Siku nilipotoa rushwa

mkuu kwenye hiyo topten mbona tanzania haimo?

Kwenye hiyo poll, Tanzania ipo kwenye range ya 50-74% ya kutoa rushwa.
Rushwa ni mbaya..Hapa nyumbani kuna maeneo ya msingi ambayo ni haki kwa mwananchi ila kuhudumiwa ni mpaka utoe rushwa. inadidimiza sana maendeleo na kadiri siku zinavyoenda imekuwa kama part ya maisha bongo.
 
kwa hiyo unadhani uwepo wa rushwa unarahisisha mambo yako kwenda vizuri?
kwa mfano umefika hospital umekuta foleni watu 50 alafu nesi akakuambia toa 10,000 akuhudumie utampa?
_au umekamatwa na mali ya magendo ya ml20 alafu wakakuambia toa ml 5 uende hata kama huo mzigo hauna hiyo faida na usipotoa wasizi mzigo na ukiangalia sheria inasema hivyo kweli na mali sio ya wizi ni yako....

Yeah mambo yanaenda murua kabisa, unajua km unatoa rushwa then hakuna mtu anaeathirika direct, no problem....ht JK ili achaguliwe kuwa Prezdaa mlungula ulitembea sn,,, hata rais ajae ili achaguluwe ni lazima atoe rushwa, either ya maneno, fedha au mali yyt, hata zile mbege tunaxopewaga na CCM kipindi cha uchaguzi ni rushwa
 
Hahahah, rushwa yangu ya kwanza inachekesha!! Shule ya msingi nilisoma kijijini so fimbo na ubabe ilikuwa kwa sana shuleni. Mimi nilikuwa mwembamba sana nilikuwa kadogo dogo sana so hata kuchezea kifinyo ilikuwa kawaida sana. Mi ni wa mwisho kwetu sasa nilikuwa na ule utoto utoto wa mwisho na ki ukweli nilikuwa mpole sana na mtulivu sana sasa siku moja nilibonyezwa na class monitor class baada ya mtawanyiko akanitafuta nje tena coz nilimzingua kidogo. Rafiki yake bro akawa anapita akampa stick za kutosha. Nkaona huu ni ujinga sana nilikuwa na vihela vyangu fulani mjomba aliniachiaga. Nkavichukua kesho yake nikaenda skul mpaka kwa mwalimu wa class nkamtoa 400 nikamwambia anifanye monitor. Akanipa mamlaka aiseee. Ikawa no vipigo hovyo tena. Daah ila by then sikujua kama ile corruption niliona ni harakati fulani tu za kujikomboa.
 
huu uzi hauna wala rushwa wala watoa rushwa au wanaogopa takukuru?
 
Kuna wakati unahitaji huduma na huna jinsi inabidi utoe rushwa ukizingatia hata huo muda wa kusema ni haki yako huna,
 
nimekamatwa na mzigo wenye thamani ya ml5 wameniomba rushwa ml2 au wausizi mzigo leo hii na baadae nikakopa pesa nikalipa ml2 ...faida ilikuwa nipate laki nne baada ya kuuza na nilipe ada ya watoto kwani mmoja kaja na barua ya kumsimamisha kwenda shule....
_hivi kama ni wewe unafanyeje alafu aliyeniwezesha kulipa kazuia mzigo hadi nimipe pesa yake na huku watoto sijalipa ada....
_maisha magumu sana!!
 
Habari,
Wananchi wenzangu ,Tanzania ni nchi Yetu ambayo tunapaswa kutambalia katika miongozo ya TANU mpaka CCM ya mwaka 1995,
Lakin kutokana na mmomonyoko wa maadili na tamaa ya baadhi ya watendaji wa serikali na mashirika binafsi wameyaweka kando maadili hayo,

Kila ofis imekuwa rushwa kila ofisi imekuwa kubaniana fursa kisa rushwa,

Tulipata faraja sana kwa kujitokeza sehem kama forum ambayo watu walipewa fursa ya kuongea bila woga na bila kubanwa, lakin suala la rushwa limekuwa hatari sana,

Naombeni tukomeshe huu mchezo, na ningeomba unisaidie suala moja tu we ndugu msomaji

Kama umewahi kutozwa RUSHWA, au unajua eneo ambalo liko na rushwa sana, taja hapa chini, au kama wahofia usalama wako niwekee katoka PM, mi najua pa kuyawasilisha hayo malalamiko,

Kumbuka kwamba habari ambayo utaleta PM Iwe ya uhakika na ukweli , na itabaki kuwa siri yangu na wewe uliyetuma hiyo PM, Nawasihi tutaje bila kuogopa, na haki yako utaipata, hakuna haja ya kujua jina lako mwanzoni wala hatuliitaji sana jina lako ila tunataka kisafisha sehem hiyo.

Tajeni hapa , kama waogopa njooni PM nafasi zipo za kutosha,

Sishangai kuona Uzi uu unaweza kunifanya kuzuiliwa maana habari nyingi zinaenda kugusa penyewe. Ila napata matumaini kuwa kwa kuwa hii ni jamii forums huu uzi utakuwa ,

Uzi uu tunaomba usiunganishwe na mwingine uache uwe huru,
Tuige mifano ya watu ambao au mataifa ambayo yanakemea rushwa kwa vitendo,

Britanicca
 
Hapa ulitakiwa ujitambulishe vizuri ila kwa kuwa umekuja hivyo hivyo nasisi tutakujibu bila kujitambilisha,

Nina maswali matatu,
1. Kwani mpaka niwe nimeathirika Mimi, au jamaa yeyote kama nina taharifa nitoe?
2. Kwani vipi hawa wakubwa wao hawajuhi kuwa rushwa imeshwheni has a kwenye kada zao
Mfano yule kijana aliyepokea hela pale annex hotel ili akiue chama cha mlengo wa kiislam huku bara, naye VIP? Pia kuna mwingine kaleta billion 12 kwenye chama kikuu cha upinzani na kukiweka mfukoni naye vipo
 
Rushwa haiepukiki ndugu na haitaisha, binafsi sipend kutoa rushwa wala upuuu huo

Ila hebu pimia umekamatwa na mzigo wa maujanja wa milion 2 alaf askari wametaka laki 5,
Na mzigo ukipelekwa TRA basi ujue umetaifishwa na umeukosa sasa8vwe hapo unadhan ungefanyaje

To rushwa responsibly panapo dharura, japo naipinga sana
 
Mkuu hongera kwa wazo lako ingawa sijui wewe ni nani lakini hakika haitaji tochi kutafuta Wala rushwa kama una nia sio siasa unaweza fanya yafuatayo:
1. Tafuta mtu yeyote anayefuatilia cheti cha kuzaliwa nenda nae vizazi na vifo,watawapa calender ila mkihonga cheti kitatengenezwa haraka sana inauma sana utadhani sio haki ya mtoto na mzazi kupata cheti, hukipati tarehe zilizowekwa kila siku nenda rudi mpaka uhonge.

2. Chukua gari ya mtu yeyote jifanye kama una kosa barabarani jamaa watataka chao honga pesa za moto kamata.

3. Nenda Sehemu za huduma mbali mbali polisi,mahakamani,Tanesco TRA, Idara ya ardhi ya halmashauri yeyote then usiwe na mkono mfupi uone mambo yako yanavyokwenda haraka hadi huruma kwa wasio na kitu.

ANGALIZO NI BAADHI WALIO KWENYE HIZI IDARA NDIO WALA RUSHWA WAPO WENGINE WANAFANYA KAZI KWA UADILI
 
Kuna kauli umesema kuwa "iwe na uhakika na kweli" hapo ndipo tunaposhindwa kutokomeza tatizo hili la rushwa, maana ukitaka mtoa taarifa awe na uhakika basi unataka aje na ushahidi mpaka mahakamani. Mimi nakushauri upokee hizo taarifa na huo uhakika ukafanye upelelezi na utafiti mwenyewe. Mfano nikikwambia kuwa taasisi fulani au kampuni fulani kuna mtu anapokea rushwa kwenye kuajiri watu, kwa nini unitake nikuletee ushahidi badala ya kwenda kufanya upelelezi mwenyewe? Hebu badilikeni ili mpewe ushirikiano.
Polisi huwa wakipewa taarifa au fununu yeyote huifanyia upelelezi na ikithibitika ni kweli huipeleka mahakamani na isipopata ushahidi huachana nayo.
 
Habari ndugu zangu wapendwa!
Leo pasipo na haya naomba tuelezane hapa; je umewahi omba au kutoa rushwa? Kitu gani kilisababisha hadi ukafikia uamuzi huo?

Mimi mwenzenu nimewahi toa rushwa; hakuna mtu ambaye alikuwa mbishi kutoa rushwa kama mimi, lakini siku ile nilikamatika; ilikuwa kipindi Mke Wangu alipokuwa hospitali moja ya serikali hapa dar akisubiri kujifungua, alikuwa na maumivu makali sana akilia, dakitari na manesi walikuwa wakimpita kama nyanya mbovu, nilipiga mkwara lakini waapi; watu ndo kwanza wanabadilisha shift tu.

Nikatafakari nikaamua kumkamata daktari mmoja, nikamshikisha kitita, Huwezi amini, madaktari na wakunga walichangamka ghafla, nakumbuka walimpetipeti Mke wangu, alikuwa chini akataftiwa kitanda ghafla, tena wakamhamishia sehemu nzuri, wakamtoa kule mchanganyiko penye kelele na vilio vya uchungu.

Wakati huo kwakuwa na mimi kidume nilikuwa nimepagawa kama vile nami Nina mimba nikaanza kupoaa! Sasa nikawa napewa update za kila hatua anavyoendelea Mke Wangu! Kwakweli walinijali sana hadi nikawaza mimba ingekuwa ni shibe ningerudi tena kesho yake!
Mkasa mwingine ni pale nilipokuwa naomba Umeme TANESCO; nilipigwa karenda hadi nikaamua kuzama mfukoni; nakumbuka baada ya kutoa; watu walifanya kazi hadi usiku huku wakipuliza miluzi Kwa bashasha.

Ipo mikasa mingi sana watu hutoa Rushwa ili kujinusuru, kuna mheshimiwa mmoja ambaye Kwa sasa ni mtu mmoja mkubwa sana, aliwahi toa rushwa ujanani Kwa kumpa mimba mtoto na akaepuka kifungo cha miaka 30, na hivi sasa ni mheshimiwa, Rushwa ilimstiri yamkini leo angekuwa mnyampara na ndoto zake zingepotelea gerezani.

Kuna mtu mmoja aliwahi sema kwamba "WAKATI MWINGINE RUSHWA HUBADILI SHETANI KUWA MALAIKA" Mwingine akasema utawala usio zingatia sheria, RUSHWA HUWA HAIEPUKIKI"

Naomba kuweka kwenu wadau tujadili kila mmoja; nini kilikufanya utoe au upokee rushwa! Ilikuwaje! Nini kifanyike!
Karibuni!
 
Back
Top Bottom