Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 2,331
- 3,071
Kuna hali ya kustajabisha ndani ya uongozi wa Simba katika kusimamia timu.
Hapo awali tuliona jinsi gani uchebe aliondolewa kwenye timu, ilianzia kwa mashabiki huko mwanza kumtupia chupa za maji na kushinikiza kocha hawamtaki, haikuchukua muda kocha akaondolewa klabuni na hali hiyo imewakuta makocha karibia wote walipewa kazi simba kipindi cha utawala wa Mo dewji huwa wanatimulia kutokana na shinikizo la mashabiki wa Simba na viongozi hawafanyi tathmini ya malengo yao bali hutimua tu.
Achana na makocha, hata wachezaji wa kusajiliwa wanasajiliwa kwa kufuata upepo wa mashabiki mfano kilio cha mashabiki ni kurejea kwa Chama na kweli viongozi wakafanya hivyo bila kuangalia uhitaji wake katika kikosi kulingana na timu ilivyo au kupata zaidi ya huyo Chama.
Luis karejea Simba ni kutokana na shinikizo la mashabiki, hivyo basi viongozi wakaufyata leo hii Luis kawa mzigo uwanjani sio Luis wa zamani.
Kuna kipindi mashabiki walijawa na hasira za kumkataa Matola hadi kutaka kuandamana lakini leo hii hiyo huyo Matola karudishwa mashabiki hao hao wamekaa kimya kwasababu roho zao za kumuona Robertinho akitimuliwa zimeshasuuzika
Uongozaji umeamua kumuachisha kocha ambaye kwenye ligi kuu kacheza michezo mingi pasipo kupoteza ila kuna swali la kujiuliza je aliyekutana nao na kuwafunga goli tano kikosi chao kinafanana na alichonacho yeye? Kwa maana ya umri, uwezo na ubora) ni mbingu na ardhi kabisa. Tukiangalia wachezaji tegemeo wa Simba ni wakongwe kiumri hata wapya waliosajiliwa na pia wengine wametumika sana hivyo wamechoka sana lakini cha ajabu zigo anatupiwa kocha kisa tu wanefungwa na Yanga.
Malalamiko yalianza muda mrefu kwa mashabiki kuwa Simba inacheza mpira wa hovyo lakini hapo hapo wanashindwa kujua kwenye mpira ni mchezo wa mbinu kutokana na timu unayocheza nayo, mbona mechi dhidi ya Al Ahly Dar, Simba ndio walioongoza kwa pasi na kucheza mpira mwingi? Ni approach tu za game lengo ni kupata matokeo mazuri lakini kelele za mashabiki jumlisha na kuchungilia mpira wa jirani (Yanga) ndicho kinachomfukuzisha Robertinho na sio kwasababu ya kupata matokeo mabaya kwenye michezo yake.
Kuna tetesi za wachezaji kusimamishwa kisa wamehujumu timu.
Hili nalo ni kituko kingine, mechi ya ngao ya jamii kule Tanga ilikuwa inaonesha wazi dhahiri shahiri kuwa Yanga wapoje safari hii, Simba walikimbizwa mwanzo mwisho hadi mtu unaomba dakika 90 ziishe. Kipindi hicho kocha wa Yanga hakuwa na first eleven, kipindi hicho Aziz Ki aliingia kipindi cha pili na Pacome kipindi hiko hakujulikana kabisa kama ni Zizuu wa Yanga, akapewa nafasi dakika za jioni kabisa hilo ilikuwa ni ishara ya kuonesha quality ya wachezaji wa Yanga ni level nyingine kabisa dhidi ya Simba lakini eti leo hii wachezaji wanashtumiwa kwa uwezo upi huo walionesha hapo kabla?
Kuna wachezaji wabovu wamesajiliwa je idada ya scouting umeajibishwa? Kuna maeneo yenye mapungufu na idara ya scouting imehusika kwa kutoleta mbadala je wameajibishwa kwa lipi?
Kuna wazee kama Saidoo hawezi mpute mpute wa mchaka mchaka hilo nalo uwanjani halionekani? Timu haina mkata umeme hilo nalo ni la kocha?
Je ukiweka mizania ya viwango na ubora wa wachezaji kati Simba na Yanga wanafanana?
Hata aje kocha gani mashabiki watamtimua tu kama wakiona wao hawafurahishwi nae. Matokeo vs mpira mzuri ni mambo mawili tofauti mashabiki wanapaswa walijue hilo.