Miezi minne tu unataka umuelewe binti na uoe? Jipe muda ndugu yangu. JIPE MUDA USIJE KULIA TATA!Wakuu habarini napoleni pia na mahangaiko ya kujitafutia ridhiki.
Naombeni ushauri maana simuelewi huyu mchumba wangu.
Nilikutana na huyu binti miez 4 iliyopita na wakati nakutana nae nilimpenda sana basi nikazungumza nae tukakubaliana kwa sharti moja tukapime afya zetu kwanza.
Tukapima na wote tupo safi, baada ya muda nilimhitaji tukutane kimwili aliniambia kufanya hvyo kabla ya ndoa ni dhambi kubwa hvyo kama nampenda nimuoe maana yeye yupo tayari nimuoe hata saa hizi kuliko kuzini.
Basi kwa vile nampenda sikua na namna ya kukataa matakwa yake, nilivyomuambia nipo tayari kufata taratibu za kulipa mahari yeye akaja niambia hayupo tayari kuolewa sahz hvyo kama nampenda basi nimsubiri adi mwaka keshokutwa 2024ndipo nimuoe.
Kumuuliza kwann ananiambia hvyo wakati alishaniambia nimuoe hata sasa anasema yy kaamua tu aolewe 2024 ana mipango yake anataka aitimize kwanza, kumuuliza ni mipango gani hyo hasemi anasema kaamua tu, je ananipenda kweli huyo?
Maana SIMUELEWI hanichuni wala nn nikikwama ananisaidia na ushauri mzuri ananipa shida hapo Nahitaj kula tunda hataki ad nimuoe na process ya kumuoa yenyewe anaipigapiga kalenda... Nisaidien mawazo wakuu