Waziri Mkuu: Wananchi ni wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya rushwa, msitoe rushwa mahali popote

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kutoa rushwa mahali popote huku akisisitiza kuwa wananchi ni wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya vita hiyo.

Ametoa wito huo leo (Jumapili, Desemba 10, 2023 wakati akizungumza na washiriki na wadau mbalimbali kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Nyerere Square, jijini Dodoma.Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt.

Samia Suluhu Hassan, amesema Mheshimiwa Rais amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kuendelea kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo:“Zingatia Maadili, Utu, Uhuru na Haki kwa Maendeleo Endelevu.”“Ninyi ni wadau wakubwa wa kukomesha rushwa.

Nyie ni wadau wakubwa wa kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ili nchi yetu isiwe na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, wananchi mnapaswa kufichua vitendo vya ukosefu wa maadili na uvunjifu wa haki za binadamu,” amesema.“Mtanzania usikubali kutoa rushwa popote, hasa kwenye maeneo unayopaswa kupewa huduma hiyo.

Wewe ni Mtanzania unalindwa na sheria za nchi za kupata huduma bure kama vile hospitali bila kutoa rushwa. Inatakiwa kila Mtanzania abebe jukumu hili kwa mikono miwili, alisimamie na alitekeleze,” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 
Back
Top Bottom