ya kusafiria na kufungua ndani na palepale alijikuta akitoa macho na kukaa vizuri huku mikono yake kuanza kutetemeka .
“Tanzania intelligence and security Service(TISS)!!!”
Licha ya kwamba hana elimu kubwa haikumaanisha kushindwa kujua kitambulisho cha mwanausalama wa taifa.
Bwana huyo alijikuta akishangaa na kujiambia ndio maana Jamali alionekana kuwa mkimya sana nyakati nyingi lakini aliweza kupata cheo kikubwa ndani ya muda mfupi tena akipita polisi waliokuwa wakifanya kazi ndani ya kituo hicho kwa muda mrefu hata yeye mwenyewe ambaye siku zote alikuwa akisotea cheo cha Senior inspector wakati Jamali alikuja moja kwa moja na kupewa cheo cha Superintendent kumbe ni kwasababu alikuwa mwanausalama aliepandikizwa ndani ya jeshi la polisi na serikali , kengele ya kukosa mafano na kiinua mgongo iligonga kwenye masikio yake.
“Chiefu vipi vielelezo vyangu vipo sawa?”
“Ndio.. ndio , siwezi kukataa hata kama ni kipofu”Aliongea huku akijaribu kutabasamu.
“Kama ni hivyo je naweza kupata majibu juu ya Miss Najma anashikiliwa kituo gani na kwasababu zipi?”Aliuliza na kumfanya Afande Mkonyi jasho kumtoka.
Mpaka kitendo cha Jamali kuamua kujitoa kivulini kama mwanausalama na kuweka wazi uhusika wake ilimaanisha mtu aliekamatwa sio wa kawaida kama alivyofikiria.
“Jamali .. ukweli ni kwamba mwanamke huyo anaieitwa Najma amekamatwa lakini hakuletwa hapa”Aliongea kwa wasiwasi mno .
………………
Dakika chache mbele Afande Jamal aliweza kutoka huku akiwa na mwonekano wa kuchoka mno kutokana na ugumu wa swala lenyewe.
Mwanzonni alijua ni swala la kawaida tu ambalo anaweza kulifanyia maamuzi lakini mara baada ya kujua muhusika aliekuwa nyuma ya kukamatwa kwa Najma alijikuta akichoka na aliona asingeweza kukamilisha kazi yake kwa cheo chake.
Baada ya kurudi ofisini kwake na kikaa chini alimpigia Omari Tozo kwa mara nyingine kumrudishia majibu maana alipata maagizo kutoka kwake.
“Kaimu ni mimi..”
“Najua ni wewe ndio , vipi kazi imekamilik?”:
“Kazi imeshindikana kutokana na uzito wenyewe , familia ya Nguzo ya Taifa inahusika katika hili”Aliongea na kumfanya Omari upande wa pili kuguna.
*******
Roma mara baada ya kufika nyumbani kwa Nasra aliweza kuwakuta wakiwa wanamsuburi nje akiwa ameambatana na Qiang.
Roma alishatoa maagizo tokea akiwa Aiport kwa Qiang kukusanya nguo za Lanlan na kuzipeleka nyumbani kwa Nasra na ataishi huko kwa muda akendelea kumlea Lanlan.
Upande wa Nasra alikuwa ashajua kilichotokea na aliweza kusikia Edna alifika Dar jana usiku taarifa ambayo ilimshangaza na alijua tu lazima kuna ugomvi uliotokea.
Wakati akijiuliza nini kilichotokea aliweza kupigiwa simu na Blandina na kupewa maagizo ya kukaa na Lanlan kwa muda mpaka Roma kuweka sawa maswala yake na Edna na Nasra alichukua fursa hio kuuliza nini kinaendelea na hapo ndipo Blandina alipomwelezea kwa ufupi.
Nasra alishangaa kile kilichotokea na kujiuliza nini kinachoendelea , ijapokuwa hata yeye mwenyewe alihisi ni swala la muda tu kwa Roma na Sophia kuingia katika mahusiano lakini swala la Edna kuchagua maamuzi hayo kwasababu ya Sophia ilimshangaza mno, Alijiuliza ni kweli Edna anataka kuachana na Roma.
Nasra alijiuliza maswali mengine na kila kitu kinachoendelea hakiku mfanya kuwa na furaha hata kidogo na alikuwa na wasiwasi sana juu ya Edna.
Baada ya Lanaln kuingia ndani ya geti akiwa ameshikiliwa mkono na Roma alijikuta akipatwa na hisia mchanganyiko mara baada ya kumwangalia Roma usoni.
Alimwangalia Roma kuona kama ana tatizo maana alikuwa akijua alikuwa akimpenda sana Edna hivyo yaliotokea yangempa mawazo lakini hakuona utofauti mkubwa sana.
“Aunt Nasra , Lanlan ana njaa “Aliongea Lanlan mara baada ya kupakatwa na Nasra.
“Lanlan hujapata chakula cha mchana bado?”Aliuliza Nasra akimwangalia Lanlan , ukweli hata yeye alikuwa na hisia tofauti mara baada ya kugundua Lanlan alikuwa ni mtoto wa damu kwa Roma.
“Bado hujashiba tu wewe kibonge licha ya kula sambusa zote zile kwenye ndege , kama utakula tena sasa hivi utazidi kuwa bonge , haya nenda kalale kwanza ukiamka ndio utakula”Aliongea Roma na kisha akamsalimia Qiang Xi.
“Qian naomba ukae hapa kwa Nasra kwa muda na
Lanlan mpaka nitakapoweka mambo sawa ”Aliongea Roma na Qiang bado alionekana kuwa na wasiwasi.
“Mr Roma je haya yote ni kutokana na makosa yangu , nadhani kama ningesema mapema mambo yasingekuwa hivi”
“Usifikirie sana , haya ni maswala yangu na Edna wewe hayakuhusu , hakikisha tu unamlea Lanlan vizuri maana wewe ndio unamjua na utamwambia Nasra mahitaji ya Lanlan.”Aliongea Roma na kisha akamgekukia Nasra.
“Nasra huyu mwanamke mwenzio hapa kasema anataka kukaa kwako maana unajua kupika hivyo nitamuacha hapa”Aliongea Roma na kisha akatoa kadi ya benki na kumpatia Nasra.
“Kwenye akaunti ya hii kadi kuna zaidi ya bilioni za kitanzania wewe chukua kiasi kinachotosha kwa ajili ya matumzi ya Lanlan, lakini usimsikilize kila anachotaka , mahitaji yake nadhani yatakuwa ni ada ya kule shuleni kwao , chakula kitamu na vinywaji , hata kama mimi ni tajiri sitaki kumharibu mtoto wangu hivyo naomba usimdekeze sana”Aliongea.
“Najua chakufanya wala usajli , ijapokuwa mimi sio tajiri kama Edna lakini nitakuwa na uwezo wa kumlea Lanlan”Aliongea huku akimrudishia Roma ile kadi na kumfanya Roma kutabasamu.
“Sijasema kwamba huna hela , ni kwamba tu sijatimiza wajibu wangu kama baba tokea alipozaliwa , hivyo nataka nifanye vitu kwa hela yangu nadhani nitajisikia vizuri , naomba tusipingane kwa vitu vidogo kama hivi”Aliongea Roma.
Nasra aliweza kujua hisia za Roma kupitia maneno yake na kimya kimya aliichukua ile kadi, ijapokuwa ni kadi yenye hela nyingi lakini kama Roma alivyosema hela sio swala la kubwa sana na alishazoea hilo tokea aanze kuwa nae kwenye mahusiano.
“Kuna swala napaswa kulishuhuglia hivyo nitaondoka na ninaweza kurudi usiku “Aliongea Roma
Alikuwa hajapata taarifa zozote kutoka kwa Omari juu ya kazi aliompatia hivyo alikuwa na wasiwasi na jambo baya kumtokea Najma na hakutaka kumwambia Nasra juu ya hilo kwani aliogopa kumfanya kuwa mwenye wasiwasi kutokana na urafiki wao hivyo aliondoka mara baada ya kuona amemkabidhi Lanlan kwenye mikono salama

OFA YA CHRISTMASS IPO NICHEKI WATSAPP 0687151346

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
Nzuri kishenzi aise
 
SEHEMU YA 576.

Wote walijikuta wakiinua macho yao kumwangalia mwanamke mwenye nywele nyeusi ndefu aliefika hapo, alikuwa hajavaa kitu miguuni na sura yake haikuonekana vizuri kwa kutambulika lakini ngozi yake ilikuwa ileile alioiona Roma nchini Korea kusini.

Ni kama vile jua limekosa nguvu muda ambao aliingia katika eneo hilo , huyu mwanamke alikuwa katika hali ya ukauzu na hali ya kujivunia kama siku zote na alikuwa ni kama vile sio yeye alietumia ngao yake kuwaokoa wale majitu na Magdalena.

Kila mmoja alimwangalia kwa namna isioelezeka , haikujalisha kuna ambao walikuwa wakimchukia katika eneo hilo lakini hakukuwa na hata mmoja ambaye aliekuwa hatambui uwezo wake.

Pengine alikuwa na haki zote za kujivunia , macho yake yalikuwa ya kejeli ni kama vile alikuwa akiangalia watu wa hadhi ya chini sana na hata baada ya kuona majitu hayo yeye hakuwa na mshangao wa aina yoyote kama waliokuwa nao ndugu zake mara baada ya kuwaona kwa mara ya kwanza.

Kwa kunyoosha mkono wake tu , ile ngao yake ilimrudia kwenye mikono yake kwa namna flani hivi ya kipekee..

Ilikuwa ni ngao kubwa huenda ambayo ilikuwa ikilingana na urefu wake huku ikiwa na michoro isioweza kutambulika kwa haraka , ilikuwa ya kizamani sana.

Athena aliangalia kile chungu cha maafa kwa macho ya masikitiko , na kwa upande wa ile roho iliokuwa ndani yake ni kama vile ilijua nani wa kushindana nae na nani sio wa kushindana nae kwani palepale kilipungua ukubwa wake na kisha kikapotea..

Roma palepale mara baada ya chungu chake kupotea na yeye alipoteza fahamu na kudondoka chini na kusaidiwa na Magdalena pamoja na Rose.

“Hubby Amka , Unajisikiaje?”Rose alijitahidi kumtingisha Roma kuamka lakini hakukuwa na majibu kabisa.

Walijaribu hata kuchunguza mwili wake kwa kutumia nguvu zao za kijini lakini hakukuwa na majibu .

Nguvu zake za ndani zilikuwa kubwa mno kuliko mwanzo lakini kwa sababu zisizofahamika hakuweza kushituka hata alivyoamshwa na hata uwezo wake wa kiuungu haukuwa ukifanya kazi.

Warembo hao walikuwa katika hali ya kutojua cha kufanya , lakini licha ya hivyo hawakuwa na hofu kubwa kutokana na uwezo wao , baada ya kuona Roma alikuwa anapumua vizuri waliamua kutulia na kugeuza macho yao kwa Majitu yaliokuwa chini.

Majitu yale yalikuwa yakijitahidi kusimama lakini kwasababu ya mashambulizi ya chungu cha maafa walikuwa dhaifu mno na hata wale ambao waliweza kusimama walikuwa wakihema kama mbwa aliekimbia maili nyingi , baadhi yao hawakuwa na miguu na mikono kutokana na kunyofolewa na Cauldron.

“Hades anaendeleaje?”Aliuliza Christen .

“Sijui haamki lakini pia hajaumia popote”Aliongea Rose.

Athena alimwangalia Roma kwa sekunde na kisha akageuza macho yake kwa yale majitu kwa mwonekano wa kikauzu.

“Pumbavu zako Athena , nilijua tu ulikuwa unafanya haya makusudi, inaonekana ulijua haya yatatokea lakini kwanini ndio umekuja sasa hivi au ndio umekuja kutukejeli ?”Aliongea Hermes mara baada ya kumtupia Prince kwa Christen.

“Bado tu mpo hai?”Aliuliza kwa kejeli..

“Unamaanisha nini? Au ndio ulitaka kutuona wakituua , usisahahu kwamba huwezi kufufua moyo wa Gaia bila sisi”Aliongea Hermes kwa hasira.

“Acha kuvuka mipaka, nilishakusamehe kwa kupanga njama na yule mpuuzi , siku zote nimekuwa mtu mzuri kwako na hivi sasa huwezi kunificha kwani najua alishaamka muda mrefu tu”Aliongea

Alikuwa akimaanisha yule mwanamke aliekutana na Hermes nchini Tanzania katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Mingu mingine walijikuta wakishangazwa na kauli yake , walikuwa wakijua nini anamaanisha lakini walikosa kuamini.

“Nilijua unabii wako ni wa ukweli lakini kwanini umeshindwa kumtafuta?”Aliuliza Hermes.

“Sina haja ya kumtafuta kwani atajitokeza mwenyewe”

“Hehe , nafikiri ni kwasababu nguvu yako ya kiroho bado ipo chini mno ndio maana unashindwa kumtafuta kwasababu amekuzidi nguvu na uwezo, hii inanipa uhakika kwamba huwezi kushindana nae”Aliongea Hermes kwa majigambo.

“Sina matamanio ya kumtafuta mtu asiejiamini mimi , kama kweli sifa unazompatia zinamstahili kwanini anafanya mambo yake kwa siri na kunipangia njama?”

“Nyie watu mnaongea nini , mbona sisi hatuwaelewi?”Aliuliza Apollo.

“Hakuna kitu , hata hivyo hampaswi kuelewa”Aliongea huku akiwaangaia na muda uleule alichezesha mkono wake na ile ngao yake ikapotea .

“Niambie nini maana halisi ya Cauldron na nguvu ya roho ya mnyama iliomo ndani yake, kwanini hatujawahi kukiona?”

“Sidhani kama inahaja ya kufahamu kinatokea wapi kwani ni ngumu sana kushindana nacho mpaka Athena alipotumia ngao yake”Aliongea Ares lakini Athena hakujibu swali la Poseidon na alipaa mpaka kwenda kusimama juu zaidi usawa wa yale majitu.

“Athena wewe mwanamke ni kichaa , unapata wapi ujasiri huo ,kwanini unatokea wakati tushakuwa dhaifu , kama kweli unajiamini shindana na sisi tukiwa tushapona”Aliongea Briareus.

“Tayari nyie ni nusu wafu , mtaweza kupona vipi?”

“Acha upuuzi , hatujapoteza pambano bado , njoo kama unajiamini”Aliongea Brontes kwa hasira kali huku akijaribu kunyanyua nyundo yake lakini kutokana na kupoteza kiwango kikubwa cha damu kwenye mwili wake alishindwa kabisa kulibeba kutokana na kuwa zito kwake.

Walianza kupatwa na kiwewe mara baada ya wote kuona wanashindwa kutumia siraha zao katika hali waliokuwa nayo , hawakuamini kama wameweza kushindwa na Pluto mpya ambaye kwao alikuwa binadamu tu.

Athena aliwaangalia kwa tabasamu la kejeli na palepale alinyooosha mkono wake na mwanga wa mng’ao rangi ya Zambarau uliweza kuonekana katika kiganja chake.

“Moyo wa Gaia!!!”

Kila mmoja alijikuta akibwabwaja kwa mshangao , wale majitu na yenyewe yalijikuta yakianza kurudi nyuma kwa wasiwasi na walionyesha kilichokuwa katika mkono wa Athena walikuwa wakikifahamu na kiliwaogopesha.

“Hapana.. hapana ., haiwezekani , kwanini una moyo wa Gaia?”Aliongea Brontes huku akirudi nyuma kwa woga.

Miungu wengine walikuwa katika hali isioelezeka wakimwangalia Athena kwa shauku kwa kile anachotaka kukifanya.

Athena palepale aliachia ule moyo wa Gaia uliokuwa kwenye mikono yake na kuusukumia upande wa yale Majitu na ilikuwa kama vile ulikuwa ukijua wapi pakwenda kwani uliongeza spidi na moja kwa moja ulianza kumvamia Gyeges aliekuwa amebakia kiwiliwili na alijikuta akitoa ukulele wa maumivu.

“Noooo..!!”

Alijikuta akitoa ukulele lakini kutokana na kuwa dhaifu alishindwa kufanya chochote na alikiona kifo, wakati huo kiwingu cha mwanga wa zambarau kilimfunika mwili wake mzima kiasi cha kutoonekana na ndani ya sekunde kumi tu kulitokea mlipuko kama ule wa mafataki na kile kiwingu kikapotea na lile Jitu halikuonekana tena, ilionekana lilikuwa tayari limekwisha kumezwa.

Moyo wa Gaia ni kama vile ulikuwa na ufahamu , huenda ulikuwa ukivutiwa na damu ya Titan kwani ulianza kushambulia yale majitu mengine kwa staili ileile iliomtokea Jitu mwenzao.

Walijitahidi kutoroka lakini walishindwa kutokana na udhaifu wao, ilikuwa ni milipuko midogo kama vile mafataki iliotokea kwa zaidi ya mara sita na palepale yale majitu hayakuonekana tena na hata yale manyundo yao na yenyewe yalipotea.

Christen na Alice alijikuta wakijawa na sura za huzuni mno ni kama vile walikuwa wakiomboleza kwa kile kilichotokea , lakini wengine walikuwa katika hali ya woga kwa kile wanachokishuhudia.

“Athena nadhanni umesubiria hii siku kwa hamu sana kwa wao kujidhihirisha ili uweze kutumia damu yao ya Titan kufufua moyo wa Gaia”Aliongea Poseidon.

Muda uleule ule moyo wa Gaia ambao sasa ulikuwa umebadilika umbo lake na kuonekana kuwa hai zaidi ulirudi katika mikono ya Athena huku ukitoa toa cheche kama shoti.

“Why can’t I do this unless you want me to use one of you to activate Gaia’s heart”Aliongea akimaanisha kwamba labda kama wanataka atumie mmoja wao kuufufua moyo wa Gaia.

“Sijamaanisha hivyo , lakini kama kweli ulikuwa ukijua haya yangetokea kwanini umekuja kwa kuchelewa?”

“Sina haja ya kuelezea matendo yangu kwa mtu yoyote”

“Haha..Unakiburi cha kuchukiza sana wewe na..”Aliongea Alice akitaka kutanguliza tusi lakini alijizuia huku wengine wote walimwangalia kwa kukunja sura .

“This is over and the revival of Gaia’s heart has just begun , I’ll leave first of you have nothing else to say”

‘Hili limekwisha na ufufuo wa moyo wa Gaia umeanza , nitaondoka wa kwanza kama hamna lingine la kuongea”Aliongea Athena akipotezea maneno yao ya kejeli na hakuonyesha alikuwa na mpango wa kubakia hapo na kuendeleza maongezi.

“Simama hapo hapo?”Aliongea Rose ambaye tayari alipaa na kwenda kusimama mbele yake.

“Unataka nini?”Aliuliza kikauzu huku akikunja sura.

“Kwahio unajiona una nguvu kubwa saana hivyo kuhitaji shukrani zetu kwa kutuokoa?”Aliuliza Rose huku akimwangalia Athena kwa sura ya kejeli..

“Unajaribu kuongea nini?”Aliuliza Athena akikunja sura kwa hasira.

“Ninachomaanisha ni kwamba unaonekana ulikuwa ukijua kila kitu kitatokea leo hii , ulikuwa ukijua maelfu ya watu watakufa hapa”

“Sina muda ya kuwazia huo upumbavu”

“Upumbavu !, uko sahihi kwasababu tayari wamekwisha kufa ni upumbavu , nilishasikia habari zako kutoka kwa mpenzi wangu kwamba unafanya juu chini kuweza kulifufua kabila lako kwa miaka na miaka , ijapokuwa sikuwahi kuwaza tunaweza kukutana , lakini nilishawahi kukuwazia kwa kukuona mwanamke jasiri , mwenye nguvu , mvumilivu na mwenye imani kubwa lakini leo hii nimekuja kugundua kwamba yale niliokuwa nikiyawazia ni tofauti kabisa , Mwanamke ninaemwona hapa ni yule anaetumia ujanja ili tu kutimiza malengo yake , mwanamke mbinafsi na mnafiki ambaye anadharau maisha ya wengine kwa ajili tu ya kutimiza malengo yake”Aliongea Rose kwa hasira na kufanya kila mmoja aliekuwa hapo ndani kuwa katika hali ya mshangao na wasiwasi , hakuna ambaye alkuwa akiamini kama Rose angechukua hatua ya kumuongelesha Athena hivyo.

Athena maneno ya Rose yalionekana pia kumgusa na palepala aliachia mkandamizo wa hewa , ilikuwa ni kama vile bomu lilikuwa likitaka kulipuka.

“Labda kwako unadhani binadamu ni tofauti hivyo maisha yetu kutokuwa na thamani lakini ushawahi kufikiria unaishi katika mwili wa nani , unaishi ndani ya mwili wa binadamu pia , nani kakupa haki ya kutudharau kama tu hata wewe unategemea mwili wa biandamu kuendelea kuishi? , Roma ameishi kwa zaidi ya miaka ishirini tu , hajui ni mangapi nyie watu mmefanya katika maisha yenu hapa duniani lakini licha ya hivyo anawachukulia kama ndugu kutokana na uungu wake , alikuwa na uwezo wa kuondoka hapa ndani na kukimbia kwani kufungwa kwa anga hakukuwa kukimwathiri lakini alijitahidi kuhakikisha anafanya liwezekanalo kulinda ndugu zako , lakini vipi kuhusu wewe , ulijua kabisa ndugu zako wapo katika hatari lakini ukaamua kuja mwishoni kabisa , huku ukianza kjifanyisha ndio mwokozi wao , wewe ni nani mpaka ujione unaweza kufanya utakalo?”Rose aliongea kwa hasira huku akitokwa machozi aliamua kumtolea uvivu The Don.

Tokea mara ya kwanza kuja kufahamu kwamba The Don alikuwa ni mwanamke aliekuwa akiitwa Athena alijikuta akimkubali na kuoan huenda ni mwanamke jasiri na mvumilivu mpaka kuwa na ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa kawaida na ule wa Underwold, lakini kitendo chake cha kuja wakati ambapo maelfu ya watu wamekufa kilimkasirisha mno.

Athena alifumba macho yake kwa dakika kadhaa na kisha palepale aliachia ule mkandamizo wake wa hewa na amani ikarudi.

“Yaliopangwa kuja kutokea yatatokea na hakuna wa kubadilisha kinachokuja, waliopangiwa kufa watakufa na waliopangiwa kuishi wataishi, sihitaji kujielzea matendo yangu kwa mtu yoyote yule , sitokuua kwa sababu ya Hades lakini siku nyingine usije ukathubutu kuvuka mpaka”Baada ya kuongea hivyo alimwanagalia kama kituko na kumpita..

“Hivi unajiona unaweza kuwa Mungu kwasababu huonekani na unaogopwa? , haijalishi kama huonekani lakini bado utabakia kuwa binadamu tu milele, mchawi mkubwa wewe”Aliongea Rose lakini Athena hakujali maneno yake na palepale alipotelewa kwenye mawingu kama malaika.

Rose aliishia kutoa tu machozi huku akihema kwa hasira, mabega yake yalikuwa yakimtetemeka kwa kulia kwa kwiki huku akimsogelea Magdalena aliemshikilia Roma.

Miungu ilimwangalia kwa macho ya mshangao hawakuamini alikuwa na ujasiri wa namna hio , lakini kwa wakati mmoja kile walichoongea ni kama aliwasaidia.

Maneno ya Rose yaliwafanya kuelewa ni kwa kiasi ganni matendo ya Athena yalikuwa ya kishetani.

“Usilie tena , Hades atakuwa sawa, Athena siku zote yupo hivyo hivyo ni tabia yake na hakuna wa kumfanya lolote”Aliongea Christen akimkumbatia bega lake.

Ukweli huenda baadhi yao hawakuona kuna haja ya kufufua ndugu zao na kabila lao kwa ujumla, huenda ni kwasabbau ya hofu waliokuwa nayo kwa kile ambacho kitaitokea dunia , lakini licha ya hivyo Athena siku zote alikuwa mkubwa kwao ndio maana hawakuwa na cha kumfanya.

Hata wao pia walikuwa na hofu kubwa kwani kama Athena angeweza kufanikisha kufufua moyo wa Gaia ilimaanisha kwamba angewatawala mpaka kimawazo na angezidi kuwa na nguvu kubwa duniani na kufanya kila anachotaka.

“Tuondoke hapa tukaangalie kama kuna waliosalia karibu na hapa na ndio tufikirie namna ya kumuasha mpenzi wetu”Aliongea Magdalena na Rose alikubali na wengine wote waliondoka katika hilo eneo.

Tukio lilikuwa limekwisha kuisha , ijapokuwa sio mwisho ambao ulitarajiwa.

Baada ya kutafuta kwa madaika kadhaa , Rose na Magdalena walijikuta wakiwa na ahueni mara baada ya kugundua Sauron na wengine wote hawakuweza kuathirika kutokana na kutokuwa karibu na uwanja .

Lakini ilikuwa bahati mbaya wale wanajeshi wote walioshiriki katika mashindano wakiwakilisha kundi la The Eagles kufariki wote na hakukuwa na miili yao kutokana na kumezwa na chungu.

Baadhi ya wanasiasa wakubwa waliweza kupona na ilikuwa ni kama walikuwa wakitegemea hilo lingetokea kwani waliweza kuondoka mapema na ilikuwa ni afadhari kwani ingeleta migaongano ya kisiasa kimataifa.

Upande wa Prnce kijana kutoka Scotland wa kundi la wachawi la Siraha kwenye Jiwe aliweza kuhojiwa na alisema alishindwa kukataa kutokana na kwamba wapendwa wake walikuwa hatarini hivyo mwisho wa siku akachukua maamuzi ambayo yalipelekea vifo vya watu wengi.

Kilichofanyika mwishoni haikuwa kumua badala yake waliamua kumkabidhi kwa uongozi unaondaa mashindano hayo kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria kuchukua mkondo wake.

Roma hakuweza kurejewa na ufahamu wake kwa muda mrefu sana na ilibidi Ron awashauri wamchukue na kumpeleka Uingereza kwa Profesa Clark.

SEHEMU YA 577.

Profesa Clark aliweza kumpokea Roma akiwa Wales na kumfanyia vipimo vya awali ili kujua hali ya afya yake lakini katika hali ambayo hakuitegemea alishangaa kuona uvimbe uliokuwa katika ubongo wake ulikuwa umeongezeka ukubwa wake kwa kiwango kikubwa sana ambacho kilikuwa ni tofauti na mwanzo kabisa.

Hali ya Roma ilimfanya kuwa na wasiwasi mkubwa kiasi kwamba alijikuta hata yeye akikosa cha kufanya na ilibidi awape maelekezo Rose na Magdalena juu ya hali ya Roma na kuwaambia kwamba wanapaswa kuelekea London kwani ndio kwenye hospitali maalumu alioijenga mahsusi kwa ajili ya kumtibia Roma.

Magdalena na Rose waliweza kuona wasiwasi aliokuwa nao Clark lakini hawakubisha na kumsikiliza na kuondoka Wales na kwenda London.

Ukweli ni kwamba katika kipindi chote ambacho Clark alimsaidia Roma kimatibabu hakuwahi kumuona akiwa na hali kama hio ya kumchanganya , mwili wake ulikuwa ukifanya kazi kawaida licha ya kwamba uvimbe katika ubongo wake ulikuwa umeongezeka ukubwa, tatizo lake lilimfanya kukosa kujua namna ya moja kwa moja kumponyesha Roma kwa kumpa madawa.

Wakati Clark akiwa katika mawazo upande wa Roma alikuwa ni kama vile yupo kwenye ndoto.

Ilikuwa ni ndoto ambayo ni kame vile alikuwa mawinguni akielea huku mbele yake akiona mtu wa kufanana nae kwa kila kitu na yeye mwenyewe.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma aliekuwa ndotoni akiangalia sura ya mtu mwingine inayofanana na ya kwake.

“Mimi ni wewe?”Ile sura ya mtu mwingine ilijibu huku ikitoa tabasamu la kifedhuli.

“Wewe sio mimi lakini unatoa msisimko ambao nishawahi kuhisia hapo kabla”

“Haha.. hata mimi nishawah kuhisia msisimko unaotoa”

“Kwanini unafanana kwa kila kitu na mimi na kwanini nipo hapa?”Aliuliza Roma , ilikuwa ni kama vile nafsi mbili zilikuwa zikiongeleshana nafsi ya Roma halisi na nafsi nyingine.

Upande wa nafsi ya Roma ilikuwa na wasiwasi na kutaka kujua kinachotendelea katika ulimwengu wa kawaida juu ya hali walizokuwa nazo wapenzi wake, yaani Magdalena na Rose ,alikuwa na wasiwasi wa kutoweza kufahamu watakuwa katika hali gani wakati huo.

“Unaonekana kuwa na wasiwasi , usiwe hivyo kwasababu kila kitu nimekusaidia”

“Wewe ndio ulionisaidia kupambana na wale majitu?”

“Hapana nimejisaidia mwenyewe kwasaabu wewe ni mimi”

“Hapana wewe sio mimi , umesema umenisaidia je wewe ndio Roho ya mnyama wa maafa iliofungiwa ndani ya Cauldron?”

“Nadhani sasa unaelewa , vipi mtoto unaonaje utamu wa nguvu yangu niliokupatia?”

“Kwanini umenileta hapa?Una ufahamu wako mwenyewe?”

“Nimekuleta hapa ili kukuambia kwamba kile chungu hakiwezi kunishikilia kwa muda mrefu , walionifungia h ni wanafiki tu , wanadhani kuharibu mwili wangu ndio nini , nilizaliwa na nguvu ya maafa hivyo mimi ni wa milele na milele , imenichukua muda mwingi mpaka kuamka katika usingizi wangu lakini shukrani muda si mrefu nakwenda kuwa huru’

“Haha..”

“Unacheka nini?”Iliuliza nafsi ya mnyama wa maafa.

“Nakucheka wewe ,unasema umeishi miaka mngi lakini bado tu unapenda kujifariji”

“Mpumbavu wewe , sijafanya hivyo bali nilikuwa nikikuelezea ukweli”

“Kama kweli ulikuwa na nguvu kipindi hicho kwanini ukaishia kufungiwa kwenye Cauldron kwa miaka yote hio , labda nikuambie kitendo cha wewe kufungiwa inamaanisha huna nguvu kubwa”

“Hivi unajua kama sio mimi ungeuliwa na wale majitu wewe mpuuzi”

“Na wewe usisahau ni roho tu ambaye upo kwenye dhana yangu , mimi ndio Master wako na unafanya kazi kwangu”

“Wewe mtukutu.. unathubutu vipi?”Nafsi ya Mnyama ndani ya Caulrdon ilionekana kuwa katika hasira.

“Kwanza kwanini ukaamua kutumia sura yangu kuongea na mimi , una uharibu uso wangu wa kihandsome”Nafsi ya Roma iliendelea kujibizana na nafsi nyingine iliokuwa ndani ya mwili wake.

“Ipaokuwa sijui hapa ni wapi lakini najua kimwili sina ufahamu , naamini kuna kitu unataka kuniambia ndio maana hutaki nikirudi katika mwili wangu , hivyo niambie na usije ukaona ukinitishia unawea kuniweza kwani siogopi vitisho tokea nilivyokuwa mdogo”

“Upo sahihi lakini sio ombi wala kukutishia bali ninakwenda kukupa nafasi”

“Nafasi!!?”

“Ndio nafasi ya wewe kuwa mmiliki wa dunia yote , nafasi ya kupita vizuizi vyote vya dunia na siri zake nitakufanya usionekane lakini kwa wakati mmoja ukiogopesha , nakwenda kukupa nafasi ya kuwa zaidi ya Mungu”

“Unanisaidiaje wakati wewe mwenyewe huonekani na umezungumzia kuhusu Mungu , je unaamini Mungu yupo?”

“Kila kitu kina mwanzo na kabla ya mwanzo wetu kuna alietuanzisha ,nakuambia unakwneda kutokuonekana kama Mungu kwasababu mbinu yako ya mafunzo ya kijini unayojifunza ni ya kipekee sana na sijui nani ambaye ameitengeneza , ni mbinu ambayo sijawahi kuona hata wale majini wa zamani kuitumia na kama sio kwa mbinu yako hii nisingekusaidia lakini hata hivyo nguvu ya kiroho ya ulimwengu huu imeshuka kwa kiasi kikubwa na kuwa nyembemba tofauti na zama zile, hivyo itakuwa ngumu kwako kufikia levo ya kutawala Radi , kama utakubali kunipatia mwili wako nitakusaidia kunyonya kila aina ya nishati katika vyanzo vyote juu ya dunia kwa kupitia nafsi yangu isiokufa na nikishamaliza kufanya hivyo utakuwa na uwezo mkubwa sana na utaweza kupita levo ya kutawala Radi na kuwa mkuu zaidi, hutovuna tena nishati ya mbingu na ardhi bali wewe ndio unakwenda kuwa nishati yenyewe na ulimwengu utakuwa chini yako , utabudiwa na kile kiumbe chenye pumzi”

“Kwahio katika kuonyonya kwako hizo nishati na binadamu anahusika ,si ndio?”

“Kiumbe dhaifu ni chakula cha wenye nguvu , hivi ndivyo dunia inavyofanya kazi”

“Wewe ni shetani , siwezi kutumia binadamu wenzangu kwa ajili ya kupata nishati na kupanda levo , ndio maana ulifungiwa kwa uovu wako, ulistahili kabisa”

“Unathubutu vipi kuniongelesha hivyo?”

“Utanifanya nini sasa kama nimeongea hivyo , ni kheri niishi bila ufahamu maisha yangu yote kuliko kukupatia mwili wangu , wewe ni mtumwa tu kwangu , inashangaza kukuona unaota ndoto za mchana kutaka kumiliki mwili wangu”

“Hehe .. unakiburi sana lakini ngoja nikuambie utafikia hatua hutokuwa na chaguo kwani muda si mrefu utakuwa mgonjwa na hutoweza kutawala fikra zako na isitoshe bado huna nguvu kubwa , itafikia mahali utahitaji msaada wangu na ukiniita nikusaidie ndio wakati ambao nitauchukua mwili wako na kuua nafsi yako na kuishi milele haha..”

“Bado tu unathubutu kunitishia , labda nikuambie utabakia kuwa chini yangu na nitakutumia kufika levo za juu na baada ya hapo nitakutupa na kukufungia milele”Aliongea Roma na kufanya ile sura ya nafsi ya Chaos Cauldron imwangalie kwa dharau na kisha ikapotea kwenye macho yake.

******

Ilikuwa ni usiku wa manane ndani ya jiji la London na Roma alikuwa hajarejewa na fahamu kwa siku tatu mfululizo.

Tokea Clark amwingize Roma hapo ndani na kuanza kumfanyia matibabu alionekana kabisa kukata tamaa kwani tatizo la Roma lilikuwa la aina yake , ijapokuwa ubongo wake ulikuwa na uvimbe lakini katika vipimo vyake vya kitabibu ilionyesha ubongo wa Roma ulikuwa ukifanya kazi kwa spidi kubwa.

Clark alikuwa amechoka mno kutokana na kukosa usingizi kwa muda mrefu na pia hakuwa na mafunzo ya kijini kama Magdalena na Rose, ukweli alijitahidi kuficha hisia zake na kuvaa taaluma yake lakini licha ya kuona hakukuwa na majibu alijihisi kunyongea sana na uvumilivu ulikuwa ukielekea kumshinda.

“Clark pumzika sasa, ilimradi mwili wake upo sawa kwa sasa nadhani ataamka tu”Aliongea Rose.

“Siwezi kulala , Uvimbe wake umeongezeka ukubwa kwa kiasi kikubwa sana , sijawahi kuona akiwa katika hali kama hii nina wasiwasi na sijui kama nitaweza kupata usingizi”Aliongea na kumfanya Rose mwenyewe kuwa katika hali ya wasiwasi , haikuwa mara yake ya kwanza kumuona Roma kuwa katika hali mbaya na ndio maana alikuwa na wasiwasi.

“Ni kwa muda gani amekuwa na hii hali?”

“Sijui ni kwa muda gani lakini naweza kusema ni tokea alivyokuwa mdogo na hali yake ilikuwa mbaya zaidi kutokana na athari alizopata kutokana na majaibio ya kisayansi aliofanyiwa na Zeros, nilisomea udaktai kwa ajili ya kumsaidia lakini tofauti na kupunguza dalili nimeshindwa kumponyesha moja kwa moja”

“Kama ni hivyo je unaamini ataamka , je atapatwa na tatizo zaidi huko mbeleni?”

“Sina uhakika lakini sayansi haiwezi kuelezea hali aliokuwa nayo na kama asingejifunza mbinu za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi angekuwa katika hatari zaidi, kadri anavyopitia hili tatizo ndio anazidi kuwa katika hatari kubwa zaidi na itafikia muda atashindwa kujitawala kabisa na maumivu yake yatakuwa ni afadhali ya kifo”Aliongea na kuwafanya washindwe kabisa kuvuta pumzi kwa wasiwasi.

“Nadhani hatupaswi kuwa katika hali ya wasiwasi kwasasa na tunachopaswa kufanya ni kuamini uwezo wake”Aliongea Magdalena na Clark na Rose walitingisha vichwa vyao kukubaliana nae na kukaa kwenye sofa.

“Ah.. ulikuwa ni usingizi mzuri kweli”Waliweza kusikia sauti nyuma yao ambayo iliwafanya wageuke.

Alionekana Roma akiamka mwenyewe na kukaa kitako katika kitanda cha matibabu.

Furaha ndio kitu pekee ambacho kilionekana katika sura za warembo hao na hata Roma mwenyewe alifuurahishwa kuona hakuna hata mmoja ambaye alikuwa amepatwa na shida.

Ukweli Roma aliamka muda kidogo na alikuwa amesikia maelezo yote ya Clark juu ya shida yake hivyo hakuwa na haja ya kuuliza sana kwani kwa kauli ya Clark tu alijua fika ugonjwa wake utakuwa umeibuka upya na kuwa hatari zaidi.

Uvimbe katika ungongo wake ulikuwa ni kama kidonda cha mgonjwa mwenye ugonjwa wa kisukari ambacho kinaanza kupona na kurudia katika ukubwa wake , mpaka hapo Roma alijua kila kitu kimesababishwa na Cauldron na mawazo ya kutafuta dhana mbadala yalimwingia akilini mwake palepale , alijiambia kama ataendela kukitumia basi ni kweli itafikitia siku hatokuwa katika akili zake yeye mwenyewe na anaweza kubadilika kabisa na kuwa mtu mwingine.

Roma aliwauliza kile kilichotokea na Magalena na Rose walimwambia kila kitu kilichotokea na namna ambavyo Athena alitokea na kuwaua wale majitu wote kwa kutumia moyo wa Gaia na kuongea kauli ya ufufuo wa Moyo wa Gaia kuanza,

Roma mara baada ya kusikia kuhusu Moyo wa Gaia moyo wake ulifurukuta na hakuwa akijua ni kitu gani kinakwenda kutokea , hakujua kama Athena kweli anaweza kufanikisha kufufua ndugu zao waliolala , lakini kwa wakati mmoja alihofia athari zake kwa dunia zitakuwaje , lakini kwa wakati huo alijiambia kabisa hilo sio la kwake la kuwazia na atasubiria kuona matokeo yake ni nini, maana hata kama aseme anataka kumzuia Athena ukweli ni kwamba asingeweza kwani uwezo wake ulikuwa mdogo sana.

Baada ya maongezi ya muda mfupi Roma hakutaka kuendelea kukaa hapo , alikumbuka tokea atoke Tanzania ni zaidi ya siku sita sasa na anapaswa kurudi mapema kama alivyomwahidi mke wake kurudi mapema ndani ya wiki moja.

Hivyo baada ya Magdalena na Rose kurudi visiwa vya wafu yeye moja kwa moja aliunganisha kurudi Tanzania.

Muda ambao aliweza kufika ilikuwa tayari ni mchana wa saa sita siku ya jumapili na mara baada ya kuingia nyumbani hakuweza kuona mtu yoyote eneo la sebuleni na hali ya hewa ilionekana kuwa tulivu mno.

Alinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Edna na ile anakaribia mlangoni aliweza kusikia sauti ya Mke wake na Lanlan na ilionekaa kuna mchezo ambao walikuwa wanacheza huku Lanlan akisikika kumtuhumu mama yake kwa kuwa mdanganyifu kwani yeye ameshinda.

Tokea Edna aachane na maswala ya kampuni muda mwingi alitumia kushida na Lanlan anaporudi shuleni na pale anapokuwa shuleni alishinda na Rufi na kumfundisha baadhi ya mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kumuona baba yake na kumkimbilia kumkumbatia kwa furaha.

“Wife njoo na wewe”Aliongea Roma kwa tabasamu akimpa ishara Edna kumsogelea ili kumkumbatia na Edna alifikiria kidogo na kiabu aibu alisimama na kumsogelea Roma na kumkumbatia.

Yale mazoea ya kumuona Roma kila wakati yalimfanya siku zote saba kumkumbuka sana na kumsubiria kwa hamu kurudi kwake na mara baada ya kumuona karudi alijisikia furaha ya kutamani kuwa kama Lanlan lakini alijitahidi kujizuia.

Baada ya wote kutoka chumbani na kushuka sebuleni Roma hakuongea sana kuhusu kile kilichotokea Sicilly bali alimuuliza kilichotokea hapo wakati alipokuwa hayupo na ukweli ni kwamba hakukuwa na kubwa ambacho kilitokea zaidi ya Edna kupewa zawadi na Amina kutokana na kumsaidia kuweza kushinda zabuni kutoka serikalini na Roma alifurahi kuona Amina na Edna wana ukaribu mzuri.

***********

Ni siku mbili tokea Roma aweze kurudi, katika siku hizo aliweza kukaa karibu na Lanlan kuanza kumpima akili yake, alitumia njia mbalimbali kujaribu kumpima uwezo wake na njia moja wapo ambayo ilimridhisha sana ni njia ya kucheza nae mchezo wa Chess.

Roma alitumia masaa sita kumwelekeza Lanlan namna ya kucheza mchezo wa Chess na ajabu ni kwamba mara baada ya Lanlan kuweza kujua namna mchezo huo unavyochezwa alimletea Roma upinzani mkubwa sana.

Ilikuwa ajabu hata kwa Edna ambaye alikuwa akiangalia namna ambavyo Lanlan aliweza kuelewa kwa haraka mchezo huo na kuanza kucheza kisawa sawa mpaka kumshinda Roma.

Roma mwenyewe alijikuta akishangazwa zaidi na zaidi na uwezo wa Lanlan kwani kwa upande wake mchezo wa Chess alikuwa na uzoefu nao kwa miaka mingi sana na alikuwa akicheza sana , lakini tofauti yeye na Lanlan ni kwamba ilimchukua muda mrefu mpaka kuweza kuujua namna ya kuucheza na hata kushinda.

“Wife hakika tunabinti ana akili sana”Aliongea Roma mara baada ya Lanlan kuweza kumshinda Roma michezo mwili mfulululizo.

“Dady Lanlan kashinda , hivyo unipeleke kuona wanyama”Aliongea Lanlan kwa shangwe maana aliambiwa akishinda michezo miwili mfufluizo atapelekwa kuona wanyama.

“Lanlan baba atakupeleka kuona wanyama”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kufurahi.

“Daddy is best”Aliongea na kumfanya Roma kuchekeshwa na kibonge huyo na kumwangalia Edna ambaye alikuwa amepambwa na tabasamu.

“Tokea urudi umekuwa karibu sana na Lanlan na kama nipo sahihi ,ni kama unaupima uwezo wake wa akili , si ndio?”

“Upo sahihi na leo hii nimekamilisha uchunguzi wangu , Lanlan ana uwezo mkubwa wa akili”

“Unataka kumfundisha na yeye namna ya kuvuna nishati ya mbingu na ardhi?”Aliuliza Edna.

“Umenipata vizuri , nadhaini ni muda sahihi kumrithisha Andiko la Urejesho lisilo na kikomo”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa kidogo.

“Lakini si uliesema bado ni mdogo na hupaswi kumfundisha kutokana na hatari?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kuwaza.

Ukweli ni kwamba mwanzoni hakupanga kumfundisha Lanlan namna ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi lakini kutokana na hali yake ya kiafya kuanza kuwa tishio aliona ni muda sahihi wa kumfudisha Lanlan ili hata kama kuna jambo lolote ambalo lingemtokea mbinu hio asipotee nayo.

“Mwanzoni nilipanga iwe hivyo lakini nimegundua Lanlan ana kipaji cha juu sana na itakuwa vizuri kama nitamfudisha akiwa na umri mdogo na isitoshe kama atakuja kuelewa kanuni ya Kimaandiko ya urejeshi isio na kikomo hatochukua muda mwingi kufikia levo ya Nafsi baada ya kukamilisha hatua zote, njia hii ndefu na itategemea zaidi uelewa wake pamoja na kipaji na akifanikisha nadhani hatutakuwa na wasiwasi wa usalama wake”Edna alijikuta akitingisha kichwa kumwelewa Roma.

“Lanlan kwanzia leo baba atakufundisha namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi , si siku zote unataka kujua namna ambavyo baba anajua kupaa , unaweza kuwa kama mimi kama utafanya kile kitu nitakachokuambia”

“Really? Daddy quick teach me”Aliongea Lanlan huku akiwa ametoa macho kwa furaha.

“Kabla ya kukufundisha unatakiwa kuniahidi mimi baba yako , kwamba hutomwambia mtu yoyote mbinu yako ya mafunzo hususani kwa mtu usiemjua , umenielewa?”

“Je mama siruhusiwi kumwambia?”Aliuliza.

“Ndio hata mimi usiniambie kwasababu mama hatokuuliza hivyo usiniambie pia , usimwabie mtu yoyote”Aliongea Edna na kumfanya Roma kumwangalia mke wake kwa tabasamu akionyesha kumwelewa na Lanlan alitingisha kichwa.

Baada ya kukubaliana Edna aliaga kwenda Supermakerk kununua mahitaji ya nyumbani huku Roma yeye akimchukua Lanlan kwa ajili ya kumfudisha.

Roma alianza kumfundisha kwa kumkaririsha maneno ambayo yalikuwa kwa lugha isioeleweka na Lanlan alirudia maneno yale kwa kuyakariri na baada ya hapo Roma alimwelekeza namna ya kufanya Tahajudi huku akiongea maneno hayo kwa kuyarudia kwenda mbele na nyuma na Roma aliridhishwa na namna ambavyo Lanlan alifanikisha kukariri kwa haraka maneno yake ya kimaandiko.

Kwake alijisikia vizuri sana kumfundisha Lanlan na ilikuwa ni kama vile ilikuwa imepangwa kukutana na Lanlan na kumfundisha namna ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi kwa njia ndefu.

“Lanlan kumbuka nilichokuambia , usiharakishe mambo , mbinu ya Maandikio ya urejesho usio na kikomo inategemea zaidi uelewa wako kuliko mazoezi ya kila siku, haijalishi ni kwa namna gani umeelewa andiko lenyewe ila usijilazimishe kwa kufikiria kipi ni sahihi na kipi sio sahihi , usifikirie kuhusu kufeli na kufanikiwa, chukulia uelewa wa kila unachokiona mbele yako ni sawa bali sio sahihi ama kutokuwa sahihi?”

“Je kama Lanlan haelewi kitu , ninapaswa kukuuliza?”

“Swali zuri Lanlan , usiniulize kwasababu siwezi kukujibu ni wewe mwenyewe unaepaswa kutafuta majibu kwasababu kila mtu ana mawazo tofauti, lakini kumbuka hakuna kukata tamaa kwasababu unadhania ni ngumu kuelewa, siku zote amini kwamba maadamu bado ungali hai ni wewe pekee unayeweza kuishinda nafsi yako mwenyewe”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kutingisha kichwa na palepale katoto hako kalikunja miguu yake kwenye kitanda cha mama yake na kufumba macho kana kwamba yupo kwenye hali ya kutafakari na Roma alimwangalia kwa dakika kadhaa na kisha akatoka nje ya chumba hiko kumuacha.

SEHEMU YA 578.

Roma mara baada ya kurudi Sebuleni aliweza kukutana na Edna ambaye alikuwa akitokea jikoni na aliegamia kwenye sofa huku akimwnagalia Roma.

“Yameendaje?”Aliuliza.

Swali lake ni kama vile amemtuma mtoto wake kufanya mtihani na sasa anataka kujua mtihani uliendaje , kwa Edna kulingana na aina ya familia yake alijua kabisa maisha yao sio kama binadamu wengine hivyo Lanlan kuwa na uwezo wa kujilinda yeye mwenyewe ilikuwa muhimu.

“Dear wife , natakuwa kukujibu vipi swali lako , kwanini umeuliza kwa staili hio?”

“Nauliza kama ameelewa au imekuwa ngumu kwake kuelewa?”

“Kwasasa sijui kama ameelewa lakini amefanikisha kukariri kila kitu nilichomwambia , sikuwa na uwezo mkubwa wa akili kama yeye lakini niliweza kufika levo ya sita ndani ya miaka kumi tu, kwa kutumia vidonge ambavyo tunakwenda kumpatia haitokuwa ngumu kufikia levo ya saba maadamu kipaji chake kitakuwa kikubwa, kuhusu levo ya nane na tisa itategemea zaidi na yeye mwenyewe”

“Kwanini usimwambie kila kitu namna ambavyo ulifanikiwa na uzoefu wako kwa ujumla , si umwambie kila kitu ili iwe rahisi kwake na asiumize kichwa”Aliongea Edna.

“Uzoefu wangu …. ?,Moja wapo ya Uzoefu wangu ni kifo cha mpendwa wangu na uzoefu mwingine ni mimi kupitia hali ya kifo na uhai ,unadhani ninaweza kumfundisha uzoefu wa namna hio?”

“Unamzungumzia Seventeen?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma aone ameropoka.

“Usifikirie sana , kipindi hicho sikuwa nikikufahamu na isitoshe kila mtu ana historia ya maisha yaliopita”

“Lakini sijasema chochote , kwanini unajielezea”

“Hehe ni kweli , nilichomwambia Lanlan ni kwamba njia hii ndefu ina hatua tisa ambazo ni: Kujifikiria mwenyewe , Kufikiria wengine , Hatima , Mwisho wa safari , Kukosa swali , Giza , Nuru , Uhai na kifo na Kuzaliwa upya, kila anapopitia hatua moja ndio ugumu unavyoongezeka ,Hatima ni fumbo kubwa kwa binadamu na Giza ndio kitu kigumu kupitia, nitampa motisha kwa kila hatua atakayofikia kwa kumpatia kile nilichomwahidi, sitegemei atafikia hatua ya Nuru ndani ya miaka michache ijayo lakini natumani atakuwa mvumilivu”

“Majina ya hizo hatua ni magumu sana na unakisumbua kichwa cha Lanlan”Aliongea Edna.

“Ni sahihi, lakini hii ni mbinu ambayo ni majaribio ya kipaji cha mu kuliko kitu chochote kile , nadhani sijafanya makosa kumchagua Lanlan kama mrithi wangu na sitojihisi huzuni kumwangusha Master kwa kufanya maamuzi ya kunirithisha na mimi , angalau andioo hili halitoshia kwangu tu”

“Mbona unaongea kama vile unakufa , naamini lazima itatokea siku ukafundisha tena”Aliongea na kumfanya Roma aone kidogo tu afichue siri yake , ukweli kuhusu ugonjwa wake alipanga kutokumwambia Edna na hata Rose na Magdalena aliwaambia iwe siri kwa wakati huo kwanza.

“Nimesahau kukuambia Queen kajifungua , Omari alijnipigia simu”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.

“Mbona kama muda ni mapema sana”

“Ndio anasema mtoto kazaliwa kabla ya muda lakini anaendelea vizuri”

Roma alijikuta akimfikiria Omari , ukweli ni kwamba alijitofautisha na Omari kwa uwezo wake mkubwa wa kuweza kumkubali mwanamke ambaye tayari ana ujauzito wa mtu mwingine.

Licha ya kwamba Omari alikubali kwamba angemlea mtoto huyo kama baba lakini mwisho wa siku angebakia tu kuwa mtoto wa Yan Buwen na kitu kikubwa ni kwamba swala hilo lisingefichika kwani rangi ya mtoto huyo ingekuwa tofuati kabisa na ukoo wao na ingefika mahali mtoto angehitaji kujua kwanini yupo tofauti na wazazi wake.

Roma alijaribu kujiweka katika viatu vya Omari na alijiambia asingeweza kufanya hivyo hata kama mwanamke amempenda vipi,

Muda wa chakula cha usiku, ikiwa ni zaidi ya masaa mawili kupita hatimae Lanlan alishuka kutoka juu huku akionekana kuwa na macho yenye viashiria vya usingizi.

“Sio mbaya angalau umetumia muda mwingi , Mtoto mzuri sana wewe”Aliongea Roma akimsifia Lanlan kwa kumshika shika kichwa.

“Lanlan amefikiria kwa muda mchache lakini akakwama na alijikuta amepotelea usingizini na nimeamka sasa hivi nina njaa”Akiongea Roma na kauli yake ilimfanya kumeza maneno yake , alidhani Lanlan alikuwa akifikiria kumbe alikuwa amelala na kaamshwa na njaa lakini hata hivyo hakulaumu kwani akili ya Lanlan haijakomaa vizuri.

*****

Siku mbili zilizofuata Roma Edna na Lanlan waliondoka kwenda Iringa kama ratiba ilivyowataka kufanya hivyo.

Haikuwa safari ndefu kutokana na kutumia gari binafsi na mara baada ya kufika Iringa mjini walikuja kupokelewa na Ashley.

Roma alifurahi kumuona mrembo huyo kuwepo Iringa na ilikuwa ni kipindi kirefu kidogo hawajaonana , ukweli ni kwamba alikuwa amesahau kama Ashley alikuwa mdogo wake wa damu kabisa na wazo hilo lilimjia mara baada ya kuonana nae.

Upande wa Edna katika wiki hio ambayo Roma alikuwa nje ya nchi alikuwa ashakutana na Ashley zaidi ya mara mbili kabla ya kuanza safari ya kuja Iringa..

“Bro ninafuraha sana kwa mara ya kwanza tunakusanyika kama familia”Aliongea Ashley na kumfanya Roma kutabasamu na alifikia hatua ya kujiuliza weupe wa Ashley karithi kwa nani kwani baba yake na mama yake wote walikuwa ni weusi.

“Vipi kila kitu kipo sawa huko nyumbani?”

“Kila kitu kipo sawa lakini mama na baba wamekuwa kwenye malumbano ya hapa na pale kuhusu Denisi”Aliongea na kumfanya Roma kukunja sura kidogo.

“Denisi!!, kafanya nini mpaka kupelekea malumbano?”Aliuliza Roma huku akipotezea swali la uwepo wa baba yake nyumbani.

Ndio Raisi Senga alikuwa Iringa katika ikulu ndogo kwa ajili ya mapumziko na ilikuwa ni fursa kwake pia kuwa karibu na familia yake yote kwa mara ya kwanza , alijua hakuwa na namna zaidi ya kumkubali Roma lakini kubwa zaidi alikuwa na changamtoto binafsi ambazo aliamini kumuweka Roma karibu zingemfanya kuzitatua na hata yeye mwenyewe alikuwa akijiuliza kama anafanya yote hayo kumkubali Roma kutokana na matatizo yake au ni mapenzi yake mwenywe.

“Denisi tokea amerudi alikuwa akifanya kazi jeshini lakini licha ya hivyo kaanza tabia nyingine mpya ya kuambatana na watoto wa matajiri na kufanya starehe na anasa, ijapokuwa tabia yake haiingilianni na kazi yake lakini inamkwaza sana baba kutokana na kuhofia taswira yake kuchafuka kama raisi wa nchi lakini Mama yeye yupo upande wa Denisi akimtaka baba asimfokee na kumuacha afanye kinachompa furaha na ndio chanzo cha ugomvi wao, ijapokuwa baba yupo sahihi lakini najua wasiwasi wa mama ni nini, anaogopa Denisi kuondoka nyumbani kwa mara nyingine”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia Roma.

“Nadhani ni tabia ya kurithi hata kaka yake hapa hana tofauti”Roma mara baada ya kusikia kauli ya Edna hakupenda lakini hakuwa na haja ya kupinga kwani ilikuwa karibu na ukweli, wakati huo alikuwa bingwa wa anasa huenda zaidi hata ya Denisi anaezungumziwa,

Nusu saa mbele waliweza kufika katika makazi hayo , ilikuwa ni mara yao ya kwanza lakini kwa pande wa Lanlan ilikuwa ni mara yake ya pili na alionekana kuwa na mchecheto mno.

Roma alifurahishwa na mazingira ya uoto wa asili wa misitu , ukiachana na Songea eneo hilo lilikaa kizungu zaidi na hali yake ya hewa ya ubaridi iliridhisha na kumfanya kuona kama vile yupo Ulaya.

Baada ya kufika Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kutoka na kukimbilia ndani ya jumba hilo huku akiita jina la babu yake.

Kulikuwepo na baadhi ya watu waliokuwa wakiwasubiria nje ya nyumba hio na Afande Kweka mara baada ya kusikia jina lake linaitwa aliweka kikombe chake cha chai chini na kusimama na kumbeba Lanlan juu juu.

“Lanlan , did you mis your Great grandfather?”

“Yes but Lanlan wants to eat roast pork”Aliongea kwa furaha akimaanisha anataka kula nyama ya kitimoto na kumfanya Afande Kweka kucheka huku akishikilia vimashavu vyake kwa furaha.

Damasi mke wa raisi Senga alikuwepo na alimsogelea Lanlan na kumshika mkono.

“Lanlan unafikiria kula nyama tu umesahau kunisalimia bibi yako , nisalimie na nitahakikisha unakula kila unachotaka”Aliongea na kumfanya Lanlan palepale amsalimie.

Baada ya kuingia ndani ya jumba hilo kila mmoja aliekuwepo hapo ndani alimsalimia Roma na Edna , kulikuwa na ulinzi mkali mno kiasi cha kumfanya Roma kuamini uwepo wa baba yake hapo ndani.

“Nyie watu mmekuja mapema kesho kuna mahali mnapaswa kwenda kuniwakilisha”Aliongea Afande Kweka mara baada ya kusalimiana na Roma.

“Unamaanisha sisi wawili tu? Mbona tutakuwa wachache sana?”Aliongea Roma.

“Haijalishi ni wangapi wanaenda ila ukubwa wa mtu ndio kinachoangaliwa zaidi hata kama ukoo mzima ukienda haitalingana na nyie wawili mkienda”

“Nimependa, ni mara chache sana kunisifia wewe”Aliongea huku Edna akiwa kimya muda wote.

“Edna nimesikia umejiuzuru nafasi yako kama raisi wa kampuni?”Aliuliza Damasi.

“Ndio mama”

“Umefanya vizuri muda mwingine sisi wanawake tunapaswa kujikita kwenye maswala ya kifamilia zaidi , watoto wanakuwa kwa haraka sana na haileti maana kuwa nao mbali kimalezi, lakini pia nikwambie tu sio rahisi kuwa mama wa nyumbani”Aliongea Damasi huku kidogo akiwa na huzuni katika uso wake ni kama vile kuna kitu kinachomsumbua na hata Edna aliweza kuona hilo , huenda sababu ilikuwa ni juu ya Denisi.

“Wifi yangu sio mama wa nyumbani moja kwa moja bado ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Ernest ni kama anamsaidia tu kwani bado ana maamuzu makubwa ndani ya kampuni”Aliongea Ashley huku akiwa amemshika Edna mkono , ukichana na Edna kubadilika kuwa wifi yake lakini walikuwa ni marafiki tokea utotoni kutokana na kusoma shule moja.

“Ni vizuri pia , kampuni ni mali yake na lazima iwe hivyo, isitoshe muasisi ni bibi yake hivyo hawezi kuiuza”Aliongea.

“Upo sahihi mama lakini kwasasa sina wasiwasi kwasababu kampuni kwasasa ina mfumo wa kujiendesha ambao haunitegemei kwenye mambo mengi ndio maana nilijiamini kutoa nafasi yangu kwa Ernest”Aliongea Edna.

Ukweli kitendo cha Edna kuachia ngazi kilimfurahisha sana Blandina mama yake Roma na aliweza hata kumpigia simu na kumpa hongera kwa kufanya maamuzi sahihi lakini Edna alivyoona na Mama Ashley anampongeza kwa kitendo hicho aliona huenda kweli alikuwa bize sana na kampuni kipindi cha nyuma na maamuzi alioyafanya yalikuwa sahihi zaidi.

“Damasi chakula cha mchana bado tu sitaki mjukuu wangu kuendelea kukaa na njaa”Aliongea Afande Kweka.

“Chakula kipo tayari baba lakini Denisi mpaka muda huu hajafika tu na alisema atakuwepo muda wa chakula cha mchana”

“Kama hisia zangu ni sahihi naamini sasa hivi atakuwa amelewa huko na kahaba akiwa pembeni yake”Sauti kutoka upande wao wa kushoto iliweza kusikika na palepale alionekana Raisi Senga alievalia koti kubwa akiiingia huku akiwa ameshikilia mkasi mkononi wa kukatia miti alikuwa ameongoza na msaidizi wake ambaye alikuwa ameshikilia mfuko wa maparachichi.

“Grandpaa..!!”Lanlan aliongea na kutoka kwenye mikono ya babu yake mkubwa na kumkimbilia Raisi Senga na kumkumbatia kwa furaha na kumfanya Roma na Edna kushangaa pasipo ya kuelewa ni lini Lanlan aliweza kufahamiana na Raisi Senga maana katika kumbukumbbu zao hakuna siku ambayo Lanlan aliweza kukutana na baba yake Roma.

Raisi Senga alimbeba Lanlan juu juu kwa furaha na kisha akamgeukia Edna na Roma na kuweka uso wa tabasamu.

Muda huo huo iliingia gari aina ya Range ya rangi nyeusi na akashuka Denisi aliekuwa katika kombati za kijeshi zenye nyota moja begani na alianza kuachama kama mtu mwenye njaa kali huku akishika tumbo lake akisogelea mlango wa kuingilia na kumfanya Roma kunasa Aura yake na kukunja sura.
Hatari sana
 
Sijui kwanini natamani Edna amuache Roma mazima, kwa kweli mwanaume anamkubali kila mwanamke anaemtaka yaani hata bi Wema akimtaka nae atamwingiza kwenye list hajali kabisa hisia za mwenzie

.Hata mimi naona Roma amezidisha ujinga, yaani asingekuwa na huo Upluto jamaa angekuwa kiazi mbaya 😄

Pia naona Edna anapata msaada wa nguvu ya kimapigano either kutokana na kwamba ana damu ya ukoo wa kijini toka kwa bibi yake upande wa baba yake Jeremy au anafanya mafunzo ya siri bila mtu yeyote kujua.
 
mzimu wa seventeen unamsaidia.
 
.Hata mimi naona Roma amezidisha ujinga, yaani asingekuwa na huo Upluto jamaa angekuwa kiazi mbaya

Pia naona Edna anapata msaada wa nguvu ya kimapigano either kutokana na kwamba ana damu ya ukoo wa kijini toka kwa bibi yake upande wa baba yake Jeremy au anafanya mafunzo ya siri bila mtu yeyote kujua.
Labda kuna seventeen ndani yake
 
.Hata mimi naona Roma amezidisha ujinga, yaani asingekuwa na huo Upluto jamaa angekuwa kiazi mbaya

Pia naona Edna anapata msaada wa nguvu ya kimapigano either kutokana na kwamba ana damu ya ukoo wa kijini toka kwa bibi yake upande wa baba yake Jeremy au anafanya mafunzo ya siri bila mtu yeyote kujua.
huyo Edina kuna kiumbe kinatumia mwili wake, ndio mana akiwa na hasira sana ndipo kinaamka.....

ni kama ilivyokua kwa ile bangili,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom