Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 302
- 1,306
Simulizi hii imeandikwa na Nyemo Chilongani
0718069269
SEHEMU YA 01.
“Mume wangu kila siku unarudi usiku tu, mwisho vibaka wakuvamie wakupore hiyo simu yako,” alisema mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia dela jekundu lililokuwa na mistari ya njano kwa mbali, alikuwa akizungumza na mume wake aliyekuwa akifanya kazi ya gereji maeneo ya Kagera jijini Dar.
Mwanaume aliyekuwa akiambiwa aliitwa Masalu Mfinanga, alimwangalia mkewe huku akitabasamu kwani kwa kile kitu alichomwambia kwake hakikumuingia akilini hata kidogo.
Alijulikana na wakazi wengi wa Tandale, aliwazoea na mara kwa mara alikuwa akipiga nao stori, alikuwa rafiki wa wahuni wengi, yaani kwa kifupi hakukuwa na mtu yeyote ambaye angembabaisha kwa lolote lile.
Tabasamu lake tu likaonekana kama kuyapuuzia maneno aliyozungumza mkewe, kwamba hicho kitu kamwe kisingewezekana, kwenye maisha yake yote, alirudi nyumbani usiku kwa kuwa kama mwanaume, wakati mwingine ilikuwa ni lazima kuchelewa tu.
Kazi zake zilikuwa zikimalizika majira ya saa kumi na mbili jioni, kurudi muda huo nyumbani kwake lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo, ilikuwa ni lazima apitie kijiweni kwake hapo Kagera kucheza bao ama drafti halafu inapofika majira ya saa tatu ama nne usiku alikuwa akirudi nyumbani kwake.
Kutoka Kagera kwenda Tandale alipokuwa akiishi ilikuwa ni lazima kupita njia ya bondeni kulipoitwa Vinyasi, unapopandisha juu unakutana na shule mbili za kata zilizojengwa eneo moja, Tandale Shule ya Msingi na Hekima, sasa ili uvuke na kutokea barabarani ilikuwa ni lazima upite hapo shuleni.
Shuleni hapo kulikuwa na miti mingi mikubwa, iliyokuwa ikionekana mizuri sana nyakati za mchana lakini ilitisha mno nyakati za usiku. Wengi waliogopa kupita shuleni hapo linapoingia giza lakini hiyo haikuwa kwa mtu kama Masalu ambaye alikuwa akipita muda wowote ule aliotaka.
Mke wake aliongea sana, Masalu hakusikia, kila siku ratiba yake likuwa ni kurudi nyumbani kwake usiku hata kama alimaliza kazi mapema kabisa, ratiba ya kurudi nyumbani wala haikubadilika.
Siku zikakatika na kukatika, hatimaye siku moja baada ya kumaliza kazi zake, akaondoka na kuelekea kijiweni kwake. Kufika huko, akacheza drafti mpaka majira ya saa nne usiku, akavaa viatu vyake na kuondoka mahali hapo.
Njia yake ilikuwa ileile ya Vinyasi, akapandisha na kutokea shuleni. Sasa akaanza kupiga hatua kuelekea barabarani, hapo alikuwa akikatiza shuleni kama kawaida yake.
Alipofika karibu na mwembe mkubwa, akaanza kusikia harufu ya manukato mazuri sana ambayo hakuwahi kuyasikia tangu kuzaliwa kwake. Akafikicha pua yake, akatamani kubaki hapo kwa dakika kadhaa kwani harufu ile ilimvutia kupita kawaida.
Akaanza kuangalia huku na kule kwa kuamini labda angemuona mtu aliyejipulizia manukato hayo, hakuona mtu yeyote yule, sasa harufu hiyo ilitokea wapi? Alijiuliza bila kupata jibu.
Ghafla mbele yake akamuona mwanamke mrembo akiwa amesimama, mkono mwake alishika simu na aliiweka sikioni kama mtu aliyekuwa akiongea na mtu kutoka upande wa pili.
Hapo kukawa na mambo kadhaa yaliyokuwa yakimtatiza. La kwanza, huyo mwanamke alitokea wapi? Wakati pua zake zikiwa zimenusa harufu nzuri ya manukato, aliangalia kila upande, hakukuwa na mtu yeyote yule, akapuuzia lakini kitendo cha kupepesa macho, ghafla tu mbele yake alisimama mwanamke. Hilo lilikuwa la kwanza.
La pili alilojiuliza ni kuhusu huyo mwanamke alichokuwa akikifanya mahali hapo. Ilikuwa ni usiku, ni vigumu sana kumuona mwanamke mahali hapo, cha ajabu, huyo alikuwa hapo, alimsubiri nani? Alionekana kuongea kwa simu, alikuwa akiongea na nani?
La tatu ni baada ya kusogea karibu naye, akapigwa na mshtuko baada ya kugundua alikuwa mwanamke mrembo sana, alikuwa na urembo ambao hakudhani kama jijini Dar es Salaam angekutana na mwanamke mrembo kama huyo.
Hilo halikumshangaza sana, duniani kulikuwa na warembo wengi tu, ila kilichomchanganya ni kwa namna gani aliuona urembo wa msichana huyo?
Kumbuka ilikuwa ni usiku. Kulikuwa na giza kubwa mahali hapo. Ilikuwa ni vigumu hata kumuona mtu sura yake, ila cha ajabu kabisa, aliiona sura yake, aliionaje na wakati kulikuwa na giza.
Hapo akachanganyikiwa!
“Samahani!” alisema yule msichana.
Sasa hapo kikaibuka kitu kingine. Sauti.
Msichana huyo alikuwa na sauti ya kumtoa nyoka pangoni, nyororo fulani hivi hata kama haukuwa na pesa, ulipoisikia ikikwambia alihitaji laki moja, haraka sana ilikuwa ni lazima utafuta pesa hiyo na kumpa.
Ikambidi Masalu asimame.
“Bila samahani!”
“Nampigia simu mdogo wangu, kumbe vocha imeniishia, unaweza kunisaidia?” aliuliza huyo mwanamke.
Kwenye maswali yote aliyowahi kuyasikia akiulizwa kwenye maisha yake, Masalu akakiri swali la siku hiyo lilikuwa la kipumbavu kuliko maswali hayo yote. Eti unaweza kunisaidia? Sasa nani angekataa kumsaidia msichana mrembo kama huyo? Hata kabla ya kujibu swali hilo, harakaharaka akatoa simu na kumpa.
“Mpigie humu!”
“Nisije kukumalizia dakika zako!”
“Wewe usijali! Humo kuna dakika nyingi mpaka zinamwagika,” alimjibu huku akitabasamu.
Msichana huyo akampigia mtu aliyetaka kumpigia, alimwambia alikuwa ndugu yake, simu ikaanza kuita na baada ya sekunde kadhaa akawa anaongea na mtu huyo.
Masalu alisimama huku akimwangalia tu, kichwa chake kilikuwa kikifanya mahesabu mazito. Kwanza akakubali kwamba alipagawishwa na huyo mwanamke, alimpenda na kitu alichotaka kutoka kwake ni kuishi naye, sasa ingewezekanaje na wakati alikuwa na mke?
“Basi wahi nakusubiri huku uwanjani! Ukichelewa naondoka!” alisema msichana huyo.
Alipomaliza, akamrudishia simu Masalu. Sasa si ushatoa msaada, ondoka zako. Weee! Kwa Masalu haikuwezekana kabisa. Unatoaje msaada halafu unaondoka bila kuupambania ule msaada wako? Hapo akahitaji malipo ya msaada huo, na malipo yenyewe yalitakiwa kuwa namba ya simu.
“Amesemaje?”
“Nani?”
“Huyo ndugu yako!”
“Anakuja!”
“Ila huogopi kuwa hapa peke yako?”
“Naogopa sana! Kunatisha! Unajua hata nilipokuona unakuja huku, bado nusu nizimie! Naomba usiondoke, unipe kampani hadi atakapokuja,” alisema msichana huyo.
Aya sasa! Hebu jiulize, hata kama ungekuwa wewe ungekataa kumpa kampani mwanamke mzuri kama huyo? Yaani baada ya Masalu kuambiwa hivyo, akatamani ampigie mkewe simu na kumwambia nitarudi nyumbani asubuhi.
Kuonana naye ilikuwa ni kama bahati. Kwanza inawezekana baada ya kumuona siku hiyo, asingeweza kumuona tena. Ni kweli kama mwanaume hakutakiwa kuwa na haraka lakini kwa mwanamke wa namna hiyo, alitakiwa kukamilisha mambo yote mapema kabisa.
Alitakiwa kumuomba namba, ila napo kwanza alitakiwa kuwa na uhakika kama angepewa ama la! Kulikuwa na mademu waliojiona watoto wa mjini kumbe walikuwa washamba tu. Mtu amesaidiwa, kutoa namba ya simu anaona kama muombaji atapata mamilioni.
Sasa akajiuliza, je, huyo ndugu yake akija, hatotaka kuondoka na kumshukuru tu na kutokomea zake? Hilo nalo inawezekana kabisa lingetokea, sasa yeye kama mwanaume rijali, aliyejinasibu mwanamke hakuwa na uwezo wa kumpinga alitakiwa kumuonyesha hilo.
“Twende tukakae pale, hapa isije miguu ikaingia tumboni,” alisema Masalu.
“Sawa haina shida.”
Wakaenda na kukaa kwenye ngazi ndogo za kupandia kwenye floo ya madarasa. Sasa hapo Masalu akaanza kupiga mahesabu yake makubwa kichwani. Walikaa, kwa jinsi alivyovaa mwanamke yule, hakika alionekana kuwa mtoto wa mjini, halafu wala siyo mchoyo.
Na kama si mchoyo?
Alitakiwa kuombwa!
“Kwanza unaitwa nani?”
“Aisha!”
“Oh! Umependeza sana aisee!” alimwambia.
“Nashukuru!”
“Unanukia vizuri! Una ngozi nzuri halafu inaonekana lainiiiii...” alimwambia, hiyo kauli ilisindikizwa na mkono wake uliokwenda mpaka kwenye paja la msichana huyo, halafu Aisha alivyokuwa na makusudi, akamsogezea upaja ili ashike vizuri.
“Huku ndiyo kuokota dodo chini ya muarobaini,” alijisemea.
Sasa akaleta utawala kuanza kulitawala paja lile.
“Una haraka jamaniiiii! Yaani ndiyo kwanza tumeonana leo,” alisema msichana huyo.
“Hamna haraka jamani! Nimeipenda tu ngozi yako!
“Aya bwana! Ndugu yangu nahisi yule pale,” alisema msichana huyo, akasimama harakaharaka na kuiweka vizuri sketi yake fupi kwa kuishusha chini manake mshika mapaja aliipandisha juu kidogo, kwa mbali kulikuwa na mtu mwingine amesimama. Akaanza kumfuata.
Masalu akajilalamikisha moyoni mwake, kwa nini ndugu yake huyo alifika mahali hapo kwenye hatua kama ile. Akabaki akiwaangalia, watu hao wakaanza kuondoka.
“Eeh! Hata namba sijachukua!” alisema kwa kushtuka, akaanza kupiga hatua, hakujua nini kilichotokea, yaani kuangalia pembeni tu na kuyarudisha macho, watu hao hakuwaona.
“Wamepitia wapi?” alijiuliza.
“Itakuwa kona hii!”
”Hapana! Ama walipitia ile kule?” alijiuliza maswali mengi, akakosa jibu.
Njia zote hakuwaona watu hao, akanyong’onyea na uondoka zake kurudi nyumbani kwake. Njia nzima alikuwa akimuwaza msichana huyo mrembo, alitembea mpaka alipoimaliza shule na kuingia kwenye barabara, akaivuka na kuingia kwenye kichochoro na kuelekea kwake.
“Usiku tena!” alisema mkewe, alikuwa sebuleni akimsubiri.
“Si saa nne mama kama siku nyingine!” alimwambia.
“Saa nne? Saa yako inafanya kazi kweli?”
Hapo ikambidi Masalu aangalie saa yake, alipigwa na mshtuko baada ya kuona ilikuwa saa saba usiku. Eeeh! Ilikuwaje?
Aliondoka Kagera saa nne, kutoka hapo mpaka shuleni ni mwendo wa dakika tano tu, akakutana na yule mwanamke, akaongea naye kama kwa dakika ishirini tu na kuondoka, sasa ilikuwaje muda huo iwe saa saba? Hiyo saa saba ilifikaje?
“Imekuwaje saa saba?” aliuliza kwa mshtuko.
“Ndiyo nikuulize wewe! Kwani ulikuwa wapi?”
Wanawake bwana! Sasa alitegemea kabisa Masalu amwambi nilikuwa na demu uwanjani! Ataanzaje? Lilikuwa suala gumu.
“Kazi tu! Halafu nilipitia mpirani! Si unajua leo kulikuwa na mechi za UEFA,” alimwambia, japokuwa hakukuwa na mechi yoyote ile, alijua mwanamke hakuwa mtu wa kufuatilia mipira.
“Ngoja nikakuwekee maji uoge,” alimwambia.
Akaondoka na kuelekea huko kumuwekea maji. Masalu akaelekea chumbani, bado moyo wake uliendelea kujilaumu juu ya mwanamke yule kutokuipata namba yake. Huku akiwa na taulo, ghafla meseji ikaingia, hakujua ilitoka wapi, akaichukua simu na kuifungua.
‘Usiku mwema msamaria mwema. Aisha wa shuleni hapa!’
Masalu akapigwa na mshangao, hakuamini alichokiona kwenye simu yake. Alikuwa yule msichana wa shuleni, alimtumia meseji, namba yake aliitoa wapi? Hakumpa, na hakuwa na namba ya huyo mwanamke, cha ajabu akatumiwa meseji, na mbaya zaidi haikuja namba tupu, bali iliseviwa jina la Aisha, kwa maana hiyo aliisevu namba hiyo.
“Mmh!” akaguna.
Halafu ghafla tu harufu nzuri ya yale manukato aliyoyanusa uwanjani yakaanza kuingia ndani ya chumba hicho. Masalu akachanganyikiwa.
Je, nini kitaendelea?