kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 14,147
- 16,132
Baada ya kumaliza kumshukuru Maanani Muumba Mbingu na ardhi. Nikapata kikombe cha kahawa, nikatafakari yale yangu ya siku na ratiba za hapa na pale lakini akili ikanisukuma kusikiliza kidogo music.
Katika kuchakura makabrasha mkono ukaangukia kwenye kazi ya kizazi cha kati cha muziki wa vijana wa miaka ile ya 90's, walioweka heshima na kuchonga barabara. Ambayo kizazi hiki hawaumizi kichwa wanaserereka tu.
Ghafla nikaona jina Msinitenge Profesa J, nikaona Ni kazeze wa OCG, nikakutana na kosa la marehemu uswahili ni matola nikaugusa bush party Sold ground family na homa ya dunia Solo thang na ingekuwa vipi Mwana FA.
Nikasema hizi zinatosha kuisikiliza kwa kweli nikiri kile nilichokisikia nikarudia nikagundua baki ya beat nzito na mistari.
Jamaa walikuwa ni wabunifu na waliumiza vichwa nina hakika kizazi hiki hata wakusanyane wote hawawezi kufikia ule uwezo, ni vile tu zilikuwa zama za kale za giza ila hawa wakongwe wanastahili kujengewa minara.
Nilipomaliza kusikiliza nikaingia kwenye vokswageni beatle yangu mgongo wa chura nikajikata kwenye mishe zangu!
Kweli ya kale ni dhahabu nini mnataka mazee!