duuuuu wanaume tuna kazi unaweza lea kumbe si wako
haijawahi kunipitia, na nadhani haitakuja kunipitia. kama yeye atawaza hivyo, hayanihusu. lakini kukaribisha mtu mwingine mgeni kwa maisha yangu........... no!Imeshakupitia akilini mwako kuwa huenda baba yako mzazi hata yeye pia hajui kama wewe ni mtoto wake??
wamama wengine nuksi kweli wanaharibu amani/upendo wa watoto wao, atabaki kuwa biological father, aliyemtunza toka utoto mpka kufika hapo ndio baba yake
Usiwe mwepesi kuhukumu! Je wajua nini kilitokea hadi hilo likajitokeza? Ungekuwa wewe usingependakumjua biological father wako?
Ushauri wangu kwa huyo kijana; amuulize kwa undani mama yake what happened, pia amsikilize baba yake mlezi kama alikuwa anajua issue nzima na mwisho akamuone bio father wake! Kuna watu hawana wazazi, yeye ni priveldged coz he has 3 parents!
Hii kali, baba aliyemlea anajua kuwa si mwanae??
yaani wamama sisi jamani!!!
Mwe huyu shetani sijui atatuacha lini....wanawake na sisi sometimes.....!
Ingekuwa mimi ningetaka mchanganuo aniambie:
1. Huyo anayedai ni baba yangu alizaa naye kabla hajaolewa? (Hapo naweza kufikiria kumsamehe kirahisi)
2. Au alicheat wakati yuko na huyu baba yangu wa sasa hivi (Msamaha uatachukua muda kutoka hapo)
3. Huyu baba yangu wa sasa hivi anahiyo habari? (Kama huyo baba hana habari siendi mahali popote mpaka kieleweke)
Pole mwaya.
Duh, mpe pole. Kitu chana kwanza ningemshauri awakutanishe wote watatu ili mambo yote yawe wazi kwanza. Then uamuzi wake binafsi utakuja tuu baada ya hili.
Usimsingizie shetani wa watu.
Jiamini - ingawa watu wengi wanamlaumu Mama mara Bailogiko Father sijui nini - lakini hawajui mazingira yaliyosababisha hali kuwa kama hiyo.
Mfano inawezekana kabisa kuwa Baba wa kufikia alimuoa Mama yako huku akijua kuwa ni mja mzito kwa mimba ambaye siyo yake na walikubaliana.
Pili, inawezekana kuwa Baiologiko father alikuwa anampenda sana mama mzazi na hata alitaka kulea mimba ya mtoto wake lakini kukatokea matatizo mengi sana katika familia au kati yake ya huyo mama mpaka mama akaamua kumsingizia baba mwingine! - mm sijui
Tatu, inawezekana kuwa mama alifahamu ila hakumuambia baiologiko father! - mimi sijui
Ila ninachokifahamu - from my personal experience ni kuwa kuna dada mmoja jirani yangu alishawahi kupata ujauzito alafu mwisho wa siku walikuja watu (wanaume) watatu! - kila mmoja anadai kuwa ni mimba ni ya kwake! - tukamuuliza yule dada akasema hajui ujauzito ni wa nani! - baada ya mtoto kuzaliwa na kufanyiwa DNA - ikajulikana kuwa mtoto siyo wa yeyote kati ya wale watatu ila ni wa mtu mwingine kabisa ambae wala hata hana interest na mtoto huyo!
So maisha tunayoishi is very complicated!
Usimlaumu Baiologiko father wala pia usimlaumu baba alie nae ... maana hujui ni kitu gani kilitokea kati yao! - I mean your Mother, your Father & your Baiologiko Father
My advice ... go see him (Baiologiko father) maana hujui kimetokea nini - na unaweza kuta kumbe hata Baba uliekuwa nae nae anafahamu!...
Life .... is very complex my friend!
Mimi ni kijana niliyehitimu kidato cha sita na kuchaguliwa kuingia chuo fulani kikuu huko Dom mwaka jana. Nimelelewa kwa mapenzi makubwa ya baba na mama ambyo yamenifanya niwe na mafanikio sana ya kishule na maisha kwa ujumla. Baba yangu amkuwa na rafiki wangu wa karibu sana na mara kwa mara huwa tunashauriana mambo mengi .
Wiki iliyopita mama alikuja kunitembelea na akaomba jmosi twende Dar. Nilipomuuliza kulikoni kwenda dar akasema eti anataka kunionyesha baba yangu, huyu aliyenilea na kunitunza kwa mapenzi makubwa mpaka leo si baba yangu mzazi! Nimepigwa na butwaa mpaka muda huu.
Naomba ushauri nifanyaje ndugu zangu? Akili inanizunguka.
***** Hii ni email niliyopokea toka maeneo ya Dodoma Kijana akiomba ushauri wa haraka juu ya hayo aliyoeleza*****
Usimsingizie shetani wa watu.