Simanjiro: James Millya vs Ole Sendeka

Kama nilivyokwishasema awali katika vichwa vingine Millya ametia nia ya kugombea ubunge Simanjiro. Millya tatizo kubwa ni kwamba hii kesi ni ya siasa. Mashahidi wake ni wanasiasa ambao Sendeka aliwabwaga 2005, kama Ole Kone ambaye aliaibishwa mahakamani kwa kushindwa kujibu maswali aliyoulizwa na wakili, alitoa statements zinazokinzana na kufanya ushahidi wake uonekane ni wa kisasi na haukuwa na ukweli wowote.
Millya kama kwa Elimu aliyopata anadhani kuwa hakuna haja ya kusikiliza wazee wa kimila au basi hata basi Baba Askofu Laizer, anapotoka na anaweza kuanguka vibaya. Millya anakaa kwenye nyumba ya Lowassa -Kwa Iddi (njia ya Nairobi).
Hapa pia amemshambulia Ole Mengi bila sababu yoyote na hii inatia shaka na qaulity ya degree zake!!!
 
Kuweka facts sawasawa, millya anaishi kwenye nyumba ya rafiki zake ambao wamepanga kwenye hiyo nyumba ya sakina tangu miaka ya 2000, yeye millya amehamia hapo mwaka jana tu.
 
Kuweka facts sawasawa, millya anaishi kwenye nyumba ya rafiki zake ambao wamepanga kwenye hiyo nyumba hiyo ya sakina tangu miaka ya 2000, yeye millya amehamia hapo mwaka jana tu.
 
Hata mimi huwa nashangaa watu humu wanaquote habari nzima halafu wanacomment mstari mmoja! Kwa nini usinukuu sehemu ya habari unayoona unataka kuitolea comments? Kama unataka kutolea habari yote, kwa nini sasa unanukuu? Kwa kufanya hivyo vertical scrolling inakuwa ndefu na inaboa!
Mkuu, avatar yako. duh umeipenda tu au ina maana gani?:D
 
Kuweka facts sawasawa, millya anaishi kwenye nyumba ya rafiki zake ambao wamepanga kwenye hiyo nyumba hiyo ya sakina tangu miaka ya 2000, yeye millya amehamia hapo mwaka jana tu.
Do you know hizo nyumba ni za Lowassa?
James anaishi na yule mzungu aliyemsomesha kwenye hiyo nyumba. Awe anapanga au anaishi bure lakini ni nyumba ya Lowassa!
 
Wahenga walisema, ficha UPUMBAVU wako onyesha HEKIMA yako. inasikitisha kuona jinsi wana JF wakichangia hoja kwa kuongozwa na chuki na ubinafsi wa hali ya juu,kila mtu ana jaribu kuonyesha mapungufu ya Millya na makosa yake kwasababu tu wanaamini EL yuko nyuma yake,sote tunasau yale aliyotendewa na Sendeka. "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni"

1. Je ni halali kwa Sendeka kumpiga yeyote kwasababu tu amejipambanua kama mpiganaji wa ufisadi na jamii itamtetea kwa misingi hiyo?.
2.Je ni halali kwa Mengi kutumia vyombo vyake kukandamiza wengine?- Mfanyakazi mwenzangu aliniambia usiamini Habari yoyote inayo andikwa magazetini mpaka itakapoandikwa kuhusu wewe utakuwa na nafasi ya kuchambua ukweli na uongo.
Ni kweli ushahidi ulikuwa dhaifu,kijana hakujipanga hata wale waliohaidi kutoa ushahidi wengine waligeuka, mfano,Telele. Mbunge huyu ananitia mashaka alimuunga mkono Millya mwanzoni lakini pale millya alipomwonyesha msimamo na kumwambia hafai kuwa kamanda wa vijana jimbo la Ngorongoro ndipo alipomgeuka,na hii imejitokeza pia katika mapokezi ya Sendeka Simanjiro wabunge ambao hawakuungwa mkono na Millya kuwa makamanda wa vijana kwenye majimbo yao walienda Simanjiro kumpokea Sendeka, Felix Mrema wa jimbo la Arusha Mjini ambao ukamanda wake umechukuliwa na Diwani mmoja kwenye jimbo lake alikuwepo, Elisa molel wa Arumetru Magharibi ambaye ukamanda wake umechukuliwa na Medeye ambaye ni mpinzani wake jimboni alikuwepo, Lekule Laizer Mbunge mwadilifu asiye na makuu ambaye ndugu millya aliamini anastahili kuendelea kuwa kamanda wa jimbo la Longido naye aliwasindikiza swahiba zake Mrema na Elisa.

Jamvi hili ni muhimu kwa mustakabali wa fikra zetu ni vizuri tusirukie kuchangia hoja bila ya kutafuta ukweli wa mambo.

Nadhani ilikuwa ni wakati kwa wana JF hasa wenye fani ya Sheria kumshauri Millya cha kufanya rather than throwing stones to him,itamsaidia kujipanga upya na yeye aweze kupata haki yake na Sendeka apate fundisho la kuacha kunyanyasa watu wa chini na kukimbilia kwenye vikao vya mila.
 
Do you know hizo nyumba ni za Lowassa?
James anaishi na yule mzungu aliyemsomesha kwenye hiyo nyumba. Awe anapanga au anaishi bure lakini ni nyumba ya Lowassa!

Is that a crime? Kumbe wewe unfahamu zaidi, anaishi na mzungu aliyemsomesha South Africa, guardian wake ambaye ameishi hapo miaka mingi bila james. Whether ni ya lowassa au siyo, ina shida gani?
 
Millya C.V ya LL.M ina mashaka 'Hapa nilipo nina shahada ya pili katika Sheria za Haki za binadamu na demokrasia niliyoipatia katika vyuo vikuu vya Pretoria, Afrika Kusini na American University of Cairo.'
Masters moja vyuo vikuu viwili, nchi mbili tofauti na siyo affiliate ya chuo kingine! Umechemsha! Ulibebwa hivyo kubali kushindwa.
 
Naona vita vinaendelea.Kwenye bold hapa niingii akilini kabisa.Kusoma au kufanya harakati mbalimbali hakumaanishi kutumika ama kutotumika...Lakini pili atuletee CV yake humu kuzungumza kama kasuku hakuna impact yeyote.
Tusome taarifa yake kwa makini halafu tuijadili kama watu makini na tuache jazba na ushabiki usiokuwa na maana. ninasema hivyo kwa sababu nimegundu humu jamvini kuna watu wanapenda kuandikia hisia/mapenzi/chuki bila kutumia logic.
 
Wahenga walisema, ficha UPUMBAVU wako onyesha HEKIMA yako. inasikitisha kuona jinsi wana JF wakichangia hoja kwa kuongozwa na chuki na ubinafsi wa hali ya juu,kila mtu ana jaribu kuonyesha mapungufu ya Millya na makosa yake kwasababu tu wanaamini EL yuko nyuma yake,sote tunasau yale aliyotendewa na Sendeka. "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni"

1. Je ni halali kwa Sendeka kumpiga yeyote kwasababu tu amejipambanua kama mpiganaji wa ufisadi na jamii itamtetea kwa misingi hiyo?.
2.Je ni halali kwa Mengi kutumia vyombo vyake kukandamiza wengine?- Mfanyakazi mwenzangu aliniambia usiamini Habari yoyote inayo andikwa magazetini mpaka itakapoandikwa kuhusu wewe utakuwa na nafasi ya kuchambua ukweli na uongo.
Ni kweli ushahidi ulikuwa dhaifu,kijana hakujipanga hata wale waliohaidi kutoa ushahidi wengine waligeuka, mfano,Telele. Mbunge huyu ananitia mashaka alimuunga mkono Millya mwanzoni lakini pale millya alipomwonyesha msimamo na kumwambia hafai kuwa kamanda wa vijana jimbo la Ngorongoro ndipo alipomgeuka,na hii imejitokeza pia katika mapokezi ya Sendeka Simanjiro wabunge ambao hawakuungwa mkono na Millya kuwa makamanda wa vijana kwenye majimbo yao walienda Simanjiro kumpokea Sendeka, Felix Mrema wa jimbo la Arusha Mjini ambao ukamanda wake umechukuliwa na Diwani mmoja kwenye jimbo lake alikuwepo, Elisa molel wa Arumetru Magharibi ambaye ukamanda wake umechukuliwa na Medeye ambaye ni mpinzani wake jimboni alikuwepo, Lekule Laizer Mbunge mwadilifu asiye na makuu ambaye ndugu millya aliamini anastahili kuendelea kuwa kamanda wa jimbo la Longido naye aliwasindikiza swahiba zake Mrema na Elisa.

Jamvi hili ni muhimu kwa mustakabali wa fikra zetu ni vizuri tusirukie kuchangia hoja bila ya kutafuta ukweli wa mambo.

Nadhani ilikuwa ni wakati kwa wana JF hasa wenye fani ya Sheria kumshauri Millya cha kufanya rather than throwing stones to him,itamsaidia kujipanga upya na yeye aweze kupata haki yake na Sendeka apate fundisho la kuacha kunyanyasa watu wa chini na kukimbilia kwenye vikao vya mila.
.

Mkuu Bubba,Heshima mbele mzee.

1.Kama nilivyoandika hapo mwanzo,wengi wetu hapa jf ni ushabiki.
Kuna Mwana JF mmoja alileta hoja hapa, jinsi mengi anavyopindisha demokrasia ya nchi hii kwa kutumia media zake,lakini ile thread yake haikuchukua hata sekunde. Mods wakawa wamiitoa na nafikiri ata huyo member pengine ameondolewa.

Hiyo thread ilimwelezea sana mengi,likiwemo la kumtuma rafiki yake USA kwenda kufanya utafiti kama Wazri wa mambo ya ndani ana uraia wa marekani.Sasa mengi yeye ni nani?.

Usomi wetu hapa ni kufuata upepo tu.
Leo hii wana jf wameanza ku question elimu ya huyo kijana,bila ata kushituka tuhumu za huyu mbunge kama vile kumpa mwanafunzi mimba.

Mafisadi papa anaowajua mengi ni wale watano tu ambao ni wahindi?Je hao ndiyo walioifanya nchii hii ifikie hapa ilipofikia?
 
Millya C.V ya LL.M ina mashaka 'Hapa nilipo nina shahada ya pili katika Sheria za Haki za binadamu na demokrasia niliyoipatia katika vyuo vikuu vya Pretoria, Afrika Kusini na American University of Cairo.'
Masters moja vyuo vikuu viwili, nchi mbili tofauti na siyo affiliate ya chuo kingine! Umechemsha! Ulibebwa hivyo kubali kushindwa.
.
Hawa ndiyo wasomi wa tanzania.
Thrread imegeuzwa kwenye vyeti.Tutafika kweli?
 
Tusome taarifa yake kwa makini halafu tuijadili kama watu makini na tuache jazba na ushabiki usiokuwa na maana. ninasema hivyo kwa sababu nimegundu humu jamvini kuna watu wanapenda kuandikia hisia/mapenzi/chuki bila kutumia logic.
.

Nakupa 100% mkuu abunwasi
 
Millya punguza jaziba. malalamiko yako yana harufu ya kutaka kujijenga kisiasa ili baadaye ugombee ubunge. Lakini kosa ulilofanya kubwa ni kudharau mila na desturi za wazee wa kimasai. Kosa hilo hutasameheka kamwe. Kumpa mimba msichana wa shule ni kosa lakini unadhani katika mila zenu watakuonea huruma kwa hilo? Ni wasichana wangapi wa kimasai wanaozeshwa wakiwa wadogo?Nakushauri umwombe kaka yako Sendeka na Wazee wa kimasai msamaa ili kufipisha malumbano yasiyo na tija na hiyo bado inaweza kukujengea heshima baadaye.
 
Millya C.V ya LL.M ina mashaka 'Hapa nilipo nina shahada ya pili katika Sheria za Haki za binadamu na demokrasia niliyoipatia katika vyuo vikuu vya Pretoria, Afrika Kusini na American University of Cairo.'
Masters moja vyuo vikuu viwili, nchi mbili tofauti na siyo affiliate ya chuo kingine! Umechemsha! Ulibebwa hivyo kubali kushindwa.
.
Haruna Malima, inawezekana kabisa kupata masters za vyuo vikuu viwili kwa kozi zinazoitwa collaboration, kama IFM wanatoa Masters in International Bussiness in colaboration na chuo fulani cha India.

Kwenye professionalism, degree inayomatter ni ya kwanza, siyo ya pili, Ole Milya anajiita mwanasheria wa haki za binaadamu na demokrasia, niliuliza LL.B yake ni ya wapi?. Sikupata jibu popote.

Kuitwa Mwanasheria kwa tafsiri ya kwetu ni LL.B holders, kupata LL.M mtu yoyote anaweza kusoma LL.M na haifanyi kuwa mwanasheria.
 
Katoto haka kanakofisadishwa na EL, kanaanza kulia lia sasa! Kalisema haki inapatikana mahakamani, imepatikana, kana ikataa! Kujua kwamba EL anakafisadisha, ona kanavyo mvaa mzee Mengi, yaaani kameingia kwenye gemu za kifisadi! Ole Sendeka moto wa kuotea mbali, hata aongeapo bungeni utapata kitu kutoka kwenye hoja zake. Sio wewe unalialia huna hata uwezo wa kujenga hoja. Unataka tu kwenda kuongeza namba ya mafisadi bungeni.
 
N ninavyomjua EL, kama hizo tuhuma alizotoa Millya dhidi ya Sendeka zingekuwa na chembe ya ukweli, leo hii Sendeka angekuwa gereza la Karanga! These allegations are simply an after thought and intended to save the boy's face baada ya kuona wenzake wameondoa oxygen kwenye chumba alichomo!
 
Ushauri wa ziada kwa Ole Milya,
1.Sababu za kutupwa kesi ni ushahidi dhaifu ambao umeshindwa kuestablish prima facie.
2.Serikali haiwezi kukata rufaa kwa weak case kama hii, kama hata yeye mwenyewe Ole Milya ameshindwa kuithibitishia mahakama alipigwa kofi/ngumi shavu gani, hakumbuki kama ni la kulia au kushoto!. Wala kwenye maelezo yake ya awali, hakuripoti kutishiwa bastola!.
3. The only remedy ni yeye Ole Milya kujipanga upya, afungue kesi ya madai, civil suit dhidi ya Sendeka, anadai milioni kadhaa, kesi itadrag mpaka baada ya uchaguzi, Sendeka atashinda uchaguzi na atashinda tena hiyo kesi, na hapa itakuwa ndio the begining of an end kwa Ole Milya.
 
Back
Top Bottom