Kisa kazi, mchumba wangu amenisaliti

JambaziSugu

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
245
203
Poleni na majumukumu.

Mimi ni kijana wa miaka 29. Miaka kadhaa yuma nilipata nafasi ya kwenda kusoma nchi fulani. Huko nikakutana na binti mmoja tukaanzisha mahusiano.

Binti huyu ni yeye ndiye aliyenitafuta na kuonesha kuvutiwa na mimi. Hakuwa mrembo, ila alionekana ni mwenye imani ya dini sana na mpole. Wakati huo mimi nilikuwa playboy sina muda wala sikuwa in a relationship.

Siku tuliyokutana, mwaka 2014 nilimtembelea rafiki yangu katika mji mwingine wa nchi hiyo ndipo rafiki yangu akanitambulisha kwake. Alionekana kunichangamkia, uso wake ulijaa tabasamu alipoongea nami. Akamuaomba rafiki yangu aniachie namba yake ili tuwe tunawasiliana. Nilifanya hivyo, siku nasafiri kurudi kwangu, nikamtext kumuaga alifurahi akasave namba yangu.

Baada ya kufika kwangu, siku kadhaa mbeleni akaanza kunitafuta, akawa anaipigia simu hadi usiku, analazimisha tuongee masaa mengi, mm sikuwa mtu wa kuongea na simu masaa mengi. Basi ikaenda hivyo, ikafika siku akaniomba tuonane. Alitaka kunitumia nauli ya ndege nisafiri tuonane. Kutokana na ratiba zangu haikuwezekana. Zikapita siku, wiki, akaniambia anakuja kwenye mji wetu.

Kipindi hiko, mimi sikuwa na mpango nae, maana niliona kama hatuendani kwa sababu mimi nilikuwa bishoo tu, na yeye alionekana mtu mwenye kujiheshimu na aliyeshika imani ya dini. Rafiki zangu, wakawa wananishawishi kuwa huyu mwanamke anakutaka, amefunga safari kwa ajili yako, malizana nae. Ukimuacha arudi kwao hivihivi utakuwa umekosea. Basi ikabidi tutoke dinner na mambo mengine yakaendelea. Hapo ndo ulikuwa mwanzo wa mahusiano yetu.

Kusema ukweli wa Mungu sikuwahi kupendwa before, kwa namna alivyonipenda huyu mwanamke. Alijitoa sana kwangu. Kila mtu alifahamu ni namna gani alinipenda. Mwanzo sikuwa na hisia nae lakini kutokana na upendo alionionesha, nikaona huruma kumuumiza. Ikabidi niachane na michepuko yote niingie kwenye serious relationship na yeye.

Baadhi ya watu walipiga vita mahusiano yetu. Walikuwa wakimuambia kuwa mimi nilikuwa namchezea tu, hatuendani. Ila hatukujali tukaendelea na mapenzi. Akawa ananiambia nimuoe sababu maisha ni yale yale na yupo tayari kuishi maisha yoyote na mimi. Japo mimi masikini lakini hajanipendea pesa. Tufunge ndoa tuishi kihalali. Basi kutokana na mapenzi yake, ikabidi nibadili mipango yangu sababu sikuwa nimewaza kuoa nikiwa chuo. Nikawapa taarifa wazazi wangu, mwanzoni walipinga ila baadae wakakubali. Nikamtambulisha nyumbani. Mimi sikuwahi kwenda kwao, ila nilikuwa najulikana.

Tukaanza process za uchumba, nikatoa mahari. Alifurahi sana. Mapenzi yalikuwa motomoto. Kila kitu kilienda sawa tukapanga kukirudi likizo nyumbani tufunge ndoa. Ila bahati mbaya au nzuri, dunia ikakumbwa na janga la covid19, mipaka ya nchi mbalimbali ikafungwa, hatukuweza kurudi likizo hivyo ikashindikana kutimiza azma yetu.

Tumedumu kwnye mahusano kwa zaidi ya miaka mitano. Mwaka jana, yeye alimaliza masomo yake, tukaagana. Mimi nilikuwa nimebakisha mwaka mmoja. Akarudi kwao, tukawa tunawasiliana, mapenzi yaliendelea, japo maisha yalibadilika financially sababu familia ziliathirika na janga la uviko. Mapenzi yaliendelea hadi hapo alipopata mchongo wa kazi.

Kuna siku alienda kugonga geti kwenye kampuni fulani, akaacha cv zake, akakutana na kijana mmoja muajiriwa wa hapo ambaye aliahidi kumsaidia kupata kazi. Alifurahi sana alinishirikisha vyote. Siku zikapita yule jamaa akamuambia arekebishe CV yake, akaniambia, mimi nikarekebisha kila kitu huku nikiwa na furaha japo nilikuwa na doubt. Sababu najua hakuna favour ya bure tu Dunia ya sasa. Nilimuonya mchumba wangu, nikamuambia awe makini. Ajaribu kuplay smart apate mchongo. Alinielewa basi michakato ya yeye kupata kazi ikaendelea.

Akaitwa kwenye interview, akapita na akapata kazi. Kipindi chote hiko alikuwa akinishirikisha kila kitu hadi conversations zake na huyo jamaa. Alimsifia kuwa ni mtu wa dini, na ni mwema sana. Baada ya muda kupita, akaanza kubadilika kuwa msiri. Akawa hainishirikishi tena mambo ya kazi. Akapunguza muda wa kunitafuta, nikimtafuta anasema yupo busy. Nikahisi kuna kitu kiaendelea baina yao. Nikawa kila nikimuuliza huwa anamtetea huyo mshkaji ma kusema ni mtu mwenye roho nzuri na amesaidia wengi. Basi tukawa tunagombana mara kwa mara, tunashuluhisha, anadai kazi zinabana, na mm sitaki kumuelewa. Ieleweke ameanza kazi miezi mitatu kabla ya mimi kurudi.

Basi kuna siku nikambana, akakiri kuwa alikuwa ananificha ni kwamba alikuwa alikuwa akikopwa hela na huyo jamaa ila hakunishirikisha, mara walikutana sehemu hakunishirikisha ila hakuna linaloendelea baina yao zaidi ya kazi. Basi mm nikasema ngoja nirudi maana hazijabaki siku nyingi.

Mungu si Asumani, nimerudi nyumbani salama. Mambo yakaenda fresh. Baada ya siku mbili nikiwa nae, naona texts zikiingia anaficha simu. Nikagundua anajaribu kunificha kitu. Baadae nachukua simu yake kusoma text, nakuta amefuta texts zote. Kumuuliza anababaika. Nikambana aniambie ukweli, nikamuambia akiniambia ukweli nitamsamehe na tutaendelea na mapenzi yetu.

Hapo ndo akakiri kuwa alianzisha mahusiano na yule jamaa, wakafanya hadi mambo yao bila kinga hata, na akapata na ujauzito ikabidi autoe. Kuumuliza why amenifanyia hivyi vyote after all we have been thru. Anasema eti jamaa alikuwa anatumia force, anamtishia kuwa atamuharibia kwa bosi na atakosa kazi. Hivyo hakuwa na jinsi.

Inavyoonekana ni kwamba jamaa alifanikiwa kumteka na kucontrol akili yake, so akawa anamtumia. Akakiri kuwa jamaa alimpiga hadi picha ya uchi akawa anamtishia ataisambaza kazini kote. Kiukweli niliishiwa nguvu, sikutegemea kama angeweza kufanya yote hayo. Kutokana na kunipenda sana, na kuwa mtu wa imani, ilipelekea mm kumuamini sana hapo kabla. Japo moja ya udhaifu wake aliokuwa nao muda mrefu ni kuamini watu kirahisi na huruma iliyopitiliza. Yani hata kuibiwa kwake ilikuwa rahisi sana.
Sijui hata nifanye nini kwa sasa.

Cha kushangaza after yote hayo, bado ananililia nimsamehe tuendelee na process za ndoa yetu. Anadai yupo tayari kuacha kazi. Mimi nimemuambia bora aniache, ili ibaki kuwa siri, nisimuharibie status yake Ila bado anasumbua. Amelia njiani na kupiga goti barabarani kiasi cha kuzua mshangao kwa wapita njia eti anaomba nimsamehe.

Kila mtu anafahamu kuhusu mahusiano yetu. Nashindwa jinsi gani ni-deal na hii situation. Cha kushanganza yote hayo yametokea within 3 months only. Naombeni ushauri wenu wakuu. Do you think this woman deserves forgiveness? What about familia yake, niwaambie kilichotoea wanirudishie mahari yangu au nifanyeje? Asanteni.


UPDATE:
Demu aliacha kazi ili turudiane, lakini ilishindikana. Nimemove on na maisha yangu na nimemblock kwenye mitandao yote. Nimeamua kurudia uplayboy wangu. Maisha yanaendelea. Asanteni kwa ushauri wenu.
 
Kuna rafiki yangu wakati nipo kibaruani kila wikiendi namchukua tunaenda kutembea .siku hizi yeye kapata kibarua Mimi sina ananiambia yupo bize.kazi zinabana simu jumapili Hadi jumapili.
vumilia ndo ukubwa huo.
Ila achana nae anza upya
 
Kuna maswali kazaa tu ya kujiuliza alafu ufanye maamuzi sahihi,

kama sasa yupo tahari kuacha kazi kwa ajili yako kwanini asingeacha kipindi icho uyo jamaa anaamtaka kinguvu?

Miezi mitatu kwa matukio ayo yote,na kubeba mimba na kuitoa,
Hakua tahari kukusubiria, ata kama ni vishawishi uo mda ni mchache sana.

Yote maamuzi unayo wewe, Amua vyema.
 
Kuna maswali kazaa tu ya kujiuliza alafu ufanye maamuzi sahihi,

kama sasa yupo tahari kuacha kazi kwa ajili yako kwanini asingeacha kipindi icho uyo jamaa anaamtaka kinguvu?

Miezi mitatu kwa matukio ayo yote,na kubeba mimba na kuitoa,
Hakua tahari kukusubiria, ata kama ni vishawishi uo mda ni mchache sana.

Yote maamuzi unayo wewe, Amua vyema.

Asante sana ndugu yangu kwa ushauri. Na mimi pia nimejiuliza maswali hayo.
 
Kuna maswali kazaa tu ya kujiuliza alafu ufanye maamuzi sahihi,

kama sasa yupo tahari kuacha kazi kwa ajili yako kwanini asingeacha kipindi icho uyo jamaa anaamtaka kinguvu?

Miezi mitatu kwa matukio ayo yote,na kubeba mimba na kuitoa,
Hakua tahari kukusubiria, ata kama ni vishawishi uo mda ni mchache sana.


Yote maamuzi unayo wewe, Amua vyema.
Mwanamke mwenzetu uvumilivu sifuri na nusu
 
Pole sana, maamuzi magumu yanahitajika. Inabidi urejee kwenye u playboy wako tu mzee ili huko mbele mambo yasiwe mengi zaidi.
 
Kiufupi sana huyo mwanamke ni "easy to get". Sio aina ya mwanamke ambaye unaweza kudumu nae kwenye shida na raha. Sasahivi anatumia excuse ya kuacha kazi ili umuoe kwasababu ya risk ya kuaibika iliyoko mbele yake. Ukimuoa tabia aliyoonesha within 3 months inaweza kuwa kubwa mara kumi zaidi.


SUMU HAIONJWI MKUU.
 
Kiufupi sana huyo mwanamke ni "easy to get". Sio aina ya mwanamke ambaye unaweza kudumu nae kwenye shida na raha. Sasahivi anatumia excuse ya kuacha kazi ili umuoe kwasababu ya risk ya kuaibika iliyoko mbele yake. Ukimuoa tabia aliyoonesha within 3 months inaweza kuwa kubwa mara kumi zaidi.


SUMU HAIONJWI MKUU.

Asante sana mkuu
 
Kuna maswali kazaa tu ya kujiuliza alafu ufanye maamuzi sahihi,

kama sasa yupo tahari kuacha kazi kwa ajili yako kwanini asingeacha kipindi icho uyo jamaa anaamtaka kinguvu?

Miezi mitatu kwa matukio ayo yote,na kubeba mimba na kuitoa,
Hakua tahari kukusubiria, ata kama ni vishawishi uo mda ni mchache sana.

Yote maamuzi unayo wewe, Amua vyema.
Case imeishia hapa.
 
Usipende kuendekeza mizaha na mwanamke yoyote ndani ya mahusiano anapoanza kuonyesha kukuletea elements za kuwa na mazoea na mwanaume mwingine hata kama atasema ni urafiki au biashara. Ukicheka na nyani utavuna mabua.

Ukishaona akili yako inaanza kukupigia kengele kuwa mwanamke wako analeta mazoea ambayo sio mazuri na mwanaume haijalishi ni mazoea gani, then una option moja tu kuwa mbogo ila sio kumuelewa.

Shida ilianza hapo alipokuwa anakujulisha kuwa kuna mwanaume ameahidi kumsaidia kupata kazi. Hapo ndipo kulikuwa sehemu ya kuokoa jahazi na heshima ya mwanamke wako.

Ni bora akuone mnoko kuliko umchekee kisha akishazingua akuangalie macho ya naomba unisamehe mimi ni kiumbe dhaifu sikujua ninalofanya.

Na ukisema usamehe hapo kifupi jua unamwambia mimi ni mjinga na nimekuruhusu unifanye unavyotaka maana sina pakwenda wala sina ujanja nje yako. Unaweka rehani uanaume wako.

Piga chini tafuta mtu mpya.
 
Kiufupi sana huyo mwanamke ni "easy to get". Sio aina ya mwanamke ambaye unaweza kudumu nae kwenye shida na raha. Sasahivi anatumia excuse ya kuacha kazi ili umuoe kwasababu ya risk ya kuaibika iliyoko mbele yake. Ukimuoa tabia aliyoonesha within 3 months inaweza kuwa kubwa mara kumi zaidi.


SUMU HAIONJWI MKUU.
Yes anawaza aibu atakayopata so anaona bora aache kazi ajisitiri kwa sasa ndo solution ya mwisho kabaki nayo.
 
Back
Top Bottom