HatariiiiSEHEMU YA 564.
Roma mara baada ya kuona namna ambavyo Sauroni anaongea aliona aongozane nae akaangalie nini kinaendelea.
“Inaonekana kuna jambo baya limetokea , kwasababu umekataa kuniambia hapa tuondoke nikajionee mwenyewe”Aliongea Roma na kisha akawageukia Rose na Magdalena.
“Nyie wawili mbaki hapa , haina haja ya kukutana nao kwa sasa’Aliongea Roma na hawakujali sana hata hivyo isitoshe ndani ya hoteli hio kulikuwepo na sehemu nyingi za kutembelea.
Baada ya kumfuata Ron nyuma nyuma , hatimae waliweza kuingia eneo la mapokezi katika floor ya vyumba vya VIP.
Karibia watu wote waliochini yake walikuwa washajikusanya ndani ya eneo hilo wakiwa wamesimama kwa kupanga mstari wakiwa katika mavazi ya kawaida ya suti kasoro tu Sauron alikuwa amevalia gwanda.
Jopo lote liliinamisha vichwa chini kwa ishara ya kutoa heshima lakini Roma hakujali sana.
Kwa muonekano wa Roma kwa nje na jopo hilo la watu wenye miili iliojengeka kimazoezi , hakika ilikuwa ikishangaza kwa namna yake , ni kama sasa amefika katika utawala wake rasmi.
Roma alizungusha kichwa chake na alipoangalia kwa umakini mbele yake alisimama kwa kuonyesha ishara ya mshangao.
“Clark!”Aliita.
Alikuwa ni mwanamke mrembo aliepiga magoti huku akiwa amefungwa na pingu kwenye mikono yake , akiwa amevalia koti la kitabibu kama daktari.
Lakini Clark huyo alikuwa akimwangalia Roma kwa macho yasio ya kawaida , akionyesha kabisa ishara ya dharau.
Roma palepale akili yake ilicheza na kuona kuna kitu ambacho sio cha kawaida na alimwangalia mwanamke yule kwa umakini mkubwa sana na akatingisha kichwa kupinga kauli yake.
“Hapana wewe sio Clark , licha ya kwamba unafanana nae, macho yako , muonekano wako vinakutofautisha kwa kiasi kikubwa na yeye”Aliongea Roma.
Wengine wote mara baada ya kusikia maneno ya Roma walijikuta wakivuta pumzi na kuzishusha lakini kumkubali mara moja Master wao kwa kumua Clark huyo ni feki kwa kuangalia tu.
“What is going on, Who is this?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikianza kubadilika , mpaka hapo alianza kuhisi maana ya kauli ya Ron dakika chache zilizopita.
Roma alijikuta akianza kuwaangalia kwa macho makali kila mtu aliekuwa ndani ya eneo hilo na watu wote walijikuta katika hali ya kunywea na kuwa wadogo kabisa.
Sauron aliekuwa upande wake wa kulia akiwa na gwanda zake za kijeshi alisogea mbele na kisha akapiga magoti mbele ya Roma.
“Your Majesty Pluto it’s my dereliction of duty, Princess Clark was kidnapped”
“Mfalme Pluto ni kutoweza kutimiza wajibu wangu , Princess Clark alitekwa nyara”Aliongea Sauron na palepale kauli yake ilipiga kama shoti katika mwili wa Roma na dakika hio hio alikuwa tayari ashamsogelea Sauron na kumshika na mkono mmoja kwenye Collar na kumuasha huku akimkaba kwa hasira.
“Will you come again?”Aliuongea akimaanisha arudie tena.
Makedon na wengine walikuwa na wasiwasi na walitaka kumshawishi apunguze hasira lakini Ron aliwapa ishara wasiongee chochote.
“Yes… Princess Clark , she was kidnapped”Aliongea Sauron.
“Ujinga Clark kama alikuwa Uingereza imewezakanaje akatekwa , unafanya nini nimekupatia mamlaka makubwa ya kamandi , hao wanajeshi wako siku hizi wamegeuka kuwa mapambo?”Aliongea kwa sauti nzito kabisa na kufanya chumba chote kuwa na ubaridi wa aina yake wa woga na wasiwasi wa kile ambacho kinakwenda kutokea.
Hakuna ambaye alikuwa akishangaa kwa Roma kuwa na hasira za namna hio kwasababu walikuwa wakimfahamu Clark na mama yake ni watu wa kipekee katika maisha ya Roma.
Roma wakati akiwa na miaka kumi na nne tayari ashamfahamu Clark , na katika miaka yote hio tokea wafahamiane alikuwa karibu sana na msichana huyo katika makuzi yake yote , mpaka kuja kuwa mtu mkubwa, ukiachana na yote Clark alikuwa kwa ndoto moja tu ya kuwa daktari ili kumsaidia Roma na ugonjwa wake.
Clark alikuwa ni mwanamke ambaye maisha yake yote aliishi kwa kujitengeneza kuwa na thamani ya kuhitajika na Roma na ndio maana pale tu Roma aliposema anashida mwanamke huyo angetimiza bila ya kujitaji malipo ya aina yoyote.
Kama Clark alikuwa akifanya kulipa fadhila basi angekuwa ashakamilisha fadhila hizo miaka mingi iliopita kwani amefanya mengi, ni yeye pekee ambaye alimsaidia Roma kuweza kudhibiti hali yake ya ukichaa.
Sasa watu wote waliokuwa hapo , akiwemo Edward, Ron na wengine walikuwa wakifahamu nini maana ya Clark katika maisha ya Roma.
Usalama wa Catherine mpaka leo hii upo chini ya Roma na hata baada ya yeye kuamua kurudi nchini Tanzania madaraka aliotoa kwa Sauron wajibu wake pia ni kuhakikisha usalama wa Malkia Catherine na Clark unaimarishwa.
“Ni kushindwa kutimiza wajibu wangu , watu waliomteka Princess Clark walitumia akili ya kumuweka mwingine feki ili isigundulike kama ametekwa , wakati nikiwa nataka kumleta kwenye Caesar Conference niliweza kugundua utofauti wa Clark na hapo hapo nikajua aliekuwepo ni feki, kwasababu Clark licha ya kuwa bize lakini hajawahi kusahau miadi yake na wengine”
Roma alimtupa Sauroni chini , kwa hali kama hio hata kama alikuwa ni komredi mwenzake katika jeshi asingeweza kumtendea vizuri kwa kosa ambalo amefanya.
“Kwahio huyu mwanamke ni feki umesema?”
“Ndio “Aliitikia huku akinyanyuka na kusimama kikakamavu mbele ya Roma na kisha akaendelea kuongea.
“Mfalme Pluto nimekuja kwa kuchelewa kwasababu nilikuwa sijui namna ya kulifikisha hili kwako na lingine ni kutoa maagizo kwa watu wangu kufanya utafiti wa kujua mwanamke huyu ni nani haraka iwezekanavyo, na tuliweza kugundua aliwahi kuwa shushu kutoka Urusi chini ya kundi la kigaidi lifahamikalo kwa jina la Black Widow l akini aliasi , sura yake imeweza kubadilishwa kwa kutumia mjumuisho wa Nanotechnology na 3D printing technology, teknolojia ambayo bado haijawa hadharani , ni teknolojia ya viwango vya juu sana”Aliongea Sauroni akimaanisha mtu huyo alikuwa akifanana na Clark kutokana na sura yake kutengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Nano na ya uchapishaji ya 3D(Three dimension).
“Kwahio unamaanisha bado hamjapata Clark?”Aliuliza na Sauron alitingisha kichwa kukubali .
“Mfalme Pluto , nimetuma majasusi wote wa Mossad waliochini yangu kutafuta kila kona ya dunia , kama kutakuwa na taarifa yoyote itaripotiwa kwetu kwa haraka sana”Aliongea Makedon na Roma alimpotezea na kumgeukia Edward.
“Catherine anajua kuhusu hili?”
“Shangazi yangu hajui chochote mpaka sasa , yupo bize na maandalizi ya Summer Bank holiday kwa zaidi ya wiki tatu sasa nchini Scotland na hajakutana kabisa na binamu yangu na hatujapanga kumwambia bado”Aliongea.
Katika maelezo yao ilionyesha kwamba ni zaidi ya wiki mbili tokea Clark kutekwa na haikuwezekana kugundulika kutokana na kwamba kulikuwepo na feki yake.
“Kama ni hivyo agiza vijana kuongezea ulinzi wake kwa siri ili isije ikawa analengwa na yeye pia kama ilivyomtokea kwa binti yake”Aliongea Roma na baada ya hapo alimgeukia yule mwanamke na kisha alinyoosha mkono wake bila ya kumshika na nguvu kubwa ya kijini ilitoka kwenye mikono yake na kumwinua yule mwanamke huku akiwa kama vile amekabwa shingonii bila ya kushikwa.
Huyo Clark Feki alikuwa na sura ya dharau licha ya kwamba alikuwa akiona kifo chake na hakutaka kuongea neno lolote ni kama alikuwa ashajiandaa kufa kwa muda mrefu.
“Najua kwamba wewe ni Ajenti ambaye una mafunzo ya hali ya juu na najua sana mbinu zenu za kujiua lakini pia hutoongea chochote licha ya kukutesa lakini hata hivyo sina mudi ya kupoteza muda kukutesa hivyo kama hutaki kutoa ushirikiano kwa hiari yako nitakupasua kichwa chako”Aliongea Roma na yule mwanamke alitoa tabasamu la kejeli.
“Hades wewe ni shetani , Umechokoza watu na kuamsha ghadhabu ya Mungu na muda wowote yatakufikia mabaya , kwasababu nilikuja kushiriki katika hii opereshini sijawahi kuwaza kurudi nikiwa hai , niue na nitakuwa kuzimu nikisubiria kila mmoja anaekuzunguka kuungana na mimi”Aliongea kwa kejeli kwa lugha ya kingereza.
“Naona umekiomba kifo chako mwenyewe na sina budi kukupatia”Aliongea Roma na palepale hakusita tena kwani alisukuma nguvu yote ya kijini kutoka katika mkono wake na ni sauti ya mivunjiko ya mifupa tu ilioweza kusikika na palepale kichwa chake kilipasuka kama tikiti na ubongo wote ukamwagika huku damu nyingi zikimwagika na kuchafua kapeti.
Kwa jinsi mwanamke huyo alivyopelekwa kuzimu ilikuwa ni kikatili mno kiasi kwamba watu wote hapo ndani walikunja sura na kujiambia ukatili huo ni kama vile Roma amerudi katika enzi zake akiwa kama shetani mwenye kiu ya damu.
Kipindi hicho ambacho hakujali kufanya ukatili huo mbele ya Seventeen na Clark.
Kila mmoja alikuwa na wasiwasi mno na hakuna ambaye alithubutu kuongea neno lolote la kutoa michango yao namna ya kumpata Clark.
Wakati kila mmoja akisubiria kwa hofu nini kinakwenda kutokea , palepale Roma aliirusha ile maiti ya mwanamke katika miguu ya Makedon.
“Nenda na chukua Fingerprint zake na DNA uthibitishe ni wakati gani ambao aliingia ndani ya maabara ya Clark , inaonyesha Clark alitekwa kwa muda mrefu na hamkuweza kujua kwasababu ya uwepo wa sura yake feki , pengine wanajaribu kuvuta muda wakitaka kupata tafiti zote za Clark alizogundua , nina uhakika mpaka sasa yupo hai , kwa hao watu naamini wanachokita kutoka kwa Clark ni kwa ajili ya kutengeneza siraha za maangamizi , hivyo basi kwa umakini mkubwa anzeni kutafuta katika maeneo yote ambayo yana viwanda vya kudhalisha siraha za kipekee”
Baada ya kusikia maelezo ya Roma wote waliunga mkono , ilikuwa ni kweli kama walimteka kwa ajili ya kutaka kitu chochote kutoka kwao wasingeweka mtu feki kama mbadala , lakini licha ya hivyo ilionekana walichagua muda mbaya kwani kipindi hicho ni cha Caesar Conference na Clark alikuwa ni moja wapo ya watu waliokuwa wakihudhuria kila tukio hilo linapofanyika”
Ron na wenzake waliogopa kwamba kama taarifa hio ingemfikia Roma basi asingeweza kudhibiti ukichaa wake uliokuwa ukimwendesha miaka na miaka na kuishia kuwaua , lakini ilionekana mfalme wao ameimarika tokea ajipe likizo ya kwenda Tanzania..
Makedoni aliahidi na kisha akawapa maelekezo vijana wake kusafisha na baada ya hapo aliondoka katika eneo hilo akiwa na watu wake kwa ajili ya kuanza kazi ya kumtafuta Clark , alijua kabisa kama chochote kikimtokea Clark basi halitakuwa jambo jepesi .
“We the Rothchild family are involved in the international undergound trading of all rare metals and elements , I will chek it ou and hope it helps”Aliongea Edward akitoa pendekezo kwamba familia yao ya Rothchild inahusika na biashara zote zinazohusu madini adimu na kuahidi kwamba atajaribu kuulizia huko ili kuona kama inaweza kusaidia.
“Ni bora uanzie kwa wanafunzi wa Clark wote wakubwa na kuona Projekti zao za hivi karibuni”
“Understood”
Roma mara baada ya hapo alimwangalia Sauron kwa muda huku akionekana kuwaza, Sauron uso wake ulikuwa mwekundu mno kwa wasiwasi akiwa amesimama katika eneo moja pasipo ya kusogea hata hatua moja.
“Sauron unapaswa kujiandaa , kama Clark asipoweza kurudi akiwa salama hakikisha haitokei wewe ndio wa kulaumiwa , siwezi kukuua lakini huu uwezo wako mdogo utakuandama kwa maisha yako yote mpaka unaingia kaburini”
“Mfalme Pluto wewe ndio ulifanya familia yangu mpaka sasa ipo hai , ni mwenye soni juu ya ahadi yangu kwa kufeli kumlinda Princess Clark , nipo tayari kwa hiari yangu kuwajibika , tafadhari nipe nafasi nyingine ya kurekebisha makosa yangu , nitamtafuta Profesa Clark alipo ndani ya muda mfupi sana”
“You better not Disappoint me again”Aliongea Roma akimaanisha kwamba ni kheri kama hatamwangusha tena na Sauron alipiga saluti ya kikakamavu akiahidi atafanya kila namna ya Clark kupatikana.
Baada ya pale wanajeshi wote wa kikosi cha The Eagles na viongozi wa juu wa New Zero walipiga saluti na kisha wakaondoka wakiongozwa na Sauron.
Baaada ya watu kuondoka aliekuwa amebakia ni Ron na alimsogelea Roma akionekana na maoni yake binafsi.
“Mfalme Pluto kama adui aliefanya hivyo akawa na uwezo mkubwa wa kimapigano Sauron anaweza asiweze kufanikiwa kumshinda”
‘Unafikiri sijaliona hilo?”Aliongea Roma katika hali ya urafiki.
“Hapana ,, najua mfalme Pluto hukutaka kumlaumu kila kitu Sauron ndio maana ukaamua kumuacha bila kumuadhibu”
“Najaribu tu kuwaaamsha watimize majukumu yao ipasavyo , yule mwanamke alichoongea ni sahihi nimeua watu wengi sana hivyo nimejitengenezea maadui dunia nzima wanaotaka kuinywa damu yangu ikiwa ya moto , ndugu zao , marafiki zao na hata wapenzi wao niliwaua , na sasa wanatafuta nafasi ya kutaka kulipiza kiasasi, hata kama nilishastaafu na kuacha mambo hayo kwa zaidi ya miaka mitatu , lakini hawa watu wana madoa makubwa ya damu na chuki katika mioyo yao, kuna msemo maarufu kutoka Asia usemao ‘Iwe ni kwa kuwahi au kwa kuchelewa hakuna muda sahihi wa mwanaume kulipiza kisasi’, hivyo hata kama hawatakamilisha ndani ya mwaka mmoja au miwili kwao hata ichukue miaka kumi haitakuwa tatizo mpaka siku wapate nafasi”
“Nafikiri awamu hii huyu adui anajaribu kutumia muda kwa faida kutokana na nguvu ya chuki za watu ambazo zinaelekezewa kwako ili kujificha , hatujawahi kutegemea kama ataenda moja kwa moja mpaka London na kuteka mtu nyara”
“Kuna uwezekano wa mambo ambayo hatujawahi kutegemea yakatokea hapo mbeleni.Halafu wale watu wa mavazi meupe kuna taarifa zozote mlipopata zinazowahusu?”
“Oh, Fidero tayari ashapata baadhi ya taarifa na nilikuwa nikihatiaji kukuambia”Aliongea na kisha alimpa karatasi iliokunjwa .
Roma alisoma karatasi ile kwa haraka haraka na palepale uso wake ulijikunja huku akitabasamu kifedhuli.
“Mbinu yao kujificha..”Aliongea.
Sababu ya kuongea hivyo ni kwamba , ukiachana na neno Deicide au godkiller washiriki wote wa kundi hilo hawakuandikwa kwa majina yao halisi bali ni namba tu zilizotumika kuwatambulisha kama washiriki.
Hata hivyo ulikuwa ni utaratibu wa wasimamizi wote wa Caesar conference washiriki wote kutoka makundi tofauti hawakutambulika kwa majina yao halisi.
“Wamekuja wakiwa wamejiandaa sana”Aliongea Roma huku akitoa kicheko hafifu.
“Mfalme Pluto je kuna ulazima wa kutuma mtu kuwafatilia ili kujua kila wanachokifanya? Nina wasiwasi kwamba inawezekana ndio waliohusika na kumteka Princess Clark”
“Achana na hilo , ukituma watu watakachoambulia ni majeraha tu , mimi mwenyewe nimeshindwa kugundua wanatokea wapi inamaanisha wamejiandaa kwa kila kitu , ngoja nisubiri Christen na wenzake wakiwa hapa nione ni kipi wanafahamu na maamuzi watakayo chukua”
Roma hakuona haja ya kumtafuta Clark yeye mwenyewe , na isitoshe Clark hakuwa na mafunzo yoyote ya nguvu za mbingu na ardhi huenda ingekuwa rahisi kumtafuta kwa kutumia Aura yake hivyo aliona njjia pekee ni kutulia na kusubiria taarifa kutoka kwa Makedo na Sauron.
Lakini pia hakutaka taarifa hio kumfanya kukosa raha na kuwaathiri Magdalena na Rose ambao ameambatana nao kuja hapo kufurahi.
Roma mara baada ya kurudi katika chumba alichowaacha Rose na Magdalena aliambiwa kwamba wanawake hao wametoka na kwenda Casino , taarifa hio ilimshangaza kwa kutotarajia Rose kuweza kupata sehemu ya kupoteza muda .
Kasino iliokuwepo ndani ya hoteli ya Casaano licha ya kwamba asilimia kubwa ya watu wanaocheza kamari wlaikuwa ni mabandidu wa makundi ya kimafia , lakini walitii sheria zote za kamari na hakukuwa na utapeli.
Cassino yao ilikuwa na kila aina ya michezo ya Kamari kutoka katika kila tamaduni dunia nzima na sio hivyo tu hali ya hewa ilikuwa nzuri zaidi kutokana na kwamba kulikuwa na wanawake warembo waliokuwa wakitoa huduma na kufanya wacheza kamari wasiathirike kimawazo , ni eneo ambalo lilikuwa likifanya kazi usiku na mchana bila mapumziko, wengine kucheza kamari wanachukulia kama kazi yao ya kujiingizia kipato.
Roma akiwa ameambatana na Ron waliweza kumpata Rose na Magdalena katika meza ya gemu ya karata maarufu kama Blackjack na walionekana kuweka umakini wao katika gemu..
Ni Magdalena pekee ambaye hakuwa akicheza zaidi ya kumwangalia Rose kwa wasiwasi kwani tokea aanze kucheza alikuwa amepoteza Chips(hela katika mfumo wa vipande) za kutosha mpaka zote zimeisha na bado tu hakuwa ni mwenye kukata tamaa.
Roma alijaribu kumshawihi Rose aache maana hatoshinda kwa wazungu hao wataalamu , lakini aliweka ngumu na kusema mpaka arudishe hela zake zote alizopoteza na Roma hakutaka kumlazimisha ilimradi alikuwa akichezea hela zake.
Ilibidi amchukue Magdalena aliekuwa na wasiwasi akimwambiwa wakatembee tembee nje maana Kasino haikuwa mahali pake.
Magdalena alipata ahueni mara baada ya kuambiwa waondoke hapo ndani maana alijihisi kukosa uvumilivu.
******
UNKOWN SECRET BASE.
Ni katika mojawapo ya kambi ya siri sna ambayo haijulikani ipo eneo gani katika dunia.
Ndani ya chumba kikubwa kulikuwa kumefungwa taa za mwanga mweupe ambazo ziliangaza chumba kizima na kufanya kila kitu kilichopo ndani yake kuonekana, ni chumba ambacho kilionekana kabisa kimejengwa kwa chuma kigumu , mathalani kama mahali pakufungia mateka.
Muda huo huo mlango wa chumba hicho ulifunguliwa kwa kuteleza kwenda kulia na alionekana mwanaume wa kizungu mwenye nywele za kahawia zilizojikunja kunja ambaye amevalia koti la maabara.
Ni mwanaume ambaye alikuwa na mwonekano mwembaba lakini macho yake yalikuwa ni yale yasiokuwa na utani huku akiwa ameyafinika kwa miwani ya macho.
Katika chumba hicho kulikuwa na meza pamoja na kiti pekee na katika kiti alionekana mwanamke ambaye alikuwa amevaaa koti pia la kimaabara akiwa amekalishwa huku akiwa ameinamisha kichwa chake na kufanya nywele zake ndefu zilizochanguka kumfunika na asionekane sura.
“Professor , I came to see you again”Aliongea yule mwanaume na kumfanya yule mwanamke kuamsha kichwa chake taratibu na kufanya angalau sura yake ionekane.
Alikuwa ni Profesa Clark ambaye sura yake ilionekana kupauka sana , huenda ni kutokana na hofu pamoja na kukosa kula na kiua ya maji.
“Jerry tafadhari naomba uache”Aliongea Clark huku akimwangalia yule mwanaume kwa macho ya kukata tamaa. Lakini kauli yake licha ya kwamba haikuwa ikichekesha lakini mwanaume alieitwa kwa kjina la jerry alianza kucheka mfululizo.
“Profesa ni kipi ambacho unaota mpaka sasa , yaani niache , tangu nilipokutembelea mara ya mwisho nilikuwa nikiisubiria sana hii siku halafu unaniambia vipi niache , hivi unajua kwamba sina mpango wowote wa kuacha eti”
“Jerry wewe ndio mwnafuzni wangu pekee ambaye ulionyesha uwezo mkubwa licha ya kwamba nilikuwa na hofu na uelekeo wa tafiti zako lakini bado nikakuamini na kuendelea kukufundisha mambo mengi lakini sikuwahi kuwaza unaweza kunifanyia hivi , umenihuzunisha sana”Aliongea na kumfanya kidogo Jerrey kupatwa na hatia lakini alipotezea.
“Teacher I will ask you again , what is the last sythethic element of FURY?”Aliuliza Jerry akimuuliza Clark ni element ipi ya mwisho ya utengenezai wa FURY, alionekana alikuwa na kanuni ambayo haijakamilika na ni Clark pekee ambaye alikuwa akiifahamu ndio maana alikuwa akimuuliza.
SEHEMU YA 567
Clark mara baada ya kuulizwa hilo swali alivuta pumzi nyingi na kuzishusha , mtu huyu anaefahamika kama mwanafunzi wake alikuwa ameuliza mara kibao swali la aina moja lakini hakuwa amempatia majibu anayoyataka.
“Kwanini unatamaa sana na kanuni hio, nilifikiri kama utakuja kujua nini maana ya FURY utaacha kuuliza kabisa”
“Kwanini niache , nilikufuata kwa miaka miwili yote na hatimae nimepata ninachokitaka kwanini niache”
“Jerry acha kuruhusu chuki zako kukufanya kipofu , unajua kabisa kama FURY itatengenezwa nini kitatokea , baada ya kutengeneza muundo kamili wa kimfumo miaka mitatu iliopita sikuwa na mpango wa kuendeleza zaidi , itakuwa ni dhambi kwa kizazi chote cha binadamu, ni kitu ambacho sisi wanasayansi hatupaswi kutengeneza na kama kuna mtu yoyote atajaribu kutengeneza basi ni matusi kwa binadamu wote”
“Lakini bado huu muundo kamili uliojaribu kutengeneza si bado unao , Profesa wewe ni Idol wangu , hapo zamani za kale wakati nilipokuwa chini yako nilijitahidi kusoma na kuelewa kila unachofundisha na nilichimba nikachimba haswa na kila ulichonielekeza na nikajua maana yake niliendelea kukuheshimu , kitu pekee ambacho kilikufanya kunipenda kama mwanafunzi ni kwasababu tuna tabia zinazofanana , wote sisi ni wagumu sana kupotezea gunduzi zetu licha ya uhatari wake , ijapokuwa unasema hutaki kuunda FURY lakini bado taafiti yake hujaiharibu na kuificha , hakuna uchizi kama huo sisi wote tunafanana”
“Inaonekana kila nitakachoongea hakitakufanya uache, kama ni hivyo unaweza kuondoka kwani hata kama nikifa hapa siwezi kukuambia kanuni yake”
“Profesa unadhani nitashindwa kuijua hio karuni hata kama hutoniambia , kuna mamilioni ya Elementi katika dunia hii ambazo zinaweza kukamilisha kanuni ya uwiano wa kikemikali, ninao uwezo wa kujaribu moja moja mpaka nifanikiwe, hivyo acha ubishi jaribu kutoa ushirikiano kwetu , nina uhakika kwa talanta yako wakuu wangu hawatokuacha bure, kwanini unajisumbua kufanya kazi kwa ajili ya yule shetani si kheri sisi”Aliongea na kumfanya Clark kucheka sana.
“Unacheka nini?”
“Shetani uliemtaja ni kweli kwamba ameua watu wengi na naelewa wapo watu wengi ambao wanataka kulipiza kisasi lakini nini unafanya sasa hivi , hebu fikiria je kama utafanikiwa kutengeneza FURY unadhani utaweza kumuua , hivi unajua uwezo wake ukoje kwanza?”
“Hilo sio juu yako , hata kama sitoweza kumuua nitawaua watu wake wa karibu wanaomzunguka ili nimwonyeshe nini maana ya sherehe ya kifo na uhai”
“Kwa kufanya hivyo utakuwa mkatili zaidi kuliko shetani mwenyewe, Roma yeye kaua watu wengi lakini mpango wako wewe ni kuua binadamu wote”Aliongea na kumfanya Jerry kutabasamu kwa kebehi.
“Profesa huna haja ya kuwazia usalama wa dunia , kama nitaingudua hii elementi ya mwisho kubalansi matokeo ya kikemia . utakuwa ndio mwanzo wa sisi kutengeneza New word order”
“Wewe ni mpumbavu Jerry , hivi unadhani mpaka mimi kuwa mwalimu wako naweza kulingana na wewe? , kama FURY elementi yake inaweza kupatikana kirahisi basi mimi sio Clark”Aliongea na kumfanya Jerry kushituka na kukunja sura.
“Kama usemavyo ni sahihi je hii elementi ni ya kutengeneza?”
“Upo sahihi katika dunia nzima hakuna ambaye anafahamu elementi hio zaidi yangu na haitokuja siku ukaweza kufahamu”Aliongea na kumfanya Jerry kuwa katika hali ya kujidharau , amefanya kazi kwa muda mrefu kuweza kgundua elementi hio lakini kazi yake inaonekana haikuleta mafanikio.
“Profesa kweli kuna gepu kubwa kati yako na mimi sikuwaza kwamba utakuwa na uwezo wa kufiria nje ya binadamu wa kawaida lakini haijalishi kama hutatotoa ushirikiano na kutuambia basi elewa lile kundi la watoto katika kanisa la Santa Maria hawatoliona jua la kesho”Aliongea na kumfanya Clark kumwangalia kwa macho makali.
“Wewe ni kichaa? Wale ni watoto tu wanakosa gani kwanini unataka..”
“Ninaweza kuwafanya chochote ndio , kwanza kama huwezi kuwatibia Saratani kwanini nisiwakutanishe na Mungu mapema, nakupa nafasi ya mwisho toa ushirikiano wako”Aliongea na kumfanya Ckark kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akainua kichwa chake.
“Okey , nitaongozana na wewe ili kukuonyesha inavyofanyika ..”Aliongea na kumfanya Jerry kutoa kicheko cha juu sana kwa furaha zote .
‘”Hahaha.. profesa ijapokuwa una akili kuliko mimi lakini bado wewe ni mtoto , angalia sasa umekubali, FURY , oh FURY wangu wewe. Haha”
Kicheko cha mwanaume wa kizungu kilisikika akicheka kama vile ni chizi.
******
Wakati Roma akiwa na Magdalena katika mgahawa pamheni ya hoteli wakimalizia kula chakula cha baharini , palepale alijiambia ni zaidi ya lisaa limepita tokea aachane na Sauroni na wengine lakini mpaka muda huo hakuna majibu , hivyo aliona atoe simu yake kujaribbu kumpigia Ron ili kujua nini kinaendelea.
Kabla hata hajaanza kupiga aliweza kuona kundi la watu likiwasogelea na aliekuwa akiongoza ni Sauron na walionekana na sura zilizokuwa na mwonekano wa wasiwasi pamoja na kuwa na msisimko.
“Mfalme Pluto , tumeweza kugundua kitu”Aliongea Sauron mara baada ya kungia ndani ya magahawa huo.
Ijapokuwa walikuwa wengi na ndani ya eneo hilo kulikuwa na watu , lakii kama ilivyokuwa kwa jiji hilo watu hawakushangaa sana wala kuhofia kwani Sauron alikuwa kwenye mavazi ya kijeshi.
“Umempata Clark?”
“Hakuna uelekeo maalumu wa sehemu aliopo lakini majasusi wa Mossad hivi karibuni wameweza kukusanya baadhi ya taarifa ambazo zina viashiria , Korea Kaskazini hivi majuzi wamefanya kazi na moja wapo la kundi la kigaidi kwa siri ndani ya Ulaya ya Mashariki kupitia mkondo wa kimawasiliano wa Kusini mashariki mwa Asia , ulikuwa ni ushirikiano wa majaribio ya utafiti wa siraha ya kinyuklia ambao ulianza mwaka mmoja uliopita , kama sio uhusikaji wa ghafla wa Korea kaskazini isingekuwa rahisi kuweza kupata viashiria kwa haraka”
“Korea Kaskazini , Majaribio ya nyuklia , Ulaya ya Mashariki … unajairbu kuamini kwamba ndio waliomkamata Clark ili kumalizia utafiti huo?”
“Inawezekana kabisa , tumeweza pia kugundua North Buyeo umoja wa siri uliopo nchini Korea Kusini ndio waanzilishi(instigators) wa mpango mzima , taarifa zinaonyesha wamenunua kiasi kikubwa cha madini adimu kutoka kwa Wamarekani wanaofanya biashara kimagendo pamoja na Maabara za siri na kuyaingiza Ulaya kitu kilichopelekea ushirikiano wa ghafla , na madini hayo adimu kwa maelezo ya Ashley Senga mwanafunzi wa karibu wa Profesa Clark anasema kwamba madini hayo licha ya kugundulika uuwepo wake lakini ni wanasayansi wachache sana duniani wanaojua kazi zake na namna ya kuyatumia na Profesa Clark ni mmoja wapo ,Pointi ya msingi ni kwamba tumeweza kukadiria muda kupitia Vinasaba vya damu vya yule mwanamke shushu wakati alipongia ndani ya maabara na imeonyesha ni zaidi ya wiki tatu sasa . kati ya wanafunzi ambao wapo chini ya Clark kuna anaefahamika kwa jina la Jerry , aliomba likizo wiki tatu zilizopita na hakuonekana mpaka sasa na hajulikani alipo , hivyo tunaamini huenda mipango yao imefanikiwa kwa kupitia mtu wa ndani wa karibu na Clark ambaye ni huyu Jerry”
“Hawa Buyeo wa Kaskazini …”Roma alitaka kuongea lakini alijikuta akianza kwaza kidogo , hakutaajia kwamba watu ambao waliomsumbua ndani ya Korea kusini walikuwa na mipango mikubwa zaidi , ijapokuwa hakujua ni sababu ipi ya kuwekeza katika tafiti za maswala ya nyuklia na wapi wanalenga lakini aliamini ni mpango ambao sio mdogo kabisa.
“You have said so much , then how narrow is the scope?”Anauliza kwa kusema ameongea sana lakini je ni namna ipi ameweza kufupisha utafutaji.
“Mfalme Pluto baada ya madini hayo adimu kuingia Ulaya yalitolewa katika mfumo wa kawaida wa kiusafirishaji na kuingizwa katika mfumo wa Black Market na tumeshindwa kujua uelekeo upi ni sahihi na upi sio sahihi na naogopa kama tukiendelea kutafuta kwa staili hii hatuwezi kumuokoa Princess Clark ndani ya muda”
“Kama ni hivyo kwanini upo hapa?”Aliuliza Roma akionyesha sio mwenye furaha.
“Ijapokuwa hatuwezi kutafuta uelekeo sahihi lakini tunaweza kujaribu kutafuta katika njia zote lakini hata hivyo kulingana na uelewa wako wa ramani ya ulaya pamoja na spidi yako inaweza kurahisisha kazi”Aliongea na sasa akamfanya Roma kuelewa kile ambacho Sauron anataka kumaanisha.
Ni kweli kama ataenda yeye mwenye kufuatilia basi ingekuwa rahisi zaidi kuliko watu wake na kitu kingine yeye alikuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa mambo yasiokuwa ya kawaida kwa haraka kuliko wao.
Baada ya kufikiria Clark amefungiwa kwa muda mrefu na huenda yupo katika hali ya kukata tamaa , moyo wake ulifurukuta na palepale alisimama.
“Kama ni hivyo niambie uelekeo upi nianzie kupitia simu yangu na nitafuta kila eneo moja baada ya lingine”
“Utuwie Radhi mfalme tunaona hata aibu ya kukuomba kulifanyia kazi hili mwenyewe..”
“Haina shida , umefanya sahihi kuja kwangu”Aliongea Roma na kisha alimwangalia Magdalena.
“Magdalena nisamehe nadhani sitoweza kukutembeza katika eneo nililokuwambia , tufanye siku nyingine”
“Hakuna shida , muhimu ni kuweza kumtafuta Clark kwanza , je unataka nikusaidie chochote?”Magdalena alikuwa akijua maana aliambiwa na Roma.
“Haina haja , huwezi kuelewa kwa ukubwa wake Ramani ya Ulaya ya Mashariki , unaweza kurudi hotelini kwa sasa ,Ron ataandaa utaratibu wote namna ya kushiriki katika mashindano ya Caesar Conference”
“Okey kuwa makini lakini”Aliongea Magdalena na kumfanya Roma amwangalie kwa dakika na kisha akatabasamu na kuondoka.
Sehemu ya kwanza ambayo alipaswa kwenda kutafuta ni katika kisiwa cha Gotland kwenye bahari ya Baltic.
****
Muda huo huo wakati akiondoka katika maabara sehemu ambayo amekamatwa Clark .
Alionekana Clark ambaye alikuwa amevalia Gloves mkononi na miwani maalumu ya kulinda macho huku nywele zake ambazo zilikuwa zimechanguka dakika chache zilizopita alikuwa amezifunga kwa nyuma, akiendelea kufanya majaribio ya kisayansi.
Maabara aliokuwemo ilikuwa ni kubwa , huenda zaidi ya maabatra kubwa za kitaifa ambayo inamilikiwa na shirika binafsi ambalo halijajulikana bado , ilikuwa na kila aina ya vifaa ambavyo vina teknolijia ya halli ya juu, ulikuwa ni uwekezaji mkubwa sana uliofanyika kutokana na ubora wa maabara hio.
Clark alikuwa amesimama kwenye tarakishi kubwa ya kioo iliokuwa imewekwa kwenye meza ya kupangusa kwa mikono na alikuwa akiandika kwa spidi kubwa akijaribu kutengeneza muunganiko wa kikanuni wa kemia ambao ulikuwa mgumu kueleweka hata kwa mtu ambaye ana msingi wa kawaida sana wa somo la Kemia.
Sasa katika sehemu aliosimama upande wa mbele kulikuwa na mkono wa roboti ambao ulikuwa ukifanya kila kitu unachoelekezwa kwa kutumia kanuni zinazo andikwa katika tarakishi.
Nyuma yake kulikuwa na wanaume wenye miili iliojengeka waliokuwa wamesimama , wakiwa wamevalia makoti ya maabara wakimwangalia Clark kile anachokifanya kwa shauku kubwa na kadri alivyokuwa akichapa kwa haraka katika keybord ndio walivyozidi kutoa macho yao , kwa muda huo walionekana kama walinzi lakini kwa wakati mmoja walionekana kama wanafunzi.
Kati ya wote ambao walikuwa na macho kodo ni bwana aliefahamika kwa jina la Jerry , alikuwa akiangalia na kukariri kila aina ya taarifa iliokuwa ikionekana kwenye Skrini hio kubwa , ijapokuwa taarifa hizo zilionekana kuwa nyingi na ngumu kukariri lakini alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuweza kupata msingi wake huku akipotezea baadhi ambazo hazikuwa na msingi, macho yake yalikuwa yamejaa tamaa kubwa.
“Its wonderfull.. I never thought that there would be such a way to perfom fusion reactuon .. the power fo FURY was originally constructed like this”
“Hakika inashangaza , sikuwahi kufikiria kutakuwepo na njia ya kuunganisha matokeo ya kikemia ya namna hio .. nguvu ya FURY ilitengenezwa mwanzoni kama hivi”Aliongea.
Mwonekano wa mrembo aliekuwa akiandika mlolongo wa taarifa, katika maisha yake aliwafanya wanawake wengine kumuonea wivu , hakujaliwa uzuri tu lakini pia amejaaliwa uwezo wa kuchanganua maarifa na kudhalisha maarifa mengine , ilifanya hata watu kuona wasiwasi kumsogelea na kumtongoza kwa kuona kwamba hawana hadhi ya kuwa nae.
“Profesa usingekuwa upande wa yule shetani hakika lingekuwa jambo zuri sana..”Aliongea lakini Clark alikuwa kama mtu ambaye hajamsikia kwani aliendelea na kazi yake pasipo kumzingatia na aliendelea kuchapa kwenye skrini kwa dakika kadhaa na kisha akaacha na baada ya hapo alisogea upande wa kulia mwa meza iliokuwa na baadhi ya kemikali na kuanza kuziandaa.
“Profesa unafanya nini , kwanini umeacha?”
“Itachgukua zaidi ya masaa nane mpaka kukamilisha muunganiko , kwasasa nahitaji kuthibitisha usafi wa baadhi ya elementi ambazo zinakwneda kuathiri moja kwa moja matokeo ya Elementi unayotaka”Aliongea.
Jerry alimwangalia Clark kwa macho ya shaka , ijapokuwa hata yeye amebobea katika fani ya kemia lakini alikuwa mbali sana na maarifa aliokuwa nayo Profesa wake ndio maana alikuwa katikati kwenye kuamini maneno yake au asiyaamini.
“Profesa nakushauri usije ukafanya hila ya aina yoyote , nadhani unajua nini matokeo yake”
“Haina haja ya kunikumbusha”Aliongea pasio ya kuamsha kichwa chake , wakati akiendelea na kile anachokifanya kumbukumbu za utoto wake zilimjjia akilini , alikumbuka siku ambayo alikuwa ndani ya hosteli ya kanisa katika jiji la Milan akiwa na mama yake , wakiwa kama watu wakimbizi na ghafla tu akatokea kijana mdogo alievalia nguo za kininja na kuwaokoa katika mikono ya maadui zao , mwanaume aliewaokoa siku hio ni mwanaume huyo huyo ambaye amkuwa upande wake mpaka kufikia umri huo, lakini katika hali aliokuwa nayo alikosa tumaini na kujiuliza je mwanaume huyu atakuja kumuokoa kwa wakati kama huo ambao anamhitaji sana, ili kuepusha kutoa kanuni ambayo ingekuwa na athari kubwa kwa watu wa dunia.
*******
Baada ya Roma kuondoka Ron aliweza kuja katika mgahawa na kulipia gharama za chakula Roma alichokula na Magdalena.
“Miss Magdalena , je utahitaji kuudi hotelini sasa hivi au unataka kuendelea kuzunguka zunguka , ninaweza kumuita binti yangu ili kuwa mwenyeji wako na kukutembeza tembeza”Aliongea Rona kwa lugha ya unyeyekevu.
“Asante sana Mr Ron kwa ukarimu wako , kwasasa nadhani nitarudi hotelini kuungana na mwenzangu”Aliongea Magdalena alionekana kukosa ile furaha aliokuwa nayo.
“Naelewa unajisikia vibaya mara baada ya mfalme Pluto kuondoka ghafla , ninatamani sana wewe na Miss Rose kuwa na furaha kwa Trip yenu”Aliongea.
Ni kweli Magdalena mara baada ya Roma kuondoka alihisi hisia mchanganyiko huku ile ya kukasirika ikiwa imemtawala zaidi ,katika maisha yake tokea ayafahamu mapenzi mtu wa kwanza kumpenda ni Roma, lakini mwanaume huyo licha ya kwamba anaishi nae karibu lakini kwake ni kama alikuwa umbari mrefu sana ambao anakosa kabisa namna ya kumfikia.
Siku hio alijisikia vizuri sana kutembea pembeni ya mwanaume huyo anaempenda na alijikuta akipenda kuweka hisia zake wakati wakiendelea kula chakula, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutembea na Roma ki upande upande , safari yao ya China ilikuwa ni kwa misheni maalumu lakini hapo ilikuwa ni kwa ajili ya matembezi na ndio maana kulikuwa na utofauti mkubwa , lakini sasa wakati akiwa ndio kwanza anaionja raha ya kukaa meza moja na mwanaume anaempenda wakifurahia chakula ghafla tu kunatokea dharula tena dharula yenyewe ni kwenda kutafutwa mwanamke mwingine kama mwanamke alijisikia uchungu.
“Ni sawa tu Mr Ron , siwezi kufa kwa kukosa mwanaume na isitoshe nimezoea maisha ya kuwa peke yangu”Aliongea na kumfanya Ron kushangaa.
“Hakika una hulka sawa kabisa na Malkia Persephone”Aliongea.
“Persephone !!.. unamanisha Edna?”
“Ndio japo imekuwa huzuni hayupo hapa”Aliongea
Magdalena aliona maneno ya Ron yamekaa kinyume, yamkini hawana uelewa kwamba mwanaume wanaemwita Pluto alikuwa akimuogopa sana mke wake na kumnyenyekea na asingekuwa hata na ubavu wa kumleta eneo kama hilo, hayo yalikuwa mawazo ya Magdalena.
Wakati wakiwa wanakaribia kuingia hotelini ghafla tu walisogelewa na mwanaume mzungu mwenye nywele nyeusi zilizojikunja , pamoja na macho ya bluu huku akiwa na tatoo kubwa eneo la shingoni , alikuwa akitembea kwa kuonyesha namna ambavyo anajiamini, hakuwa mbaya wa sura alikuwa na mwonekano mzuri.
Magdalena baada ya kumwangalia vizuri tu aliweza kumjua kwani sura yake alishawahi kuiona.
“Hades yuko wapi?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza mara baada ya kumsogelea Magdalena.
“Ares”Aliita Magdalena , alikuwa akimfahamu Ares kwani aliweza kumshuhudia kipindi alipokuwa akipambana na Roma katika mlima wa Oldonyo ole lengai , waliweza kumfahamu mara baada ya kufanya uchuguzi wa kuijua sura yake chini ya jeshi na yeye kama mkuu wa kitengo cha wachawi aliweza kuwa na taarifa ya sura yake licha ya kwamba uchugnuzi wao ulifanywa kuwa taarifa za siri za jeshi.
Magdalena hakushangazwa na uwepo wa Ares katika maeneo hayo kwani Roma aliongea nao na kuwaambia kwamba angeita miungu mingine kuja mpaka hapo, upande wa Ron ndio kwanza anamfahamu Ares kwani alikuwa akimsikia tu na palepale aliinama kuonyesha heshima baada ya kumfahamu.
“Mfalme Ares , Mfalme Pluto ameelekea bahari ya Baltic na ataendelea kusafiri kuzunguka baadhi ya maeno ya Ulaya kumtafuta mtu kwa zaidi ya siku mbili”
“Nini!!, kwahio unamaanisha kwamba hayupo hapa visiwani , ndio maana imenishangaza namtafuta simuoni”Aliongea huku akionyesha hali ya kutokuwa na furaha.
“Nilikuwa nikipanga angalau twend raundi moja ya mapambano, nadhani siwezi kufanya lolote”Aliongea.
Upande wa Magdalena huenda kabla ya kuingia levo ya Nafsi angemhofia Ares, lakini tokea aifikie levo hio alijihisi kabisa kuwa mkubwa juu ya binadamu wengine, moja ya athari kubwa ya nguvu za kijini ni hali ya kuwa na aina flani hivi ya ukiburi na hali hio ilimvaa Magdalena kwa wakati huo.
“Inahaja gani , ulipoteza pambano kipindi kile kule Tanzania, alikuwa na nguvu kidogo lakini kwasasa amezidi kuimarika , unafikiri unaweza kuwa mshindani wake?”
“Wewe mwanamke unajua nini , sikuwa nikipambana kwa uwezo wangu wote kipindi kile na pia nilimdharau adui yangu , kama ningejua alikuwa na mbinu zilizojificha kipindi kile ningejipanga , unaniambia ameimarika kwasasa , ngoja nikuelezee sisi tushapigana na wale viumbe wasionekana na tukawashinda licha ya levo zao kuwa za juu, unafikiri naweza kumuogopa Hades”Aliongea lakini licha ya hivyo haikumuogopesha Magdalena kwani alikuwa na taarifa zote juu ya kwamba Ares ndio aliekuwa dhaifu kuliko wote.
“Haha.. inapendeza , ni muda mrefu sana tokea mara ya mwisho tulipokutana lakini bado tabia yako ya kujikweza haijaisha tu”Sauti ya kume ilisikika nyuma yao na kuwafanya wote kugeuka
Alikuwa ni mwanaume mrefu , mzungu na ‘Handsome’ alievalia shati la mikono mirefu lenye michoto , hakuwa peke yake ameongozana na mwanamke mrembo mwenye nywele zake nyeupe., alikuwa ni Stern aliembatana na Alice ambao walifahamika kwa jina la Apollo na Artemis.
Alice mara baada ya kumwangalia Magdalena alitoa tabasamu pana na kumnyooshea mkono kumsalitimia.
“Hello beutifull wewe ni mmoja wa wanawake wa Hade pia ? Hehe naona unatoa msisimko wa nguvu za mbingu na ardhi . sio mbaya..”Aliongea
“Kuna haja gani ya kuuliza , kama sio mwanamke wa Hades ningekuwa nishamuua sasa hivi , hujui kuna sheria ya kuua binadamu na majini yote yaliofikia levo ya Nafsi yanayotuingilia katika ulimwengu wa kawaida?”Aliongea Ares.
“Acha kujigamba , swali muhimu la kujiuliza je unaweza kuniua?”Aliongea Magdalena kwa kiburi
“Unasemaje wewe?”Aliuliza Ares huku akianza kupandisha hasira zake.
Hamjui
Hapo ndipo anapokosea, wadau au wateja hawakomeshwi isipokuwa anajiharibia mwenyewe coz;singanojr anajua kuwakomesha wapenda bwereree.Hebu mlioko kwenye magroup ya whatsapp tupieni humu muendelezo!
Mbona watu mnapenda kulalamika sana? Mtu kaleta mwenyewe kwa nafasi yake, halafu tumpangie as if ni Lazima alete story humu. Kama anaandaa hsijakamilika alete tuu? Ni mali yake acha atambe nayo. Anaweza hata kuacha kuleta humu na maisha yakaenda poa tuu. Story kuishia njiani humu ni kawaida sana. Ni story nyingi na waandishi wengi hawajamalizaga story zao wakasepa.Hapo ndipo anapokosea, wadau au wateja hawakomeshwi isipokuwa anajiharibia mwenyewe coz;
1. Anaonekana he is not a man of his words(haaminiki) kwa hiyo jihadharini na mtu wa namna hii ipo siku mtalia.
2. Hajui kupanga ratiba yake.
3. Si mtu wa kujali hisia za wengine au ana majivuno na haonekani kujutia kwa mambo madogomadogo.
4. All in all mimi ndo naacha kufuatilia story yake maana lengo ilikuwa kupata burudani na si karaha. (Tafuteni mbadala).
5. Wengine hatukushindwa kununua hii story isipokuwa tulikuwa tunajiuliza je pesa yetu inakwenda kwa mtu sahihi au ndo wale wa story zisizoisha?.(Mtu aliyeng'atwa na nyoka hata akiona ung'ong'o hushituka). Bye
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ktk majukumu yako huzingatiii muda na ratiba uliyojiwekea? Au we unajiendea tu ka gari bovu.Mbona watu mnapenda kulalamika sana? Mtu kaleta mwenyewe kwa nafasi yake, halafu tumpangie as if ni Lazima alete story humu. Kama anaandaa hsijakamilika alete tuu? Ni mali yake acha atambe nayo. Anaweza hata kuacha kuleta humu na maisha yakaenda poa tuu. Story kuishia njiani humu ni kawaida sana. Ni story nyingi na waandishi wengi hawajamalizaga story zao wakasepa.
Kuna maisha mengine sawa na mimi na wewe hawa waandishi wanaishi. Yaani mtu aache kwenda kwenye vibarua vyake vya hapa na pale abaki kukuletea story humu wewe ufurahi?
Mm siachi nipo hapa hapa till the endHapo ndipo anapokosea, wadau au wateja hawakomeshwi isipokuwa anajiharibia mwenyewe coz;
1. Anaonekana he is not a man of his words(haaminiki) kwa hiyo jihadharini na mtu wa namna hii ipo siku mtalia.
2. Hajui kupanga ratiba yake.
3. Si mtu wa kujali hisia za wengine au ana majivuno na haonekani kujutia kwa mambo madogomadogo.
4. All in all mimi ndo naacha kufuatilia story yake maana lengo ilikuwa kupata burudani na si karaha. (Tafuteni mbadala).
5. Wengine hatukushindwa kununua hii story isipokuwa tulikuwa tunajiuliza je pesa yetu inakwenda kwa mtu sahihi au ndo wale wa story zisizoisha?.(Mtu aliyeng'atwa na nyoka hata akiona ung'ong'o hushituka). Bye
Sent using Jamii Forums mobile app