Simiyu: Watoto wawili wafariki kwa kula mboga yenye sumu, saba wanusurika kifo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Watoto wawili wa Familia ya Tandula Ngasa, katika Kijiji Cha Mwakiloba Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, wamepoteza maisha na wengine saba kunusurika kifo baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu.

Akiwa kwenye mkutano wa Jukwa la tatu la Ushirika Mkoa wa Simiyu ambapo alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda amesema kuwa watoto walipoteza maisha mara baada ya kula chakula hicho.

Dkt. Nawanda amesema kuwa watoto wengine saba ambao walinusurika, wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Nawanda amesema kuwa Tandula Ngasa ambaye ni Baba wa Familia aliamka asubuhi na kwenda kupulizia sumu ya kuua wadudu kwenye shamba la Pamba, ambapo jioni mke wake naye alikwenda kwenye shamba hilohilo bila ya kujua na kuchuma mboga za majani kwa ajili ya chakula.

“Mama baada ya kuchuma mboga hizo na kwenda kupika bila ya kujua kama mume wake asubuhi alipulizia sumu ya kuua wadudu, walikula mboga hizo ndipo watoto wakaanza kuumwa,” amesema Dkt. Nawanda na kuongeza:

“Watoto wawili walipoteza maisha (hakuwataja majina) lakini wengine saba walikimbizwa hospitali Bugando Mkoani Mwanza na wanaendelea na matibabu.”

Akizungumza na wafiwa, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Anna Gidarya amewataka wananchi kuwahi kupeleka wagonjwa hospitali mara inapotokea changamoto ya kiafya badala ya kupoteza muda kutafuta njia mbadala za matibabu.
 
Aisee poleni sana wana Simiyu...
msiba wa Fisi mwenye hirizi haujaisha mara huu hapa mwingine wa poison
 
Mambo ya kilimo ni kuwa makini... nina mama yangu mdogo miaka hiyo ya 87 akiwa kazini mwanae alikunywa mbolea akidhani maziwa akafariki.
 
Back
Top Bottom