Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #41
Mwanakijiji,
Mimi jana nimetoa rushwa BRELA, ndio, nasema kweli, hakuna haja ya kuficha wala kuona aibu.
Nimekupata.. nilidhani hapo mwanzo ulikuwa unawajibika wewe mwenyewe. Unajua kitu ambacho nadhani kinasumbua kuhusu hii rushwa ya nyumbani ni kwamba haionekani kuwa ni "adui ya haki" kwa sababu kama ukilipa kitu kidogo unapata unachotaka (kwenye mfano wako faili) na usipolipa inakuwa ni kuzungushana basi mtu anajikuta analipa na hivyo anarahisisha anachokitaka.
Ndio katika minajili hiyo najiuliza tunaweza vipi kushindana na rushwa wakati rushwa inaonekana kana kwamba iko upande wetu?