Simbachawene aelekeza kusimamisha mishahara ya viongozi walioshindwa kusimamia Watumishi kutekeleza zoezi la PEPMIS

fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
5,023
5,000
#HABARI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Juma Mkomi kusimamisha mishahara ya viongozi walioshindwa kuwasimamia watumishi wao kujisajili na kujaza mipango kazi yao katika Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma na Taasisi za Umma (PEPMIS/PIPMIS) na kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo lenye masilahi mapana katika utumishi wa umma na taifa kwa ujumla.

Mhe. Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo mkoani Iringa alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakati akifungua Baraza hilo.

Amesema ujenzi wa mfumo wa PEPMIS/PIPMIS pamoja na mifumo mingine ya TEHAMA ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kwa dhati kuwa na Serikali ya kidijitali itakayorahisisha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Vilevile, amekemea tabia ya baadhi ya Waajiri kukataa kuwapokea watumishi wanaohamishiwa kwenye taasisi wanazoziongoza na baadhi kutoruhusu watumishi kuhama hata pale inapoelekezwa na Mamlaka kwani kwa kufanya hivyo ni ukosefu wa maadili na ni jambo ambalo halikubaliki.

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema elimu ya utekelezaji wa Mifumo ya TEHAMA ikiwemo Mfumo wa PEPMIS/PIPMIS na Mfumo wa Kubaini Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) imetolewa nchi nzima lakini kumekuwa na kutowajibika kwa baadhi ya viongozi katika kuwasimamia watumishi wao kutekeleza zoezi hilo.
 
George-Simbachawene-780x470.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi kusimamisha mishahara ya Viongozi walioshindwa kuwasimamia watumishi wao kujisajili na kujaza mipango kazi yao katika Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma na Taasisi za Umma (PEPMIS/PIPMIS) na kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo lenye masilahi mapana katika utumishi wa umma na taifa kwa ujumla.

Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo mkoani Iringa alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakati akifungua Baraza hilo.

Amesema ujenzi wa mfumo wa PEPMIS/PIPMIS pamoja na mifumo mingine ya TEHAMA ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kwa dhati kuwa na Serikali ya kidijitali itakayorahisisha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Mfumo huu wa PEPMIS na PIPMIS ni mbadala wa Mfumo wa Wazi wa Upimaji wa Utendaji kazi (OPRAS) na Mfumo wa Mikataba wa Utendaji Kazi wa Taasisi (IPCS) ulioonekana kuwa na changamoto za usimamizi wa utendaji kazi zilizojitokeza katika utekelezaji wa mfumo wa awali wa OPRAS hivyo mfumo huu umeboreshwa ili kuondokana na changamoto hizo, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mfumo huu muhimu,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Amesema mifumo hii ya TEHAMA ni nyenzo muhimu katika kutekeleza majukumu na inalenga kuleta tija, ufanisi na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya watumishi wa Umma na nchi kwa ujumla.

Amesema wanaotakiwa kuwajibishwa kwanza kwa kushindwa kutekeleza zoezi hili la PEPMIS/PIPMIS ni viongozi ambao wameshindwa kuwasimamia watumishi wao, hivyo hatua za kusimamisha mshahara zianze kwa viongozi huku watumishi ambao hawajatekeleza wapewe muda wa kutekeleza na wakishindwa, hatua zichukuliwe kwa watumishi hao.
 
Haya mambo ya kuingiza siasa kila mahali ndio hua yanaigharimu serikali. Ifike wakati kila jambo lifuate utaratibu, na wanasiasa wawajibishwe kulipa gharama za fidia serikali inapo shindwa kesi zinazo tokana na matamko ya kisiasa.
 
Simbachewene kila nikijilazimisha kumuona ni kiongozi mwenye akili na anaefaa lazima anithibitishie tofauti...

Kwanza kuropoka vitu ..
Pili kuleta taharuki...
Waziri mzima anaongea watumishi wafananane mshahara?
Daktari wa Muhimbili atafanana mshahara na daktari wa zahanati Kisiju?

Je wanafanana wingi WA kazi?
Mhasibu Halmashauri atafanana mshahara na na mhasibu tra?

Haya mawazo wanatoa wapi?
 
Back
Top Bottom