Simulizi fupi: Mtoto wa miaka 8 alifanya nikajuta kuishi ugenini

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,992
Habari za asubuhi wakuu Nina story fupi ya mtoto wa miaka 8 alifanya nijute kukaa UGENINI lengo la story hii tujifunze na tukemee vitendo visivyofaa kwenye jamii ili kudhibiti matukio ya ubakaji na wazazi tujitahidi kwa malezi Bora. Asanteni

Mwaka 2018 wakati nipo chuo hapa jijini baada kumaliza semester ya Kwanza tulifunga chuo kwa ajili ya likizo baada ya kufikiria Sana sikutaka kurudi home nikapanga nikabadilishe mazingira niende kwa mama mkubwa ambaye anaishi hapahapa jijini maeneo ya kinyerezi ilibid nipige simu home kuwataarifu likizo hii sitarudi
naenda kuishi kwa mama mkubwa mama akanipa usia kidogo nikaishi vizuri ugenini na niache tabia yangu ya kuchagua chakula siunajua wa mama kiafrika maneno mengi

Baada kumaliza process zangu vizuri siku ya jumamosi nilimpigia simu mama mkubwa nakuja kumtembelea kwake alifurahi Sana alisema taarifa zangu za kuja kwake anazo mama alishampigia simu kumpa taarifa
Saa 10 jioni nilimpigia simu mama mkubwa kumpa taarifa nimefika mitaa anayoishi Mana nyumba aliokuwa anaishi nilikuwa sipajui sijawahi kufika kabla alitumwa kijana wa babaj aje kunichukua maeneo hayo

Dereva bajaji: Halo nimetumwa na mama M nije nikuchukue uko sehemu gani
Mimi: Niko hapa kwenye kwenye fremu hizi karibu na kijiwe Cha bodaboda nimevaa form six ya blue na jinsi jeusi
Dereva bajaji: nimeshakuona
Mimi: sawa

Baada ya bajaji kuja Safari ikaanza mwendo dakika 10 tukawa tumefika nje ya nyumba moja kubwa mpya haina fensi na ujenzi ulikuwa unaendelea nikapokelewa na mama mkubwa akiwa kwenye sura ya ucheshi na tabasamu nikasema kimoyoni kumbe mama mkubwa Yuko piece hivi nitaenjoy baada ya kunipokea begi langu nikapelekwadi sebuleni kwa maongezi zaidi.

Mimi: shikamoo mama mkubwa
M mkubwa: marahaba mwanangu za chuo uko
Mimi: Safi tu tunapambana
M mkubwa : mjitahidi kusoma simnaona wazazi wenu tunazeeka Sasa
Mimi: sawa mama ,
M mkubwa: kipindi kile nakuona ulikuwa kadogodogo saiz umekuwa mbaba mkubwa
Mimi: hahaha siku zinaenda mama tunakua na miaka hii inavyoenda haraka
M mkubwa: kweri baba ngoja nikuandalie chakula
Mimi: sawa mama

Baada maongezi marefu na chakula ukaja muda kuwajua niliowakuta pale.

Ngoja niwatambulishe kidogo familia na watu niliowakuta pale mama mkubwa ni mama wa watoto wa 3 wa Kwanza kiume ni mwanajeshi na wa pili kike anasoma chuo hapa jijini na 3 ni wa kiume Yuko nje ya nchi anasomea udaktari pale nyumbani anaisha na kijana mkubwa ni ndugu yetu binti wa kazi na shemeji mke wa Kaka mwanajeshi mke wa Kaka ni mtanga binti flani hivi wa miaka 28 au 30 ni mama watoto 3 wa kike mmoja na kiume wa 2 huyu wa kike ni mtoto nje sio wa kaka.

Baada kuijua familia kidogo ya bi mkubwa, tuendelee wakati tumekaa sebuleni tukiangalia tv yule mtoto kike wa shemeji alikuwa akiniangalia Sana nikapotezea siunajua ugeni nikaoneshwa chumba cha kulala nikaenda kujipumzisha.

Visanga na matukio ndo vinaanzia hapa mtoto wa Kaka wa nje wa miaka 8 ndo tatizo lenyewe

Itaendelea...

NB: Sijataja maeneo usika na nimebadirsha sehemu na kuficha baadhi ya vitu
 
Inaendelea sehemu ya 2
Jumapili majira ya saa 3 asubuhi baada ya kuamka sikumkuta mama mkubwa Wala shemeji au watoto wake(shemeji yetu na mtoto wake wa kike ni waislam bado hajafunga ndoa na Kaka ), walienda kanisani Misa ya asubuhi aliyebaki nyumbani ni binti wa kazi ni muislam na mtoto nje wa kaka tumpe jina Aisha baada ya kunywa chai nikarudi chumbani kwangu kujipumzisha Mana nje hakuna kazi yeyote ambaye nitaifanya .

Majira ya saa sita na nusu mchana Mara nasikia bajaji nje kutoka namkuta mama mkubwa na mkwe wake na wajukuu zake baada ya salaam nikapokea vitu walivyobeba nikapeleka ndani
Maisha ya pale yalienda vizuri kabisa wiki ya Kwanza ikaisha ikaja wiki ya pili nyumba nzima wakawa washanizoea hasa yule wa kike tumpe jina Aisha alikuwa muongeaji Sana afu mchangamfu labda sababu wazazi wake wote ni watanga

Kuna siku majira ya mchana nilikuwa peke angu seburani nikichek tv nilikuwa naangalia mpira marudio nimejilaza kwenye Kochi Mara nasikia sauti ya Aisha akiniita alishanizoea kuniita kaka nikamuitikia nikamwambia Niko sebuleni alivyofika ghafla akaja kwenye Kochi niliojilaza namsikiliza aseme Nini shida Mara ghafla namuona Aisha ananishikashika mwilini nikajua ni utani wa kitoto nikawa nimetulia Mara akawa anapeleka mkono wake anataka kunishika sehemu za zangu za Siri kila nikimkata mtoto anielewi anaendlea tu siku hiyo nilivaa track na jezi nikamtoa mkono wake nikamuuliza shida Nini mtoto akawa ananiangalia tu nikampiga mkwala akatulia wakati nimetulia Tena Mara aje anibusu anishikeshike nikasema hapa ugenini hii misala nikija kukutwa hapa nitaeleza Nini nikaondoka barazani nikaenda chumbani kujifikiria huyu mtoto vipi mbona anayofanya hayalingani na umri wake kwa mfano pale akinikuta shemeji si tatizo hili
Nikawa mtu wa kushinda ndani tu nikitoka Mara moja au naenda kutembea kuyaona mazingira vizuri ya mtaa Ile...

Kuna siku moja nipo na Aisha naenda dukani sikutaka anizoee Sana Kama wakati nakuja njia nzima alikuwa yey ndo muongeaji me Niko bize na simu Mara aisha akaniambia Kuna kitu NATAKA nikwambie nikamjibu eh sema unajua leo mama amepanga kwenye chakula chako aweke sumu
Ghafla nikashituka unasemaje akarudia ndo hivo mama anataka aweke sumu kwenye chakula chako
Nilistukaa mapigo ya moyo yakawa yanaenda Kasi Ina maana shemeji hapendi nikae pale mpaka atake kuniua.....???????

Itaendelea...........................
 
anyway, msaada kwa yeyote anitag pindi huyu bwana atakapoamua kupandisha sehemu inayofata.
 
Anyways kwenye kuanza kusoma hii story yako nilipofika hapa

"baada kumaliza semester ya Kwanza tulifunga chuo kwa ajiri ya..."

Nikaacha na kuacha nikaja ku-comment... kwahiyo wewe kwa kusoma kote chuo hata kutofautisha kuandika kati ya "kwa ajili na kwa ajiri" hujui?! 😳

Rest in peace! 😄😄😄😅👍🏾
 
Anyways kwenye kuanza kusoma hii story yako nilipofika hapa

"baada kumaliza semester ya Kwanza tulifunga chuo kwa ajiri ya..."

Nikaacha na kuacha nikaja ku-comment... kwahiyo wewe kwa kusoma kote chuo hata kutofautisha kuandika kati ya "kwa ajili na kwa ajiri" hujui?! 😳

Rest in peace! 😄😄😄😅👍🏾
Mkuu kikubwa umenielewa type error kweny uhandishi kawaida au we ukosei
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom