Simuelewi Mume wangu

Endelea kupenda tu na kuweka savings zako; si mumeo bwana!
Yah huyu nae kilaza kweli...wanawake wenzake wanahangaikaga pesa ziwe mikononi mwao bila kujali wanapendanaje...yeye anaweka kwa mwanaume...lol imekula kwake tena atakapojua jamaa huko mbali aliko ana kabinti kabamtoa upweke tena kwa hela za nyumba kubwa anazowekaga.....
 
Account ipo kwa jina lake tu si unajua kupenda sikuona kama ni shida na isitoshe ni mume.
Dada yetu Mautana,
Kwanza hongera kwa kupenda kwa dhati na hivyo ndivyo Mungu alivyodhamiria!.
Kwa mujibu wa maelezo yako unaonyesha wewe ndio unapenda kweli, ila umeambiwa unapendwa!.
Usikute wewe umeambiwa tuu unapendwa ila kiukweli, kinachopendwa kwako ni pesa.
Muombe mumeo bank statement uone!.
Kupenda endeleo kupenda ila kuwa mwangalifu usije kulizwa mara mbili, ukalilia penzi na kutumia pesa kulelea hilo penzi, ukaishia kupoteza penzi na pesa juu!.
 
Yani mtu kujadiliana mustakabali wa pesa unayoihangaikia anakuja juu? chukua hatua kukugombeza ni defencive mechanism yake au. au la hajali! Chukua hatua! uko mbali maelewano yalikuwa ni kitu cha msingi! ndoa inahitaji kila mtu ajali feelings za mwingine hiyosamaha ya kuomba hujakosea si suluhisho ni kukomaza tabia zilizojificha nyuma ya pazia! wanawake acheni kuendekeza ujing huu japo hata kwa baadhi ya wanaume inatokea hasa wale waliolazimisha wanawake wasio size yao! unaomba msamaha yaishe? check out mara ngapi! mana kujishusha kunaruhusiwa kwenye mahusiano but si kila wakati tena kwenye utata!
 
Kwanza pole sana sababu unaonyesha hamsikilizani vizuri na mme wako.

Pili kuna uwezekano mkubwa wewe ndo wale wanao weka pesa kwenye account, hazikai hata siku tano unataka kuzidraw.

Tatu jifunze kutunza siri zenu za nyumbani, kelele mara nyingi hazisaidiii ni akili ndo inasaidia.
 
Account ipo kwa jina lake tu si unajua kupenda sikuona kama ni shida na isitoshe ni mume.

Nenda lafuatilie balance, I guess utakuta pesa hakuna. na ulifanya ujinga sana kimapenzi kumuamini.

jitayarishe kukutana na shoki kubwa.

Pia mfatilie kama ana nyumba ndogo

mwambie muende benki mkaangalie balance na kuchukua statement, usilie sha maana nahisi kuna mambo makubwa hutayaamini yatatokea.

Mie kamwe kama sie joint account pesa zangu zitakaa acount yangu.
 
Kwanza pole sana sababu unaonyesha hamsikilizani vizuri na mme wako.

Pili kuna uwezekano mkubwa wewe ndo wale wanao weka pesa kwenye account, hazikai hata siku tano unataka kuzidraw.

Tatu jifunze kutunza siri zenu za nyumbani, kelele mara nyingi hazisaidiii ni akili ndo inasaidia.

hivi umeandika nini humu? kakuomba ushauri na tunamwambia wewe unasema aweke siri kwani tunamjua? au kasema katangazia mtaa?????
 
Very easy. Kwa kuwa upo mbali nae kwa sasa, anza Account yako binafsi. Siku ukirudi home, ndipo mtakapounganisha kila kitu.
 
Wana JF nahitaji msaada wa kimawazo kichwa kimestop kuwaza.

Nina mume wangu wa ndoa ninaye mpenda sana, na huwa naamini kuwa ananipenda zaidi shida inakuja nipo nae mbali kwa sasa ila tuliamua kufungua account itusaidie kwenye mipango yetu na nimekuwa naweka pesa huko kila mwezi cha kushangaza nikimwambia tununue kitu kwa hizo pesa ananizungusha. Pia nikimuuliza sana kuwa simuelewi anakuja juu kuwa simuamini.

Nifanyeje na sipendi malumbano inaniumaje? pesa niitafute na nisifanyie kitu cha maendeleo.

yeye anaweza kuzitoa hizo hela bila ya wewe kujua? Kama anaweza basi itakula kwako................kama hawezi bali ana kigugumizi basi mweleze ya kuwa unaanzisha mipango binafsi kwa sababu wakati ni ukuta.....
 
Hiyo itakuwa imeshanyewa biere na matumizi kwa small hausi .
 
yeye anaweza kuzitoa hizo hela bila ya wewe kujua? Kama anaweza basi itakula kwako................kama hawezi bali ana kigugumizi basi mweleze ya kuwa unaanzisha mipaRngo binafsi kwa sababu wakati ni ukuta.....

Ruta hajui kinachoendelea kwenye hiyo acc mana sio joint ni ya mume tu! namna hii ilitakiwa mtu awe hata anasema saivi tumefikia hatua hii! hataki maongezi ya hivo na wanawake tulivo wepesi kudanganyika basi hata angekudanganya! nina wasi wasi sana na kinachoendelea huko! hata kukudanganya anaogopa!
 
Hii imeniacha hoi, nimekusoma ila nauliza swali we unapotafuta hiyo pesa na kuipata kinakuwasha nini ndugu yangu kuweka katika hiyo account yenu wakati unao uwezo wa kununua kitu then ukaja weka pesa mwezi mwingine, haina maana ya kumuuliza kama ushamjua ni mlalamishi. We nenda kanunue then akikikuta kitu ndani atatulia tuu, wanaume sometime wabishi for nothing kwakweli. take care
 
this could be a source of a huge future conflict... either kubalianeni kuhusu priorities za kutekekeleza au kila mtu aweke pesa zake kivyake
 
hivi umeandika nini humu? kakuomba ushauri na tunamwambia wewe unasema aweke siri kwani tunamjua? au kasema katangazia mtaa?????
Nimeandika kiswahili wewe umeona kizungu.

Step ya kumjua au kutomjua inategemea sidhani wote waliopa hapa hawamjui, kama wewe humjui wengine wanamjua.
 
pole sana ...
  1. ni nani anayeitunza account hiyo au kutoa pesa kwenye account??
  2. je wewe una mamlaka na account hiyo(kutoa au kupata statement)?
  3. je nii tofauti ya kipato chenu?>?
  4. tangu muanze kuweka kwa pamoja je yeye alishakuthibitishia kaweka pesa??
 
kama umeolewa na mwanamme hela ziko salama, ila kama ndo vivulana, umekwisha!

kwenye hela hamna cha mme wala ndugu na wanaoathirika zaid ni wanawake mi ninao mfano hai tena kutoka kwenye familia yangu na huwa inanikera sana ila huwa sina jins ni wazazi siwezi ongea kitu kwan mimi kiujumla mama ni mtu anayejituma na anajua kutafuta hela lkn baba cku zote ndo anamualibia maendeleo yake make hata kama amenunua mazao kayaweka stoo akisafiri akija kurudi hakuti hela akiuliza ndo ugomvi mifugo ndo usiseme atamchagua ng'ombe mzuri ndo anataka kumuuza na hela hamuon anapoziweka au kitu cha maana anachofanyia ila ndo ivyo utasikia mama anasema ndoa uvumilivu wanangu
 
Kafungue account nyingine na uanze kuweka pesa huko ufanyie hayo unayotaka kufanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom