Ashikiliwa kwa tuhuma za kuua Watoto wake kwa kuwanywesha sumu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dainess Paul Mwashambo (30) mkazi wa Kijiji cha Mashese katika halmashauri ya Mbeya vijijini anayetuhumiwa kuwanywesha sumu ya kuulia magugu shambani watoto wake wawili Mario Semen Adamson (4) na mdogo wake wa kike aitwaye Beonis Semen Adamson (2) wote wakazi wa Mashese ambapo walipoteza maisha walipofikishwa Hospitali.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 09, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema kuwa, awali Machi 05, 2024 mtuhumiwa Dainess Paul Mwashambo akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese - Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu shambani aina ya "Pare Force" watoto wake wawili na kusababisha vifo vyao muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu.

Aidha, Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliosababishwa na kutuhumiwa kwa matukio ya wizi na Serikali ya Kijiji cha Mashese. Mtuhumiwa baada ya tukio hilo naye alikunywa sumu hiyo na kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linatoa wito kwa jamii kuwa pindi unapopatwa na tatizo suluhisho lake sio kujichukulia sheria mkononi bali ni kutafuta ushauri au kufuata sheria inavyoelekeza ili kuepuka madhara kwako na jamii inayokuzunguka.
 
Wapumzike Kwa amani hao Marehemu.

Wanaume kabla hatujawapa ujauzito Wadada/Wanawake basi tujitahidi kujipanga kwaajili ya malezi ya hao Vijacho.

Kwenye Case hii, inaonesha huyo Mama wa hao watoto alikuwa anawalea peke yake hao watoto huku huduma zikiwa ni za kusuasua.

Pia Wanawake ukiona Mwanaume haeleweki, msifanye kosa la kumbebea mimba.

Kumbuka sio Wanaume wote wanaweza kuwa responsible kwenye malezi ya watoto
 
Pili unaweza walaumu wanaume kumbe wanakimbia tabia mbaya za wanawake pana wanawake Wana negative energy ( hasira,matusi,mdomo mchafu,wagomvi,Malaya,nk ) utamani hata sekunde kuwa nae.
Ila tu mwanaume usitese damu yako kwa upumbavu wa mwanamke,we timiza wajibu wako usiwakimbie wanao.
 
Ni kweli Mkuu

Mimi nimejiapiza hata ikitokea bahati mbaya nimezaa huko nje, lazima nihudumie damu yangu

Mambo ya kuja kutesa watoto wako kisa tabia mbaya ya mama yao si nawachukua nawapeleka Boarding huko.

Uzuri Sheria inaruhusu kumchukua Mtoto wako kutoka Kwa Mama yake akifika miaka 7
 
Pili unaweza walaumu wanaume kumbe wanakimbia tabia mbaya za wanawake pana wanawake Wana negative energy ( hasira,matusi,mdomo mchafu,wagomvi,Malaya,nk ) utamani hata sekunde kuwa nae.
Ila tu mwanaume usitese damu yako kwa upumbavu wa mwanamke,we timiza wajibu wako usiwakimbie wanao.
Kukimbia mwanamke ndo ukimbie watoto wako? Hakuna sababu yoyote ya kuweza kuhalalisha mwanaume kukimbia damu yake.
 
Hata kama mwanamke akiwa mshenzi hakikisha watoto wako wanapata mahitaji yao yote. Mama wa watoto wawili kutuhumiwa wizi na serikali ya kijiji ni jambo lenye mambo mengi ndani yake. Hapo lazima kuna mwanaume mpumbavu aliyekimbia majukumu yake kama bado yuko hai.
 
Back
Top Bottom